aina ya bango litalotumika katika kampeni ya TTB na TFF ya kuhamasisha umma kwenda kuishangilia Taifa Stars itapocheza na Ivory Coast January 4, 2010 katika uwanja wa taifa jijini Dar
Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya FIFA 2010 Mh. Dr. Shukuru Kawambwa akiongea leo na wanahabari ofisini kwake jijini Dar kuhusu maandalizi ya kamati hiyo na kampeni ya kuhamasisha nchi washiriki wa michuano ya Kombe la Dunia kupitia hapa nchini ama kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi kuelekea nchini Afrika kusini katika michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kufanyika mwakani nchini humo. Wengine toka kulia ni Dan Mrutu Kutoka Baraza la Biashara na Frolence Turuka katibu mkuu wa wizara ya Sayansi Teknolojia na Elimu ya juu

Rais wa TFF akifafanua jambo wakati wa mkutano huo. Wengine ni Dk Shukuru Kawamba, Mh. Frolence Turuka na Bw. Dan Mrutu.

BILIONI SABA ZATENGWA KWA KAMPENI YA FIFA WORLD CUP 2010
Jumla ya shilingi Bilioni 7 zimetengwa kwa ajili ya kugharamia kampeni ya kuhamasisha nchi washiriki wa michuano ya Kombe la Dunia kupitia hapa nchini ama kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi kuelekea nchini Afrika kusini katika michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kufanyika mwakani nchini humo.

Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu, Dk Shukuru Kawamba, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya FIFA 2010, amesema leo pesa hiyo itatumika kwa matangazo katika vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na vya kimataifa, ulinzi na kuzigharamia timu na wageni.


Dk Kawambwa kasema televisheni za Supersport kutoka Afrika Kusini na SunVideo kutoka Brazil ziko tayari kufanya kazi ya kutangaza mambo mbalimbali yanayohusu Tanzania na maadalizi ya timu mbalimbali zitakazokuwa hapa nchini. Vyombo vingine ni BBC, Dautchwelle, Al jazeera VOA na vingine vingi.

Ameelezaa kuwa kampeni hiyo itaanza mapema wakati Timu ya Ivory Coast itapowasili nchini Januari 2 na kucheza na timu ya taifa Taifa Stars januari 4 na pia itacheza na timu ya Rwanda Januari 7 ambayo itawasili hapa nchini Januari 6 kwa ajili ya mchezo huo.

Rais wa Shirikisho la Mpira nchini Leodegar Chilla Tenga amesema tayari TFF wana mawasiliano na nchi nyingi zilizofanikiwa kuingia kwenye Fainali za Kombe la Dunia chini Afrika Kusini.

Tenga kazitaja nchi walizokwisha wasiliana nazo kuwa ni pamoja na Ujerumani, Italy, Denmark, New Zealand, Brazil, Australia, Korea Kaskazini,Japan, Argelia na Nigeria na nchi zingine ambazo bado mazungumzo yanaendelea.

Wakati huo huo Bodi ya Utalii (TTB) ikishirikiana na TFF wameanza kampeni ya kuhamasisha umma wa watanzania kwenda kuiunga mkono na kuishangilia Taifa Stars wakati wa mechi yake na Ivory Coast katika mchezo wa kirafiki Januari 4 kwenye uwanja wa Taifa.

Katika kampeni hii kutakuwa na mabango makubwa na madogo ya matangazo, vipeperushi, matangazo ya redio, magazeti na televisheni pamoja na vijarida ili kuhamasisha mashabiki kwenda kushangilia timu yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Good stuff. Next time we'll be bidding to host the World Cup...

    ReplyDelete
  2. am i missing something here? $7 earmarked for what? why couldn't we spend the same amount of money to make sure our team qualified even for Angola?

    i fail to understand who comes up with such pathetic ideas, and they are approved and implemented.


    i might be missing something in the whole abracadabra.

    ReplyDelete
  3. NI KUPOTEZA PESA ZA MMA BILIONI 7, HUO NI UJANJA NI NJIA ZA KUCHOTA PESA ZETU KWA MLANGO WA NYUMA WAKATI KUNA WATOTO WANASOMA CHINI YA MIEMBA HAMNA BANDA LA DARASA WALA DAWATI, KOMBE LA DUNIA HALITUHUSU KWA VILE HATUMO KATIKA MASHINDANO, NI KURNGRNEZA ULAJI TU KWA MLANGO WA NYUMBA KWA VILE UMESHASHUTUKIWA KATIKA TENDA ZA UMEME SASA MNA-CREATE WIZI WA KIINI MACHO MNATUPIGA MABAO YA KISIGINO NA CHANGA LA MACHO, WIZI NI WIZI TU HATA KAMA NI WA KUIBA KWA AJILI YA CHAKULA CHA WATOTO

    ReplyDelete
  4. I do not have a problem with us spending 7 billion. I suppose the question is what are we getting in return?

    What are our priorities?? kuendeleza timu zetu za ndani au kushabikia timu za wenzetu??

    Probably not worth it, really.

    ReplyDelete
  5. OK!

    Watu wa Ngurudoto Mountain Lodge wamelala au??? Hali ya hewa ya Arusha itakuwa karibu sawa na hali ya hewa ya Bondeni - pale Ngurudoto ipo hoteli ya nyota 5 na wana uwanja mzuri tuu wa mpira. Changamkieni dili hiyo nyie akina Mrema!!

    ReplyDelete
  6. AHA KUMBE PESA ZIPO, SASA KWANINI MNASHINDWA KUUJENGA UWANJA WA NYAMAGANA UA MNAULINDA UWANJA WA CCM? HII NI HATARI KWA NCHI KUTEGEMEA VIWANJA VYA VYAMA VYA SIASA NA HASA KILICHOPO MADARAKANI. LICHA YA KUWA ULIJENGWA KWA PESA NA NGUVU ZA WANANCHI NA SERIKALI CCM IKAUPORA NA BADO INAENDELEA KULIPWA KWA KITU AMBACHO HIKUKIGHARAMIA! TFF JENGENI VIWANJA BADARA YA DILIHILI LITAKALOISHIA KUSEMWA KUWA LIMEIINGIZIA HASARA TFF.

    ReplyDelete
  7. Waziri wa miundo mbinu ndio kiongozi anashindwa kutupatia umeme halafu hela tunaitumia kwa kushabikia timu za wenzetu haya sasa mmemshtua mpaka mzee kawawa sasa mwaka mpya wote umeharibika!

    ReplyDelete
  8. Nimependa wazo, ila uamuzi umechelewa mno. Nchi nyingi Afrika zimefika mbali katika suala hili. Endapo tnataka kufaidika zaidi tungetengeneza ndege ztu za air Tanzania ili zitumike kuleta watalii. Vinginevyo tutawapa faida KQ na SA tu. Kufufuliwa kwa AIR TZ ndio ingeleta faida zaidi.

    ReplyDelete
  9. Hii ni pesa nyingi sana na si busara ikatumika eti kwa ulinzi na kuzigharamia timu na wageni. Nani kasema timu hizo za nje zitakazoweka kambi hapa hazina uwezo wa kujigharamia zenyewe? kuna nini hapa?. Ushauri, pesa hiyo itumike kuiandaa timu ya taifa iweze kufuzu na kushiriki mashindano makubwa ya kimataifa, faida yake itakuwa:- kuitangaza nchi yetu kwa kutumia timu ya taifa, wachezaji watakaong'ara watapata ajira kwa kununuliwa na timu kubwa hivyo kuitangaza nchi yetu na kukuza utarii.

    ReplyDelete
  10. hey guys tuwe serious kidogo.......billion 7 for what? do you think there is a team that can come to tanzania while here in sauz kuna more than 42 stadiums.alafu ni ngumu cause here its cold alafu unaenda kuweka kambi kwenye nchi ya joto.....izo team zenyewe hazitaki kwenda durban because most of the fixture there in jozi,cape town and bromfointein( here sometimes comes to negative) how come waje dsm 32celcius....they can come 4 2 days and not more than a week...sometimes wawe wanauliza hata makocha wa tz kama its possible maana hali ya hewa ina change and affect the performance....its up to u guys

    ReplyDelete
  11. hahaaa sasa hivi ndio mnakumbuka hayo wakati wenzetu walishaanza tangu 2006

    too late..

    ReplyDelete
  12. Kwa nchi za Ulaya kwenye kamati ya Ufundi hutumia zaidi ya Billioni Mia.Na pia kila mchezaji huwa na kamati yake ya Utaalamu.Nashauri ili tuweze kufikia kiwango cha Mpira wa Kimataifa.

    ReplyDelete
  13. Same old story!! that's what you can do best enh. 7 billions could save lives of how many starving families? could supply clean water to how many tanzanians. could help improve health services provision tohow many provinces in that poor tanzania. watanzania mna matatizo.
    Wanjuki Mkenya wa london.

    ReplyDelete
  14. hapa nashindwa kufahamu! hivi uwaja wenyewe mmoja,timu ngapi zitaweka kambi? si waongee tu na timu moja ya africa bas kuliko kutenga hela zote hizo kwa kampeni

    ReplyDelete
  15. Too late. Some of us had this idea as early as 2008 and mentioned it to the CECAFA during the CECAFA cup hosted in Dar. Then the government very reluctantly let the 2 high standard stadia for the tournament and by then the stadia had been complete for quite a while but had never been used. It seemed such a waste. Idle stadia built to a very high standard! The idea is great but this should have been started as soon as it was known that SA was going to be the World Cup host because our stadia were already at an advnaced stage of construction. So we built the stadia and we were not sure what we wanted to do with them. Very late indeed and the countries that qualified for the World Cup would never have qualified if they operated on such a short term/ surprise planning as TFF and this committee are operating on. Besides, I don't see anyone from the hospitality industry industry involved they are key players for anything like this to succeed. What is Kawambwa doing on this committee- core members should have been TFF, hospitality industry, Tanzania Tourist Board. We really should have been contacting qualifying teams on the very night of their qualifying matches with a congratulatory message and an offer to acclimatise to African weather with a detailed offer of packages including posible dates the satdia could be used, accommodation,training and fitness facilities when teams are not on the pitch transport, security, diet/meals, health and medication and so on. I doubt if these guys have thought to that level of detail even at this 11th hour that they thought fit to make this announcement. Good idea but too late by at least 2 years.Can it guys!

    ReplyDelete
  16. TFF hii ngoma mngesuka dili na ESPN wakaionyesha kimataifa ingekuwa bomba sana. Wacha mechi ionekane dunia nzima, watu waone wabongo walivyojaa uwanjani na uwanja ulivyo bomba.

    ReplyDelete
  17. upumbavu Nyerere angepiga bakora wote wenye mawazo ya kipombe pombe..bilioni saba kwa ajili ya kuwaandalia wageni..wakati ndani ya nyumba watoto wanalia njaaa..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...