Brother Michuzi,
Kuna wizi katika ATM za CRDB,Jana nimetoa LAKI
Mbili(200,000/-Tsh)katika Waterfront CRDB Branch ATM nimefika officini
nakuta imepungua elfu 30,Mke wangu leo ametoa laki 8, amekuta imepungua
ELFU 40 katika CRDB Lumumba ATM.
Sijui kama hili tatizo limeshakuta mtu mwingine. ??
Tafadhali wadau Count your Cash Before Leaving the ATM


Wishing you Mary X-Mass and Happy New Year

Mzalendo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Mdau mbona hii haijakaa vizuri? Kwenye ATM kwa siku mtu unaweza kuchukua hela not more than 500000 sasa hiyo laki 8 alichukuaje?
    Hii habari inaonekana uwongo kwa watu wanaojua mambo.

    Nawasilisha
    Mdau D...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Laki 8 inatoka ATM ZA CRDB sio jambo la kushangaa

      Delete
  2. mimi
    nadhani suala siyo tu ATM za fulani nadhani CRDB kama benki wanahitaji kulifanyia kazi kwa kuwa wakati mwingine unaenda kwenye ATM unakuta zile printout hazipo japokuwa ATM hizi huuliza kama je unapenda kuendelea na transaction zako ama la hasha japokuwa wengi wetu tunaenda kwenye hizi huduma pale tu tunapokuwa katika shida kubwa ya kipesa lakini mimi nashauri benki husika iwe na umakini zaidi na sisi tuwe makini pia katika mahitaji mbali mbali je pale ATM inapomzidishia mteja huwa inakuwa vipi !!!

    ReplyDelete
  3. Je ukihesabu ukiwa kwenye ATM na ukakuta pungufu, kuna uwezekano wa kupewa kilicho pungua au ndo inakuwa basi sadaka kwa benki?? Maana kuna kipindi jamaa yangu aliibiwa hela na watu wasiojulikana kupitia ATM(kutokana na rekodi zilivyoonyesha), lakini benki(jina kapuni) iligoma kutoa ushirikiano kwa kutumia kamera zilizokuwa installed kwenye ATM. Sasa kwa tukio la wizi alilofanya mtu mwingine inakuwa ngumu je kwa tukio la hela pungufu linalohusisha benki itawezekana?Just curious!

    ReplyDelete
  4. receipt ilionyesha hela ngapi umetoa? na balance kwenye account inaonyesha hio pungufu imetoka? jibu kwanza hilo kabla hujaconclude kwamba umeibiwa. ATM unless kama ni mbovu otherwise kinachotoka ndicho kinachoandikwa kwenye risiti. Unachotakiwa kufanya ni kuingia ndani ya bank na huo ushahidi

    ReplyDelete
  5. sio kweli tena CRDB bank hata ATM zao unaweza kuweka pesa naukakuta zimeingia kwenye account sahihi bila kupunjika jana nimechukua hela crdb mbagala nanikadeposit pale azikiwe bila kupungua helaa,dont find excuses for your own poverty!

    ReplyDelete
  6. aisee,sasa ulivyouliza wahusika wakijibu nini?

    ReplyDelete
  7. Pole kwa wizi huo, hata hivyo nashangaa kiasi siku hizi CRDB wameongeza kiwango cha kutoa pesa kwenye ATM toka laki 4 kwa siku???? Maana sielewi ni vipi mkeo alitoa Laki nane kwenye ATM??

    ReplyDelete
  8. ebwana hayo matatizo huwa yanatokea any atm lakini ndo usikae kimya bira kwenda ku comprent,lazima record wanayo,kwenye statment yao,na wewe lazima unapokuwa unatoa pesa make sure unachukua list ya pesa ulizotoa,nasema hivyo kwani siyo atm za bongo tu,mie ilisha nitokea uk,lakini nillikwenda ndani ya bank na wakaona tatizo ni lakwao,hivyo ikabidi walipe money back.usiishie kuwish happy xmas tu nenda ukadai pesa yako watachukulia mwanya huyo kama hutaenda.marlesa mussa wa 22 hapa uk.

    ReplyDelete
  9. yawezekana ukakuta hela imepunguwa kutoka kwenye ATM ila ulitakiwa kuhesabu kuangalia kama ziko sawa.Pia kwa wadau wengine wasiojuwa CRDB unaweza kuchukuwa hela kwenye ATM mpaka milioni moja utaratibu huu umeanza mda mrefu kwa
    Mazoko

    ReplyDelete
  10. Mdau wa kwanza si vyema ukawa unakurupuka kabla hujafanya research. Mtu hawezi kusema jambo hilo out of blue. Pia kuna sehemu nimesoma last week kwamba max amount ya ATM withdrawal ya CRDB ni 1M kwa sasa, I'm not so sure about this.

    ReplyDelete
  11. ninachojua ni kwamba,
    1. pesa nyingi zinazowekwa kwenye ATM hazina kiwango bora, kwenye ATM inatakiwa note mpya kabisa.
    2.replenishing ya ATM pia ni tatizo, mwekaji akichanganya note tu, basi! ukiweka 5000 kwenye magazine ya 10,000, ni tatizo sana.
    3.ATM zenyewe bwana ni mbovumbovu, most of them ni second hand.
    4.servicing of them ni tatizo, utakuta journal imeisha, staff wa kupeleka hawaendi in time.
    5. kwa kifupi bado tuko nyuma sana, inatakiwa uweke risiti yako mara unapotransact, iwe kama ushahidi wako.
    6.wale ambao hela inaanza kutoka kwenye mashine yeye ndio anatoa wallet au anapokea simu, hela itarudi ndani, ile ni automated kitu.
    7. usivute vute note, kama zinatoka zitatoka tu,
    i hope nimesaidia kidogo.

    ReplyDelete
  12. Minimum amount ya kuchukua hela kwa mkupuo mmoja ni $400 au laki tano unaweza kuchuka nyingine tena kwa mkupuo mwingine lakini jumla kwa siku ni milioni moja. Ukitaka zaidi unaenda ndani. Na huyo inawezekana kweli kachukua kwani ni lazima mke na mume wawe na joint account inawezekana kila mtu anayakwake. Kwa sisi tulio kwa watu CRDB kutoa maximam ni $700 kwa siku, ila kwa mkupuo ni $400 kwa hiyo kufikisha 700 inabidi utoe tena mkupuo mwingine wa 300 natumai wenye mawazo sana na Xmass na kushindwa kufikiria kwa haraka wataelewa sasa

    ReplyDelete
  13. si kwa watu wanaojua mambo, ni kwa watu wanaojua taratibu za CDRB .
    Taratibu zinatofautiana .

    ReplyDelete
  14. MIMI NI MTUMIAJI MKUBWA SANA WA ATM ZA CRDB NA NIMEZITUMIA ATM ZOTE HAPA MJINI LAKINI HILI TATIZO BADO TATIZO SIJALIONA.

    NAKUBALIANA NA MDAU MMOJA HAPO JUU QUALITY YA NOTE INAWEZA IKAWA SABABU. NOTE ZILIZOCHAKAA ZINAWEZA KUSABABISHA UPUNGUFU WA FEDHA ZINAZOTOKA KWENYE ATM.

    KWENYE ATM ZA CRDB UNAWEZA KUTOA LAKI 8 KWA MIKUPUO MIWILI YA LAKI 4 KILA MOJA, INAWEZEKANA.

    ReplyDelete
  15. HILO LINAWEZEKANA KUTOKANA NA STANDARD YA PESA KAMA NI CHAKAVU INAWEZEKANA KABISA PIA COMPUTER MULFUNCTION INATOKEA HADI HUKU ULAYA ONE DAY IN MANCHESTER ONE OF BARCLAYS BANK ILIKUWA INKUNYA PESA TU, UKIENDA TOA POUND KUMI INAKUTELETEA MIHELA KIBAO WATU WAKAAMBIZANA MTAA MZIMA KILA MTU AKAJA MBIO KUJA TOA PESA ZA BURE, RISITI INAONYESHA UMETOA KUMI NA COOUNT YAKO IMECHUKULIWA KUMI LAKINI MIPESA BWELELE ILITOKA NA ILIKUWA WEEKEND, JUMATATU ILPOFIKA WAKAGUNDUWA WAKAANZA KUFUATILI WATU WALIOCHUKUWA PESA WEEKEND LAKINI MAHAKAMANI ILISHINDIKANA KWA VILE KILA MTU ALIDAI AMETOA KUMI NA ACCOUNT YAKE IMEKATWA KUMI NA RISITI NI KUMI BASI HASARA IKAWA YA BENK NA NINAHISA HATA HAPO KAMA RISITI INAONYESHA LAKI NANE NA AKAUNT IMETOKA NANE SI RAHISI SANA KUIBANA BENKI CHA MSINGI NI KUWAALIFU WAFANYE MATENGENEZO, INAVYOONYESHA HAPO KUNA TATIZO LA PROGRAMMING YA HIYO COMPUTER.

    ReplyDelete
  16. kutoa hela crdb mwisho ni shs milioni moja kwa siku. kwa mkupuo mmoja ni shs laki 4 kwa hio unaweza kufanya laki 4 mara 2 na laki 2 mara moja katika siku moja.
    wadau wanaohoji kutoa laki 8 kwa siku bila kuwa na taarifa kamili ndio muelewe sasa.

    kuhusu swala la kuibiwa inabidi uende benki ukaongee nao. hawa crdb wana uzembe fulani. washaniharibia junior jumbo account ya mtoto wangu wakafungua kwa jina la mama yake.

    ReplyDelete
  17. hii kitu imekuwepo kwa muda sasa, December 21 mimi pia nimekwenda kwenye ATM mlimani city, nitataka kutoa 50,000 ikaniambia please wait, kama dakika tano, kadi ikatoka na msg kwamba am sorry ur request can not be completed at the moment, the next day nikawa town, nikataka nitoe hela 50,000. ila nikaona niangalie mini statement. statement shows 50,000 was withdrwan on Dec 21 while i didnt get any money.

    ReplyDelete
  18. Kwenye atm ZA crbd unaweza kuchukua mpaka 1M kwa siku na ni huduma inayotolewa kwa muda mrefu sasa.Kuhusu kutoka fedha pungufu report CRDB,najua mtua ambaye ilimtokea hivyo na wakam refund.Mara nyingi zinapungua kati ya 10 na 50 thou.CRDB wanalijua tatizo hilo.

    ReplyDelete
  19. fri Dec 25, 01:19:00
    mdau hapo juu mimi pia naunga mkono hoja yako coz hata mimi ilishawahii kunitokea tena ilikuwa january so hili ni tatizo la muda mrefu tuu, nalivyoenda bank kucoplain wakaniyayusha eti pesa yangu itarudi automaticaly kwenye Ac yangu baada ya few dayz. Na nilivyo hoji what seemz to be the problem wakaniambia coz card niliyokuwa natumia ni ya nje(Europe) so matatizo kama hayo huwa yanatokea.Nikasubiri hizo few days for my money to get back to the Ac but honestly nothing has happened..so mi nadhani ATM zetu za nymbani bado haziko kwenye standard za kimataifa ukizingati Banks husika pia hawako serious na huduma ya ATM au may be hawajui nini umuhimu ya ATM meaning kwamba hawajazingatia misingi ya huduma ya ATM kama ilivyo kwa wenzetu wa mataifa yaliyoendelea.So in my own opion nadhani banks usika wanatakiwa kuwa makini na kutake into considaration all the complian received about hii huduma ya ATM.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...