JK akimzawadia jezi ya TAifa Stars nyota wa Ivory Coast na Chelsea Didier Drogba katika dina la mchana alilowaandalia wachezaji na viongozi wa Taifa Stars, Rwanda na Ivory Coas mchana huu hoteli ya Golden Tulip jijini Dar.
JK katika picha ya pamoja na timu ya Ivory Coast
JK na Ivory Coast
JK katika picha na timu ya Taifa ya Rwanda ambayo imedhatua nchini kucheza na Ivory Coast kesho neshno
Kocha wa Taifa Stars Marcio Maximo na vijana wake
Baadhi ya wachezaji wa Rwanda

JK akoshwa na ziara ya Ivory Coast
*Awaandalia chakula maalumu Golden Tulip
*Amwagia sifa Drogba, amkabidhi uzi wa Stars
Awaombea watwae taji, aahidi Watz kuwashangilia
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, ameelezea kufurahishwa na ujio wa timu ya taifa ya Ivory Coast ‚The Elephant’ kwani umeutangaza nchi kutokana na wachezaji wake nyota wa kimataifa kujulikana akiwemo mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Didier Drogba.
Akizungumza katika hafla maalumu ya chakula cha mchana aliyoiandaa kuwakaribisha Ivory Coast, kwenye Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar leo JK kasema Tanzania imepata sifa kubwa duniani baada ya kutangazwa kwa mara ya kwanza katika kituo cha televisheni cha Sky News, kuhusiana na ziara ya The Elephant katika habari za michezo, sambamba na kuonyesha picha.
Kikwete alisema, kutangazwa kwa mechi kati ya Tanzania na Ivory Coast ni sifa kubwa kwa nchi, hasa ukizingatia Taifa Stars iliweza kuwamudu The Elephant ambao walikuwa wamesheheni nyota wa kulipwa na kutoka na ushindi mwembamba wa bao 1-0, lililofungwa na Drogba.

Rais alimpa pongezi kubwa mshambuliaji huyo ambaye pia ni tegemeo wa klabu ya Chelsea ya England, kwa kuitangaza Tanzania alipokuwa akihojiwa na Sky News Sports, ambako hakusita kusifu kiwango cha wachezaji wa Stars, kuwa ni kikubwa.

"Jana nilifurahi sana nilipokuwa nikiangalia kituo cha Sky News Sport, kwa mara ya kwanza kuona wakitangaza timu ya Ivory Coast ikiwa nchini, ambapo mchezaji nyota wa kimataifa Drogba alikiri kwamba, Tanzania soka lipo huku akisifu kiwango cha Stars," alisema Kikwete.

Kikwete alisema, kutokana na Drogba kuwa mchezaji maarufu duniani, kwa kupitia umaarufu wake, Tanzania imeweza kujitangaza duniani kote na hiyo itasaidia kuwavutia nyota wengine kufanya ziara hapa nchini.
"Hivi sasa Dunia nzima inatambua kiwango cha soka la Tanzania, natoa shukrani nyingi kwa Ivory Coast kuichagua nchi yetu kupiga kambi ya kujiandaa na fainali hizo za Angola," alisema Kikwete.

Aidha alisema, alipanga kuandaa hafla hiyo na kuwaalika wachezaji wa Ivory Coast, lakini baadaye akaona ni bora ajumuike na timu zote tatu, ambazo ni wenyeji Tanzania, Rwanda na Ivory Coast.

Katika hatua nyingine, Kikwete aliwataka wachezaji wa Rwanda ‚Amavubi’, kucheza kwa kujituma na ushirikiano mkubwa ili kuwafunga Ivory Coast, baada ya Stars kufungwa 1-0 licha ya kuwa, angalau wangeweza kutoka sare, lakini bahati haikuwa yao.

Aliongeza kuwa, Tanzania itajivunia hivi sasa katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, kutokana na Ivory Coast kuichagua pekee kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na fainali za Angola, pamoja na Kombe la Dunia litakalofanyika Afrika Kusini.

"Ninaamini kuwa, Bara hili la Afrika lina timu nyingi huku Ivory Coast ikiwa inaongoza kwa ubora, hivyo kwa kuchagua kuja nchini kwetu kufanya mazoezi ya mwisho ya kujiandaa kwenda Angola katika Fainali za Afrika, ni jambo la kujivunia kwa kila Mtanzania," alisema Kikwete.

Wakati huohuo, Kikwete alisema, anawaombea kwa Mungu na Miungu mingine kutwaa ubingwa wa Afrika, ili kurejea na Kombe hilo kama walivyopanga kulileta na kulipeleka Mlima Kilimanjaro na kuongeza kuwa, ana imani watashinda.

Aidha alisema, Tembo hao wa Ivory Coast watakapotinga hatua ya fainali, Watanzania watakwenda kuipa sapoti ili kutwaa taji hilo.

Mwisho wa hafla hiyo, Rais Kikwete aliwakabidhi jezi ya Taifa Stars, wachezaji nyota wa kimataifa wa Ivory Coast, Didier Drogba, Kolo Toure, Emmanuel Eboue, Solomon Kalou na Yaya Toure.

Fainali za Mataifa ya Afrika zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 10 hadi 30, mwaka huu nchini Angola.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 46 mpaka sasa

  1. mzee wa bunjuJanuary 06, 2010

    KIKWETE NDIO NYERERE WETU, NAMPENDA SANAA RAIS HUYU WA WATU, KWA MASIKINI YUPO, KWA MASUPA STAR PIA, MATAJIRI YAANI KIKWETE NI WA KILA MTU NI FAHARI ILIOJE KUA RAIS KAMA HUYU, KITENDO ALICHOFANYA CHA KUA INVITE DINNER SIJUI LUNCH KIMENIFURAHISHA SAANA , KWA SASA IKULU NI YETU SOTE WANANCHI HONGERA RASI WETU. MAANA NAJUA KUNA WANAOKUPONDA WALLAHI WALA USIWAJALI MAANA BAADHI YA WATANZANIA NDO ZAO, HATA BABA YAKO NYERERE WALIMZODOA SAANA TU ENZI ZA UONGOZI WAKE LEO AAAHHH KILA MTU TUMUEZI NYERERE WAKATI WALISHAMSEMA WEEEE MPAKA WAKACHOKA, MARA OOO MJIMA SIJUI NINI, KASHFA KIBAO, TANZANIA TUMEZOEA KUMSIFU MTU AKIFA, KAWAWA SI HUYO LAKINI ENZI ZAKE WENGINE WALIMKASHIFU SAAANA TENA SANA TU LEO LULU YA KILA MTU. UNAFIKI WATANZANIA TUACHE, HASA HAO JAMAA ZETU WA NG'AMBO KWA WAZUNGU HAO KILA KITU KIBAYA NA ALWAYS WANALINGANISHA NA MAREKANI NA ULAYA WENGINE WANATHUBUTU HATA KUSEMA HAWATORUDI, ACHENI BWANA HATUBABAISHWI NA MTU, MAANA MKATAA KWAO MTUMWA KAMA WAO NI BORA SI WAJE WAONGOZE??

    VIVA KIKWELI NA ALLAH ANAJUA YOTE YALIYO GHAIBU NA DHAHIRI

    MZEE WA BUNJU

    ReplyDelete
  2. JK unaonesha ni mpenda maendeleo sana,sema voingozi wa chini wanafanya nini,hapa unajaribu kuipromote nchi yako peke yako muheshimiwa,hivi bodi ya utalii iko wapi,kwenye bango la hii mechi si waliweka logo yao,hongera rais,watu wa bodii ya utalii wanadhamini miss tz wanawacha matukio kama haya,hawa ivory coast ni mamilionea na wengiu wao wana wake wazungu,ilikuwa ni wakati muafaka kwa bodi ya utalii kuitangaza nchi kwa hawa watu,ili siku wake zao na watoto wakitaka kuiona africa,iwe ya kwanza nchi yao then tz,maana kuna kila kivutio,yani bodi ya utalii haifai kabisa,wameweka tangazo cnn wiki mbili,hatujaliona tena,ona kenya wanavyoitangaza nchi yao 7times a day cnn,alafu mnalalamika eti kenya wanatuzidi.big JK

    ReplyDelete
  3. Hongera sana Mhe Rais Jakaya Kikwete.Kwa ukarimu wako mzuri juu ya wanamichezo wetu na wageni, hii inatupa Heshima sana miongoni mwa Nchi nyingi duniani, na hasa kwa watanzania walioko nje.Hongera sana Rais!!

    ReplyDelete
  4. Diet ndio inatofautisha wachezaji wetu na hawa wanaocheza ulaya.Sisi kila siku ni Nguna-ndondo,wali-ndondo.Wenzetu wanakula kwa mpangilio sio kila leo hicho hicho.

    ReplyDelete
  5. tanzania tunajulikana duniani kwa ukalimu na sio udini

    ReplyDelete
  6. "MHESHIMIWA RAIS KIKWETE UMEWEKA HISTORIA YA SOKA LA TANZANIA"

    Soka lilikuwepo kwa juhudi na moyo wako sasa limefikia hatua ya kukomaa tayari kwa michezo ya kimataifa.

    Mchango wako kwa soka la Taifa unastahili sifa zote kama kiongozi wa kwanza kuelewa "kilio" cha watanzania katika maendeleo ya soka kilijificha moyoni mwa kila mtanzania.

    MAXIMO ndiye mshika usukani,kelele za wanaotaka ubadilishaji wa kocha ni wale wasioulewa mchezo wa mpira zaidi ya kuingiza " siasa" za upinzani wa kibinafsi,hakuna umuhimu wa kubadilisha makocha kila wakati tunapopata matokeo yasiyoridhisha,timu zinazocheza kwa maelewano zimewachukuwa muda mrefu kufikia hatua ya kimataifa.

    Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha "BBC-WORLDTVSPORTS LIVE" wameonyesha "Klip" ya mchezo wa Taifa Stars na Ivory Coast kwa ulimwengu kushughudia kiwango cha
    Taifa Stars kimefikia hatua ya juu.

    Katika historia ya uongozi wako pamoja na uzinduzi wa soka nchini utakumbukwa daima,naamini "There`s a Hope" ipo siku vijana watakukabidhi kombe la Afrika,pia Taifa Stars itakuwa mojawapo ya nchi nane za mashindano ya mwisho katika "World Cup" ya miaka ijayo.

    "MAKE NO MISTAKE MAXIMO IS THE ONLY SOLUTION FOR OUR FUTURE TANZANIA NATIONAL TEAM"

    Mickey Jones Amos
    Denamrk

    ReplyDelete
  7. this guy Drogba is very humble! u just look at his face and u see it! its very hard to not like him, best wishes and may he bring the World cup home to Africa in June!
    Amandla!

    ReplyDelete
  8. MHE. JK HUNA MPINZANI. MAMBO UNAYOYAFANYA NI MAKUBWA. YOUR SO SIMPLE, HUMBLE AND INTELLIGENT I BELIEVE. WANAOKUPONDA WACHA WASEME MWISHO WATACHOKA. NA DAIMA, KELELE ZA MLANGO, HAZIMFANYI MWENYE NYUMBA AKOSE USINGIZI. UMETIMIZA AHADI NYINGI IKIWEMO HIYO YA MICHEZO. WANAO TAKA UIGEUZE TANZANIA IWE PARADISO ALL OVER THE SUDDEN WATAJIJU. WATU WAMEKALIA MAJUNGU MITAANI NA UVIVU WA KUFANYA KAZI HALAFU WANATAKA MAISHA BORA!! WATAYAONA KWENYE TV TU. LANGU MOJA TU KWAKO ENDELEA KULITUMIKIA TAIFA KWA MOYO NA UADILIFU ILI SIFA YAKO, HATA KAMA HAITAMFIKIA HAYATI BABA WA TAIFA, LAKINI NAAMINI UKO KARIBU SANA. KAZA BUTI, 2010 WALA USIKOSE USINGIZI MZEE. SUBIRI KUSHINDA KWA KISHINDO NA WENGINE KUANGUKA KWA KISHINDO!! ILA WABUNGE WAKO WENGI USITEGEMEE KUWAONA NA WALA USIWASAIDIE KWA LOLOTE ILI WAVUNE WALICHOPANDA. WENGI WAO HAWANA LOLOTE. MUDA WOTE WALIKUWA DAR NA DODOMA. MWAKA HUU WANAKWENDA VIJIJINI KUTOA MISAADA YA MIFUKO MIWILI YA SARUJI. WASHINDWE NA WALEGEE

    MDAU

    ReplyDelete
  9. Jamani chakula cha mchana kinaitwa dina? Hata kama ni kukiongezea kiswahili msamiati hii kuita chakula cha mchana dina ni wendawazimu. Tafuteni neno lingine, heck tafuteni hata neno la kimatumbi lenye maana ya chakula rasmi cha mchana tutalikubali, ohh where is kifimbo cheza when you need him arrrgh.

    ReplyDelete
  10. Raisi wetu anatuonyesha kila njia sisi usingizi zzzzzzzzz.atusaidieje????????.wabongo wanadhani hapo kawakaribisha kuburudika kama tu burudani.Mzee wetu anatuunganishaa na channels kibao.Hebu nendeni UDOM kachunguze mambo yake.US,kilimo,Hao muwaoneni hivyo tu wana njia nyingi za kututangaza.TUKO NYUMA SANA.MAJUNGU SAWA.HATUNA HATA UTAIFA.Mara POLLISI kanyanyasa waandishi wa Habari mara mpiga picha kafungia kamera.at the end of the day HASARA NI YA NCHI YETU.kitu kikubwa ni MAJUNGU,UJUAJI,RUSHWA,UZEMBE,KUKWEPA UWAJIBIKAJI,KUJIWEKA JUU BASI.KAZI-NOTHING.MZEE ANAFANYA KAZI ILA SISI NYUMA YAKE ZERO.MKURUKUTWA

    ReplyDelete
  11. kaka sahihisho, hakuna dina la mchana. Dinner chakula cha usiku na lunch ni chakula cha mchana.But hongera kwa kazi nzuri ya kutuweka up 2 date.

    ReplyDelete
  12. HONGERA SANA RAIS WETU,
    MUNGU AKUZIDISHIE, AKUJAALIE NA NAOMBA UENDELEE NA MOYO WAKO WA UKARIMU.

    MWANGA MWANGA

    ReplyDelete
  13. ALHAJ ABUBAKARYJanuary 06, 2010

    MUHESHIMIWA KIKWETE BASI JARIBU KUWAAMBIA HAO VICHWA VYA WANDAWAZIMU PENGINE WEWE WATAKUSIKIA WAJITAHIDI SANA HATA NA SISI TUWAONE KWENYE RUNINGA KATIKA FAINALI ZA MATAIFA HURU YA AFRICA 2012.

    ReplyDelete
  14. Mzee wa Bunju umenifurahisha sana wewe ni shtui!!! Kwa lugha yangu ya Mahenge yaani wewe ni kichwa kwa maana umeongea Kifalsafa!!! safi sana Mtuwa! yaani mzee!
    you made my nice day man!

    Mdau Marekani!!

    ReplyDelete
  15. hivi watanzania tunajisifu kuwa kiswahili chetu ni sanifu. lakini kila siku hapa kuna kuja watu na maneno ya ajabu, na leo hata wewe michuzi umeandika "imedhatua" nini maana ya "imedhatua"

    halafu kuna mwengine kaandika "ukalimu" nini "ukalimu"?

    ReplyDelete
  16. UKIFANYA JAMBO ZURI LINALO ELEWEKA TUNAKUPA HONGERA, UKIFANYA JAMBO LA HOVYO TUNAKUKOSOA... MICHEZO NDIYO YENYEWE HONGERA JK...There is lot's of $$$ and Tsh..in Sports

    ReplyDelete
  17. We mchangiaji unayehusisha chakula na miili ya wachezaji lazima uwe mwangalifu kuelewa kuwa kwa wastani watu wa nchi kama Ivory Coast, Senegal na Cameron ni warefu kuliko sisi wa Afrika y amashariki. Hii suala ni genetic na hata ungeshinda na kukesha mkahawani huwezi kuondokana nalo. Ni kweli zipo features zinaweza kubadilika kwa chakula na kwamba katika muda mrefu mabadiliko ya genes yanatokea. Baada ya kusema yote hayo, nakubali kwamba pengine kuna ukweli kuwa baadhi ya wachezaji wetu hawana miili ya kiriadha na hili ni jambo ambalo halianzi mtu anapokuwa na miaka 18 umri ambao kwa bahati mbaya ndio wengi wa wachezaji wetu hujitokeza jukwaani.

    ReplyDelete
  18. michuzi ulinyimwa kuingia kwenye munuso nini mbona sioni unamukumbatia/mikonozzz didia globula? siyo kawaida yako kukaa mbali hahahaha tetetehteh

    ReplyDelete
  19. Na sifa hii ya ukarimu ndo inatufanya tuwe mabwege tunaibiwa kila siku na wazungu,waarabu,wahindi sasa wachina nao wamejichanganya ktk kula bila kumbakizia baba.Hii sifa ya ukarimu ingekuwa inatuletea mazuri tungekuwa mbali.

    ReplyDelete
  20. nchi nyingi zinatamani kuja bongo tatizo usafiri, barabara zetu zimejaa foleni kila kona. utaratibu wa usafiri ndo' unaowanyong'onyeza wageni

    ReplyDelete
  21. Tanzania tuna ukarimu na Rai wetu ni mkarimu na anajua kuvaa

    ReplyDelete
  22. Shida zote za nini, Maisha yenyewe mafupi. Bora ukafurahia maisha na watu, utakumbukwa utaenziwa. Ni fahari kuwa na Rais mpenda michezo nas tuko nyuma yako! Hao mafisadi wanajenga nyumba za mabilioni washughulikie kwelikweli! Tutafika tu! Zamani walikuwa wanakula kimyakimya siku hizi ukiguza tu wazee wa libeneke watakuanika within 5min habari iko alaska!

    ReplyDelete
  23. No!
    ningependa kumrekebisha mdau wa 06:18:00pm!
    Tanzania hatujulikani kwa lolote!! Tunajulikana kwa kupakana na KENYA. thats all!!
    'Biashara matangazo'
    Mheshimiwa president has great ideas, but I think he should learn to delegate to appropriate departments and hold them reswponsible if they dont perform.
    You can not advertise tanzania in tanzania!!!

    ReplyDelete
  24. dinner:the main meal of the day siyo lazima iwe usiku. Wamatumbwi bana! elimu ndogo ubishi mwingiiiiiiiiii....

    ReplyDelete
  25. nilijiuliza saana wakati drogba anabadilishana bendera na nsajigwa baadae niligundua kilichosababisha tofauti ya maumbile ni unga wa yanga ambao uliletwa miaka ya 80 wakati wa njaa... ule unga ulikuwa na sumu ambayo ilikuwa inaathiri mfumo wa ukuaji wa binadamu... vimelea vyake vilikimbilia hadi kwenye kizazi cha binadamu. wale ambao enzi hizo walikuwa bado wanaendelea kukua ukuaji wao ulisitishwa na wale ambao walikuwa wamesha kua walianza kuzaa viandunje na ukweli unajidhihirisha ukiangalia wachezaji wa zamani ambao ukomo wa kukua uliwafikia kabla ya huo unga wengi saana walikuwa na maumbile makubwa viandunje ni vya kuokoteza wakati miaka hii wakina adebayor ni wa kuokoteza.. angalia karibu nchi zoote zilizoizunguka TZ kama Rwanda,Burundi,Congo,Kenya,Uganda na Malawi wao ni warefu.

    NONDO

    ReplyDelete
  26. Mageni ya humu kwenye libeneke utayajua tu.Kwa akili zenu mnategemea mtu kama Ankal hajui tofauti ya Lunch na Dinner?Msitujazie utumbo wenu,lugha ya humu iacheni kama mlivyoiona.

    Teacher mkuu.

    ReplyDelete
  27. din·ner (dĭn'ər)
    n.

    1. a. The chief meal of the day, eaten in the evening or at midday.
    b. A banquet or formal meal in honor of a person or event.
    c. The food prepared for either of these meals.

    2. A full-course meal served at a fixed price; table d'hôte.


    [Middle English diner, morning meal, from Old French disner, diner, to dine, morning meal; see dine.]

    Word History: Eating foods such as pizza and ice cream for breakfast may be justified etymologically. In Middle English dinner meant "breakfast," as did the Old French word disner, or diner, which was the source of our word. The Old French word came from the Vulgar Latin word *disiūnāre, meaning "to break one's fast; that is, to eat one's first meal," a notion also contained in our word breakfast. The Vulgar Latin word was derived from an earlier word, *disiēiūnāre, the Latin elements of which are dis-, denoting reversal, and iēiūnium, "fast." Middle English diner not only meant "breakfast" but, echoing usage of the Old French word diner, more commonly meant "the first big meal of the day, usually eaten between 9 A.M. and noon." Customs change, however, and over the years we have let the chief meal become the last meal of the day, by which time we have broken our fast more than once.

    The American Heritage® Dictionary of the English Language, Fourth Edition
    Copyright © 2009 by Houghton Mifflin Company.
    Published by Houghton Mifflin Company. All rights reserved.

    GO FIGURE!

    ReplyDelete
  28. Jamani najua kuwa wengi wa watoa maoni humu wako nchi za watu Ulaya, Marekani na kwingineko duniani why msirudi nyumbani na kushirikiana na viongozi wenye moyo wa nchi yao kama Kikwete? Kama kweli mnajali mngerudi home TZ na kufanya kweli ili mpunguze msururu wa waomba visa kwenda nchi za watu kufanya kazi ambzo hapa nyumbani mngeweza kuleta manufaa kama mnavyojitahidi kutoa maoni ya kujenga na kua-appriciate mambo ya viongozi wachahce kama Kikwete, Magufuli na wengineo. Njooni mpambane na hao mnaodai ni mafisadi wa nchi yenu badala ya kukaa pembeni na kukosoa kila jambo.Ala!?

    ReplyDelete
  29. Mdau Ola,
    Na wewe ni kukosoe siyo kwa kupakana na Kenya bali kwa mauaji ya Albino ili kutajirika.

    ReplyDelete
  30. Na hawa wanaojifanya kukosoa habari za dina la mchana wana ka-uwehu nn?
    Ina maana hamjui hiyo ndio lugha ya humu?
    Au mnafikiri ankal hajui tofauti ya dina na lunch?
    Changieni mada sio kutia ujuaji humu,ebo!

    ReplyDelete
  31. jamani jamani!!!! hebu nyie mnaodai dina ni chakula cha jioni rudini kwenye kamusi. main meal of the day sio lazima iwe jioni jamani. nadhani ankal amefafanua vizuri dina la mchana sasa ina maana kiswahili hatujui na kithungu pia hatujui?!.

    ReplyDelete
  32. Dinner is the name of the main meal of the day. Depending upon region and/or social class, it may be the second or third meal of the day.[1] Originally, it referred to the first meal of the day, eaten about noon, and is still occasionally used in this fashion if it refers to a large or main meal.

    http://en.wikipedia.org/wiki/Dinner

    ReplyDelete
  33. Dinner is the name of the main meal of the day. Depending upon region and/or social class, it may be the second or third meal of the day.[1] Originally, it referred to the first meal of the day, eaten about noon, and is still occasionally used in this fashion if it refers to a large or main meal.
    However, even in systems in which dinner is the meal usually eaten at the end of the day, an individual dinner may still refer to a main or more sophisticated meal at any time in the day, such as a banquet, feast, or a special meal eaten on a Sunday.

    ReplyDelete
  34. Tembea uone wewe uulioshangazwa kusikia chakula cha mchana kinaitwa dinner, kwa taarifa yako Waingereza wenyewe wanaita chakula cha mchana dinner na cha usiku wanaita tea....utajiju hapo sasa.

    ReplyDelete
  35. nyie watalii mliovamia blogu ya jamii kuna lugha spesho zinazo tumika humu ndani na sio mjifanye kukosoa kwani mnadhani misupu hajui nini maana ya dina la mchana na usiku?? wabongo woote humu ndani wanajulikana kama wamatumbi ingawa hilo ni kabila la watu fulani hukoo mkoa wa pwani na hili pia kosoeni sasa nyie kukuru kakara za nini lakini?? hizi ni lugha za humu ndani kunogesha libeneke na bado kuna konoz wewee mtajiju

    ReplyDelete
  36. ankal kiboko.Wadau wananirudisha mbali sana nakumbuka nikiwa sekondari nilikuwa kiranja wa bweni la meru.Nikitoa matangazo mbele ya wanafunzi kama mia 7 hivi 'PLEASE PLEASE FORM ONE LETS ASSEMBLE HERE AFTER SUPPER.nikimaanisha Lunch.sasa wakosoaji bado wako hiyo lerning satage.MWACHENI MSANII WETU MITHUUUUP anajua anaowakonga nyoyo.KWENDA ZENU NI VINGEREZA VYENU UCHWARA NYAMBAAAAAAAF.

    ReplyDelete
  37. ni kweli Rais ameonyesha kweli mpenda michezo kilibaki hawa TFF pamoja Serikali Tujenge viwanja vingine 5 vya kimataifa sio mradi uwanja tu wa kuingia watazamaji 45,000 wa kukaa sio kusimama katika miji ya MORO,MBEYA,MWANZA,ARUSHA,DODOMA,ilihata nchijirani watakuja kuona mashindano hayo,tuombe CAF,FIFA tuandae mashindano ya kimataifa ya kuanzia miaka 14,17,20 n... hata baada ya miaka 10 ijayo tuombe uzima tu wantanzania tunaweza wenzetu wanawezaje?

    ReplyDelete
  38. Jamani kujua lugha raha! Ninavyojua mimi katika shughuli kama hiyo kulikuwa na faragha kidogo ya kubadilishana maneno mawili matatu! Sasa I'm just wondering hivi wakati huo wa faragha wachezaji wetu walijichanganya kweli na Mapros?? Au ndio ilikuwa kila mtu kivyake!! Mimi naona sometime rahisi wetu anafanya vitu kama hivi ili wachezaji wetu waweze kupata contacts za wenzao wachezao Ulaya! Lakini sasa kama lugha haipandi utafanyaje?? Maana unajua sometime mtu kama Drogba akiku recomend katika kitimu fulani cha daraja la kwanza huko ulaya baaasi ujue ndio nitolee!! Sasa sijui hilo wachezaji wetu walitumia mwanya huo au vipi!! Haya nyie mtabakia hivyo hivyo "MIMI NI MAIMUNA"

    ReplyDelete
  39. Mnaumizana vichwa bure. Hata kule Uingereza kwenyewe ukiuliza maana ya "dinner" utapata jibu ambalo litategemea umemuuliza mtu kutoka sehemu gani ya Uingereza. Maana ya neno hilo kwa mzawa na mkulia wa jiji la London inatofautiana na ile ya mzawa na mkulia wa Halifax - ajabu hizi tofauti ndo mnapigizana kelele hapa!

    ReplyDelete
  40. kaka haka kamjadala ka dinner kanaonekana kutoa changamoto na kuonyesha kuwa watu wengi wanatembelea blog hii. Ni vyema watu wakachangia hata kwenye mambo mengine ambayo hayana mjadala kwa kuwa kuna matukio mengi mazuri na ambayo kweli watu wanahitaji kusaidiwa kwa namna moja au nyingine lakini watu hawatoi maoni. Ukiangalia mara nyingi utakuta 0 kwenye upande wa maoni. Tutoe maoni ili kuboresha blog hii kwa kuwa inatujuza mengi.

    ReplyDelete
  41. ujinga sio tusi dinner inaweza kuliwa mchana, its time to learn ,
    na kula sana sio tija sana sana utajitia ugonjwa tu watu wa east africa wote wana asili ya uandunje ata uleje, ndio maana watumwa wengi walitoka west africa sababu jamaa walikuwa fit na mara zote ukiwa andunje unajaliwa mdomo, tuendelee kuchonga....hao wachezaji wa tanzania kama wangekuwa fit physically na mentally tungeshakuwa na maproffessional zamani lakini kila anaojaribiwa medical anaonekana unfit...haya tuchonge kama kawaida yetu

    ReplyDelete
  42. Nyie mapimbi mnaomaindi kujifanya wasomi hebu tutokeeniiii humu ndani ya globu yetu...mnakeraaa sanaaa kujifanya wajanja kumbe wamatumbii wakubwa nyie na inglish zenu uchwaraa!
    Kama vipi mzee Michuzi wape picha nyingine ukisema "dinner la asubuhi au breakfast la jioni" tuone kama ndio kinachowaletaga humu.Changia main agenda ya MADA,na sio kukalia kitu kidogo ambacho kila mtu anajua ni lugha ya humu ndani!!!acheni utoto kujifanya wajuawaji!

    ReplyDelete
  43. Mimi nina dada yangu anaitwa dinner

    ReplyDelete
  44. kuna mtoa mada kachapia kwenye issue ya Rwanda eti kiranja anakazania michezo kuliko mambo ya maendeleo.Mimi nasema michezo ni mojawapo ya investments kubwa sana tu.sema angesema apanue wigo wa kukazania.TUSHUKURU MKUU ANAPOFANYA KWELI

    ReplyDelete
  45. KWA UFUPI NYOTE MMESHINDWA HAPO IMETUMIKA LUGHA YA YA MUJINI MBONA HAMUULIZI NINI MAANA YA MIKONOZZZZZZZZZZZZ!!!!!! WASHAMBA NYIE MNAVYOFIKIRIA MICHUZI MJINI JANA NINI? ASHINDWE KUJIKOSOA! NYOTE MLIOCHANGIA MADA HII MIJITU YA KUJA . MICHUZI WALIKUWA WAPI ENZI YA RSVP? KAAAZZZZZZIII KWELI KWELI.

    mdau italy

    ReplyDelete
  46. WABONGO BWANA KWELI VICHWA MAJI NA NDIO MAANA HATUENDELEI! MADA ZA MAANA ZIKITOLEWA WALA HAMCHANGII KAZI KUNG'ANGANIA VITU VISVYO VYA MSINGI. SI MCHANGIE ZILE MADA ZA MAANA NA MUONYESHO U SMART WENU! MADA YA MSINGI IKIWEKWA MAONI 8. DINNER, BASI KILA MTU ANAJUA! DAH!WATU WAFUPII HALAFU WABISHII HARAFU WANAONGEA HARAKA HARAKA!! KAZI IPO HAPA!! WOTE NI "MIMI NI MAIMUNAAAA" TUU!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...