ZAWADI YA HARUSI INANIFANYA MTUMWA!
Ndugu Michuzi Habari ya kazi msee?
Naomba maoni ya wadau kuhusu
Naomba maoni ya wadau kuhusu
tatizo kidoko iliyonipata siku sa hivi karibuni.
Mimi ni mzaliwa wa Rombo mkoani Kilimanjaro. Najishughulisha na biashara sangu hapa Moshi mjini na maisha kwa ujumla ni masuri-bomba kabisa.
Siku ya harusi yetu mwaka jana, baba mkwe wangu alitupatia gari nsuri sana Raf4 new model. Gari hii aliitoa kwa masharti kuwa nisimpakie mwanamke mwingine saidi ya mke wangu, yaani mwanae.
Hivi majuzi nikitokea Machame kibiashara niliombwa lift na dada mmoja ambaye alikuwa anampeleka baba yake mzazi hospitali ya KCMC. Nilikubali tu kwa sababu ya baba yake na nikawachukua. Yule baba alikaa kiti cha nyuma na yule dada kiti cha mbele.
Nilipofika pale KCMC nawateremsha, baba mkwe wangu naye alikuwa pale akaona kinachoendelea. Nilitoka kwenda kumsalimia na hakuitikia kwa furaha, kwani hakupenda kitendo changu cha kumpakiza yule dada. Nilijaribu kumweleza ukweli wote lakini hakuelewa somo. Baadaye nilipofika nyumbani nilimweleza mke wangu situation nzima na akaelewa. Hakuwa na neno. Lakini mpaka leo (after three months) baba mkwe wangu bado ana kinyongo na mimi.
Sasa wadau kweli nilifanya kosa kumsaidia yule mgonjwa?
LASWAI P.J
SOWETO, MOSHI
Mimi ni mzaliwa wa Rombo mkoani Kilimanjaro. Najishughulisha na biashara sangu hapa Moshi mjini na maisha kwa ujumla ni masuri-bomba kabisa.
Siku ya harusi yetu mwaka jana, baba mkwe wangu alitupatia gari nsuri sana Raf4 new model. Gari hii aliitoa kwa masharti kuwa nisimpakie mwanamke mwingine saidi ya mke wangu, yaani mwanae.
Hivi majuzi nikitokea Machame kibiashara niliombwa lift na dada mmoja ambaye alikuwa anampeleka baba yake mzazi hospitali ya KCMC. Nilikubali tu kwa sababu ya baba yake na nikawachukua. Yule baba alikaa kiti cha nyuma na yule dada kiti cha mbele.
Nilipofika pale KCMC nawateremsha, baba mkwe wangu naye alikuwa pale akaona kinachoendelea. Nilitoka kwenda kumsalimia na hakuitikia kwa furaha, kwani hakupenda kitendo changu cha kumpakiza yule dada. Nilijaribu kumweleza ukweli wote lakini hakuelewa somo. Baadaye nilipofika nyumbani nilimweleza mke wangu situation nzima na akaelewa. Hakuwa na neno. Lakini mpaka leo (after three months) baba mkwe wangu bado ana kinyongo na mimi.
Sasa wadau kweli nilifanya kosa kumsaidia yule mgonjwa?
LASWAI P.J
SOWETO, MOSHI
ndugu yangu pole sana na mkasa huo, najua ukuifurahi sana ulipopewa Rav 4 new model bila kujua ipo siku litakuja kukuharibia piece na baba mkwe wako, mimi nakushauri hilo gari usiendeshe tena wewe mwachie mke wako awe anaendesha na wewe kama maisha ni mazuri basi jitahidi ununue hata bito lako mwenyewe na lisilokuwa na masharti, ipo siku utampakia mfanya biashara mwenzako wa kike ambae unaheshomiana nae sana na kwa bahati mbaya ukakutna na baba mkwe wako akakushusha kweny gari lako, upo hapo bwa shee!!!
ReplyDeletePole sana, kaza msuri ununue lako!! kwani we hujui ile methali isemayo nguo ya kuazima haistili makalio (maana hili gari kama bado lake).
ReplyDeleteNa cha msingi kama mkeo kaelewa hiyo ndio la msingi, unaishi na mkeo na sio baba wa mkeo!
we mrudishie gari lake. amemwoa binti yake na siyo gari. jitahiji upata lako pia. aisee pole sana shee
ReplyDeletewe mrudishie hilo gari lake, alimwoa binti yake na siyo gari.
ReplyDeleteUmekosea mwombe radhi mzee, very simple.
ReplyDeleteIt's a free car you didn't pay a single cent. Sharti la wewe kupewa gari ni kutekeleza hayo masharti uliyopewa na baba mkwe. Ulikubali ukapewa gari. Sasa kama ungeona ugumu kutekeleza hayo masharti basi hukupaswa kulichukua, ungeliacha.
Wewe siyo mwaminifu. Kwanza, kwa nini unajirahisisha kwenye lift?? Hufai.
ebo hata mimi ningekupa gari lazima ningetaka masharti.
ReplyDeleteyaani akupe gari halkafu utegemee akuachie uwapandishe wanawake wengine.
ndio huyo jamaa anaumwa, je huyo mzee ana uwakika gani kama wewe unaongea ukweli au unamdanganya.
ukae ukijua kuna vitu ukimweleza mwanamke anakubali lakini mwanaume anaona ni kamba tu
Rudisha gari la watu fanya kazi kwa bidii na nunua la kwako kama lina masharti namna hiyo au mpe mkeo alitumie yeye na wewe omba lift. Inamaana baba mtu amekuhonga hilo gari ili usimwache bintiye?
ReplyDeleteCha msingi mpe mkeo aendeshe au mrudishie mkweo alitumie mwenyewe kisha kamata daladala kama kawa!
Pole, cha msingi kama mkeo ameelewa somo yeye ndio amwelekeze baba'ake kwa kuwa wewe alishindwa kukuelewa. Kama inakuwa shida kwa mkeo pia kumweleza baba yake apitie kwa mama yake. Pia huyo mzee aache mambo ya kishamba, sasa kama ungempa lift mdogo wa kike wa mkeo au mama mkwe wako angemaind?maana hao wote sio wake zako. Mdau
ReplyDeleteUkweli waujua wewe na Mungu wako. Kama msaada umeutoa kwa haki ni hazina yako Mbinguni. Cha msingi tafuta chako uwe na uhuru nacho.
ReplyDeletedingi kama anona ishu sana mrudishie mkoko wake halafu we anza kiaina ukiwini mwenyewe atakutafuta pia kwa kuwa una ishi na mwanae poa tu atabana mwnyewe ataachia we komaanae tu usijali wala nini mkeo si kakuelewaacha dingi achukie tu we si unajua madingi wa long time walivyo kwa kumaindi ishu ndogondogo?
ReplyDeleteLaswai,
ReplyDeleteUshauri wa bure.
1. Rudisha gari kwa baba mkwe ubaki na mkeo kwa amani.
2. Mwachie mkeo aliendeshe full time, wewe tafuta lako au piga teke.
Ndugu yangu pole sana, Mrudishie baba mkwe gari lake akitaka kumpa binti yake atajua mwenyewe. Wewe jitahidi ununue gari lako achana na magari yenye masharti usiyo yaweza katika maisha ya kawaida hasa ya TZ.
ReplyDeleteUKIRUDISHA GARI LAKE ATAKUAMBIA NIRUDISHIE NA MWANANGU, CHA KUFANYA HAPO NI AMA USILIENDESHE TENA, AU ENDELEA KUPAKIA MTU YOYOTE ANAYEKUOMBA MSAADA UKIRIDHIKA KUMPA MSAADA MPE AU BINTI AU BWANA, NA MWISHO KAMA UTAAMUA KURUDISHA GARI BASI MRUDISHIE NA BINTI YAKE KATAFUTA MKE ASIYE NA MASHARITI, IT IS AS SIMPLE AS THAT. MTU ASIKUPE ZAWADI NA TENA MASHARITI JUU, KWANI NI MKOPO HUO? SIO. AKALALE MBELE UKO NA KIGARI CHAKE.
ReplyDeletekaka hayo ni mateso tena mazito sana,kesho na kesho kutwa utashindwa hata kumpa mama yako mzazi lift kisa gari ina sharti gumu,kama upo safi nakushauri utafute simpo car kaka,sio maisha hayo....ThE cOmPaNy
ReplyDeleteTahadhari kabla ya Ajali .lazima uchunge sana. Baba kakupa Mke na Gari , Sasa unafanya mchezo na masihara .Penye mali siyo mchezo, Chunga sana .Au utapoteza mali na mke.Ikiwa wewe ni muungwana na mtu wa heshima basi katika lift,ukitaka kumpa mtu toa katika fedha zako mkodishie Taxi.thawabu unapata katika mali uliyoitoa katika jasho lako siyo uliyopewa kwa sharti na wataka shoo off..
ReplyDeleteAsikuzingue. Kwahiyo ukimpakiza mwanamume ambaye kwa mfano mtoto wa watu(sh**a) atajua??
ReplyDeleteMpe gari yake au mpe mkeo, ataharibia amani huyo mzee. Maisha sio kufungwa namna hiyo. Uaminifu uko moyoni kwa mtu.....!
Laswai ni matajiri umtoka wapi wewe masikini wa kupewa gari ya bure unanyanyasika kha nenda kwa wakubwa zako utapata mchango uwe na lako
ReplyDeletePole sana ndugu kwa haya yanayokukuta. Ila hapo kuna tatizo la kipuuzi kabisa. Huyo mzee asiwasumbue na hilo gar alilowapa. Nawashauri kwavile mnaelewana na mkeo basi wewe acha kabisa hilo gari aendeshe mkeo tu na wewe uwe mpkiaji. Huyo baba asiwapangie jinsi ya kusihi na familia yenu! Huo nauita ni upuuzi na kuvurugiana ndoa. Huyo mzee ajiheshimu na aiheshimu ndoa yenu pia. Asipoelewa hilo basi mhame kabisa mkae mbali naye. Kila la kheri kaika ndoa yenu.
ReplyDeletePole Bro!!
ReplyDeleteHiyo si ni zawadi? Zawadi haina masharti ndugu yangu na ukipewa hurudishi wala hudaiwi kwa kuwa ni zawadi.
Hilo gari ni lako kwa kuwa ulipewa na baba mkwe na unao uhuru wa kulifanya utakacho bila kubugudhiwa na aliyekupa wala ndugu yake yeyote.
Hilo sharti alilolitoa ni la kipuuzi na linaonesha ni jinsi gani alivyo mduwanzi, ina maana yeye huwa hapakii jirani zake kwenye gari zake? Kama huwa hapakii ujue kuwa ni mbaguzi na mnyanyapaa, ikiwa anapakia kwa nini akuambie wewe usipakie watu na gari ni lako.
Hana sababu yeyote ya kukuchagulia marafiki wala watu wa kuwapakia kwenye hilo gari. Ningelikuwa ni mimi ningepakia mabinti mtaa mzima mbele yake, ndo akili imkae sawa. Kwani anadhani kuwa ukiwapakia ndo unaenda kuwachimba? Inaelekea hizo ndo zake, hampakii mwanamke mpaka awe na mipango naye.
Wewe endelea na maisha na mkeo, hilo gari ni lako, vinginevyo kama lipo kwa jina lake ki sheria litakuwa bado ni lake. Ila kama mlihamisha umiliki na kuweka jina lako kwenye kadi ya gari basi ni lako na asikusumbue wala kukupa masharti ya kipumbavu.
Wajibu wako wewe ni kwa mkeo tu, si kwake wala takataka nyingine yeyote. Kama mkeo hana noma na unachokifanya na mnaelewana, hao wengine wafumbie macho na masikio, yaani fanya kama ni mawe barabarani.
Next time akitaka kukupa zawadi yeyote mkatalie mwambie akae nayo hutaki kuwa mtumwa wake. Ila kwa sasa gari ni lako na tumia utakavyo. Achana na ushauri wa wapumbavu wachache wa humu wanaodai ulirudishe ununue lingine. Huna sababu ya kujitia gharama ya kununua gari wakati tayari unalo.
Bro hujui kwamba gari hilo ulipewa kwa muda tu, na ni la mke wako tu.Kitu cha maana nunua gari lako tena kali kuliko hili ili urudishe heshima yako mbele ya jamii.
ReplyDeleteCha kupewa utumwa
Kama alikupatia zawadi tena mbele ya mashahidi hilo gari ni la kwako na yeye hana haki ya kukuambia nani umpakie wala nani usimbebe humo. Pili usirudishe hata siku moja kitu ulichopewa bure halafu ukaenda kununua kitu kama hicho kwa pesa (Nimeona ushauri wa wajinga humu ndani). Wewe ni mfanya biashara na unajua uchumi.
ReplyDeleteCha kufanya ni kuhakikisha kuwa hilo gari lipo kwa jina lako, yaani uhamishe umiliki kwenda kwenye jina lako, lisiwe kwenye jina la baba mkwe, halafu mfuate mwambie kuwa wewe ni mtu mzima unajua unachokifanya, hivyo asikupangie nani wa kumbeba wala kuongea naye. Yeye nani anampangia?
Hukuwa na sababu yeyote ya kwenda kujielezea kwake alipokuona umepakia mwanamke, wewe si mtoto mdogo wala si mtoto wake wewe ni mkwewe. Una wajibu kwa mkeo tu na si kwa kinyangarika mwingine yeyote kuhusu ndoa yako.
Usirudishe gari hilo na wala usipoteze pesa kununua jingine ili kushindana naye, wewe ndo utakula hasara, wacha roho imuume, pakia watu unaojisikia kupakia na waache usowataka na tena usikae kujielezea kwake kwa nini unampakia furani na kwa nini humpakii furani.
inaonekana kuwa yeye ana tabia ya kupakia vimada kwenye magari yake sasa anadhani kuwa na wewe utafanya hivyo. Watu kama hawa ni wagonjwa wa akili, wanahitaji tiba.
Hilo gari ni lake sio lenu, rudaisha haraka angekuwa kawapa kweli asingewapa masharti hayo, tafuta hela zako ununue lako huo ndo uanaume!!! Pole meku...
ReplyDeleteYaani mimi hata siku moja sitakaa nijielezee kwa baba mkwe wala ndugu gani wa mke wangu kwa ishu yeyote inayohusu mimi na mke wangu, never. Huna sababu yeyote ya kujielezea kwa baba mkwe eti kwa kuwa amekuona umepakia mwanamke kwenye gari alilokupa (That is bullshit). Yaani huyo baba mkwe ni mjinga kiasi gani akununie wewe kwa kupakia wanawake kwenye gari? Mzee, naona umeoa kwa watu wenye matatizo ya akili, watafutie daktari.
ReplyDeleteBwana ee, kwenye ndoa, unayepaswa kujitetea kwake ni mkeo tu na hiyo ni kama umekosa kweli si kwa kukudhani. Huwezi kuanza tu kuomba samahani kwa kosa ambalo hujatenda hata kama huyo mtu andhani kuwa umetenda, huo ni utumwa na ujinga wa akili.
Hilo gari umepewa, ni lako na hakuna kiumbe wa kukuambia nani umpakie na nani umuache. Wewe ndo uamue nani wa kumbeba na nani wa kumuacha. Kwa maana nyingine unaweza amua hata kutokumpakia huyo baba mkwe akiwa na shida nalo
Pole dogo, Kumbuka wema hauozi, ulishatenda wema utakumbukwa daima na Mungu atakupa vingi vizuri.
ReplyDeleteUshauri wangu ni kwamba, usiendeshe hilo gari kama mke wako hayumo ndani.Pia mfundishe mkeo aendeshe hilo gari muda wote.
Usithubutu kulitoa hapo home kwenu isipokuwa una mke wako ndani yake.
Ndiyo hayo wengine tulikwepa kuoa watoto wa wenye mipesa tukaoa waliotoa ujinga na kuanza kuchakalika nao kufurukuta kujenga maiha yetu wenyewe na sasa tunaona baraka tupu kutumia vitu tulivyovitolea jasho wenye.Hayo masharti ya nini kisa eti gari, I cant accept that.Gari linasaidia hata wengine binadamu si kisiwa, hata ukifa huo mgari utabaki hapo tu ukioza.Pole kijana wangu baba mkwe huyo anakufuatilia hata kwako kisa anakuona huwezi kununu gari wewe.Njoo huku ughaibuni magari yapo kama mchanga wa baharini utaokota hata mkweche wa $200
sasa mbona mzazi husemi msasi????
ReplyDeleteAcha kutuzuga hapa.
Afu, ogopa kupewa zawadi na baba ama mama mkwe na ukajifanya wanakupeenda sana. Kwa taarifa yako, huyo baba ka anakauwezo fulani hivi atakupelekesha puta ile mbaya. hapo utapangiwa na muda wa kuzaa na mwanae usimzeeshe. tatizo hukupenda NKE ulipenda mali za babake. Ngoja ukome. Mama mkwe hajaanza hapo. Atamweka kitako mwanae na kumuuliza wakati wa kusaa mnasaa mara ngapi usije ukamseesha mwanae. Utakoma kuringa, umekuja Machme kichwa kichwa.
SIMPLE ULIKOSEA KUMWEKA MWANAMKE MBELE.UNGEMWEKA MWANAUME BABAKE MWANAMKE MBELE ALAFU MWANAMKE NYUMA.WE UNGEKUBARI KUONA MKEO KAMPA RIDE MWANAUME TENA KAMKARISHA MBELE?????????NA NYUMA MWANAMKE MWENZIE SI BORA MWANAMKE MWENZIE MBELE?
ReplyDeletesanyingine mwanamke wako bwana kama kawaida ya wanaume wa bonga hawakosi mwanamke wa nje
sasa wewe hujui hilo gari ni la mkeo, kwanza ametoa baba yake na pili ni rav4. cha kufanya mpe mkeo hilo gari na wewe nunua gari bomba zaidi kama prado, honda crv etc.
ReplyDeleteRUDISHA PLS!
ReplyDeleteBaba mkwe anakujua tabia zako ndo sababu akakupa masharti kama ningekuwa mie ndo ba mkweo umevunja mashrti kwanza nakulamba vibao alafu nachukuwa gari yangu na namtafutia mume mwengine binti yangu fullstop kwanini huridhiki weye mwana
ReplyDeleteRudisha gari 'faster...' Na huyo baba mkwe wako hana akili... kwanini awape zawadi ya gari? hakuna zawadi nyingine ya maana kama shamba, nyumba, mtaji n.k Rudisha hiyo gari, usimpe hata mkeo... HAIWAFAI... SIO YENU!
ReplyDeleteKosa lako ni kutonunua Rav4 ya kwako. Kosa ulilofanya ni sawa na kama ukimkuta mkeo anananihiwa na mtu mwingine kwenye kitanda ulichokinunua wewe.
ReplyDeletecha bure kina garama, rudisha uchume chako uki2mia kwa amani.
ReplyDeletendugu pole ila nakukumbusha tu kuwa cha mtu mavi,nunua lako bwashee...upo...zinduka!!!
ReplyDeletemboha mmeku achana nalo litakupa shida
ReplyDeletemboha lasway ola lovo chnnave neksumbwa,
ReplyDeleteinaonekana huyo babamkwe ndio zake kwa wanawake anamhisije mkwewe kama na yeye si kiwembe?
ReplyDeleteMbura!!! Yeeesu na Maria..Kiki Laswai? Sisi ma bwashee hatujasoea fitu vya bure, nunua vyako msee wangu.
ReplyDeleteNunua gari yako utumie hiyo muachie mkeo atumie kwa matumizi ya familia na nyumbani. UNAPENDA VYA DEZO!!! Baba mkwe yuko right gari anunue yeye kwa ajili ya mwanae halafu wewe upandishe vichupi vingine? KWA KIFUPI HIYO ZAWADI NI YA BINTI YAKE, AKUNUNULIE GARI WEWE KWA MPANGO GANI?? UMEOA AU UMEOLEWA??? GET REAL
ReplyDeletepole sana ndugu yangu lakini mi nikushauri hivi usiumie sana moyo, cha msingi kama mke wako amekwelewa basi paki gari nyumbani au mkabidhi mkeo harafu wewe tafuta usafiri mwingine au tembea kwa miguu, maana ni kulala na njaa kwenye nyumba yako kuliko nyumba ya kupanga baba si unafahamu?
ReplyDeleteWakati mwingine tunafanya kazi ya kusumbua vichwa vyetu kwa kujibu ama kushauri vitu vya kufikilika zaidi ya ukweli wenyewe.kila nikiifuatilia hii hadith na mlolongo mzima na shawishika kutoamini kilichoandikwa.
ReplyDeleteyote kwa yote pole sana kwa yaliyokutokea kama ni kweli!!!!
RUDISHA HIYO GARI USIWE MTUMWA WA KISIASA. GARI HAITAKUSAIDIA KATIKA MATATIZO YA KIMAISHA KIJUMLA YAANI YA KIJAMII; VINGINEVYO LINAKUWEKEA MIPAKA NA JAMII NA KUKUTENGENEZEA TABIA MBAYA KWA JAMII KIYU AMBACHO NADHANI HUKUWA NACHO.
ReplyDeleteSIKILIZA, KOMAA KABISA WAKATI WA KUIRUDISHA GARI. WEWE NI BINADAMU, UNAHITAJI KUCHANGANYIKANA NA WANAJAMII. GARI ISIKUTENGE NA JAMII. ZINGATIA HAYO.
Pole Mzee
ReplyDeleteNaungana na wadau hapo juu, kama mizunguko yako inahitaji sana gari kwa wakati huu vumilia mzee ila ndio akili kichwani ukifikiria lako, maana hilo litakufanya mtumwa.
Kwa huyo Baba akumbuke Biblia inasema Mwanaume atawaacha wazazi wake na kuambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja. Sasa mzee ukishatoa zawadi usiweke masharti hao ni mwili mmoja na wanajua wanavyoendesha maisha yako. Iko siku mkweo atatoa lift kwa jirani yake ambaye ni best wa familia ya mkweo nawe kuanza kuhisi vibaya utaaibika... Hao ni watu wazima na wana maisha yao...
Ni hayo tu
Wabongo kwa wivu. Hivi sasa msha muonea jamaa wivu, mnamshauri arudishe gari alilopewa bure halafu akanunue jingine. Ninyi ni watu wa aina gani?
ReplyDeleteBwana mdogo, nakushauri usijaribu kurudisha gari kwa baba mkwe na hakuna gari ya mke wala ya mume. Pili, kukimbilia kununua gari nyingine eti kwa sababu ya wivu wa baba mkwe ni upuuzi mtupu. Unajitia hasara bila sababu ya maana.
Kwa kuwa gari umepewa, shukuru Mungu kwanza kwa kuondolewa usumbufu wa usafiri na kwa kuwa baba mkwe ameshaonesha kuwa yeye si mtu wa kuheshimu uhuru wa mtu, achana naye, gari tumia kwa sana na usilirudishe, wala usinunue jingine, la nini nawe gari unalo tayari?
Mpe raha mkeo, baba mkwe atachemsha mwenyewe, tena usisumbuke hata kwenda kumtembelea wala kujipendekeza kwake tena, aje kwako.
Siku nyingine, hakuna kujielezea wala kujitetea kwa baba mkwe, yeye anapaswa kukuheshimu kwa kumuondolea usumbufu wa wajukuu wasio na baba nyumbani na kwa kumpa heshima ya kuitwa babu na baba mkwe, aache ujinga wake huo.
USHAURI ,wangu ni kwamba UZA hilo gari halafu nunua lingine.
ReplyDeleteMBONA HIYO HESABU RAHISI SANA HAINA HAJA YA MJADALA MREFU SANA UMEPEWA GAR KAMA ZAWAD BURE UKAPEWA SHART LA KUTOPAKIA MWANA DADA HUKUPEWA SHART LINGINE,SASA FANYA HIVI UZA HILO GARI HIYO HELA FANYIA MAMBO MENGINE YA MAENDELEO MANAKE HAJAKUPA SHART LA KUTOLIUZA UNAWEZA KULIUZA UKANUNUA GAR NYINGINE HALAFU UANZE KUPAKIA MADEM KAMA KAWA KWENYE HILO GAR LINGINE.
ReplyDeleteHili ulishike na ulielewe maishani kwako! Ukioa, na ukawa na usafiri kama gari, hakuna mwanamke yeyote hapa Duniani atakayekaa kwenye kiti cha mbele cha gari lako isipokuwa mkeo. Hata mama yako na dada zako hawastahili kukaa kiti cha mbele cha gari lako. Labda katika mazingira ya kuokoa maisha ya binadamu.
ReplyDeleteChukua funguo uendelee kuendesha gari,
Pole sana,
ReplyDeleteKurudisha gari si vizuru kwa baba mkwe, ni jinsi ya tabia nzuri kwani wewe usimwonyeshe mkweo tabia mbaya, ila sasa.
1. Peleleza kwa mkeo kama kweli baba mkwe anachochukia ni hicho kitendo cha siku hiyo au kuna lingine(nadhani mko vizuri na mkeo). Mtake radhi kwa lolote ili muwe vizuri.
2. Mwachie mkeo hilo gari aendeshe kama hajui mfundishe tu, kwani hilo sharti lake ni gumu mno hutaliweza na kwasababu alisema mbele ya watu wengi hujue walilipokea ila wewe kwa raha ya harusi ukaona sawa tu. Kesho hatakuona baba mkwe, ila mkeo atakuona na akihisi jambo tu atakukumbusha.
3 Kama huna gari husijali kabla ya kuoa ulikuwa unafanyaje shughuli zako, endelea hivyo hivyo.
MI WALA SIKUPI POLE WEWE ULIKUWA NA AJENDA YA SIRI HAO ULIOWAPA LIFTI MTU NA BABA YAKE SI WANGEKAA NYUMA ILIKUWAJE MGONJWA AKAE PEKE YAKE NYUMA NA MBELE UMWEKE MREMBO WEWE HUNA NIDHAMU NA HUKUFUATA KILE ULICHOAMBIWA AU NDO MASIKINI JEURI?HALAFU WATU MNAOSAIDIWAGA HUWA MNA MATATIZO HAPO UNATAKA USEME UNASIMANGWA
ReplyDeletehuyo ba' mkwe ana gubu usilirudishe hilo gari ng'oo je angekuwa yeye ndo mgonjwa aache hizo kwani anaweza kumuoa bintiye na masharti yake ya kipumbavu kakupa zawadi na zawadi haina masharti ulitoa msaada na endelea kutoa ebo hii midingi ya longi ina mambo acha tu dingi yangu naye mithili hili hii hii mdogo wangu kaolewa na ana mdomo mrefu kweli basi mumewe akimjia juu tu ati dingi na maza wanaingilia basi oneday moja nikawanyamba kisawasawa wamekoma huu ni upuuzi wa hali ya juu umemuoa mwanaye na si yeye na wewe mchunie na gari tumia kwa kwenda mbele
ReplyDeletemdau manka