MAITI 14 kati ya 25 wa ajali ya mabasi ya Chatco na Mzuri Trans katika kijiji cha Kwangahu, Handeni mkoani hapa wametambuliwa na ndugu zao, baadhi kwa kutumia vitambulisho vya kupigia kura.

Pamoja na vifo hivyo, ajali hiyo ilisababisha watu 52 kujeruhiwa wakiwamo wanawake 17, wanaume 35 ambao wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Korogwe ya Magunga na wengine saba katika hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo.

Katika majeruhi hao saba waliofikishwa Bombo yumo mtoto wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu, aliyeumia kichwani na hajatambuliwa na ndugu zake; Jackson Abel (20) wa KCMC (Moshi); Ramadhani Msuya (65) na Rajabu Musa (55) ambao wamelazwa wodi A2 baada ya kupasuka kichwani, kuvunjika shingo na miguu, huku watatu ambao hawajatambuliwa wakiwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.
kwa habari kamili



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. INASIKITISHA KUONA KILA KUKICHA AJALI ZA MABASI HUKO BONGO JAMANI HIVI KWELI HAWA DRIVERS WANAHAKIKIWA KWAMBA WANA UJUZI WA KUTOSHA KUENDESHA MABASI YA ABIRIA? AU NDO YALEYALE KWAMBA KAMA UNA PESA BONGO UTAPATA CHOCHOTE?LAKINI CHA KUSIKITISHA NI KWAMBA HIZI ROHO ZA WATU ZINAPOTEA NA NI WATU AMBAO WANATEGEMEWA NA FAMILIA ZAO NI BABA,MAMA,DADA,KAKA,BABU,BIBI AU NI WATOTO WA FAMILIA HUSIKA,NDIO MAANA AJALI HIZI ZINATIA ZIMANZI NYINGI MNO,HALAFU KUNA MAJERUHI AMBAO WANAACHWA KUWA VILEMA WAMAISHA NA MZIGO HUO UNAWAENDEA FAMILIA HUSIKA,INASIKITISHA.NADHANI UMEFIKA WAKATI TUWE SERIOUS NA ZOEZI LA KUCHUJA DRIVERS WOTE WANAOENDESHA MAGARI YA ABIRIA(PUBLIC TRANSPORTATION).MADEREVA HAWA WAWEZE KUPIMWA MARA KWA MARA ENDAPO WANATUMIA VILEVI AU MADAWA YA KULEVYA ILI WANAOKIUKA AU KUKUTWA NA USHAIDI HUO BASI WAFUNGIWE KUENDESHA ABIRIA PERMANENTLY.HATUA ZA HARAKA ZINAHITAJIKA KUOKOA MAISHA YA WATU COZ THIS IS TOO MUCH

    ReplyDelete
  2. Hivi mambo mengine tutaendelea kulalamika hadi lini?? Tunajua kuna malori (yamegeuzwa kuwa mabasi) barabarani yanabeba abiria. Hata kama ajali haikwepeki, impact inakuwa kubwa kama ni lori limehusika kwenye ajali.

    Unaposoma habari hii kuna mamia ya watanzania wanakimbizwa ndani ya malori sasa hivi!!

    Sasa je tutaendelea kuomboleza hadi lini?? Ikitokea ajali zinatoka amri nyingi tu, amabazo hazina meno!!

    ...haya mambo yanatokea Bongo tu!!

    Ehe Mola walinde wasafiri wote!!

    ReplyDelete
  3. Kwanza ninatoa pole kwa familia na majeruhi waliopatwa na msiba huu mzito. Binafsi nimeguswa moyoni kwani tumewapoteza watu muhimu sana katika ujenzi wa taifa letu.
    Ushauri wangu ni kwamba nchi yetu itaendelea kuwa na ajali nyingi siku za usoni kutokana na ufinyu wa miundo mbinu. Barabara zetu ni finyu sana na kunapaswa kuwe na barara zilizotengwa yaani (One Way) na katika kila barabara kuwe na angalau lane mbili za kwenda na mbili za kurudi na zinatakiwa kutenganishwa kabisa katikati ili pasiwepo na madereva wanao- overtake. Overtake ndo sababu kubwa ya kusababisha ajali na watanzania wengi wataendelea kupoteza maisha kama miundombinu hii haitafanyiwa kazi. Kwa barabara zote zinazoenda mikoani zinatakiwa ziwe one way or High ways kama nchi zilizoendelea.
    Nafikiri hili ndo swala linalotakiwa kufanyiwa kazi katika miaka 20 ijayo nchi yetu iwe na miundo mbinu ya uhakika.
    Asante kwa kupokea maoni yangu.
    Mdau wa Damu USA

    ReplyDelete
  4. the government has to come with a strong measures and enforce those measures, it is unacceptable two buses to collide head on. They can issues new DL for all buses driver and requirements that they should be taking some kind of training yearly for their DL to be active otherwise will be suspended. also this new DL should have some kind of number and points and fines will be given for any offenses committed if drivers reach certain points on certain period of time their license will be suspended.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...