JK akijiunda na waumini wengine kumuombea marehemu Rajabu Kianda kabla ya mazishi yaliyofanyika kijiji cha Kangokoro kata ya Kihuria wilayani Same, mkoani Kilimanjaro
Shehe akiongoza sala ya maziko
JK akiweka udongo kwenye kaburi la marehemu
mazishi
waombolezaji kinamama msibani
Wakuu wa wilaya za Kilimanjaro wakiwa msibani
baadhi ya waombolezaji

Habari na picha na
Dixon Busagaga,
Same
RAIS Jakaya Kikwete jana ameongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa mnikulu marehemu Rajabu Kianda aliyefariki dunia Februari 7 mwaka huu kwa ugonjwa wa shinikizo la damu.

Akizungumza baada ya mazishi yaliyofanyika kijiji cha Kangokoro kata ya Kihuria wilayani Same,Rais Kikwete aliitaka familia ya marehemu kuwa wavumilivu na moyo wa subira hasa katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.

Naye katibu mkuu wa Ikulu Bw Michael Mwanda akisoma wasifu wa wa marehemu Kianda alimtaja marehemu kuwa alikuwa ni mchapa kazi hodari na kwamba ni mfano wa kuigwa..

Kwa upande wake baba mdogo wa marehemu ,Bw Said Nyika akitoa neno la familia ameishukuru serikali kwa msaada iliyotoa wakati wa matibabu ya ndugu yao hadi mauti yalipomfika.

Mazishi hayo pia yalihudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo wakuu wa wilaya,wabunge, viongozi wa vyama vya siasa, taasisi mbali mbali za serikali na zisizo za serikali.

Marehemu Kianda aliyefariki dunia Februari 7 katika hospitali ya Muhimbili ,amezikwa katika makaburi ya familia yaliyopo eneo la Mashine kata ya Kihurio na ameacha mjane na watoto sita.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Natoa Salaam zangu kwa wafiwa na wafanyakazi wote wa Ikulu wakiongozwa na Mheshimiwa wetu Rais.

    Ila kwa kweli maelezo niliyoyapata hapa kuhusu maana ya mnikulu na chimbuko la neno Ikulu yamekuna hisia yangu ya siku nyingi.

    Nayo ni ni kuwa na Majina ya kwetu kwa ajili ya vyombo vyetu na vyeo vyetu badala ya kutumia ya Waingereza Waliotutawala kama vile bado wanatutawala.

    Kwa mfano Ireland ambako wana mfumo wa bunge kama UK lakini hawatumii waziri Mkuu bali "Taoiseach" na bunge lao linaitwa
    Dáil.

    Sasa tayari tuna IKULU naona linatufaa kabisa ila sijui neno BUNGE lillitokea wapi labda nisaidiwe hapa.

    Sasa kwa nini Raisi asiitwe "MKULU" (Generali Ulimwengu aliwahi kutoa wazo hilo)
    Tukichambua makabila yetu mbalimbali tutapata majina ya vyeo vingine pia ili tuondokane na huu utumwa..Mfano Sisi wachaga Kule kwa mangi karani wa mangi aliitwa "MCHILI" ..hivyo katibu mkuu Ikulu anaweza akaitwa Mchili...nk
    Maana Marais wako wengi hata wanafunzi wana raisi lakini MKULU atakuwa mmoja tu na jina litalindwa kisheria.

    Kwa kweli hili limenikuna sana hivyo Waheshimiwa wadau wa Tanzania na bulogu hii naomba nitoe hoja:
    Mdau

    ReplyDelete
  2. poleni wafiwa.
    hapa naomba bwana kaka michuzi unisaidie jambo kidogo,maranyingi katika matangazo ya matukio ya msiba nimeona ukiwatakia wafiwa kuwa na MOYO WA SUBIRA.lakini mimi ninavyofahamu subira ni pale unapokuwa unatarajia jambo fulani litimilike.
    hivyo basi nadhani lugha sahihi ni kuwatakia wafiwa MOYO MKUU au WAJIPE NGUVU na KUYAKUBALI YALIYOTOKEA KAMA YALIVYO maana hiyo ndiyo njia apitayo kila binadamu.
    nadhani ankal sijakukwaza na sijawakwaza wadau wengine pia.
    mwisho nawatakia wafiwa MOYO MKUU NA WAJIPE NGUVU KATIKA KIPINDI HIKI CHA MSIBA.
    mdau.

    ReplyDelete
  3. Naomba kujua maana ya neno "mnikulu". Hicho ni cheo gani? Asante sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...