Na Ripota wetu, Zenji
Baada ya wananchi wa zanzibar kukaa kizani kwa kipindi cha miezi mitatu(10/12/2009 - 09/03/2010),huduma ya umeme imerejea katika hali yake ya kawaida kwa takriban maeneo mengi ya kisiwa isipokuwa baadhi ya sehemu za Migombani.

Kukosena kwa huduma hii kulisababisha budget kukaza mno kutokana na kupanda kwa kasi ya ajabu bei ya bidhaa mbalimbali na mahitaji mengine ya kila siku. Licha ya ukosefu wa huduma hii,lakini baadhi ya kinamama wamesema ilileta faraja kwa kiasi fulani.
Wengi waliozoea kuwa nje ya nyumba zao kwa kisingizio cha kucheza karata au kuangalia big match kama ya WIGAN V/S LIVERPOOL na nyenginezo walikuwa wakirudi mapema mno na wengine kulala mapema kama wanafunzi wa chekechea.

Kwa ujumla hali ni shwari ila wanachi wengi bado wamekuwa katika wasiwasi mkubwa kuwa huenda hali ikarejea tena muda wowote kwani waya unaotumika sasa ni uleule ambao umeelezwa kuwa muda wake wa matumizi umekwisha kitambo.
Hata hivyo uchunguzi wa Ripota huyu umebaini kwamba hakuna haja ya wasiwasi kwani mambo sasa ni shwari hadi itapotangazwa vinginevyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Yani kaka yangu furaha usipime.
    Juzi watoto waliimba nadhani jana waliamka sauti zimekauka.

    Lakini cha kushangaza umeme umerudi na gharama zimepanda.

    Ghafla juzi Petrol ilijisapia.

    Vyakula jana jana vilipanda bei mara dufu. Matunda ya Juice hayakamatiki sasa, samaki, nyama usiseme.

    Inaumiza sana, ukizingatia mtu wa chini alikuwa hapati chochote ndani ya kipindi hiki cha miezi mitatu.

    Serikali inabidi iangalie hili suala kwa undani zaidi.


    disminder.

    ReplyDelete
  2. MADA YANGU HAIHUSIANI NA UMEME ZNZ. INAHUSU KERO YA HUDUMA ZA TIGO!!

    KERO YA HUDUMA ZA TIGO!!!! INAKERA!!
    Yaani inakera sana pale ambapo mtu una sh 2000 kwenye simu ya tigo, unaomba kuunganishwa na mini extreme ya simu ambapo ulitakiwa ukatwe sh 250 tu na kupatiwa dakika 25 za maongezi, watu/ sijui computer za tigo wanaamua kukukata sh 1500 na kukupa dakika 100 za maongezi...imeshanitokea mara mbili. Ukiwapigia kwanza wanakukata sh 100, then unaambiwa hebu sema hilo neno mini umeliandikaje? herufi kubwa au ndogo? ooh nadhani umekosea, utakuwa umeacha ile i ya mwisho...Yaani wanakupa majibu rahisiiiiiiiiiiiii wakati mtu una uhakika hujakosea. IWEJE NIWE NINAKOSEA TU NINAPOKUWA NA PESA KWENYE SIMU INAYOFIKA 15OO NA KUENDELEA?? MBONA SIKU NIKIWA NA SH 500 AU 300 HUWA SIKOSEI??? IMEFIKIA HATUA KAMA NINA PESA ZAIDI YA SH 250 kwenye simu yangu inabidi niihamishe kwenye simu nyingine kwanza ili nibakiwe na hiyo sh 250 niweze kuomba na kupewa MINI EXTREME ya dakika 25.

    Cha kuchekesha au kushtusha ni kwamba leo imenipata kadhia hii ya kukombwa sh 1500 yote iliyokuwemo kwenye simu. ikabidi nichukue simu ya mtu mwingine niitumie kupiga TIGO. Nilichojibiwa "nimeangalia hapa umekosea kuandika neno MINI, umeacha herufi I mwishoni..." nikamwambia, dada mbona hata namba yangu sijakupa hii ninayotumia ni ya mtu mwingine wewe umejuaje? OOH KAMA NI HIVYO BASI NJOO OFISINI...Jamani nitoke Tegeta hadi ofisi za tigo kwa ujinga/uzembe? wao kwa gharama za nani?

    Najua wataisoma wengi wakiwamo waliowahi kukumbwa na kadhia hii au hata wale watu wa customer care ambao mnatoa majibu ya haraka haraka tu tena rahisiiiiiiii UTAKUWA UMEKOSEA!!! BILA HATA YA KUWA NA UHAKIKA YA MNACHOKIONGEA.

    TIGO MNATUBOA WATEJA WENU...!!

    MICHUZI NITASHUKURU KAMA UTAUPA UJUMBE HUU UZITO UNAOSTAHILI (USIIBANIE HII MISOUP) ILI UJUMBE UWAFIKIE WAHUSIKA MANAKE SINA NAULI YA KUFIKA OFISINI KWAO!

    ReplyDelete
  3. Poleni sana ndugu zetu wa visiwani na hongereni kwa uvumilivu wenu mkubwa mliouonyesha katika kipindi chote kigumu cha kukosa nishati muhimu.
    Na kukosa hiyo nishati iwe ni funzo kwa serikali zote mbili ili tatizo hilo lisijitokeze tena, kuwa makini na kukagua mitambo mara kwa mara.

    ReplyDelete
  4. Naungana na anony. 10:40am japo hapa si pahali pake. Labda itamfanya Ankal alifungulie topic pia hili.
    Mi pia ilinitokea kote Tigo na Vodacom. Mi dakika 100 za kazi gani? sina kazi ya kufanya ? kutwa napiga talalila?

    Voda nilikombwa 5,000 yooote iliyokuwepo nilipoandika zile nyota 147 reli za Jirushe. nikapewa dakika 300 kwa siku tano! Za kazi gani?
    so ni kama utapeli. Mi nakwambia hakuna jema Bongo hii. Promotion ni kama njia ya kuwaibia watu. Na usipojisajili kwenye hizo promo, ukipiga simu ndo wanakukong'oli kwa bei ya Premium hadi basi!
    Wizi mtupu!

    na ole wako upige simu Voda to Tigo au Tigo to Voda ( cant speak of Zain maana sina hiyo namba! utajuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuutttaaah!)

    Bora tu mtu kama ana BlackBerry mchati naye freely kwa internet chat ya BlackBerry to Bb. maana hakuna jema.

    ndo maana mobile companies na staff wake wananeemeka tuuuuu ukiwakuta malipustiki hayyyooo!!! mijitai hiyyyoooo! maringo teeeleee! Migari hiiiyyyyyyyoooooo! na inavyoendeshwa rafu sasa! hata ikibomondwa/ndeka si wana replace tu kesho yake.
    We cheki mi Nissan na mi Toyota hilux ya mashirika ya simu!
    aku miye
    Mnfffyyuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  5. sam-kilimani znzMarch 10, 2010

    aah Ankol si kila kitu kibaya huwa na ubaya tuu,na uzuri japo kidogo huwa upo,maana siye huku gari zetu zote zinastara ( tinted) basi aah jioni kabla ya usiku mwingi aah kule sehemu sehemu kama kwaraju, messi ya polisi,club ya nyuki mambo yalikuwa yanakuwa safi sana,usiniulize ilikuwa nini jua tuu mambo yalikuwa safi sana,aah kukaa bila bili ya umeme kwa miezi mitatu safi sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...