Udzungwa Mountains National park sio hifadhi maarufu kwa wengi kama zilivyo Serengeti, Manyara, Tarangire, Ngorongoro na nyinginezo. Kikubwa kinachofanya wengi tusiifahamu yawezekana kuwa ni kutokana na kutokuwepo kwa wanyama wengi ambao ndio huwa kivutio kikubwa kwa wazalendo wengi. Ukweli unabaki kuwa Udzungwa Mountain National park ni hifadhi ya kipekee ambayo ni mahususi kwa wale wanopenda kwenda kuona miti, Viumbe hai wadogo na wa kati ambao hustawi ktk misitu ya ki-tropiki. Hii hifadhi ipo mkoani Morogoro. Kufika huku unapita bwawa la Kidatu.
Mambo haya na mengine mengi kuhusu utalii na hifadhi zetu nenda:
http://tembeatz.blogspot.com/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. MnyalukoloApril 01, 2010

    Naomba kusahihisha: Udzungwa Mountains National Park ipo mkoa wa Iringa na si Morogoro lakini access yake nzuri na inayojulikana sana ipo Morogoro kama mdau alivyoelekeza hapo.

    ReplyDelete
  2. Milima ya Udzungwa ina viumbehai aina nyingi ambavyo havipatikani katika maeneo mengine duniani.

    Mfano kuna aina ya ndege (Partridge), aina ya kima (Kipunji) na vyura wanaozaa wa Kihansi.

    Watanzania tuuthamini na kutambua urithi wetu. Tusisubiri mpaka wazungu waje kutembelea watwambie vitu hivyo. Tujitahidi tutembelee maeneo hayo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...