Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Prof. Juma Kapuya (shoto) akitangaza viwango vipya vya mishahara kwa kima cha chini kwa wafanyakazi wa sekta binafsi leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Viwango hivyo vya kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi vinazigusa sekta za Afya,Huduma za Kilimo, Viwanda na Biashara, Mawasiliano, Sekta ya Madini, Bandari na sekta ya Uvuvi, Wafanyakazi wa majumbani,sekta ya ulinzi Binafsi na Hoteli. Habari na Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.


Ufafanuzi wa viwango hivyo.
1. Huduma za Afya - Tshs 80,000/=
2.Sekta ya Kilimo - Tshs 70,000/=
3.Viwanda na Biashara - Tsh. 80,000/=
4. Usafirishaji na Mawasiliano
-Huduma za anga 350,000/=
- Clearing and Fowarding 230,000/=
- Mawasiliano ya Simu 300,000/=
- Usafiri wa nchi kavu 150,000/=

5.Madini - Migodini 350,000/=
- Wachimbaji wadogo -150,000/=
- Wauzaji wadogo na watoa leseni 250,000/=
- Brokers Licenses 150,000/=

6. Maji (Bahari na Uvuvi) - Tsh. 165,000/=

7.Majumbani:
- Majumbani (mabalozi na wafanyabiashara wakubwa)- isiwe chini ya Tsh 90,000/=
- Maafisa wenye sitahili ya kulipiwa huduma hii -isiwe chini ya Tsh.80,000/=
- Wengineo - Tshs 65,000/=

Mahotelini:
- Hoteli kubwa za kitalii - 150,000/=
- Hoteli za kati - 100,000/=
- Hoteli ndogondogo,mabaa, nyumba za wageni na migahawa- 80,000/=

8. Ulinzi Binafsi.
-Makampuni makubwa na makampuni ya kigeni - 105,000/= - Makampuni mengineyo- 80,000/=

9. Sekta nyingine ambazo hazikutajwa - 80,000/=

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 40 mpaka sasa

  1. nchi hii kweli mbugilambugila...ya serikalini hatangazi

    ReplyDelete
  2. Walimu mbona hawajawekwa au wanangukia wapi? Na kwanini isiwe tu 100,00 maana maisha yanazidi kuwa magumu kila siku

    ReplyDelete
  3. Hujui kama Serikali maana yake ni SIRI KALI?Natania tu mjomba,Tutatangaza tu tunaogopa wasigome.

    ReplyDelete
  4. Wabunge vipi?Kapuya mbona hajawataja,wao hawaongezewi?

    Mdau

    ReplyDelete
  5. sasa huyu mwenye mshahara wa Tshs. 80,000/- ataweza vipi kumplipa mtumishi wa ndani Tshs. 65,000/-

    ReplyDelete
  6. mimi ni clearing& fowarding nikilipwa laki?

    ReplyDelete
  7. Ma-bank binafsi mbona hayakutajwa?kama Barclays,SCB,Exim,Bank M,City n.k au ndo yanaangukia kwenye "nyingine ambazo hazikutajwa TZS80,000"....au kasahau!!!!!!???

    ReplyDelete
  8. mheshimiwa naona kazidiwa, tunachojua madai yanahusisha sekta zote iweje yanatangazwa ya sekta binafsi tu? kigugumizi cha nini?

    ReplyDelete
  9. Hii nchi jamani inachosha!! Sasa kima cha chini kwa nini kibague Sekta?? Kwani walioko kwenye sekta nyingine sio watanzania????!!!!! Unapoweka kiwango
    cha mshahara wa chini unaweka kw wafanyakazi wote kwani hao wengine sio watanzNia???!!! Igeni kwenye nchi za wenzenu minimum wage ni kwa raia wote!! Set minimum wage for every citizen to benefit

    ReplyDelete
  10. Ni rahisi kweli kumsemea mwanzako afanye nini ila wewe ufanye nini ni ngumu kinoma.

    Unapokuja na artificial figures za mishahara bila kueleza basis ni upuuzi na ignorant ya hali ya juu. Kaa chini piga mahesabu je ili mtu anayeishi Dar es Salaam kapanga vyumba vitatu( Kimoja yeye na mkewe/mumewe, cha pili watoto wawili wa kiume na cha tatu watoto wawili wa kike) pale Mbagala rangi tatu kwenye nyumba yenye maji na umeme(Maisha bora kwa kila mtanzania) anatakiwa kutumia kiasi gani kwa mwezi ili aishi?.

    1. Vyumba vitatu + sebule @ 20,000 = 80,000 kwa mwezi
    2. Bili ya umeme Tshs 10,000 kwa wiki = Tshs 40,000
    3. bili ya maji(Dawasco + Kununua) = Tshs 30,000 kwa mwezi
    4. Gas ya kupikia Tshs 45,000 kwa mwezi
    5. Chakula familia ya watu sita Tshs 70,000 kwa wiki = 280,000
    5. Nauli ya daladala watoto shule 6,000 kila mtoto = 24,000 kwa mwezi
    7. Nauli ya kuendea kazini Tshs 150,000 kwa mwezi
    8. Kumuona daktari na dawa(matibabu) = Tshs 200,000

    9. Ada ya shule kwa mwaka kwa kila mtoto (Tshs 600,000@4children 2,400,000) Igawe kwa miezi 12 = 200,000

    Jumla ni Tshs 1,049,000 kwa mwezi ili mtu wa hali ya chini aweze kuishi Mbagala rangi tatu halafu assume kuwa mtu huyu atafanya masaa tisa kazi kila siku kwa muda wa siku tano ni masaa 45 kwa wiki zidisha mara nne = masaa 180 kwa mwezi. Then gawanya 1,049,000 kwa 180 takriban ni Tshs 5,828 kwa saa

    Then toa tamko kuwa kima cha chini cha sekta binafsi ni Tshs 5,828 kwa saa. Sasa mwajiri atatakiwa kulipa kwa saa siyo kwa mwezi. Hii itatoa mwanya kwa wahindi wanaopenda kuwaweka watu kazini hata kama hawana cha kufanya kuwaachia wakalime mashamba yao au kutafuta masaa ya ziada sehemu ingine.

    Pia kulipa kwa masaa kutapunguza wizi wa muda kwa mwajiri na wizi wa ujira kwa waajiriwa.

    ReplyDelete
  11. Serikali iache ku-kukuruka...sasa 100% ya ongezeko la mshahara lipowapi?

    ReplyDelete
  12. Maisha bora kwa Kila mtanzania... Chagua CCM chakua Kiwete 2010.

    Usisahau kuchagia CCM. Tuma CCM kwenda 15399.

    ReplyDelete
  13. Mtoa maoni wa Tarehe Fri Apr 30, 05:17:00 PM, Ndugu yangu kweli umepiga mahesabu mazuri lakini mshahara huo pia bado hautoshi maana umeacha mambo kadhaa wa kadhaa.

    1. Hukujumuisha Kodi (PAYE) pay as you earn

    2. Hukujumuisha Makato ya pensheni (PPF,NSSF,GEPF,LAPF,PSPF,NHIF).

    3. Hukusema lolote kuhusu mfanyakazi wa Ndani sasa sijui mmoja wenu atakuwa baba/mama wa nyumbani?

    Pamoja na hayo nakupa pongezi kwa uchambuzi mzuri!

    ReplyDelete
  14. Hapa ametangaza "Vima vya chini", sio "kima cha chini"

    ReplyDelete
  15. MAISHA KWELI BADO MAGUMU SANA HUKO NYUMBANI NA NAWAHURUMIA SANA WANA JAMII HUKO

    YANI MTU ANAKULA MSHAHARA WA ELFU 80 KWA MWEZI MZIMA DUUUUUH!!!!!!
    ATAKULA NINI ATALIPIA NYUMBA NINI ATASAFIRI NA NINI ATALIPIA HUDUMA MUHIMU NA NINI???????????

    NDIO SABABU NDUGU ZETU WENGINE WANAFIKIA KUSEMA MANENO MABAYA KAMA WENGINE HUSEMA AFADHALI YA KUWA MBWA ULAYA

    SIO SIRI HUKU TULIPO SISI WABEBA BOKS MAISHA YAMEBADILIKA KIDOGO YAMEKUWA MAGUMU SANA KWA MIPANGO MUUNGANO WA HIZI NCHI ZA UGHAIBUNI

    LAKINI PAMOJA NA HAYO UKIPATA KAZI PIGA UWA KOSA KOSA MFUKONI HUKOSI EURO 70 KWA SIKU

    SASA EURO 70 KWA SIKU UKILINGANISHA NA HELA ZETU ZA MADAFU NI KAMA LAKI 1 NA ELFU 30 KWA SIKU

    JAPOKUWA GHALAMA ZA HUKU ZIPO JUU LAKINI NA KIPATO KINATOSHELEZA KULIPIA HUDUMA ZOTE AMBAZO BINADAMU ANASTAIRI KUPATA

    MUNGU IBARIKI NCHI YETU MUNGU WABARIKI WATU WA NCHI YETU.

    ReplyDelete
  16. Huu kwa kweli ni ulaghai wa daraja la kwanza wa kisiasa! Kapuya angeeleza au hata kutoa msingi wa mchakatuo huo wa viwango hivyo. Kwa watu wanaoishi kwenye mji mmoja na kupata huduma za msingi zile zile kwa nini kuna tofauti kubwa ya kima cha chini?

    Na kama serikali imeweka kiwango cha chini kwenye sekta binafsi na hata serikalini, kwanini isiweke kima cha juu kabisa au wao huko juu ndio "freefall!"?

    Tatizo watanzania hawahusishi haya na serikali waliyoichagua. Wanapoteza haki zote za kulalamika kwani watapewa nafasi mwaka huu kuwaondoa madarakani lakini katika mawazo yetu hatuoni kama tunastahili kitu kingine zaidi ya hiki kilichopo.

    Ni mpaka pale Watanzania watakapoweza kuhususisha hali zao za maisha na utawala uliopo madarakani wataendelea kuogelea katika madimbwi ya mafuriko, wataendelea kukaa kwenye foleni kama za kungojea hukumu ya mwisho, na wataendelea kuridhika na uongozi mbovu wa chama ambacho kimepoteza kila chembe ya itikadi na mwelekeo!

    Watanzania wajiunga na CCJ kama wanataka mabadiliko, CCM ndio imetoka hiyo!!

    ReplyDelete
  17. I hate mambumbumbu...that's just me

    ReplyDelete
  18. Nikiona haya ndio maana sitaki kabisa kukanyaga nchini.....

    Kwanza wao wameficha mishahara yao. Kwanini wasiweke kila mishahara ya watu tukaona yote na tukajua kila mtu anaishije hapo bongo.

    Pili alivyoweka hivi kwa nini asiweke mishahara ya kiwango cha chini kiwe kimoja...Huu nikuoneana tu...nani atakubali kuwa yeye ni mfanya biashara mkubwa alipe kiwango cha juu mfanyakazi wake. Na huyo mfanya biashara mkubwa anatambulikaje?

    Siji bongo mpaka apatikane kiongozi mwanamke naona ndio kutaendeshwa kwa uhalali.

    ReplyDelete
  19. Mhhhhh My lovely home country. Nifanya kazi masaa 10 kazini kwa siku ninatengeneza sawa na wanaolipwa top salary Tanzania.

    Mbona hawajaweka mishahara ya serikali na ya Executives tuone pia. Mabank nayo yamefall katika category gani? Ina maana hayo maisha tunayoyaona hapo Tanzania watu wanalipwa 350,000 tu kwa mwezi? Au hizo nyingine zinatoka wapi?

    !!!!

    ReplyDelete
  20. Kuna mahesabu mazito yanaendelea ambayo kwa 'wananchi wa kawaida' ni magumu sana kuyaelewa.
    Mimi kama mwananchi wa kawaida nilidhani kwamba kima cha chini kinawekwa na serikali ili kuhakikisha kwamba mfanyakazi yeyote nchini anaweza kujikimu kwa matunda ya kazi yake. Sasa inapokuwa wafanyakazi wa sekta tofauti wana mishahara tofauti nashindwa kuelewa ina maana sekta zinazolipwa zaidi zinafanya kazi nchi nyingine au? Au ndio mambo ya divide and rule, kujaribu kutengeneza mifarakano kati ya wafanyakazi ili wasishirikiane kugoma?
    Halafu serikali inapoongeza mishahara kwa wengine wakati haijaongeza ya watu wake inatoa wapi 'moral authority' ya kufanya hivyo? Kwa mfano wa enzi za Yesu (kunradhi wadau wa imani tofauti), kweli serikali imejijengea uhalali wa kurusha jiwe la kwanza kumpiga mawe kahaba katika suala hili?

    ReplyDelete
  21. Haaa haaa haaa!
    Kwa haraka haraka wafanyakazi wenye kima cha chini cha chini kabisa ni kwenye sekta ya kilimo.
    KILIMO KWANZA!!!

    ReplyDelete
  22. Ebwana nchi hii viongozi hawajali maisha ya wananchi kwani wao na watoto wao wana 100% ya kula kulala na elimu so kwa mtindo huu wizi makazini kwa sana pamoja na majambazi kuongezeka kwani life kila cku linazidi kuwa tite na mbaya zaidi watanzania ni watu ambao mi nasema c waelewa hata wawe educated namna gani bado 2 kwani upuuzi serikali inafanya lakini wanancnhi wana kuwa kimya sasa hivi kilicho baki unachokiona kinaweza kukutoa ili life libadilike unafanya kama ni kushika GUN MZUKA 2 kwani real mapinduzi kwa tz bado sana labda itakuja fanyika miaka kama 100 ijayo KILICHOBAKI NI KUFANYA UHARAMIA 2 HAKUNA KUOGOPA KIFO KWANI HA2JAZALIWA TUISHI MILELE 2NAPITA 2

    ReplyDelete
  23. Mi nauliza swali huyu Waziri anapo kaa chini na kuanza kutangaza kima cha chini Tshs. 80,000/- je anajua hali halisi ya maisha ya mtanzania wa hali ya chini au anasema tu nae aonekane kwenye vyombo vya habari..??? Maana huo mshahara utaishia kwenye nauli tu sasa sijui huyu mtu atakula nini atalala wapi..kisha mseme wizi utaisha na rushwa kweli...

    Mheshimiwa Waziri naomba ukae chini tena utafakari hiyo mishahara ya watu... huduma ya afya ni kitu muhimu sana kwa jamii ukianzia wewe mwenyewe au ndio ukiugua utaenda kutibiwa majuu????

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 01, 2010

    kweli bongo wanajua kudharau proffesionals,yaani huduma ya afya ndo wanapata mshahara mdogo kuliko wote??hivi nani wa muhimu kati ya nurse/doctor anayekutibu au huyo mtumishi wa ndani??hizi nchi za wenzetu huwezi kukuta utumbo kama huo.ma doctor wanalipwa sana,pamoja na proffesional wengine,teachers,engineers.hebu msidharau proffesional bongo.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 01, 2010

    kweli bongo watu hawajali elimu na ni bora kutokusoma kuliko kusoma sasa wewe nesi ukimlipa mshahara mdogo kuliko mfanyakazi wa ndani ubalozini si kichekesho hicho??! kweli bora wengine waozee ughaibuni.
    hayo hayatabadilika hadi tubadilishe chama na tuwe na viongozi walioenda shule.Bongo kweli noma.

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 01, 2010

    Mdau hapo juu umenichekesha mpaka sana KUHUSU KILIMO KWANZA.
    Ni kweli ukiangalia wafanyakazi wenye mshahara mdogo kuliko wote ni wa Idara ya kilimo.
    Sasa nyie jamani mnashangaa kima cha chini kuwa 70n ulezeni zanzibar kima cha chini cha mshahara ni kiasi gani?
    Ngoja tu nikujibuni ni Elfu thelathini yani SHS 30,000.
    Na tunapeta tu.

    ReplyDelete
  27. kwa mtindo huu Tanzania kilimo na afya tutaendelea kulalamika kuwa tuna kufa kwa njaa na magojwa na wataalamu tunao,kwa viwango hivi vya mishahara halafu tupambane na rushwa,ni kupigana changa la macho,
    Hivi mimi sielewi huyu Kapuya na team yake wanafanya kazi gani.
    Nikiendelea nitasema vibaya bure.
    KAPUYA AFANYIWE MDAHALO NA WANANCHI KUPITIA TV/REDIO JAMII IMUULIZE MASWALI.

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 01, 2010

    After four years ya u nurse na kuhangaika sana na bahasha ya kaki nakuja kulipwa 80,000, hiyo ni miaka 10 iliyopita inamaana hamna kilichobadilika hapo.
    nimekuja ulaya nafanya kazi siku nne kwa wiki nalipwa 3500 pound hapo PAYE wameshachukua chao,sawa na milioni 7 za madafu.
    bongo tambarare, halafu utaniambia nirudi bongo, nikafanye nini? nilipwe alfu 80,000?

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 10, 2010

    Kweli tunataka wabunge na walimu wawekwe wazi pia>>>

    Ministers and some other govnment officials, we want a transparent government... we wanna knw kama kuna kuumizana au tunakaribia wote kufanana kimasilai.

    ReplyDelete
  30. Mhudumu wa afya 80000, clearing & Forwarding 230000 halafu mnalalamika watu wanakufa kwa sababu hakuna wataalam. Hivi huyu waziri alikaa chini na kutafakari kabla ya kusoma huu utumbo? Halafu ndio profesa. Tanzania hatuhitaji misaada tunahitaji "Common sense"

    ReplyDelete
  31. Kila mtu ametoa maoni yake kwa mtazamo wake na ugumu wa maisha anaoupata mi naomba nimuombe Waziri Kapuya avae uhalisia wa mtu wa kima cha chini halafu akokotoe hiyo 80,000/= tuone kama ataweza kumaliza hata siku 2,jamani mwenye shibe hamjui mwenye njaa yote haya tunabanwa kwasababu ya mafisadi kweli TZ ni kisiwa cha umasikini katikati ya bahari ya utajiri.
    (Few people make things happen,Hundred talk about,Thouands see what would happen then millions become affected )

    ReplyDelete
  32. Ukweli serikali inabidi mtafakari sana hicho kima cha mishahara na hali halisi ya maisha, kama mtu anapata shs. 80,000/= per month na na familia, anahitaji kula, kulipa umeme, na kusafiri pia. Na ukizingatia bili ya umeme ndo kwanza imepanda, hivyo huyu mtanzania ataweza kumudu gharama za maisha kweli kwa mtindo huo? Na hiyo ndo inasababisha watu kuingia majaribuni kama rushwa, wizi, ujambazi na matendo yoyote yasiyo ya halali. Tunaomba muwe wastaarbu katika hilo. Wewe waziri huwezi kugombea gari, wala kulala na njaa na hata ukiugua wewe na familia yako hamna shida ya matibabu kwani kiasi chochote cha pesa uko tayari kulipia, sasa sisi walalahoi tutaishije?
    Tunaomba mkumbuke wote tumeumbwa na mungu ila tunatofautiana kiuwezo. Kwahiyo mnapofanya bajeti zenu mujaribu kuangalia mtu wa chini kabisa ambaye anategemea kila kitu kulipia kuanzia nyumba ya kupanga, daladala, chakula nk.

    ReplyDelete
  33. Daa! Walimu vp?

    ReplyDelete
  34. Ovius mambo siku hizi yamebadilika Brother Kapuya ingekuwa fresh kwa kila ,mwajiri wa tanzania alipwe mshahara wake kwa masaa pindi awapo offisin kwa Mfano: kwa kila lisaa limoja isipungue chini ya sh 5500 na wala isizidi 6500 apo ndipo 2tasema Maisha bora kwa kila Mtanzania aya mambo yakulipana kwa mwenzi yamepitwa na wakati

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 23, 2011

    nina maswali mengi kwa serekali.....
    1. mafuta ni bei gani???
    2. ada kwa shule za serekali ni shilingi ngapi???
    ..
    au hiyo mishaara ni kwa vijana wanoishi kwa wazazi wao..??????

    ReplyDelete
  36. wizi mtupu:

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 17, 2012

    bado mishahara ya serikali inaendelea kuwa siri hadi lini mwisho wake unakuja cjia wameongeza 7000 ktk hela ya mwanzo hv mbona munaangalia sekta binafsi wakati inawatumishi wachache kuliko walio serikalini

    ReplyDelete
  38. neema mcharoJuly 25, 2012

    hivi m2 analipwa laki2 alafu maisha yapo juu kiasi hiki atamlipaje mfanyakazi wa majumbani kiwango hicho hapo walichotaja?boresheni maisha kwanza ndo mpange kiasi cha mishahara mtakavyo. tunaomba mtaje na mishahara yenu

    ReplyDelete
  39. Tuna hitaj na break down ya matumizi vitall na mshahara. otherwise wizi na rushwa vitakwisha wapi? wao wamejieekea mishahara minono,nyumba wamepewa wanalipiwa kila kt still wanaiba pesa za walipa kodi na kuzilundika ugaibuni hii nchi inakwenda wapi?mishahara na maisha halisi katu haviwiani.

    ReplyDelete
  40. SASA SHILINGI ELFU 80000/- NAULI YENYEWE 400*2=800*30=24000/- CHAKULA 2000*30=60000 MCHANA, 2000*30=60000/- USIKU HAPO HUJANYWA CHOCHOTE BADO NGUO KODI MALAZI HIVII NYIE SERIKALI MNAJUA HESABU KWELIIII????????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...