BAADA YA KUENDELEZA LIBENEKE KWA TAKRIBAN MIAKA MINNE MFULILIZO BILA KUCHOKA, HATIMAYE LEO ZE FULANAZZZ YA GLOBU YA JAMII IMECHUKULIWA RASMI KUTOKA KWA ANKAL NA KUWEKWA PEMBENI TAYARI KWA KUPIGWA MNADA ILI KUCHANGISHA PESA ZA MAENDELEO YA WADAU.

KAMPUNI YA USAFIRISHAJI MIZIGO YA HILLVIEW FAMILY COMPANY LIMITED ILIYOKO READING, UINGEREZA, IMEINUNUA ZE FULANAZZZ KWA PAUNI 1,000 ILI KUINADI NA KUCHANGIA MABLOGA KUENDELEZA LIBENEKE KWA UFANISI ZAIDI.
SIKU YA MNADA UTAOFANYIKA ONLINE ITATAJWA KARIBUNI, NA MABLOGA WANAOTAKA KUNUFAIKA NA LIBENEKE LA MNADA WA ZE FULANAZZZZ WANATAKIWA WALETE MAOMBI YA MSAADA NA EMAIL ADDRESS ZAO KUPITIA issamichuzi@gmail.com ILI KUWEZA KUFIKIRIWA NA JOPO LA GLOBU YA JAMII NA WATAALAMU WA HILLVIEW FAMILY COMPANY.
JUMLA YA MABLOGA WACHANGA 10 WATANUFAIKA NA MPANGO HUU AMBAPO WATAPATIWA LAPTOPS, MODEM ZA INTERNET PAMOJA NA PESA ZA AIRTIME YA INTERNET YA MIEZI MITATU ILI KUWAWEZESHA KUANZIA KAZI. MWISHO WA KUTUMA MAOMBI NI APRILI 10, 2010. MPANGO HUU UNAMHUSU BLOGA YEYOTE MCHANGA POPOTE ALIPO DUNIANI.

PICHANI ANAONEKANA ANKAL AKIKABIDHI ZE FULANAZZZ KWA MKURUGENZI WA KAMPUNI YA HILLVIEW FAMILY BW. HASSAN ABDULLAH JIONI HII HUKO READING BAADA YA KUTOA KIASI HICHO CHA PESA HUKU WAKISHUHUDIWA NA WADAU GARDOL NA MAALIM ABDULLAH AMBAYE NI MWEKA FEDHA YA KAMPUNI.

PAMOJA NA KUSIKITIKA KWA KUIKOSA ZE FULANAZZZ AMBAYO IMEKUWA KAMA NEMBO KUU YA GLOBU YA JAMII, ANKAL AMEISHUKURU HILLVIEW FAMILY COMPANY LIMITED KWA KUJITOLEA KUSAIDIA MAENDELEO YA LIBENEKE NDANI NA NJE YA TANZANIA.

HILLVIEW COMPANY NI KAMPUNI INAYOSAFIRISHA MIZIGO YA AINA YOYOTE DUNIANI KUTOKA UK KWA MIAKA 15 SASA. INAPATIKANA:
UNIT 13,
ACCESS STORAGE CENTRE
62 PORTMAN ROAD
READING
BERKSHIRE
RG30
1EA

SIMU NAMBA: 0118 957 6667
FAX: 0118 907 6241
WEB:
http://www.hillviewfamilycompany.com/

--------------------------------------------

Napenda kuchukua nafasi hii kutuma maombi yangu kama mmoja wa Mablogga wachanga wanaotaka kunufaika na mpango uliofadhiliwa na HILLVIEW FAMILY kwa kushirikiana na BLOG YA JAMII. Kama ujuavyo sisi mablogga wachanga moja ya changamoto tunayopata ni ukosefu wa vitendea kazi kama Computer, Modem na hata wakati mwingine pesa ya kuweka balance kwa ajili ya kutuma post za kila siku. Hii inapelekea Mablogga wengi kushindwa kuendeleza Blog matokeo yake Libeneke kuishia njiani au kutuma post moaj kwa wiki hata wakati mwingine kwa mwezi kutokana na hali ngumu.
Hivyo mpango huu wa kusaidia mablogga wachanga ambao umefadhiliwa na HILLVIEW FAMILY na BLOG YA JAMII ni sehemu ya kuleta maendeleo kwetu sisi mablogga ili kuendeleza libeneke la kukuza sekta ya habari na mawasiliano.
Ni matumaini yangu kuwa ombi langu litasikilizwa.

Wako katika kuendeleza libeneke
teknohabari webmaster

KALLEY PANDUKIZI

http://teknohabari.blogspot.com/

-----------------------------------------

kwa wadau wote wa Glob ya Jamii.
Maombi yangu ni kwamba hii fulanazi ya jamii ambayo Issa alikuwa ana ivaa ipelekwe makumbusho ya Taifa kwa kuweka kumbukumbu katika jamii kuhusu mchango mkubwa wa Issa Michuzi katika jamii ya kitanzania. Iwekwe na kuambatanishwa na historia ya maisha yake tangu michuzi alipoanzia na kufika hapa alipo. ni watu wachache sana ambao wameweza kuwaunganisha watanzania wote kwa kutumia mtandao kama huu. Michuzi ni mtu ambaye jamii ya Kitanzania hasa ya Diaspora haita msahau hata kidogo. Ametufanya tufamiane kama tuna kaa nchi moja. Leo hii jambo linatokea Tanzania au Japan tayati tuna jua na kuona picha na video. huu ni mchango mkubwa sana. Na vile vile bila kusahau roho ya unyenyekevu wa michuzi aliyo nayo kwa watu wote na ukaribu wake wa watu wa hali zote. Naomba hii " the fulanazi" ipelekwe makumbusho ya taifa.

Mdau
USA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. SASA ANKO UTAMJIBU NINI MZEE KALUMANZILA WA BAGAMOYO, AMBAYE ALIKUWA MBIA HIYO FULANA NDIO KILA KITU.MHHH DALILI ZA KUFA BLOG YA JAMIII, THE FULANAZZ IMEKWENDA, TUTAIMISS SANA.SASA ANKO VEKESHEN BASI TENA.

    ReplyDelete
  2. No offence !
    nataka kumuona atakaye inunua!

    ReplyDelete
  3. This is Serious,
    OOOh. Sasa Ankali nina Ombi moja tuu. Katika huo mshiko ulioupata mimi naomba utoa angalau laki moja ununulie vyandarua au mashuka kwa ajili ya vitanda hata kama ni viwili vya wodi ya wazazi au watoto ktk hoispitali yoyote ya Umma Tanzania. Nashukuru!
    Aisee hii deal imetulia..

    ReplyDelete
  4. Mzee Wa Chama Mbona hii hujaiweka?????????

    Mbunge wa CCM Fred Mpendazoe Ajivua Uanachama na Kutimkia CCJ

    Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kishapu (CCM) Fred Mpendazoe akiwapungia mkono waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mara baada ya kutangaza nia yake ya kuondoka CCM na kujiunga na Chama cha Jamii(CCJ). Picha na Tiganya Vincent-Dar es Salaam.

    --------

    Kauli za Fred Mpendazoe wakati wa kikao chake na waandishi Leo jijini Dar es Salaam

    ---

    Mbunge wa jimbo la Kishapu (CCM), Fred Mpendazoe ametangaza rasmi kikiahama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama Cha Jamii (CCJ) na kutuma salamu kwa vigogo wengine kuwa milango hipo wazi.

    Akizungumza na waandishi wa Habari leo katika ukumbi wa Idara Habari MAELEZO, Mpendazoe ambaye alitangulizana na wapambe wake wawili, aliongea kwa kujiamini, aliweza kisema kuwa Taifa linakoelekea kwa sasa ni kubaya hasa kwa utawala huu wa CCM, ambao unaongoza kwa kubahatisha.’Nimekuwa ndani ya CCM, muda mrefu lakini hukunikishuhudia hali ya mambo yakienda kombo, hivyo ilikujinasua ni heri kujivua uwanachama” alisema Mpendazoe.

    Mpendazoe aliendelea kusema kuwa: ‘Kuna maneno mengi yamesemwa sana juu ya CCJ, na hata kuwahusisha watu mbalimbali juu ya chama hichi, ninachosema kwa sasa ni kuwa, nimefuatilia kwa umakini Katiba yake na kugundua kuwa hichi ndicho chama thabiti kilicho na nia ya dhati nay a kweli ndani ya nchi hii.

    ..Ifahamike kuwa CCM si Hellena…yaani Mama yangu Mzazi,,natakangaza rasmi kutoka CCM na wala sijutii dhamira yangu na kujiunga rasmi na CCJ na kuleta maendeleo thabiti ya nchi.” Alisema Mpendazoe kwa kujihamini na hamasa kubwa.

    Kwa hali hiyo Mpendazoe aliweza kuhishukia Serikali ya CCM, Ikulu na Shehe Yahya Hussein kwa kile alichodai kuwa,mambo yao na maamuzi wanayoyatoa yanaipeleka nchi pabaya

    ReplyDelete
  5. mmmh umetuhabarisha haya mambo wakati wapiga box wamechoka na box wamelala subiri kesho wakiwa na nguvu utaona comments zao

    ReplyDelete
  6. Hii fulanaz ndio kizizi cha ankal kupiga mikonozz dada zetu na wenyewe hutulia kama maji ndani ya mtungi.

    Hii kitu itakuwa habari za siku ya kwanza ya mwezi aprili.

    Wapi Peter Nalitolela wa Muzumbe jamani?Mbona mdau ameadimika sana, kama gharama za internet cafe zimepanda mimi naoendekeza globu ya jamii imchangie kitu kidogo ili atuletee burudani za Muzumbe?

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  7. Japo nisha-comment but bado kuna watu wataingia kichwa kichwa, hahahaa raha kuona jinsi wasivyokua makini...

    Mdau, China

    ReplyDelete
  8. IWEKWE MAKUMBUSHO YA TAIFA KWA KUHESHIMU MCHANGO MKUBWA WA ISSA MICHUZI KATIKA JAMII YA TANZANIA

    ReplyDelete
  9. mimi blog hii nilikuwa napenda ze fulanazzzz kuanzia leo ndio basi kuangia humu ndani yaani umeiuza ankal yaani vekeshen hii umekwenda kwa ajili ya hizo paundi 1000 naisi blog hii ndio mwisho wake wadau wa mji wa kusoma mumefanya vibaya sana

    ReplyDelete
  10. Ankal, Ze Fulanaz ndio ilikuwa alama au chapa ya blogu! sasa umekubali kuuza chapa kwa bei ya bure kiasi hicho!
    Waambie jamaa wakurudishie Ze Fulanaz, tutawa-refund pesa yao na interest!

    ReplyDelete
  11. teh teh teh teh.........

    ReplyDelete
  12. Ankal, mie najitolea kukuletea ze fulanazzz mpya kabisa ku-replace hiyo uliyoinadi ughaibuni. Kama unakubali ombi langu nijibu basi.

    Mdau wa Mwenge

    ReplyDelete
  13. Michuzi katupata sana hapa Leo ni April one (1/4) na hakuna cha fulanazi kuuzwa wala nini yote ni Mambo ya michuizi

    ReplyDelete
  14. happy foolish day

    ReplyDelete
  15. siku ya wajinga duniani !
    wajinga ndio waliwao.
    aaaka, ze fulana haijanunuliwa wala nini !
    poleni mliotuma maombi .


    mdau no 5 !

    ReplyDelete
  16. Wadau wa mji wa kusoma tuko REAL,hao jamaa wa HILLVIEW FAMILY office yao ina desktop pc 3 na all in printer/fax/scaner/copier lakini wameweza kununua ZE FULANA kwa £1000,japokuwa Hijja na Mloka wa QMC walibidi mpaka £999.
    Hii inamaana kwamba wadau wa miji na nchi zingine mnaongea sana lakini kisu hamna,watu wa mji wa kusoma tunatumia QMC kuload container na HILL VIEW kusafirisha,acheni kuwaunde estimate watu kwa kuwa office hazina canon copier na fax machine

    Big Up HILLVIEW

    ReplyDelete
  17. tarehe moja mwezi wa nne............

    mdau chiggs

    ReplyDelete
  18. HEHEHEHHEE WABONGO KWAKUPENDA ZACHAPCHAP WASHAKAMAPWA
    HAPPY FOOLISH DAY
    LOL ANKAL UMEWAPATA

    ReplyDelete
  19. Siku ya wajinga leo

    ReplyDelete
  20. kaka michuzi.mmmmm .ahsante sana umefanya nicheke sana leo nilirudi college nimenuna....loll

    hatari,hesabu maombi ulopata utuambia....

    your fan..

    ReplyDelete
  21. Acha utani ankal. Si unakumbuka mi nilishakufuata na pesa taslimu Tshs. milioni tano mkononi uniachie hiyo fulana lakini ukanichomolea.

    Eti leo ndo uiuze kwa tupaundi alfu moja tu!

    Aha nimekumbuka ... leo ni siku ya wajinga.

    Ila seriously bado ile milioni tano ipo niachie hiyo ze fulanazzz ukirudi Bongo tuwasiliane.

    ReplyDelete
  22. Hii comment imetoka kabla ya fools day. So it cant be all fools deal, this is real deal

    ReplyDelete
  23. jamani chonde!chonde! mliofika bei fulanazzzzz!!!! ya Globu,tunaomba kama kuna njia nyingine na upatikani wa fedha basi fulanazzzzz!!!!irudishwe,maana siye wajeshi wa FFU! uipigiaga saluti kwa mkuu wa libeneke !sasa ?tutampigiaje saluti mtu asiye na madaraka katika mamlaka ya libeneke????
    Chonde Chonde! fulanazzzzz!

    ReplyDelete
  24. tafadhali TUNAITAKA ze fulanazz yetu,nyie vipi bwana?????
    kwanini kutufitini ivi ebu mrudishieni ze fulanazz mie nimeizoea na inampendeza sana tu na ni charter yake ya blogu ketu

    aaaah michu mbona haitanoga tenaa??

    URUDISHWE NA MICHU USIACHE KUIVAA

    ReplyDelete
  25. sijapenda kabisa kuuzwa ze fulanazz
    nahama hii blogu na wafuasi wote nilowashawishi kuingia umu!!

    na habari ndo iyo

    ReplyDelete
  26. Mdau unayesema T-shirt ipelekwe makumbusho ya Taifa nakuunga mkono, wazo zuri.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  27. it was an april fool joke???? au... hii ikiondoka basi na blog kwishnei..if it is true mimi nitainunua nikurudishie

    ReplyDelete
  28. hivi we michuzi ina maana ilikuwa sikukuuu ya mafala?! hata hivyo ilikuwa ni idea nzuri tuu hiyo dark blue tshirt imekupendeza zaidi ya fulanazz

    ReplyDelete
  29. we ankal mjanja unazo nyingi hizo, umetoa isiyo original mbona hainuki mchuzi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...