Mkuu wa Wilaya ya Mbeya aliyehamishiwa Wilaya ya Ilala Mh. Leonidas Gama akiwasili soko la Sido, Mwanjelwa, jijini Mbeya alikoenda kuaga wafanyabiashara ambao alisota nao toka siku walipounguliwa na soko la zamani la Mwanjelwa na kuhakikisha wanapatiwa sehemu mbadala mara moja. Wengi wameseikitika na kuondoka kwake na kumtaka aendeleze moyo huo wa upendo na uchapa kazi
Mh. Gama akiongea na wafanyabiashara wa soko la Sido, Mwanjelwa
kwa herini ya kuonana jamani...
chapa kazi kijana...
Mh. ututembeleage mara moja moja basi..





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Pole Bw. Gama unaacha vinono vya Wilayani Mbeya.. ebu jionee mwenyewe hapo; wembaba wakuhesabu. Wasalimie Ilala.

    ReplyDelete
  2. Diet jamani! Die jamani!

    ReplyDelete
  3. hivi kwa nini bongo kila mtu mzima from 40 anakuwa mnene au huwezi kuhashimiwa bila kunenepa je serikali ana habari kwamba karibia nusu ya watz wana obesity ambaya ni hatari kuliko hata AIDS?

    ReplyDelete
  4. Huyu Mheshimiwa ni mchapa kazi saana. Nakumbuka sana enzi zile nafanya kazi Lindi alikuwa mkuu wa Wilaya ya Nachingwea. Kwa muda mfupi alifanya mambo makubwa sana Nachingwea ikiwemo ujenzi wa Boma la mfano Tanzania nzima, kuacha lile la Manyara.

    Natumaini atafanya makubwa zaidi Wilaya ya Ilala kwani Resources za kumwaga Ilala.

    Mtabata

    ReplyDelete
  5. What can I say?!
    "Same size"

    ReplyDelete
  6. kaka michuzi ebu tuambie hiyo stendi ilo eneo gani,wengine tuliondok muad huko

    ReplyDelete
  7. Huyu jamaa kwa umbo lake kama Mkapa natabiri huko mbeleni atakuja kuwa rais.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...