Mwanasheria wa manispaa ya Moshi Bi. Kyssa Limo akimtaka Diwani wa kata ya Mji Mpya Bw. Abuu Shayo kutoka nje ya lilao cha baraza la madiwani kwa kilichodaiwa kukiuka kanuni za vikao
Madiwani wa Chadema toka shoto Bw. Abuu Shayo na Bw. Jafary Michael wakiwasilikiliza askari mgambo walipotakiwa kutoka ndani ya ukumbi wa mkutano
Diwani wa kata ya Pasua Jafary Michael akilalamika kwa Meya baada ya kutolewa kwa amri ya kutaka kutolewa nje ya kikao kwa diwani huyo
Diwani wa kata ya Rau Christopher Limo akisoma taarifa iliyokuwa ikizungumzia mafaniko ya Halmashauri jambo lililopelekea kutokea varangati hilo
Mh. Lucy Owenya akiongea kwa hisia
Mkurugenzi wa manispaa ya Moshi Bernadete Kinabo akiomba mwongozo wa Meya Lameck Kaaya wa kumtaka kumtoa nje ya Kikao Diwani wa Pasua Japhary Michael
Madiwani Abou Shayo na Japhary Michael
Habari na picha na Dixon Busagaga
wa Globu ya Jamii, Moshi
HOJA ya kuipa hati Usu ya miaka 33 kampuni ya Discovery Tanzania Heritage (DTH),kumiliki uwanja wa Uhuru Park mjini Moshi, leo ulizua tafrani baada ya madiwani CHADEMA kufanya vurugu katika kikao cha baraza la madiwani kwa kuwapiga Meya na mkurugenzi wa manispaa hiyo kwa kutumia majoho na kofia zao.

Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ilitoa hati ya eneo la Uhuru Park kwa kampuni hiyo ili iitumie hati hiyo, kukopa Shilingi Bilioni 1.5 benki kwa ajili ya kuendeleza eneo hilo.

Huku wakitoka nje ya kikao cha baraza hilo,Madiwani hao sita wakiongozwa na diwani wa kata ya Mji Mpya, Bw. Abuu Shayo alikuwa akirusha joho, kofia na koti lake la suti katika meza kuu ya viongozi huku wakisema wamechoshwa na vitendo vya kuburuzwa.

Katika kikao hicho ambacho kiliitishwa kwa dharura ili kutengua uamuzi wa awali wa baraza hilo kumpa nusu hati mwekezaji kampuni hiyo ya jijini Dar es salaam,kilitengua rasmi uamuzi wake wa awali wa Machi 31 mwaka huu.
Tafrani katika kikao hicho na kuibua malumbano na baadaye madiwani hao kutoka nje ilitokana na kitendo cha diwani wa kata ya Rau kusoma agenda nyingine badala ya mwenendelezo wa agenda kuu iliyotolewa na diwani wa Kaloleni, Michael Mwita ambaye aliomba kubatilishwa kwa uamuzi wa awali.
Wakati akisoma hoja iliyohusu ujenzi wa shule za msingi katika baadhi ya kata,madiwani hao akiwemo wa kata ya Pasua,Japhary Michael alianza kupinga kitendo hicho kwa madai kuwa agenda ilikuwa ni moja ya kubatilisha uamuzi huo na si vinginevyo na hata hivyo kanuni hairuhusu.

Kauli hiyo iliunga mkono na madiwani wa Kiborloni Vicent Rimoy, viti maalum Hawa Mushi na mbunge wa viti maalum Lucy Owenya ambao walisema hawakubaliani na baraza hilo kuleta hoja juu ya hoja.

Kutokana na kitendo cha diwani Lyimo kuendelea kusoma taarifa hizo,madiwani Shayo na Michael walisimama na kutaka meya wa manispaa hiyo kuwapa nafasi ya kutoa taarifa lakini walipoona hawasikilizwi waliamua kutoka nje ya kikao.

“Mheshimiwa Meya nini mnatufanyia hapa……agenda ilikuwa ni moja ya Uhuru Park, hili suala la ujenzi wa madaraja na madarasa linatoka wapi,
Aliongeza”Umesikia yaliyotokea nchini Ukraine!! Acha kusoma hiyo taarifa yako nenda kaisomee katika vikao vya CCM, hamuwezi kutuchezea hapa, hii hoja si mliipitisha ninyi wenyewe, leo yamewafika mnataka kutunyima nafasi ya kuijadili”.

Kutokana na hali hiyo Meya Kaaya aliagiza madiwani Shayo na Michael kutolewa na askari nje ya ukumbi na askari wa manispaa,ambapo walikuja askari Dismas Raphael na Mwasiti Shabani ambao kwa maelekezo ya mwanasheria,Kisa Lyimo waliwatoa nje ya ukumbi madiwani hao huku wenzao wakiwafuata.

Wakati wakitoka nje ya ukumbi,diwani Shayo alivua joho lake na kumtupia meya Kaaya huku akivua kofia yake na kumtupia mkurugenzi Kinabo kwa madai kuwa wanayumbisha na madiwani wa CCM hivyo kushindwa kufuata kanuni na sheria zilizopo.

Kufuatia vitendo hivyo,Meya Kaaya alitangaza madiwani hao kufikishwa katika kamati za maadili huku diwani Shayo akisimamishwa kutohudhuria vikao vitatu vya baraza hilo.

Mapema mwezi Machi kampuni ya DTH iliyokuwa na mkataba wa mika 10 iliomba kupatiwa hati Usu ya kumiliki eneo hilo ili waweze kuomba mkopo huo wa Bilioni 1.5 ili kuendeleza bustani hiyo.

Baadaye wadau mbalimbali wakiwemo wananchi walipinga uamuzi wa madiwani hao huku wengine wakitishia kufanya maandamano ili kupinga hatua hiyo .
mwisho.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. wachaga bana!!! wanagombana hapo badae wanakutana kwenye chibuku lazima kitimu timu kiendelee !!
    na hao wagambo vipi tena jamani huyo mama mgambo ndo wakumtoa mtu nje kweli!! yeye mwenyewe anashangaa

    ReplyDelete
  2. Mh. Michuzi tafadhali tupostie taswira ya Hiyo 'UHURU PARK'.

    ReplyDelete
  3. Haya ndio maendeleo ya kisiasa. Kama Madiwani wakiweza kuzuiya mambo ambayo wanaona hayana faidia kwa jamii, wana haki ya kukataa mikataba isiyo eleweka. Hivi ndivyo kuzuiya ulaji wa KI-RICHMOND

    ReplyDelete
  4. CCM BILA RUSHWA HAIWEZEKANI. HAPA DILI NI KUWA ENDAPO KAMPUNI HUSIKA ITAPEWA ENEO HILO ITAICHANGIA CCM PESA ZA UCHAGUZI.

    ReplyDelete
  5. mmh jamani ktk hiyo halmashauri Ukiuliza manispaa zate au halmashauri zote alizoziongoza huyu mama mkurugenzi Bi Bernadetha Kinabo zinakuwa na maendeleo mazuri sana ! hongera sana mama kwa mafanikio yako!!

    ReplyDelete
  6. Wadau msistuke. Hamna watu waliopigana katika kikao hicho. Baada ya kikao hicho hakukua na uhasama wa kibinafsi. Hizi ni jazba za kidemokrasia tu. Mdau wa hapo juu, ni kweli kuwa B. Kinabo ni mchapakazi. Nasisitiza: madiwani hawakutukanana wala kupigana. They were simply airing their views strongly. Nadhani ndiyo maana mji wa Moshi ni msafi na unaendeshwa vizuri kuliko Arusha, licha ya kuwa mapato ya "jiji" la Arusha ni karibu mara tano ya yale ya Moshi!!!! Hemedi wa mji mpya.

    ReplyDelete
  7. Article imeandikwa kishabiki sana.

    ReplyDelete
  8. nilitaka nije mo-town kugombea udiwani. kama mambo ndo hayo itabidi nitafute bidhaa moja toka tanganyika arms kwanza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...