Na Veronica Kazimoto - MAELEZO
Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Deos Mndeme kuwa Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania kuanzia mwezi Aprili, 2010.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dkt Florens Turuka imesema kuwa, Bwana Mndeme alikuwa kaimu Posta Masta mkuu kwa kipindi kisichopungua miaka miwili.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kabla ya uteuzi huo Bwana Mndeme alikuwa ni mfanyakazi wa shirika hilo kwa muda wa takribani miaka thelathini lililoanzishwa kufuatia kuvunjwa kwa Shirika la Posta na Simu la Afrika Mashariki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 21, 2010

    Hongera kaka sukuma gurudumu la posta mbele!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 22, 2010

    ni matumaini yangu tukituma vitu vitakua salama,tatizo wizi wizi wizi wizi...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...