Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2010

    naona kwenye kichwa cha habari cha east african nuclear giant bids to build power plant in tanzania,safi ila angalieni msije mkawatia kibiriti mama zetu,baba zetu na jamaa kwa kuwapa tender watu feki.na huo muungurumo ni wa generator au???kweli bongo tambarare

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 20, 2010

    kaka MISUPU jamaa kanifurahisha kinoma yaani miaka ishirini bado amekomaa kwenye gemu la uuzaji magazeti safi sana imetulia mno.kuhusu swara la hizo credit cards benki nyingi bongo wababishaji na ni kweli hazifanyi kazi.kuhusu magazeti ya nje tutafanya mchakato wa kumdonoshea hayo magazeti tukishuka bongo.aandae hizo Pounds tu kaka.
    Mdau-Ukerewe!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 20, 2010

    Heri bado uko mjini, kwlei Bongo ina wenyewe.

    Tena umekua mswalihina, safi sana Mungu akubariki.

    Ankal umenikumbusha mbali sana.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 21, 2010

    Sasa naamini Muhidin upo tayari kuanzisha website maana siku izi unatupatia vitu vya live. Vipicha picha na vihabari vya kukopa ndio kazi za blogs. wewe kamua na habari za ukweli toka kwa watu wa ukweli kama uyo ustaadh. Kamwe usituwekee mafisadi.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 21, 2010

    Heri, vipi mambo?

    Mimi nafanya kazi MC hapa marekani na pengine naweza kukusaidia kujua zaidi biashara za credit card.(CC)

    Kwa usalama wa benki na mteja, CC za nchi nyingi ni vigumu kutumika katika internet kwa sababu wajanja wengi hasa Warusi, Mafioso na wengine wanatengeneza au kununua namba au kuiba katika internet na kutumia kununua vitu. Benki yangu inapata hasara ya milioni 30 kwa mwaka lakini wateja wanalipa katika card fees.

    Sijui vipi Tanzania, lakini marekani au canada, nyuma ya kadi una namba ya customer service. Software zetu zinanasa gharama za mteja zinazotoka nje ya nchi uliyopo, zinafikiri umeibiwa. Hapa marekani, wateja wanapiga simu na kulalamika kuwa kadi hazifanyi kazi vile vile. Tunawaomba watupe information zao (security questions) kama tarehe ya kuzaliwa na kathalika halafu mteja anaweza kutumia papo hapo tena. customer care hii ni masaa 24. Nadhani bongo lazima kuna namba ambazo unaweza kupiga ili customer care wakuhudumie, pengine lazima upige nchi jirani, labda Afrika Kusini? Hatuwezi kuruhusu kadi kutumika bila ya namba za simu masaa 24 za customer service nyuma ya kadi. Sisi ndio tunafungua kadi yako ikinasa.

    Kadi za ulaya sasa zina chip ndani na imepunguza sana wizi kwa kuwa lazima utumie kwa kodi ya namba 4 za siri na hata fingerprint katika internet kabla ya kupewa ruhusa kutumika, pengine Bongo vile vile mtapata karibu na kadi yako itakuwa poa. Lakini piga simu kama una simu nyuma ya kadi, ili uhudumiwe mara moja. Umuhimu wa kadi ni kwamba unaweza kutumia duniani kote.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 21, 2010

    Duh kaka michuzi umekumbusha mbali sana huyo Maalim m2 wangu wa zamani sana nilikua naagiza sana magazine za nje za fashions,basketball na hip hop..ameongea ukweli bomba la magazine lilikuwa Aliance Airline those dayz remember sana lkn mbishi bado yupo hapo hapo samora..ila m2 smart sana hana ubabaishaji ukiagiza kitu anakwambia ukweli njoo lini utapata na kweli tuwasiliane kaka tukutumie magazine za huku plzz umeniuzia sana wakati nipo forodhan scul hapo magazine za nje....Mdau westmidland UK

    ReplyDelete
  7. babu michuzi nimefurahi sana kumuona jamaa kakomaa hasa na magazeti mpe salam mimi naitwa agili ahmed au bariadi mtoto muuza nyama maarufu temeke nimesomanae hapo waires temeke mwambie niko oxford anataka magazeti gani nitamfanyia hiyo kazi ila ustadhi kachoka miaka kumi toka niondoke bongo salam zingine kwa juma pinto mwambie timu menage wa tp vita agili anampaa salaam

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 21, 2010

    Du huyu msela long time nilikuwa namuona ame-post up pale salamander anahustle magazines n stuff!....Tip ur hat to that bwoy,OG is a hustler for real

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 22, 2010

    nucler plant ijengwe tz mi nawasiwasi saanaa.
    watanzania niwatu wa rushwa wakileta watu uchwara watatujengea tanuru kosa kidogo dar nzima mtapata mionzi ya nuclear si mchezo chondechonde

    warusi yaliyowapata na wao ni makini sana sembuse watanzania.
    na isiwe ni mitambo iliyochoka wanatafuta sehemu ya kuitupia

    yaha tukaangeni sasa

    ReplyDelete
  10. mambo ya kuwekwa nuclear plant tanzania sidhani kama itakuwa ni kwa manufaa ya watanzania... kinachonishangaza serikali yetu imeshindwa kuanza kutatua masuala ya muhimu kwa jamii kama afya, miaka nenda rudi watanzania wanatibiwa nnje ya nchi kwa gharama kubwa, ambazo zingetosha kabisa kufungua vitengo vya kupandikiza figo, operesheni za moyo, hata joint replacement surgury.. cha kusikitisha hata vipimo vinavyoweza kupima kiwango cha dawa mgonjwa anayoitumia ktk mwili ili isiweze kumletea side effects au kutengeneza sumu mwilini hakuna mpaka mgonjwa apelekwe india au nchi nyingine..dialisis yenyewe hapo mhimbili ni taabu kwelikweli.. mpaka regence au agakhan. tumeshindwa kufungua vituo katika hospitali za rufaa kama KCMC, Bugando, Mbeya referal ili visaidie wananchi wanaoteseka kutokana na magonjwa amboyo mengine yanasababishwa na madawa feki au overdose au magonjwa sugu.. mfano Blackwater fever inayosadikika kuwa ni complication ya Quinini ktk mgonjwa wa malaria na kusababisha kufeli kwa figo hivyo mgonjwa kuhitati suportive management kama dialysis ambayo kuipata tanzania ni taabu kwelikweli.. hao wazee wanaokalia na kutotekeleza mahitaji kwa wananchi wake lazima siku moja yatawakuta kwani magonjwa mengi wanayougua kama kisukari, presha hata gaut hupelekea kufeli kwa figo na madawa wanayoyatumia kwa muda mrefu yatawarudi..ni lazima kufumbua macho na kufanya mambo sasa..
    pesa ya tanzania inaporomoka kila siku mi sijui taunaafanya nini HATA TOOTHPICS NA TOILET PAPERS ZINAAGIZWA NCHI ZA NJE.... sasa hii imezidi jamani.. madini yote serikali inachukuwa asilimia tatu mrahaba.. hata anayechimba kokoto analipa asilimia tatu mrahaba sasa viongozi wetu hawajui tofauti ya dhamani kati ya kokoto na tanzanite au gold au almasi? hii ni noma.. kampuni inayochimba tanzanite merereni haijawahi kulipa kodi kila kipindi inapewa miaka mitano ya expedition na inabadilisha majina kila kipindi... ilianza SAMAX,then AFGEM then tanzanite one,sasa ni tanzanite expedition. madini inayoyachimba dunia nzima hakuna pengine wanachimba lakini mtanzania hajafaidika na rasilimali za nchi yake sijui mbunge wa simanjiro anafanyanini bungeni au naye anaasilimia yake? au viongozi wa serikali ya kijiji na hata TRA.. je hiyo nuclear plant nani atafaidika nayo? kama kweli serikali inania njema ni bora wangefungua kiwanda cha kusafisha mafuta kama ilivyokuwa TIPA, tuweze kupunguza bei za mafuta na tutafaidika zaidi, na ajira zitapatikana na maisha bora kwa mtanzania yatapatikana. wabongo poleni kwa mgomo wa vituo vya mafuta serikali iliyopo imara ingetakiwa kuvifutia leseni vituo vyote vilivyogoma.. sasa sijui vituo vinavyomilikiwa na viongozi wa ngazi za juu serikalini itakuwaje...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...