THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

UJUMBE KWA BENKI YA NMB TAWI LA MOROGORO ROAD

Kaka Michu,
Naomba unifikishie ujumbe huu kwa
waheshimiwa wa NMB tawi la Morogoro road.

Mimi ni mteja katika tawi hilo.
Kwa kuwa siku hizi huduma ya ATM imepamba moto siku nyingi nilikuwa sijaingia ndani ya tawi hilo. Juzijuzi kadi ikaanza kusumbua hivyo leo 26/05/2010 nikaamua kwenda kuripoti tatizo.
Nilivyoingia ndani nikashangaa sana. Ground floor yote ni counters tu, hakuna ofisi wala ofisa wa kusaidia wateja. Mimi kwa bahati mbaya/nzuri ni mlemavu natembea kwa msaada wa cluches. Customer care yao wameihamishia mezzannine (kama siyo first) floor.
Any way nilijitahidi kupanda kitu kingine kibaya nilichokutana nacho ni kwamba ngazi haziko friendly designed ziko so steep. Kulikuwa na uwezekano mkubwa sana wa kuteleza na hata kuvunjika mikono.

Ushauri wangu ni kwamba kuwe na ofisi japo moja ground floor kwa ajili ya watu kama mimi. Wapo watu wanaotembea kwa wheel chair na wazee ambao hizo ngazi hawawezi kupanda, je? wao sio wateja?
Nawasisilisha,
Mdau Mkereketwa


Kuna Maoni 20 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Noted for compliance!

  SHYROSE BHANJI

 2. KILO Anasema:

  VERY GOOD POINT.....next time usiweke account number yako, huwezi jua maana bongo kwa visasi unaweza kuta account yako imepotea!!

 3. Anonymous Anasema:

  Why would I care to consume Tanzanian Products while the very producers don't care about the consumers? Why would i care to be a Tanzanian while the government and fellow citizens don't even care about their own people and colleagues? Upumbafu wetu umetufikisha hapa!! Mungu Ibariki nchi yetu ya daraja la tatu na produce zetu zilizopo daraja hilo hilo.

 4. Anonymous Anasema:

  Da, pole sana ndugu yangu kwa yaliyokukuta, huo utaratibu wao haufai kabisa ni bora waweke ofisi hata moja kwaajili ya wateja floor ya chini kuna wagonjwa kama ulivyosema au watu wa namna yako, wao hawana nafasi ya kupata huduma katika benki hiyo? wafunge akaunti zao?

 5. Anonymous Anasema:

  Na huu uwe ujumbe kwa maofisi mengine yote nchini.

 6. Anonymous Anasema:

  LABDA NAANZA KUWA KIPOFU, KWANI MIMI SIJAONA MAHALA HUYU MDAU AMEWEKA AKAUNTI NAMBA YAKE, KAMA MDAU ANVYOMSHAURI HAPO JUU. HII NI SWALA LA WIZARA YA USTAWI WA JAMII INATAKIWA KUPITISHA SHERIA ITAKAYOWAAMURU WATU WOTE WANAOFANYA SHUGHULI NA JAMII KUZINGATIA MATWAKWA YA WENZETU HAWA, NA IWE NA MENO WASIPOFANYA HIVYO BASI KUWE NA ADHABU, HII IWE HATA KWENYE USAFIRI NA MAHALA POPOTE PALE PANAPOTOWA HUDUMA KWA JAMII

 7. Anonymous Anasema:

  Akauti namba ilikuwepo, ni vizuri Michuzi ameiondoa mapema.

  Wazo zuri sana...laiti kama wale wote wenye kero wangekuwa wanalalamika kwa ushahidi namna hii.

 8. Anonymous Anasema:

  Mdau ametoa maoni haya kuhusu NMB lakini nchi ina tatizo kubwa sana la kutofikiria walemavu katika usanifu wa mambo mengi, sio maofisi tu. Hata njia zetu za waenda kwa miguu hazirahisishi maisha kwa anayetumia baiskeli ya walemavu. Hakuna maegesho maalum kwa walemavu ili kuwapunguzia umbali wa kufika maofisini nk.

 9. Anonymous Anasema:

  Ujumbe Huu ni kwa ofisi zote zisizojali baadhi ya watu

 10. Anonymous Anasema:

  Ujumbe Huu ni kwa ofisi zote zisizojali baadhi ya watu

 11. Anonymous Anasema:

  Hawa NMB nadhani imefika wakati waamue moja tu kupunguza wateja na aina za wateja kulikono kuendelea kufanya kampeni ya kuongeza wateja wakati huduma zao haziendi sambamba na ongezeko la wateja. Pia nawashauri wawapeleke training mara kwa mara watu wa Huduma kwa wateja kwani ukweli ni kwamba wengi wanaokaa pale ni wale wenye stashahada au shahada za Banking, Accounting,commerce au business adminitration tu lakini sio qualified customer care persons ndio maana pale unaweza kwenda kwenye desk lao kisha ukajutia ni kwanini ulikua mteja wa benki yao.Kuna rafiki yangu mmoja alitaka kufungua akaunti pale Mlimani city akapewa form ya kufungua akaunti akajaza vizuri, kapeleka picha na barua ya serikali za mitaa alipofika pale akakataliwa kufungua account ati barua ya serikali za mitaa imeomba apewe ushirikiano NMB lakini haikusema NMB tawi gani,yaani haiku address NMB MLIMANI CITY hii kutotaja MLIMANI CITY kwenye barua yake ya serikali za mitaa ikamkosesha kufungua account siku hiyo hadi jamaa atakapoleta barua nyingine inayoaddress NMB MLIMANI CITY! kwa hasira jamaa akaona isiwe tabu akatoka akaenda zake benki ya ushirika na maendeleo vijijini! Sasa ukiangalia hapo utaona kuna ka percentage flani ka profit NMB wamepoteza kwa kumkosa huyu mteja kutokana na Customer care desk(CCD) kufanya kazi kwa mazoea. Tubadilike jamani CCD sio NMB tu benki zote. Punguzeni huo msemo wenu wa "hivi ndivyo ilivyo" badala yake "use the principles and sometimes common sense" sio routine tuuu kila siku.

 12. Anonymous Anasema:

  Shyrose!
  For that comment you deserve to there, thank you. Very few manager admit mistake and respond to change.

  I call other to learn from that girl. Big up. Sio mtu anaambiwa anavimba mdomo na kuanza jeuri.

  Jamani wa kiswaili, Dada huyu anastaili kuwepo hapo alipo kwani anajua anachaofanya.

  Asanten. Michuzi nawe ubarikiwe kwa kablog kako haka. Mimi mdau wako sana hapa sweden japo unabana tucomment twangu.

 13. Michelle Obama! Anasema:

  Naungana na mdau hapo juu kumpa big up da Shyrose! Manake kwa tabia zetu bongo navojua angelalamika hapo ofisin kwa hao kina dada customer service angebinjuliwa midomo mpaka ashangae mwenyewe! makarani wa benki bongo punguzeni nyodo! hiyo ni biashara kama biashara ingine yoyote na bila kuwa na wateja hata nyie kazi hamna! Da Shyrose hivi huwa mnawapa kozi mara kwa mara hao customer service wenu? they really need to be reminded frequently to do their job!
  thanx.

 14. Anonymous Anasema:

  SHY ROSE BANJI: sijui kama huyajui matatizo ya NMB au nawe ushkuwa mtu wa siasa sasa. Hili linalosemwa la ofisi ya huduma kwa wateja kutokuwepo chini ni moja tu, la pili ni kukosekana kwa sehemu za haja (vyoo) sijui kama ni sera za mabenki. Hata kama vitakuwepo nashani hata kwenye ofisi nyingi ni vya kibaguzi (havijui kuna walemavu.

  Inafafana na ile milango inayozunguka kama pale International House ambapo hakuna kwa kupita mlemavu....

  NMB kwa ujumla huduma kwa wateja ni zero kabisa kwa sasa ni afadhali hata Benki ya Waalimu ya "Sidanganyiki" (TPB) wameboresha huduma zao.

 15. Anonymous Anasema:

  We unayesema bank ipunguze watena are you serious...Nani anajukumu hilo? Ni wewe mwenyewe..usijali matangazo bali jali huduma hupendi huduma za mahali fulani funga account yako hapo fungua kwenye bank nyingine yenye huduma nzuri.

  Bongo hawajui kuwa mteja ni mfalme. Wanatreat wateja kama vile sijui nini wakati kama sio wewe mteja hiyo huduma yao isingeweza kuendelea.

  Inabidi watu wajifunze..Huku tuliko wenye kutoa huduma wanatulamba miguu na ukilalalmika tu ukaacha contact information zako watakupigia simu na kukubeembeleza na hata kama ulinunua kitu utarudishiwa hela yako na kam ani huduma za bank wamekucharge hovyo watakuomba msamaha na kama kunakitu walikosea watakurudishia zote na fees zilizoingia kutokana na hiyo transaction. Yote hiyi ni kunifanya niendelee kuwatumia hao.

  Tanzania wanazania wakiwa na mteja mammilionear wawili basi wasio na hela nyingi hawawataki kumbe hawajui kidogo kidogo hujaza kibaba. Kila mteja ni faida

  Tujifunze kutumia power zetu mtu anakutreat vibaya hama

 16. Anonymous Anasema:

  Am very shocked!! Inakuwaje kampuni inafungua benki na kupitishwa kuhudumia wananchi bila kuwa na sehemu ya WALEMAVU??? AMERICANS CALL IT "ADA" AMERICA DISABILITY ACT- THIS MEANS ALL THE FINANCIAL INSTITUTIONS MUST HAVE A SPECIAL COUNTER FOR DISABLED PEOPLE!! THIS WOULD HAVE BEEN A JUICY LAWSUIT IN AMERICA!!! Ndo maana wenzetu wa nchi za majuu wako juu siku zote na wanamaendeleo. TZ twatia huruma sana-wananchi wananyanyasika hadi sehemu wanazo weka hela zao jamani??? kweli TZ imefikia pabaya sana!! am so sorry to hear that! Duu!

 17. Anonymous Anasema:

  mimi niliwahi kuchana barua ya mtendaji mbele ya mhudumu wa benki ya muleba nmb kutokana na maswali ya kijinga nilichomwambia kuwa hela si zangu naondoka nazo

 18. Anonymous Anasema:

  Mimi natoa lawama kwa vyama na vikundi vya walemavu. Moja ya kazi zao ni lobbying ili vitu vifanyike kwa kuwajali wao pia. Ni wao wakuwabana wadau watekeleze majukumu yao. Waajiri wengi utakuta kwenye nafasi za kazi wanasema wanatoa nafasi za upendeleo kwa wanawake wakati wanatakiwa watoe nafasi za upendeleo kwa vilema pia. Muanzishe aina ya certification kwa mashirika na asasi zinazowajali walemavu, mnawapelekea vigezo vyenu na atakaevifanikisha mnampa haki ya kutumia nembo yenu kwenye matangazo na bidhaa zake kama wanavyofanya UK.

 19. Anonymous Anasema:

  MICHUZI NA MDAU ALIYETUMA MADA NAWASHUKURU SANA,YANI ME MWENYEWE KWELI NMB MOROGORO RD, WAMENIBOA SANA KUNA SIKU NIMEENDA KUDEPOSIT CHEQUE YA BOSS WANGU,KWANZA NIMEPELEKA NIKAAMBIWA MPAKA UPELEKE UKAGONGE MUHURI HUKO JUU WANAPOSEMA FLOOR YA 1,NIMERUDI KUJA KUPANGA FOLENI TENA NAAMBIWA MUDA WA KUPOKEA CHEQUE UMEISHA MPAKA KESHO JAMANI KWELI HII NI HUDUMA?ALAFU HAO WADADA SASA WANAVYOKUANGALIA KWA DHARAU,YANI WANAONA MTU UKIENDA PALE HUNA UNALOLIJUA WAO NDIO WAO,MSIWE HIVYO SISI NDIO TUNAOWAWEKA HAPO JAMANI,YANI HAWATAKI KUKUBALI KAZI ZAO,KWASABABU MTU KAMA UMEIKUBALI KAZI YAKO ALWAYS YOU HAVE TO SMILE NA UWAHUDUMIE WATEJA WOTE SAWA HATA KAMA UNAMATATIZI YA NYUMBANI KWAKO,PALE WEKA KANDO,YANI MTU ANGEPATA KUJA KUNIONA OFICE KWANGU ME NI RECEPTIONIST KWELI UNGEFURAHI SANA,DADA SHYROSE WW UMKARIMU SANA TUONMBA UWE UNAWAPA DARASA HAO WANAWAKE WENZIO SIO WAWEWANANUNA TU KILA MTU WANAMDHARAU,NA HII SIO KWA NMB PEKEE,NBC NA BENKI ZINGINE ZOTE

 20. Anonymous Anasema:

  Nashauri NGOs pamoja na serikali zifanye jitihada kuwafunza architects/ building designers kuhusu michoro inayokubalika kwa walemavu wote. Nashangaa Manisipaa na serikali zinapitihs michoro hiyo bado. Nilifurahishwa sana na majengo na miundo mbinu ya Mzumbe University jinsi inavuojali walemavu. Au ni kwa kuwa misaada ilitoka Norway/NORAD?. Watanzania tubadilike, miaka 50+ ya uhuru sasa.
  Richard Mazingira