Habari zilizoingia sasa hivi kutoka eneo la Mbwewe mkoani Pwani muda mfupi uliopita ni kwamba kuna ajali ya ndege ndogo ya Jeshi yenye namba 9119 ambayo imegongana na gari la watalii la kampuni ya african tours, baada ya kutua kwa dharura katika barabara kuu ya Dar-Arusha.
Habari zinasema rubani aliamua kuishusha barabarani baada ya kupata matatizo ya kiufundi wajkati ikiwa katika mruko wa kawaida wa mazoezi. Hivyo baada ya kutua barabarani ndege iliivaa gari hiyo ya watalii ambalo lilipinduka.
Inasemekana rubani ameshaondolewa ndegeni wakati juhudi zinafanywa kuondoa abiria wawili walionasa kwenye ndege hiyo hivi sasa. Hali ya rubani inasemekena ni ya kukatisha tamaa. Hakuna aliyekufa kwenye gari ya watalii.
Vikosi vya dharura vya Jeshi la Ulinzi na polisi viko eneo la tukio hivi sasa, na kipaumbele ni juhudi za kuisogeza pembeni ndege hiyo ambayo kwa sasa imeziba kabisa barabara na kusababisha foleni ndefu kila upande wa barabara hasa wa mabasi ya abiria na malori ya mizigo yanayohudumia barabara ya Dar-Arusha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Duh Bongo noma. Ajali kila sehemu, barabarani, majini, sasa ni "colabo" ndege zinaanza kugonga magari!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 29, 2010

    mdau umeniacha hoi,colabo sio,duh,michuzi yani comment za humu

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 29, 2010

    yep!!!that's africa anything its possible falling plane from the sky like rain kweliiii God's must be crazy in africa......waiting for falling snow..no worry in africa....edwin urasa

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 29, 2010

    tuleteeni picture mkiweza...
    mdau,
    USA

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 30, 2010

    Ajali za ndege kugonga magari sio kitu kipya, kwa sababu huku U.S. hutokea pilot aki lose engine, anatua kwenye highway kwa sababu airport iko mbali. Ni tukio jipya kwa huko Tanzania. Imeshatokea Texas, na hata Illinois, actually Chicago Midway Airport ambapo jet ya Southwestern ili over shoot ni kugonga fence na kusimama barabarani baada ya kugonga gari. Ni ajali, lakini sio kitu kipya.

    ReplyDelete
  6. Colabo.
    mani umeniacha hoi

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 30, 2010

    kwaa kwaaa eeh mdau umechizi ati collabo

    ReplyDelete
  8. ShuShuShuJune 30, 2010

    We Anony ndege kutua barabarani wala sio kitu kipya hapa Tanzania.

    Miaka michache iliyopita ndege ndogo ilishawahi kutua barabarani Dodoma njia Kuu ya Dodoma/Dar, kilomita chache kabla ya kufika Kiwanja cha ndege cha eapot ya dodoma, lakini haikuleta madhara.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 30, 2010

    colabo!
    duh!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...