sehemu ya ndege iliyopata ajali baada ya kutua barabarani kwa dharura na kugonga basi la watalii ambalo linaonekana juu kushoto likiwa limeanguka
askari wa jeshi la ulinzi na polisi wakiwa eneo la tukio

msururu wa magari yaliyokuwa barabarani

Askari wawili ambao ni marubani wa Jeshi la Wananchi Tanzania wa Kambi ya Ngerengere ya Morogoro, wamekufa baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kutua barabarani kwa dharura na kugonga gari la watalii na kupinduka jana katika eneo lijulikanalo kama Zimbabwe katika kijiji cha Manga wilaya ya Handeni, Mkoa wa Tanga.

Katika basi la watalii inasemekana kulikuwa na watu 24 ambao 19 kati yao ni raia kutoka Uholanzi, wanne kutoka Kenya na mmoja Mtanzania. Wote walinusurika kufa.

Inasemekana kuwa marubani hao walikuwa katika mazoezi ya kawaida katika anga ya eneo hilo, na kwamba wakati ikiwa angani ndege ilipata hitilafu ndipo rubani akaamua atue barabarani ili kuokoa maisha yao, kabla gari hiyo ikiwa kwenye mwendo mkali iliigonga.

Ndege hiyo ndogo ya JWTZ yenye namba F59119 ilikuwa inatumika katika mafunzo ya kijeshi. Kaimu kamanda wa polisi mkoani Tanga, Afande Jafari Mohammedi, aliwataja waliokufa kuwa ni rubani wa ndege hiyo Meja Kathbet Leguna (41) na mwanafunzi wake Luteni Andrew Yohana Kijangwa (31).

Taarifa zinasema Meja Leguna alikuwa ni mwalimu wa mafunzo ya ndege za kivita katika kikosi hicho cha Ngerengere na alikuwa anamfundisha urubani Luteni Kijanga.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 30, 2010

    hakuna kitu kiguma katika urubani kama kutua ndege ikiwa salama. To paly with an altitude is another shock.
    Mdau Mbije,A

    ReplyDelete
  2. Afande Mwamunyange, "JAMBO AFANDE".

    Afande kwa kweli haya ma JET FAITA asas yameshachoka mnunue mengine.

    We toka Vita vya Kagera vya Idd Amini mpaka leo?
    Kama ni mtu keshaoa na familia yake sasa.
    Halafu teknolojia imeshabadilika sana mno tu. Nunueni mengine Afande.

    JAMBO AFANDE.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 30, 2010

    Exclusive? Maana yake ni nini kwa hapa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 30, 2010

    jamani wafiwa poleni sana wa tz wenzangu kumbuka kwenye ndege kuna emegence place za kutua moja wapo ni barabarani

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 30, 2010

    HAPO SIJUI TUSEMEJE SASA! HIYO NDEGE YA LINI? NA SERVICE YA MWISHO IMEFANYIWA LINI? MAANA TUSIJE TUKAWA MASHOHORO WA KAFARA ZA UCHAGUZI! WATCH JAMA OOH.....

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 30, 2010

    hao wajamaa wenye vikofia nyekundu na magitaa yao ?Si akina nanii?ras naniini? sasa katika ajali wao na magitaa ya hatari hatari vipi tena?

    ReplyDelete
  7. oh my god
    meja kathbet leguna ameacha mtoto mdogo sana,second one.na alikua tegemeo sana,si la familia yake tu hata ndugu wote mpaka kijijini huko.
    yani ni pigo lisilosahaulika hata mwisho wa dunia.
    MAY YOUR SOUL REST IN PEACE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...