TAARIFA KWA VYOMBO HABARI

.NATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE MBEYA MJINI KUPITIA CHADEMA

· NATOA TAMKO RASMI KUHUSU KUHOJIWA KWANGU NA POLISI

Mimi, Joseph Mbilinyi ambaye najulikana zaidi katika anga ya muziki kama “Sugu” ama “Mr II” leo tarehe 29 Juni 2010 natangaza rasmi nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kwa muda mrefu katika maisha yangu ya kimuziki pamoja na kuimba nyimbo za kuburudisha nimekuwa zaidi mstari wa mbele kuimba nyimbo za kutetea haki za makundi mbalimbali katika jamii na taifa kwa ujumla.

Wakati umefika sasa wa kuhamisha jukwaa la mapambano ya kudai haki kutoka jukwaa la muziki mpaka jukwaa la siasa kwa dhamira ile ile ya kutumia kipaji changu alichonijalia Mwenyezi Mungu kuimba na kuhutubia kwa ajili kuleta mabadiliko ya kweli katika taifa letu.

Nyimbo zangu zimekuwa zikibeba sauti ya watu wasio na sauti ili zisikike na watawala; lakini hata hivyo kwa kipindi chote ambazo nimekuwa nikifanya harakati hizi watunga sheria na wafanya maamuzi ya kisera chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameshindwa kuongoza vizuri taifa kuweza kufanya mabadiliko ya kweli yenye kuhakikisha watanzania wananufaika na vipaji vyao ambavyo Mwenyezi Mungu amewajalia na taifa linanufaika na rasilimali na maliasili ambazo tumejaliwa kuwa nazo.

Hivyo natangaza nia ya kugombea ubunge ili kuchangia katika kuongeza nguvu ya chama mbadala katika Bunge letu; niwe sehemu ya sauti mbadala katika kutunga sheria, kuwawakilisha wananchi, kuandaa sera na kuiwajibisha serikali kuweza kutekeleza yale ambayo mimi na wanaharakati wenzangu katika sanaa tumekuwa tukiyapigia kelele muda mrefu kupitia muziki wetu na maisha yetu.

Uamuzi wangu wa kugombea ubunge Mbeya Mjini ni haki yangu ya kikatiba na natambua kuwa kwa kuwa mbunge nitafanya kazi ya kuwawakilisha wananchi wenzangu na kama ambavyo wakati wote nimekuwa nikipambana katika harakati mbalimbali ndivyo ambayo nataka niwe mstari wa mbele kupambana katika kuleta maendeleo.

Huu si wakati wa kampeni hivyo niwaahidi wananchi wa Mbeya kwamba nitaeleza mengi kuhusu sera zangu na ahadi zangu kwao mara baada ya kupitishwa na CHADEMA kugombea ubunge katika jimbo letu.

Hivyo, nachukua fursa hii kuwajulisha watanzania wenzangu kwamba siku chache sijazo nitachukua fomu ya chama ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini.

Lakini kwa ujumla uamuzi wangu wa kugombea umesukumwa na harakati zangu za miaka mingi na ufahamu wangu kuhusu hali halisi ya maisha yetu wananchi wa Mbeya Mjini.

Natangaza nia ya kugombea nikiwa ni mgombea mpya kutoka chama mbadala ili kushirikiana na wananchi wenzangu wa Mbeya Mjini kuondokana na siasa za makundi, ukabila, ubaguzi, na migogoro ambazo zimekuwa zikitawala katika Jimbo letu na Mkoa kwa ujumla na hatimaye kusababisha tuwe na uongozi mbovu unaokwamisha maendeleo.

Jiji la Mbeya linakabiliwa na ubovu wa barabara ukiondoa barabara kuu inayokwenda Tunduma; barabara za mitaani ni mbovu wakati ambapo kuna fursa ya kuwa mkoa wenye makaa ya mawe ambayo mabaki yake yangeweza kutumika kukarabati barabara za mitaani Uyole, Soweto na kwingineko.

Natambua kwamba wafanyabiashara wa Mbeya Mjini wanamalalamiko mengi kuhusu kubambikiziwa kodi huku wafanyabiashara wadogowadogo wakiwa wananyanyaswa katika maeneo wanayofanyia biashara kwa kuwa hata mimi mwenyewe nimewahi kuwa mfanyabishara katika soko letu la Mwanjelwa.

Natambua kwamba jiji letu la Mbeya ni kitovu cha elimu katika mkoa wetu hata hivyo lugha zinazotolewa na uongozi wa Mkoa zinawadhalilisha walimu wakati uongozi huo unashindwa kuweka mazingira bora ya elimu na kusababisha Mbeya mjini kuanza kudorora kielimu. Kwa upande mwingine, kadiri mji unavyopunuka ndivyo kero ya usafiri wa wanafunzi inakithiri na shule za pembezoni zinakosa walimu.

Natambua kwamba kwa muda mrefu Mbeya Mjini yetu ina kero ya umeme wakati ambapo tupo jirani na Mgodi wa Kiwira ambao ungeweza kuzalisha umeme wa kututosheleza lakini kutokana na ufisadi tunashindwa kuondokana na hali hii ambayo inasababisha ugumu na kupanda kwa gharama za maisha na kukosa taa za barabarani hali ambayo inaweka mazingira ya kuongezeka kwa uhalifu.

Natambua kwamba viwanda vyetu vya Mbeya Mjini vimeuzwa kwa bei chee na vingine vimeshindwa kuendeshwa na kubaki magovu na kusababisha vijana kukosa ajira na uchumi kuathirika kama ilivyokuwa kwa viwanda vya pamba, mafuta na nyama.

Natangaza nia ya kugombea ubunge wa Mbeya Mjini kwa kuwa naamini kwamba kero ya maji inayotukabili inaweza kuondolewa tukiwa na uongozi mbadala ambao utaweza kutumia vyanzo mbadala vya maji kama mto Mzovwe, Ivumwe na kutoka katika Mlima Igamba.

Natangaza nia ya kugombea Ubunge ili pamoja na kuingia bungeni niweze kuingia katika halmashauri ya Jiji la Mbeya nishirikiane na wananchi wenzangu kuibua ufisadi na udhaifu iliopo unaosababisha ubadhirifu wa fedha za wananchi na mali za umma kama ilivyotokea kwa milioni 68 zilizobaishwa kwenye ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2007/08; tuhuma za kutaka kuuza kiwanja cha wazi eneo la Sokoine na kushindwa kulipa fidia wananchi wa Kata ya Kalobe waliondolewa katika viwanja vyao.

Wakati huo huo; napenda kuchukua fursa hii kuwafahamisha wananchi wenzangu wa Mbeya Mjini, wapenzi wa muziki wangu, wanachama wenzangu wa CHADEMA na watanzania kwa ujumla kwa jana tarehe 28 Juni 2010 nilikamatwa na polisi kwa kile walichonieleza kuwa kuna malalamiko dhidi yangu kuwa nimemtishia kwa maneno kumuua Ruge Mutahaba kupitia wimbo uitwao “Wanna Kill” uliopo kwenye album iitwayo “Anti Virus”.

Walinikamata saa 5 asubuhi nikiwa naingia ukumbi wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa ajili ya kutoa Mada kuhusu “Tathmini ya Muziki wa Kizazi Kipya na Hatma yake nchini” na kunihoji kwa takrabani masaa matano mpaka saa 10 jioni.

Wameniachia kwa kile walichonieleza kuwa ‘dhamana ya kujidhamini mwenyewe’ na kunitaka niripoti kwao siku ya jumatano tarehe 30 Juni saa 5 asubuhi siku ambayo nilipanga kwenye ratiba zangu kurejea nyumbani Mbeya Mjini kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge kabla ya tarehe ya mwisho ya utoaji na upokeaji fomu ndani ya CHADEMA.

Katika mahojiano nao yaliyofanyika Makao Makuu ya Upelelezi Wizara ya Mambo ya Ndani; maofisa usalama (CID) walionihoji walirejea mstari mmoja katika kiitikio cha wimbo husika wenye maneno “I Wanna Kill Right Now” na kusema kwamba mlalamikaji ameutafsiri mstari huo kuwa ni tishio la kutaka kumuua.

Napenda kuwajulisha mashabiki wangu na watanzania wenzangu kwamba nimelieza wazi jeshi la polisi kwamba hakuna wimbo wala maneno niliyowahi kutamka kwa lengo la kukusudia kumuua binadamu yoyote. Niliwaeleza jeshi la polisi kwamba sanaa ya muziki inalugha zake zake za kifasihi.

Maadhui ya wimbo mzima yamejikita katika harakati zangu za siku zote za kupambana na wanyonyaji dhidi ya maslahi ya wasanii Tanzania na wimbo huo una maudhui ya kutaka “Kuondoa ama kuiua dhamira ya mbovu na nia zao ovu”.

Ni vyema mashabaki wangu, wanachama wenzangu na watanzania kwa ujumla wakarejea katika Kamusi mbalimbali za kimataifa ambapoo neno KILL linamaana zaidi ya 10 zikibeba pia maana ya KUKOMESHA, KUONDOA nk.

Katika wimbo huo nimeghani kwa kutumia fasihi mambo ya ukweli yanayotokea katika sekta ya sanaa na wala hauna dhamira yoyote wala maudhui ya kufanya kosa lolote la jinai; hivyo kama kuna mtu ameguswa na ukweli uliomo katika wimbo huo na hakubaliani nao basi aupinge kwa hoja ama akafungue madai badala ya kukimbilia kutaka kuliingiza jeshi la polisi kwenye masuala ya sanaa.

Aidha nimeshangazwa na hatua ya jalada hilo la polisi kufunguliwa ndani ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Wizara ya Mambo ya Ndani yaliyopo Wilaya ya Ilala wakati mimi na mlalamikaji wote ni wakazi wa Wilaya ya Kinondoni.

Baada ya maelezo niliyoyatoa ni matumaini yangu kuwa jeshi la Polisi ambalo lina kazi muhimu zaidi ya kukabiliana na ujambazi na vitendo vingine vya uhalifu ambavyo vinazidi kuongezeka katika Mkoa wa Dar es salaam ambapo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi yapo litaelekeza nguvu zake katika kukabiliana na vitendo hivyo vya makosa ya Jinai badala ya kupoteza muda wake kushughulikia masuala ya kifasihi ambayo yanasura ya madai yasiyo na uzito wowote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 51 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 29, 2010

    Mr. Sugu,
    Angalia facebook inbox yako. Nipo tayari kukusaidia kwenye kampeni yako mkuu, huu ni mwaka wa vijana haya majambazi tunayamaliza moja hadi mwingine

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 29, 2010

    Jumba bovu hiloooo...

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 29, 2010

    Nakusapoti Mr.II ili wabunge vijana wenye uchungu na nchi hii watuletee maendeleo.
    Michuzi Blog mko juu ila usiibanie hii.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 29, 2010

    Mh Sugu
    the mission is good,just make sure you have a good team for compaign,i would suggest Mfalme Sele to lead your compaign team,iam read to support you in anycase.GO SUGU GOOOOOOOO

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 29, 2010

    Nimekubali wewe sugu! Hutetereki hata wakitumia zana za Kiporisi?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 29, 2010

    haongera kaka kwa uamuzi uliofikia wa kutumia vyema haki yako ya msingi kikatiba tunakuunga mkono Tanzania itajengwa na watanzania wenye moyo na machungu na nchi yao go sugu go

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 29, 2010

    Bwana Hu Jintao, mwaka wetu huu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 29, 2010

    mbona huyu kijana anahangaika sana na maisha???kwa kipi hasa mpaka awe mbunge???bongo fleva au???

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 29, 2010

    ..Ishu ya malaria, ishu ya malaria NANI ALIIANZA?..

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 29, 2010

    tupo pamoja sugu kuondoa unyonyaji

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 29, 2010

    Watanzania mkimchagua Sugu mm ndo ntaamini tumekwisha kabisa..jamani kiongozi si umaarufu...we need talent on him....ask ur self..hw many graduates who got potentials to lead are there...are not getting chance because ar nt popular..huh!...thats right....wabongo angalieni..ataenda fanya nn huyu bungeni..kuimba mistari during lunch time or what...find somebody who can handle the position not just popular..kha!
    Mdau.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 29, 2010

    Sawa Sugu naona maelezo mareeefu, na nina hakika utapata wa kukuunga mkono. Hata hivyo naomba nikuulize kwamba shule ulishamaliza? Kuona matatizo ni hatua moja, lakini utatuzi pia utatokana na elimu inayoweza kutupa mwanga wa hatua za kuchukua. Wewe ulipata bahati ya kuishi Uingereza na Marekani, huko kote hukupata shule? Utawahamasishaje wengine kutafuta elimu kama wewe mwenyewe uliishia kubeba mabox tu huko? Kila la heri.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 29, 2010

    haya twendeni tu.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 29, 2010

    sugu mimi ni kijana kama wewe, na ninapenda sana mabadiliko, lakini nakushauri kama unataka mabadiliko ya kweli basi na wewe uwe na busara, natumaini unayo lakini kusema ukweli ule wimbo wako hauna uelimishaji wowote, mimi sitaki kabisa hata watoto wangu wausikilize, maana umetumia kiswahili fasaha chenye matusi na kashfa, kama ulikuwa na bifu na Ruge, watangazaji wengine wa Clouds walikukosea nini?? hakuna kipengele kilichoniuma kama kusema "Kibonde anaeneza ngoma" una vithibitisho anao? na hata kama anao, una haki gani ya kumtangaza wakati yeye hajajitangaza, kuita wanaume wenzio mashoga, ulishalala na hata mmoja wao au una ushaidi gani, hukutumia busara, na siku zote kiongozi ni mfano wa kuigwa, kama unataka kusaidia vijana, jaribu kuwa smart kwanza, (sio mavazi) kuna vijana kama wakina MO, Jerry Silaa, wanafanya kazi nzuri, hawaropoki kama wewe na wimbo wako. ur wrong man. jisafishe kwanza kabla hujasafisha wenzio.
    huo ni mtazamo wangu na mawazo yangu finyu. thx Misupu kwa updates.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 29, 2010

    Hotuba ya kutangaza nia yenyewe inajikanganya hata kabla hujaanza kuhutubia wananchi wakati wa kampeni. Hivi muziki umekushinda mpaka unaenda kwenye siasa? Nani sasa ataghani mashairi ya muziki kama kila mmoja anatimukia kwenye siasa? Haya Mr. Sugu, safari njema. Acha visingizio kwamba umetakiwa uripoti polisi siku amabyo ndiyo ya mwisho kuchukua form za ubunge. Je siku zingine zote ulikuwa wapi? Umeiingia kwenye chama juzi, leo ubunge! Je wale waliokuwemo muda mrefu? Nadhani ungelisubiri mwaka 2015 utakuwa umekomaa kisiasa.
    Mdau,
    Mbeya mjini

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 29, 2010

    Tatizo la nchi hii ni kwamba kila kitu kimechakachuliwa kuanzia jumba jeupe pale magogoni,polisi na watawala wote nchi hii wote wamechakachuliwa na mtindo wao ni chakachua tu;ndio maana wameikalia tu cheap politike asubuhi na mapema yote upuuzi mtupu yaani bifu la Sugu na hiyo redio ya propaganda ya waganga njaa wa mjini mpaka ikulu nayo inashughurika!!!?....upuuzi mtupu....hivi hamna kazi muhimu za kufanya za kitaifa?

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 29, 2010

    Kuna somo kubwa sana la kujifunza hapa.

    Charles De Gaulle aliyepata kuwa rais wa Ufaransa miaka kati ya 50 na 60 aliwahi tanabaisha; "siasa ni jambo nyeti sana kuwaachia wanasiasa wenyewe"!

    Hapa linaweza ibuka swali; nani mwanasiasa haswa?

    Kwa urahisi nikitumia msingi wa mwanafalsafa Aristotle; "kila binadamu ni mnyama wa kisiasa"

    Kwa misingi hiyo, msanii mathalani Sugu, Nakaaya, Mkoloni, G-Solo nk ambao hivi karibuni wamejiunga na CHADEMA si kosa. Wao ni binadamu, pili wanahaki kikatiba ya kushiriki katika shughuli za siasa kama ilivyo tu kwa Kapteni Komba wa CCM ambaye alikuwa akiimbia muda mrefu sana Chama Cha Mapinduzi-CCM.

    Tusisahau katika demokrasia tunayoifata nchini Tanzania ni demokrasia ya uwakilishi.

    Kwa mujibu huo, makundi yote katika jamii yapaswa kuwakilishwa ipasavyo.

    Hapa tuangalie kwa kina; siasa ya uwakilishi wa makundi si kwa wanasheria, wasomi wenye shahada ya udaktari nk.

    Uongozi ni zaidi ya elimu ya kimtaala. Na uongozi wa kweli haufungwi katika kiwango cha elimu.

    Je tunakumbuka viongozi mahiri waliopata kusimamia misingi nchini mathalani Hayati Moringe Sokoine wakati wanaingia ulingo wa siasa walikuwa na elimu ya kiwango gani?hebu tujikumbushe historia tafadhali.

    Kitu cha msingi ni kutathimini sifa za kiuongozi ambazo zaweza kuwa za kuzaliwa ama kujengwa mathalani kwa uchache tu;
    1. Dhamira na nia ya dhati ya mhusika katika kuomba nafasi ya uwakilishi

    2. Uwezo wa usikivu na kukubali kushauriwa.

    3. Kuwa tayari kutetea maslahi ya wanyonge na kundi kandamizwa.

    4. Kuwa sauti ya sauti zisizosikika na kandamizwa.

    Muhimu: Ni wakati wa kuwa na bunge lenye uwakilishi wa makundi yote katika jamii. Na huu ndiyo ukomavu wa kidemokrasia!!

    Na wasilisha.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 29, 2010

    Safi sana Mr II. hapo bongo ndiyo panawafaa viongozi vijana , nilikuwa hapo juzi juzi tu foleni haiishi , wageni wametawala nchi then wananchi wenyewe wanasema kuwa wamezoea. Najua kuishi kwako ng'ambo kutasaidia kuongoza taifa na wasitake kukushtua na vyombo vya dola .. tupo pamoja hakushtui mtu ikiwezekana tunaweza kukuchangia fedha za Mwanasheria atakayekurepresent Kotini na atatoka ng'ambo vile vile , najua wewe unaanza then tupe miaka mingine 10 .. vijana wote tuliohitimu mafunzo ng'ambo tunakuja kuongoza nchi yetu , hakuna cha Wahindi wala Wachina hapo.. Michuzi usiibanie hii kwani Wachina wanaingia bAHARINI MIDA YA USIKU NA SEHEMU YENYEWWE KARIBU na Ikulu.. jamani waTanzania tuamke!

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 29, 2010

    Miminauliza swali langu. Ni kwa ujumla wala si kwa huyu mtu ....Mimi sio CCM kwa hiyo siniseme....NInauliza tu hivi kugombea ubunge sehemu fulani si lazima uwe kmkazi wa huko japo kwa miaka miwili? Au unaruhusiwa tu kugombea sehemu yeyote vile hata kama hujakaa huko. This is strange nasooma kila siku nimeona mkuu wa mkoa Manyara anagombea Lushoto etc etc najiuliza utaelewa matatizo ya hao watu vipi wakati huishi huko?


    Siijui katiba inasemaje kuhusu hili lakininadhani mtanielewesha..

    Good luck Sugu. Naona Police walivyokushika ndio wakakuongezea ariya kutetea maslahi ya watu

    ReplyDelete
  20. Misupu,Please fanya juu chini tupate kuusikia huo wimbo wa mhe.Sugu kabla cjapiga kura yangu nanukuhu "uliosheheni tuhuma e.g:Ruge,Kibonde e.t.c"

    Ushauri wa bure,Sugu tulia,soma na umalize shule then utakuwa angalau umekomaa kisiasa.Leadership is a talent na si umaarufu,kuona makosa ya wenzako si hoja,hoja kutuletea maendeleo.Porojo porojo za kisiasa hazikufai kwasasa,kama unamuda wa kupoteza rudi kashughulikie mambo yako ya malaria na si kupigana michanga ya macho "oooh,napigania haki.ebo"

    I love Chadema,ila kwa style hii tunapoteza jimbo.CCM Oyeeeeee!!!

    ReplyDelete
  21. KalagabahoJune 30, 2010

    Sasa akichaguliwa huyu msanii wa bongo flava ndo nitaamini kwanini watoto wa vigogo wanakimbilia siasa, maana hakuna talents wala potentials. Wa akina Kippi, Mongella, Tom Apson, January, Ridhiwani hata dada Mwamvita akigombea poa, maana shule imepanda na wanaonekana wanazo talents and potentials.
    Huyu Mr II, alianza ku rap zamani kidogo, shida za wananchi anazijua, ila ningemshauri, kunyimwa tenda ya kukomesha malaria isiwe kisingizio cha kujiunga na chadema ili apete ulaji, politics is a dirt game, Mr II utaweza? Je ikitokea ukawa mbunge, na ikabidi usaini mikataba, na kama ujuavyo hasa yale maneno madogo madogo kwenye mikataba huwa ndo yanatushunda, wewe Mr II utaweza kuyasoma na kuyaelewa?
    Ningekua mshauri wa Mr. II, ningemshauri aaende shule kidogo, hata akiishia adanced diploma poa tu, lakini at least atakua anaupeo. Sasa leo hii ndugu Mr II unataka nikuchague, kwasababu nilizozitaja apo juu, je ikitokea ukagombana na watu wengine wazito na sema tayari ukiwa mbunge utawafanyaje? Naogopa hata kufikiria.
    RUDI SHULE, ISOME SIASA, HALAFU UJE, MIE NTAKUPIGIA KURA LAKINI SIO SASA ULIVYO MBONGO WANGU, HAPA NAKUONA MSANII TU!

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 30, 2010

    Na yeye naona ni mtoaji tu wa ahadi za uwongo kama wanasiasa wengine. ETI nitawatatulia matatizo yenu, utatue matatizo wewe umekuwa BILL GATES? Maana ukiwa na pesa zako mwenyewe hutasubiri bajeti ya serikali ikupangie kama jimboni kwako kutakuwa na mradi wa barabara, umeme au maji. Lakini pesa huna, kwa pesa za bajeti ya kupangwa na mtu mwingine serikalini ndio utangaze unataka kutatua matatizo ya wananchi!!! Uwongo gani huo? Na watanzania wamezoea kudanganywa kweli kweli, hakuna mwanasiasa hata mmoja anaweza kutatua matatizo yenu zaidi ya serikali yenyewe labda wakazane kulobby majimbo yao yaingizwe kwenye bajeti ya serikali!!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 30, 2010

    nanukuu: mimi ni mkazi wa knondoni iweje kesi ifunguliwe ilala?

    HAPO TU UMESHAJIKANYAGA HATA KATIBA NA SHERIA ZA NCHI HUJUI. LEO UNATANGAZA KUWANIA UBUNGE MBEYA HUKU UNALALAMIKA KUFUNGULIWA KESI WAKATI WEWE NI MKAZI WA ENEO LINGINE?
    HII INAONYESHA DHAHIRI ULIVYO NA ELIMU FINYU. HIVI KWELI UNAFIKIRI WAKAZI WA MBEYA WATAJIKANYAGA NA KUKUCHAGUA ETI KWA VILE NI MPIGA KELELE JUKWAANI KWA KISINGIZO CHA USANII.
    KAMA UNAFIKIRI UMAARUFU MBUZI UTAKUPA UBUNGE, MWAMBIE MICHUZI ANAYEJULIKANA NAYE AWANIE UBUNGE UONE KAMA ATAUPATA?
    MAISHA YA JUU MAKALI BOX LIMEKUSHINDA. BENEFIT SIKU HIZI HAKUNA, KADI ZA KUCHANJA HAKUNA UKAONA HAPA UTALOST SASA UNAWANIA UBUNGE...TENA MBEYA...UNAOTA MCHANAAAAA

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 30, 2010

    Alah! basi na mimi nagombea kwetu Nyegezi.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 30, 2010

    Penye nia pana njia,tafuta njia utafika tu sugu lkn jamani viongozi wa huku nchi za nje wanaweka biograpghy zao wazi kwa wananchi ila kama Tanzania, kibao wamejaa madarakani kutia joto viti hata hawasikiki. ningependa biography za viongozi zitafutiwe kipindi maalum na kuwachambua mmoja mmoja tujue elimu yao imefikia wapi si kupiana kisa tuliishi jirani utotoni.
    Namkubali Mkapa ki elimu,

    Benjamin Mkapa was born on November 12, 1938, in Masasi, Tanzania. He got arts degree in 1959, 1962 akapata bachelor degree in English.....akapata masters in international affairs in 1963 from the United states chuo kinachoitwa Columbia University...and Obama went this Uni.. 2degrees and got masters too!! Haya nipewe Bio ya waziri hata mmoja au wabunge..
    Mdau,
    USA

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 30, 2010

    Naona ubunge umekuwa wa kuchezewa tu. Wananchi wamekuwa jalala la matatizo ya watu. Kila anayekwama sehemu pa kukimbilia ni ubunge. Jamani hivi hawa wananchi hatuwahurumii. Ebo tumwogope hata Mungu jamani. Kesho utasikia Afande Sele ubunge Morogoro, keshokutwa TID, siku inayofuata Mwisho Mwampamba, then Bi. Kidude, jioni yake Lady Jaydee, n.k. Huu sasa ni utani. Kwanza wewe Mr. Sugu taaluma yako yako level gani kweli? Std 7, form 4 au???
    Tusiwatanie wananchi wa Tanzania kwa kutangaza nia hovyo hovyo.
    Mdau
    Oslo

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 30, 2010

    teh teh teh teh! Imbofu isya mandeleni!(Sugu mwenyewe unaelewa maana yake)! Ungerudi huku USA ili upige kitabu kwanza! uongeze upeo wa akili, nina wasiwasi na uwezo wako wa kuchambua mambo! Juu ya kwamba ni mzaliwa wa mbeya bado itakusumbua sana Mbeya ya sasa siyo ile uliyoiacha miaka ya 90!

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 30, 2010

    Mr.Sugu unanipa mashaka na chadema yako.jana umechukua kadi ya chadema na leo unaomba kugombea ubunge. Chadema haina probation period?SUGU ana frastrution zake Chama makini kisingempa nafasi ya ubunge mwananchama ambaye hana hata siku tatu kwenye Chama.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 30, 2010

    I WANNA KILL RIGHT NOW! TUIMBE PAMOJA IWANNA KILL RIGHT NOW! SAY OOOOOOOOH! OOOOOOOOOOOOOH! F***CK BIG F******CK FULANI NA FULANI YEAH IWANNA KILL RIGHT NOW! ULICHOKOSEA SUGU KUTAJA WATU MAJINA. YASIJE YAKAWA YA 2PAC NA BIG. NB NYIMBO HIZO ZIMEPITWA NA WAKATI.

    ReplyDelete
  30. Elimu ya Juu haina tija saaana, maana kigezo kikubwa hata unapochukua fomu ni kwamba uwe na akili timamu ujue kusoma na kuandika kiswahili au kiingereza.. uongozi ni kipaji, mf. tunao viongozi wasomi saaana lakini hawana jipya na nchi bd iko gizani, busara haisomewi darasani. hata hivyo ni muhimu kuenda class. SUGU USIKATISHWE TAMAA.. GO ON..TIME WILL TELL BRO!

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 30, 2010

    Sugu,
    Kiongozi ni mtu ambae anatakiwa awahamornize watu ili waweze kujiletea maendeleo wenyewe. Kama alivyofanya Thomas Sankara na Baba wa Taifa. Kiongozi anaewaambia watu nitawafanyia hiki na kile kama yeye ana blank cheque huyu ni wa kumuogopa.
    Ukilielewa hili una kura yangu Bro.

    ReplyDelete
  32. MnyalukoloJune 30, 2010

    Congratulations Mheshimiwa mtarajiwa Joseph Mbilinyi! I guess kuhusu elimu yako itajulikana siku zijazo manake watu wengi wanaulizia hivyo - hopefully hutakuwa na degree fake au kutoka diploma mills online kama za wabunge na mawaziri wengi.

    Pole na misukosuko kukamatwa na polisi but nimependa sana kiteteo chako especially kuhusu neno "kill" na nikaingia online fasta na kulitafuta hilo neno na nikalipata! http://dictionary.reference.com/browse/kill

    Inaonekana uchaguzi huu utatawaliwa na bongo flava - upande mmoja CHADEMA bongo flava ukiongozwa na Sugu, Nakaya, Mkoloni, G-Solo etc na upande mwingine CCM Bongo flava ikiwa na wengine wote, sijui akina Ngwear, Dully Sykes, TMK etc

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 30, 2010

    Hawa wanaosema oh elimu ndio hao hao wenye beef naye. Forms zasema ujue kusoma na kuandika na akili timamu ndo maana hata komba mbunge na wale wa zenji ndo usiseme vihiyo plus hamna jipya ndo maana mnapanda miti mizima mizima mkiona wageni sucks. Go SUGU wasikutatishe tamaa, watu wameshika nchi ndo wakasoma Uni itakuwa weye make your dream come true. Amani

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 30, 2010

    ..Tunapojadili uamuzi wa sugu kugombea ubunge sioni kwanini watu tunashikilia suala la elimu.Tanzania tunawafahamu viongozi wengi tu waliofanya mambo makubwa kiuongozi amabayo leo hakuna kiongozi anayekaribia mafanikio hayo? Tumuangalia marehemu Abeid Amani Karume, he was a visionary leader! Huyu inaelezwa alikuwa kuli bandarini. Mfano ulio hai leo, JACOB ZUMA he has NEVER had a formal education, yet anaongoza the strongest economy in AFRICA, sembuse kuwa mwakilishi tu wa wakazi wa Mbeya mjini....Tuwe realistic, huhitaji elimu ya Chuo kikuu kuwa mbunge, Marehemu Bomani alishindwa ubunge wa Mwanza mjini na Pascal Mabiti,sasa ni mkuu wa wilaya, the guy was a secondary school teacher, a diploma holder.Samwel Chitalilo mbunge wa Buchosa kila kukicha analalamikiwa kufoji vyeti vya Shule huyu ni standard seven! uliza aliwashinda akina nani? Dr. Tizeba, PHd holder in engineering...Nashauri tunapojadili suala la elimu na uongozi tufikirie nje ya box.Elimu kwa maana ipi, tusifunge kuwa elimu ni lazima kuwe na academic awards kama bachelor degree, masters, Phd etcTusisahau hata JK, Karume, Marehemu Hukwe Zawose ni PHD holders..LOL!

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 30, 2010

    Nakuunga mkono Mr. Sugu kwauamuszi wako. Wanaosema elimu wanakosea kwani wasomui wa Tz wanaonesha kufeli kwenye uongozi kwani naamini hatakama tukiwa nakiongozi ambaye hana shule kama mnayotaka ninyi wengine mambo yataenda vizuri cha muhimu ni kupiga rushwa na ufisadi ambao wasomi wetu hasa watz wanaufanya.
    Embu angalia wasomi wenye digrii1,2,hadi3 lakini wanashindwa kutumia elimu yao kupinga ufisadi na mambo mabaya yanayofanywa na serikali ya Tz kwani wanaofia kazi zao. Hivi wewe umesoma mpaka ukawa profesa au PHD lakini unauoga wakufukuzwa kazi na serikali hivi unashindwa kupata kazi nchi nyingine kama kweli PHD yako ulipata kialali?
    Nashindwa kuielewa wasomi wa TZ, wanapenda matanuzi sana, hivi ujui hapa duniani tupo kusaidiana kwani wote siku moja tutakufa na kuacha mali zote, wakowapi wakina mabutu, iddiamini na madikteta wote duniani? Hivi atujifunzi jamani mbona wakina mandela, castro wanaishi kwa amani kwani walipenda haki nakutoa msaada kwa wananchi maskini.
    Natamani Nyerere, Sokoine na viongozi wengine waliopita wangekuwapo nazani mambo yanayofanyika sasa Tz yasingekuwapo. WATU WANAFANYA NCHI HII NI YA UKOO, ANGALIA WANARITHISHANA NAFASI LEO HII MTOTO WA MASKINI KUPATA UONGOZI SERIKALINI LABDA HAWE AMEJIUNGA NA WATOTO WAVIGOGO. LEO HII MTOTO WA MASKINI HAPATI KAZI, ANGALIA MAKAMPUNI YOTE, MASHIRIKA MBALIMBALI WAMEJAA WATOTO WA VIGOGO AMBAO WALICHUKUA NAFASI NYINGI KWENDA KUSOMA ULAYA HASA INDIA,UK, NA USA KWANI NAFASI HIZO NIKWAWATANZANIA WOTE LAKINI LEO HII MASKINI UNAAMBIWA USOMEE HAPA HAPA TZ HIVI WEWE MASTERS ZA TECHNOLOGY KWELI HAPA TZ TUNADANGANYANA SANA KWANN SERIKALI HISIWE NA UTARATIBU WAKUSOMESHA MASTERS NA PHD ZA COMPUTER,TELCOMMUNICATION ULAYA,ASIA NA AMERIKA KWA WANAOFANYA VIZURI KWENYE DIGRII YA KWANZA NA KUWEKA MKAZO SEHEMU ZA UTAFITI UONE KAMA HATUTAPATA MAENDELEO?
    HIVI SASA ELIMU BONGO IMESHUKA SANA SANA, NAJUTA KWANINI WATZ HATUTAKI KUWAJIBISHA SERIKALI YETU KAMA HIHI HILIYOPO MADARAKANI AMBAYO HAKUNA TIJA NI WIZI MTUPU.
    HATA KAMAUSIPO WEKA MAONI YANGU HAPA LAKINI UJUMBE UMEFIKA NA KAWAFIKISHIE WALENGWA KWAMBA SIKU INAKUJA MWISHO WAO WAKUONGOZA TZ KWAWIZI UNAKARIBIA.
    LEO HII TUNA MADINI LAKINI HAKUNA CHOCHOTE YANATUSAIDIA ANGALIA BOTSWANA, MADINI YANAWAFANYA KUWA NA MAENDELEO. HIVI NYERERE HALIKUWA HANA AKILI KUYAACHA MPAKA WATZ WAPATE ELIMU? MBONA MNATUFANYA SISI WENDAWAZIMU LAKINI? NINAUCHUNGU SANA LAKINI IMANI YANGU INANIPA KWAMBA SIKU ZA MAFISADI WA TZ ZINAESABIKA.
    MUNGU IBARIKI TANZANIA WABARIKI WANANCHI WALIO VIJIJINI HASA AMBAO HAWANA MAITAJI MUHIMU KAMA MAJI, MALAZI BORA, MAVAZI.
    ALUTA KONTINUA, HATA NIKIFA MIMI NAJUA WENGINE WAPO WAKUTETEA WANANCHI MASKINI.
    mpiganaji.

    ReplyDelete
  36. AnonymousJune 30, 2010

    SUGU MIMI NI MTU WAKO WA KARIBU SANA,SANA,SANA, AND I SUPPORT YOU KWA KILA UNALOFANYA, LAKINI HILI LA KUTAJA SIJUI FULANI ANA "NGOMA" HALIJANIFURAHISHA KABISA KABISA, OTHERWISE ALL THE BEST.

    ReplyDelete
  37. AnonymousJune 30, 2010

    Acheni kumwandama sugu! kwani ana kosa gani? anatumia haki yake kikatiba sasa kina wauma nini? mmeambiwa wabunge wote ni wasomi? ama kuna mbunge anayesaini mikataba! acheni kuwakatisha watu tamaa, kama wewe huwezi mwenzio anaweza mwache!! hongera sugu nenda kagombee ubunge wala usikatishwe na watu wasiojua hata katiba ya nchi yao inasema nini.

    ReplyDelete
  38. AnonymousJune 30, 2010

    NI KWELI KABISA KWAMBA CLOUDS REDIO NI KIBARAKA WA CCM NA NDIO MAANA ILIWEZA KUMSUPPORT JK ALIVYOTOA HOTUBA YAKE NA WAZEE PALE DIAMOND, MR II TUPO NYUMA YAKO NA WALA USIOGOPE KUSEMA UKWELI MPAKA KIELEWEKE NA TUTAHAKIKISHA UNAPATA UBUNGE WA MBEYA MJINI.
    ALUTA CONTINUA...............

    ReplyDelete
  39. AnonymousJune 30, 2010

    ukiwa na bifu na mtangazaji mmoja wa Clouds basi wengine wote wanakushambulia kupitia vipindi vyao kwa nyakati tofauti, Mr. II au too proud nae hakukosea kuwachanganya wote kwani issue ya Malaria Kibonde aliivalia chuga kama vile msemaji wa ikulu na kumkejeli mwenzake vibaya kupitia Jahazi, akisahau kuwa sooo yake iko wazi na inajulikana wazi hata kama hakujitangaza. Silaha ya Mr. II kuondoa hasira yake ili asikike na umma ni kupitia wimbo kwani yeye hana kituo cha redio hivyo ili na yeye asikike hewani ilibidi ni lazima awapindie juu kwa maverses ya nguvu kama wanabisha na aliyoyasema waje na ushahidi kama hawajaumbuka. hapa mjini bwana na wanamjii si ndio hao hao ukimuudhi rafiki yako anatoa siri yako full stop.

    ReplyDelete
  40. AnonymousJune 30, 2010

    mamaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa tumeingiliwa, yaani Mr 2 anagombea ubunge,
    Busara yake iko wapi. Mungu tusaidie Watz.
    Du hata siamini kuwa kwa matusi yale kwenye wimbo wake CHADEMA watakubali kumteua, hata wakazi wa mbeya mjini sidhani kama watakubali, Sugu amejiharibia pale alipotoa ule wimbo, isipokuwa imekuwa vizuri umemwelezea yukoje, ili pia hata wakazi wa mbeya wajue zipi chuya na upi mchele.
    Du hata siamini hayo matusi ilikuwa ni njia ya kutokea.
    Kwanza nina wasiwasi siku atakayoteuliwa tu kugombewa KIBONDE atampeleka mahakamani kwa kumkashifu kuwa ana ngoma kwani si haki kumtangaza mtu ni muathirika bila ridhaa yake hata kama ni kweli, huo ni unyanyapaa.
    Nasikitika kusema mr 2 hana Busara, nina wasiwasi degree yake, au alikwenda marekani kupiga box,akanunua cheti akarudi kutuongopea ana degree.

    ReplyDelete
  41. AnonymousJune 30, 2010

    mama yangu mambo ya madagasca yanakuja bongo. uuuuwwwwiiiii. twafwa. niende wapi sasa

    ReplyDelete
  42. mzuluasiliJune 30, 2010

    natangaza nia ya kugombea kwetu kanyerere pia nakuunga mkono sugu umeonyesha mfano wacha wakuponde ila waelewe vijana ndo chachu ya mabadiliko na tutakuunga mkono pia pole na matatizo ya kukamatwa hawana mpya hao lakini napenda kukushauri punguza jazba

    ReplyDelete
  43. AnonymousJune 30, 2010

    MR II UNAINGIA PABAYA KATIKA UKUMBI WA SIASA NA KUANZA KUONESHA LIVE UNA CHUKI NA WATU FULANI,INAKUBIDI MWANZO UENDE KITAALUMA NA KUKAA CHINI NA WATU,UJUE KWANZA UTAISHI VIPI?HILO SUALA YA LA SIASA NDUG YANGU KWAKO ,BORA UWE MUIMBAJI WA RAP KAFANYIA WATU KAMPENI,NA HUNA UMAARUFU WOWOTE,KAMA UNATAKA KURUDI KATIKA MAISHA YAKO YA UKIMBIZI ULAYA,RUDI KWA AMANI ,KABLA SIRI ZAKO AZIJAFICHUKA,USITAJE WATU MAJINA,WALA USIENEZE CHUKI KWA MTU USIEMPENDA,ANAEKUCHUKIA MPENDE,ATAJIREKEBISHA,JE UNAANZA MATATIZO BADO KIJANA?,NAFASI ULIZOPATA ULAYA,AMERIKA ULIKUWA NIKUJIENDESHA KIELIM,NA KUISHI KWA AMANI,NA UNGEENDA ATA SHULE YA MZIKI,AU YA SANAA,ANGALIA KINA MR BLUE,WAMERUDI SHULE,AKISEMA ANATAKA KUWA MBUNGE WA TEMEME ATAWEZA KUFIKIRIWA NA WANANCHI,UBUNGE SI CHAMA CHOCHOE ,NO MUTTER ATA UKIWA MGOMBEA BINAFSI,UKIWA NA SERA NZURI UTAPATA KURA,JARIBU KUOMBA RADHI ULIOWAKOSEA,USICHUKULIE JINA SUGU UKAENDA NALO KIUSUGU,one love joseph mbilinyi.

    ReplyDelete
  44. KUNA NYAKATI HUNA NASONONEKA SANA NINAPOSOMA COMMENTS KWENYE HII BLOG. JAPOKUWA SI WOTE ILA UKILIANGALIA SANA HILI NI TATIZO LA WATANZANIA WENGI JAPO SI WOTE.

    NANI KASEMA LEADERSHIP LAZIMA UWE UMESOMA CHUO KIKUU KUNA VIONGOZI WANGAPI WANA ELIMU YA JUU NA WAMESHINDWA KUWAONGOZA WANAINCHI WAO. KAMA AMEKUWA MKWELI NA NAFSI YAKE MA KUONA KUWA ANA KIPAJI CHA KUONGOZA KWA NINI AULIZWE ELIMU YAKE.

    KWANZA KUNA HILI MOJA NATAKA NIWAELEZE MTAZAMO WA SUGU KATIKA MAENDELEO UNAWEZA HATA KUMSHINDA MIJTU ILIYOMALIZA CHUO KIKUU SABABU KUSOMA SI KUPATA CHETI NA KUANDIKA KWENYE MAKARATASI ULIYOYASIKIA KUTOKA KWA MWALIMU WAKO. KUNA KUSOMA KWA KUONA NA KUGUSA. NA NINA IMANI KABISA SUGU ANAWEZA KUWA NA ELIMU YA KUONA AMBAYO INATOSHA KABISA KUBARISHA MKOA KAMA SI WILAYA KAMA ATAPATA SUPPORT YA WATU.

    MAENDELEO YATALETWA TANZANIA KAMA TUTAONDOA KASUMBA NDOGONDOGO NA KUWA WAKWELI WENYE KUPENDANA BILA KUWA NA TOFAUTI KATI YETU.

    NAJUA MTASEMA MBONA YEYE KAONYESHA TOFAUTI KATI YAKE NA RUGE. JIBU NI HILI KUNA WASANII WENGI WANAUMIA KICHINICHINI HAWANA GUTS KAMA SUGU YA KUONGELEA UKWELI HII SUGU KAIPATA KWA KUTEMBEA NA KUONA DUNIA YA NCHI NYINGINE JINSI ZILIVYO. KUNA SANAA NZURI TU ZA MUZIKI HAZIPIGWI REDIONI SABABU HAWAJAMSHIKA MIGUU RUGE AU HAWAJATOA HONGO KWA MA-DJ WA CLOUDS. TUTAE TUKUBALI CLOUDS NI MAARUFU NCHINI LAKINI WAKIWA BIAS WATAKUWA KWA KIASI FULANI WANACHANGIA KUSHUKA KWA MUZIKI WA TANZANIA NA KUWAUWA KISANII WASANII WASIO NA HATIA.

    MDAU NG'AMBO

    ReplyDelete
  45. AnonymousJune 30, 2010

    Hivi ni mbunge gani mtarajiwa anaweza publicly akatamka maneno kama fuck you, i wanna kill right now n.k, sisis jamii tukuchukulie we ni mtu wa namna gani? I dont see any diplomacy in you, can you account for this?

    ReplyDelete
  46. AnonymousJune 30, 2010

    michu wacha kubana comment na ww ni mtoto wa mjengoni nini? naona inakuuma sana tukiweka mambo wazi unaogopa nini wakati sugu keshaimba?

    ReplyDelete
  47. AnonymousJune 30, 2010

    Mimi namuunga mkono Sugu kujitangaza kwake kugombea Ubunge ili kutetea haki za walala hoi. Kikubwa atakapofanikiwa kupata hiyo nafasi afanye kweli yale atakayoahidi na isiwe ahadi hewa.

    Wanaosema kugombea nafasi ya uongozi lazima uwe na elimu, upeo wao ni mdogo. Enzi za Mwalimu viongozi wengi tu walikuwa hawana elimu kubwa ya degree/diploma ila walikuwa watetezi tu wa wananchi.


    Kama elimu ni uongozi bora, haya viongozi wengi tuliuonao sasa wana elimu na elimu yao wanaitumia kufanya mambo ya UFISADI na kutokuwafikiria wale waliowapa kura zao wakati wa uchaguzi. Wanatumia elimu yao kuwadanganya wananchi wengi ambao hawakubahatika kupata elimu kama walizonano na kuhonga ili wawachague.

    JAMANI TUWE NA UPEO WA KUFAHAMU SIFA ZA UONGOZI KWENYE MAMBO YA SIASA NA UONGOZI WA KITAALUMA (DAKTARI, MWANASHERIA, UHASIBU N.K)ambao unahitaji uwe na elimu. Kwenye jukwaa la siasa elimu ni ziada tu lakini haina umuhimu sana.

    ReplyDelete
  48. AnonymousJune 30, 2010

    jamani mtu ametunga wimbo na video kama hiyo, halafu anagombea ubunge???????????? thats is a recipe for disaster. RAP za siku hizi watu hawatumii violance materials au violence videoS. WAKE UP MR WHO?

    ReplyDelete
  49. NALEZOWAGAKABISAJune 30, 2010

    Ukisikiliza nyimbo yako, imejaa chuki binafsi na ni kweli ukiimba nyimbo ambayo unataka kuua basi lazima vyombo vya sheria vikuchukulie hatua, umeimba bila insha, hakuna message ya maana hapo.
    Inaonyesha jinsi bado ulivyo check bob, na jinsi unavyoitaji elimu tena sana.
    Huwezi kunidanganya eti wewe unaweza kuwaongoza watu na kuwaletea maendeleo jimboni kwao.
    Kwanza hata sijui kama una mji zaidi ya kumtegemea kaka ambaye amechacha kwa kutokua na kadi za kuchanja na za wizi, na kama angeendelea kufanya kazi apo royal mail na kuendelea kukwiba angekua jela sasa. Kila kukicha kaka yako anasaidiwa na mke wake kwa vi benefit anavyopata Uingereza, ukumbuke ni wewe Mr II uliotokea kwenye TV eti kuonyesha crib yako (ambayo ilikua ni ya kaka na vitu vyote), na wajanja wakaja wakakomba, halafu leo hii eti unataka kuwawakilisha wananchi bungeni! Utaongea nini? Zaidi ya kutaka kupata hivyo vihela vya ubunge na kufanya matanuzi na kutukana watu!
    Kama kweli wewe hupendi wizi na unyanyasaji basi ungeanza nyumbani, kwa kukataa kutumia mahela ya wizi ya kaka na kuukana ufuska wake, hapo kweli tungekuona wa maana.
    Huwezi kujilinganisha na wanasiasa maarufu ambao hawakusoma, zaidi ya kuwadhalilisha maana wao hawakufanya haya mambo yako, wao waliwakilisha wananchi, walituletea uhuru, walituongoza mpaka hivi sasa. Wewe utaweza?
    INAONYESHA JINSI CHADEMA WALIVYOWABABISHAJI KISIASA, NA NDIO MAANA CCM WATAENDELEA KUWA MADARAKANI TENA KWA SANA KWA MFUMO HUU WA KISANII WA VYAMA VYA UPINZANI!

    ReplyDelete
  50. AnonymousJune 30, 2010

    Elimu haina kitu exposure aliyopata inatosha kabisa. Wabunge wangapi wameishia darasa la saba. Ukiweza kuishi tu USA kwa mwaka mmoja kama hujaletwa na baba yako fisadi ni elimu tosha.

    Nyie mnaompinga wote ni CCM na ni wapinzani wake mnajua fika anajua walala hoi wanaonewa kiasi gani...

    GO SUGU GO SUGU GO SUGU

    ReplyDelete
  51. AnonymousJuly 01, 2010

    Natambua kuwa hili jambo si la mchezo, na nina uhakika idadi kubwa ya wachangiaji hasa wanaojaribu kupotosha harakati hizi, waweza kuwa ama hawaufahamu muziki wa tanzania ulivyoharibika, au ni moja kati ya kile kikosi kazi kilichoundwa madhubuti kwa ajili ya kuhakikisha kuwa ujumbe wa msanii huyu unapuuzwa na watanzania wengi ambao mengi yaliyotajwa yanawahusu.

    Nilidhani, kuwa hii ni hoja binafsi ya SUGU ndo maana sikusikia anamobilize watu waungane naye, na hii ni kweli kuwa, uchungu wa kutapeliwa huwezi kuufahamu mpaka utakapotapeliwa. inauma sana kuibiwa, inauma sana kudharirishwa na watu kama akina kibonde kupitia Redio hiyo ilotajwa na Sugu. Ni nani asiyejua juu ya tuhuma mbalimbali za KIBONDE juu ya kuwakejeli na wakati mwingine hata kuwatusi, tazama sakata la kakobe, sakata la TUCTA,sakata la Sugu, na la Mpendazoe, huyu jamaa alitumia hii media kuwaponda na kuwadharirisha utafikiri kama wao hawana akili. Eti KIBONDE anajiona kuwa anajua kila kitu zaidi ya hawa watu wanaoongoza maelfu ya watu, hii si haki.

    Nina uhakika kama watu wamesoma vizuri maelezo ya SUGU, hakuna haja tena ya kusikiliza propaganda Feki za timu angamizi inayotumiwa kupotosha habarri hizi, na ndiyo maana haja jeshi la polisi lilimkamata na hatimaye kumwachia kwa dhamana binafsi, hii ni heshima kwa sugu na pia inaonesha jinsi alivyo wa muhimu katika jamii lakini pia kuonesha degree hafifu ya shitaka linalopikwa.

    watanzania wenzangu, sipendi na wala sihitaji watu waishi kwa visa na mikasa, lakini pia sishabikii unyonyaji na uonevu wa aina yoyote na hasa ule unaofanya kwa dharau na hadaa za hali ya juu. Kama mtu anajisikia kudai haki yake na tena kwa haki bila kificho, basi ni kheri aachwe afanye hivyo, na kama kuna mtu yeyote anayedhurumiwa na yeye akanyamaza bila kunena basi huyu ni mtu wa kusaidiwa sana. Asaidiwe kugundua haki yake, jinsi ya kuidai na wakati mwingine afahamu mbinu mbadala zitakazomshia katika mazingira yoyote ya mapambano.

    RUGE kaka, acha tabia yako hiyo, hii siyo kwa huyu kijana tu, bali pia na kwa wale vijana ulionao hapo kwenye nyumba uliyopewa na kikwete kwa ajili ya kusaidia watanzania na badala yake ukaigeuza kuwa yako na kambi yako.Jitahidi sana kuwalea hao watoto wanaokuja kufundishwa hapo, usiwaache wakawa wake zako wadogo hii ni hatari kwako, kwao , na pia familia yako.

    HAYA BWANA KAMA MANAJUA KUSOMA ALAMA ZA NYAKATI BASI FANYENI HIVYO, ANGALIENI MATUKIO YANAYOWAANDAMA NA KISHA MREKEBISHE. HAKUNA ANAYEWACHUKIA ILA TU MNATAKA KUJENGA MAZINGIRA YA HUO MWELEKEO.

    MWISHO, KESI SIYO SULUHISHO YA HAKI YA WATU, ACHA DHARAU NA KISHA WEKA MAZINGIRA HALALI YA KUJADILI NA WATU UTAWEZA KUEPUKANA NA MATATIZO KAMA HAYA.

    NAWAPENDA WOTE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...