Baadhi ya wanachama wapya wa CCM kutoka vyuo vikuu mbalimbali mjini Dodoma wakila kiapo cha utii mbele ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma leo mchana.
Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika vyuo vikuu mbalimbali mjini Dodoma walishiriki katika maandamano ya kumuunga mkono kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi ya Urais mwaka huu kwa tiketi ya CCM.
Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaongoza wanachama wapya wa CCM kula kiapo cha utii kwa Chama Cha Mapinduzi muda mfupi baada ya kuwakabidhi kadi za uanachama wakati wa maandamano ya kumuunga mkono yaliyofanyika mjini Dodoma.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo George Mkuchika, Kaimu Mwenyekiti UVCCM Beno Malisa, na Katibu mkuu wa CCM Yusuf Makamba.
Baadhi ya wanachama wapya wa CCM kutoka vyuo vikuu mbalimbali mjini Dodoma wakila kiapo cha utii mbele ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma leo mchana
(picha na Freddy Maro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 13, 2010

    Kwa raha zao wanajidai wanamuunga mkono wakikosa mikopo wanagoma..hata siwaelewi.Hakuna vijana wakuchambua mambo na kuleta mabadiliko as if they're brain washed by ccm..wish to get other nationality than TZ as no one own it.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 13, 2010

    ni malimbukeni hawa nadhani hawana hata sifa za kuwawezesha kusoma hapo ila wamekuwa promoted kwa ajili ya kampeni siasa na shule wapi na wapi?hebu acheni kuwapotosha wengine nyie ndio mnaotegemewa kuleta mabadiliko bado mnafikiria ccm? hasa raisi asieyejali maslahi ya wafanyakazi na wanfunzi kwa ujumla kila kukicha yeye na safari fikirieni kwanza kabla hamjaamua kumuunga mkono. bila shaka haya ni malipo ya takrima

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 13, 2010

    sasa mbona wanaunga mkono kitu ambacho kimeshapitishwa? hivi hasigombee urais jk halafu agombee 'si mwenzetu' nani ndani ya ccm?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 13, 2010

    Namna hii ndiyo tutegemee nchi itasonga mbele ? Kama Hao ambao wanategemewa wawe wachambuzi wa mambo wanaonekana wamezibwa macho, mwenzangu na mimi niliyeko kijijini ambaye sijui hili wala lile nitaweza kweli ?
    Tusishangae namna hii tukabaki masikini kwa miongo mingine mitano.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 13, 2010

    Njaa ni kitu kibaya sana.. ngoja nikaangalie work cup math.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 13, 2010

    Wabongo mmezaliwa kwenye njaa na kwenye njaa mtarudi na njaa itawanyima haki maisha yenu yote na CCM inatumia udhaifu huu kutawala milele.Poleni kwa msiba huo mzito na kwa uoga wenu wa njaa mtalia mpaka mwisho wa Dunia and nothing will change.R.I.P wabongo,Amen.Mars native.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 14, 2010

    Tatizo ni kuwa hawajui kuna option nyingine.

    ReplyDelete
  8. Mpalang'ombeJune 14, 2010

    Ingekuwa wanamuunga mkono CUF au CHADEMA wangetishiwa kufutiwa udhamini wao, maana sheria inasema wazi kuwa wanafunzi hawaruhusiwi kujishghulisha na siasa vyuoni kwani ni moja ya mambo yanayoweza kumfanya mtu kufutiwa mkopo wake.

    TZ Baaaadoooo, ila nina hakika wengi wa hao wakimaliza vyuo watajiuliza mara mbilimbili hivi ni nini walikuwa wakikifanya wakati wakiwa vyuoni, baada ya kutafuta ajira mpaka vihela vyote walivyosave wakiwa wanasoma kuisha na bado hakieleweki. Mimi nilikuwa muumini mzuri sana wa CCM na nilijipendekeza sana ila mwisho wa siku nilikuja fahamu kuwa "In Tanzania you are on your own don't expect the best from policians especially those in power, they think nothing about you rather than retain their power because for them that is their livelihood"

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 14, 2010

    Mimi sidhani kama ni njaa tu, bali ni UBINAFSI. Wanajipendekeza tu kwa rais wapate manufaa yao, wanasahau kuchambua na kuwatetea masikini wa Tz ambao ni asilimia 95%. Wananchi wengi wanaishi hali ngumu hususani vijijini, na hakuna wa kuwatetea, ni ubinafsi na ufisadi uliokidhiri. Lakini haitasahaulika kuwa imeandikwa: ''KILA ADHULUMUYE ATAPATA MAPATO YA UDHALIMU WAKE''.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 14, 2010

    nafikiri wanatakiwa wakatwe vichwa kwa kuwasaliti walala hoi hususani wakulima wanaozalisha na pesa hizo kuwalipia wasomi wasome kisha leo wanawasaliti. Vichwa vyao ni hasara kwa taifa hivyo ni bora vikatwe kabisa

    ReplyDelete
  11. "When I was a boy I was told that anybody could become President -- I'm beginning to believe it."

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 14, 2010

    TUMEKWISHA!

    mdau chiggs, deslam

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 14, 2010

    Bangi nyingine bwana...

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 14, 2010

    vichwa vimejaa maji. wataanalyze nini? ni kukopi na kupaste tu. Hakika nchi imekwisha. Sheria si msumeno - ukisapoti CCM sawa, CUF si sawa. Duh. Bongo bwana?!!! Kazi kweli kweri.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 14, 2010

    Ankal kwani hakuna habari za World cup uweke badala ya hawa vichwa panzi?

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 14, 2010

    Tangu Rais Kikwete aingie madarakani, ajenda kuu inayoongoza nchi ni ufisadi; na rais kwa makusudi ameacha ajenda hiyo iendelee kupoteza muda na raslimali adimu za nchi.
    Kwa jinsi hiyo, Rais anakwepa majukumu yake ya kufanya maamuzi kwa kuwafanya watu waendelee kulumbana bila mwisho.
    Kwa upande mwingine, mijadala hii inamkinga rais dhidi ya ghadhabu za wananchi wenye shida, kwani inawaondoa kwenye hoja zinazohusu matatizo yanayowakabili.
    Kundi hili lilihitimisha kwa kusema kuwa ndiyo maana serikali haitumii tena kauli mbiu ya “Maisha bora kwa kila Mtanzania,” wala ile ya “Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya.”

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 14, 2010

    ukiangalia kwa umakini picha zao wanaonekana wale wanaosomeshwa na world bank au mashirika mengine,wanahisi labda anazitoa yeye(kikwete).Wamekunywa maji ya ccm.
    Nawashauri kuwa ndani ya ccm kuna viongozi wengine wengi tena wazuri mara elfu kuliko huyo aliyewaweka juani.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 14, 2010

    Hawa si wasomi kitu bali wasomi nepi wanaofikiri kwa utumbo badala ya vichwa. Hawa ndiyo wanaotuchelewesha ambao usomi wao unawazamisha kwenye ujinga na ubaradhuli badili ya kuwakomboa. Tuwachukie na kupambana nao. Kesho utawasikia hawa hawa wakilalamika kuwa mikopo ya elimu ya juu haitoshi. Wapumbavu hawa wanaojikomba kwa watesi wao
    Mpayukaji MSEMAHOVYO

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 14, 2010

    Wanafunzi wa chuo kikuu huko nyuma ndio walikuwa wanaleta challenge kwa maendeleo, sasa hawa wa sasa ni bongo lala wapoteza muda wa kusoma kushabikia upuuzi wa kisiasa na wakipigia kura CCM mwezi wa kumi wahesabu maumivu miaka mitano na wakimaliza shule ajira ahakuna watakuta ajira zao wapo wachina,wakenya, wazimbabwe, wazambie etc.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 14, 2010

    KuNA MANENO KWENYE MAANDIKO (bIBLE) YALISEMWA NA YESU
    "WASAMEHE MAANA HAWAJUWI WALITENDALO"
    KWA HIYO TUWAACHE HAWAJUWI WALITENDALO, HAO HAO NDIO WATAKAOMGEUKA NA KUKIGEUKA CHAMA SIKU ZA USONI WATAKAPOKOSA KILE WANACHOKITARAJIA MIAKA IJAYO,
    ILA TUSIWALAUMU, MAANA KUNA WATU KIBAO WANAHAMA CUF NA CHADEMA KURUDI CCM.TATIZO NI NJAA, MAISHA YENYEWE MAFUPI KWA MTZ
    ccm NI WAJANJA SANA.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 15, 2010

    Kazi ipo.
    tunategemea wasomi walete mabadiliko. Waondoe kilio kwa walala hoi.
    Ebu rudini darasani mkasome. be ready to analyse things.Mnasona kupata A's au kujua namna ya kubadili sura ya maisha.
    Shame on you

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 02, 2010

    Dunia inaelekea ukingoni ss ila hizi mambo mbona UDSM hazifiki??????????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...