Wasanii wa DCMA Zanzibar wakikabidhiwa
bendera na Mh. Mahmoud Thabit Kombo, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo (mwenye baraghashia) kabla ya kuanza safari ya China

Wasanii saba kutoka Chuo cha Muziki cha DCMA Zanzibar wanategemea kuondoka nchini wiki ijayo kwa ajili ta kuiwakilisha Tanzania nchini China ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya kimataifa ya World Expo. Kundi hilo ambalo lipo kambini katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) litashirikiana na wasanii wa taasisi hiyo kwa madhumuni ya kuunda onyesho la pamoja lenye vionjo vitakavyo wakilisha sehemu zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika sherehe za kuwaaga rasmi wasanii hao, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo alilitakia kundi hilo mafanikio kundi katika kuiwakilisha Tanzania.

Maonyesho hayo ya kimataifa yanayofanyika nchini China kwa mara ya kwanza yamekuwa yakifanyika mjini Shanghai kunzia mwezi wa Machi na yataendelea hadi mwezi wa Septemba 2010. Taasisi za DCMA na TaSuBa wamepata fursa ya kushiriki katika maonyesho hayo kama sehemu ya uwakilishi wa kitamaduni wa nchi shiriki kupitia mwaliko wa Bodi ya Taifa ya Biashara za Nje.


Taasisi hizo mbili ni washika wa jadi katika miradi mbali mbali ya maendeleo ya mafunzo na miradi ya muziki hapa nchini. Wakiwa katika Maonyesho hayo, kundi hilo la pamoja linatazamiwa kufanya onyesho moja katika banda la maonyesho la pamoja la nchi za Afrika baina.

DCMA ni taasisi ya kimisaada na isiyo ya kiserikali (NGO) yenye kuendesha mradi mkubwa zaidi wa kusambaza elimu ya muziki nchini Tanzania kutoka makao makuu yake yalioyopo Mji Mkongwe, Zanzibar.

Kheri A. Yussuf
Development, Marketing & PR Manager
Dhow Countries Music Academy, Zanzibar
Mobile:077.362 0202

Email:press@zanzibarmusic.org

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 30, 2010

    Rekebisha kichwa cha habari wanawakilisha ZANZIBAR au huoni hiyo bendera?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 30, 2010

    Nilikuwa sijui vizuri kumbe Zanzibar siyo Tanzania!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 30, 2010

    Zanzibar ni mojawapo ya nchi mbili inayounda Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, nchi nyingine ni Tanganyika.

    Ukiitazama vizuri hii bendera ya Zanzibar ktk picha utaona kwenye kona ya bendera juu kulia kuna bendera ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikimaanisha kuutambua Muungano.

    Sasa sijui bendera ya nchi ya Tanganyika ambayo pia inaunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipo dizaini gani kuonyesha kutambua Muungano wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar?!.
    Mdau
    Idodomiya
    Tanganyika

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 30, 2010

    Huu Muungano wetu ni kizungurumti kwa nini tusiwe na bendera moja? Ikishindika basi tuwe na bendera tatu kama vile Mtikila anavyotaka iwe.Tanganyika tuwe na yetu na Zanzi-bar wawe na yao afu pawepo na ya Muungano.Upuuzi mtupu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 30, 2010

    Bendera ya tanganyika ni ile ya Chi chi emu

    ReplyDelete
  6. HII IWE NI CHANGAMOTO KWA TANGA-NYIKA KUWEKA HADHARANI BENDERA YAO.

    IBUMU ZANZIBAR!!

    ZANZIBAR MOTO JUUUUUUUUUU!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...