Ndugu Watanzania,

Tumepata habari za kuaminika kutoka vyombo vya habari kutoka Marekani na WHO kwamba wanasayansi nchini Marekani wamegundua chembechembe za kinga ambazo zinauwezo mkubwa wa kupambana na kuua virusi vya ugonjwa wa Ukimwi ambao hadi sasa hauna chanjo wala tiba ya uhakika.

Ugunduzi huo tayari umethibitishwa na wataalamu mbalimbali, ikiwemo Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani.

Vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa vimeripoti kuhusu ugunduzi huo ambao unaelekea kutoa mapambazuko mapya kwa ugonjwa huo hatari ambao umekuwa ukiathiri nguvu kazi sehemu mbalimbali duniani, hususan nchi zinazoendelea.

Wanasayansi hao wa Taasisi ya Magonjwa ya Kuambukiza na Mzio (Niaida) walieleza katika taarifa yao ya wiki iliyopita kuwa kwenye utafiti huo wamebaini aina mbili za chembechembe zinazoweza kumsaidia binadamu kupambana na virusi vya ukimwi.

Mkurugenzi wa Niaida, Dk Anthony Fauci alizitaja chembechembe hizo za kinga kuwa ni VRCO1 na VRCO2 ambazo utafiti wake umeonyesha kuwa zinaweza kuua virusi vya ukimwi kwa asilimia 90.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) dawa huthibitishwa pale uwezo wake wa kupambana na ugonjwa unapozidi asilimia 60.

Dk Fauci alisema hayo ni mafanikio makubwa ya kisayansi tangu wataalamu mbalimbali duniani waanze kufanya utafiti wa namna ya kutibu ugonjwa huo.

Alisema chembechembe hizo za kinga hizo VRCO1 na VRCO2 zinaweza kutumika katika kubaini aina mpya ya chanjo ambayo itamuwezesha binadamu kuwa na kinga dhidi ya virusi vya Ukimwi.

Kwa namna chembechembe hizo zinavyofanya kazi, alisema, zikitumika kama chanjo, mwili wa anayechanjwa unajenga kinga ambayo inavishambulia virusi vya Ukimwi na kuviua.

“Kwa sasa soko lina dawa za kupunguza nguvu na kasi ya virusi vya Ukimwi kuathiri chembechembe nyeupe za kujikinga na maradhi na hakuna tiba,” alisema Dk Fauci.

“Lakini utafiti huu ni njia mpya ya kuelekea kupata ufumbuzi wa kudumu katika utaalamu wa tiba.”

Hata hivyo, alisema utafiti huo unaweka matumaini zaidi katika kutoa chanjo ingawa baadaye utawezesha kusaidia kupatikana kwa tiba kamili.

Jinsi walivyoendesha utafiti huo, Dk Faci alisema walichukua sampuli mbalimbali za damu zenye virusi vya ukimwi kutoka maeneo mbalimbali duniani.

Katika sampuli hizo, alisema waliweza kupata aina karibu 200 za virusi vya ukimwi na walipozipambanisha na chembechembe za kinga za VRCO1 na VRCO2, virusi vilikufa bila kuathiri chembechembe nyingine za damu.

Hali hiyo aliilezea kuwa inathibitisha kuwa VRCO1 na VRCO2 zina uwezo wa kupambana na aina zote za virusi vya ukimwi.

Haya jamani habari njema ndo hizo, Lakini isiwe sababu ya kuanza kufanya mapenzi ovyo ovyo.

Matokeo yake yatakua kukua kwa kasi kwa yale magonjwa ya zinaa ya zamani kama kswende na gonorea na mengine, mimba kibao zisizotarajiwa, na matokeo yake watotot zaidi wa mtaani, vibaka, mateja n.k Tumia Kinga.

Maisha Mema,
Katibu T.A Reading.
--
Jumuiya Ya Watanzania Reading-UK
Blog :http://www.tanzaniaassociation-reading.blogspot.com/
Email:tzra2009@gmail.com
Tel No: +447865673756

Habari zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 17, 2010

    UKIMWI UPO NA UNATISHA. UPATIKANAJI WA DAWA SI HOJA KWANI MALARIA INA DAWA LAKINI INAUWA WATU KULIKO UKIMWI, SO HOJA BADO IKO PALE PALE TUJIKINGE NA UKIMWI PAMOJA NA MAGONJWA MENGINE

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 17, 2010

    Yaani kweli katibu mzima wa umoja unatoa hii habari???Umoja huo umekubali kutoa hii habari au ni wwe mwenyewe umejiamulia kutumia power you cannot use your title uliyopewa kupitisha habari ambazo umesoma kwenye google....

    Huu ugonjwa upo na unatisha bado wewe ukikimbilia kusikia habari hizi na kupeleka hewani haraka haraka...mbona hii havbari ilitoka muda kidog USA...Na usiweke information ambazo ni za kitalamu bado FDA hawajaipitisha ndugu yangu slow down.....

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 17, 2010

    Nikaombe Visa mie ya Marekani nakujaaaaaaaaaaaaaaaaa.... Msanii maarufu mie Bongo hapa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 17, 2010

    Tafadhali msianze kuwapotosha watu kwani dawa hiyo mpaka ianze kutumiaka itachukua zaidi ya miaka 30 ijayo, katika kipindi hicho watu wangapi watakuwa wameambukizwa na wamekufa. Na hiyo itatibu only asilimia 95 kwa maana hiyo haitatibu asilimia mia ila itaongeza maisha ya mtu. Na mpaka ifike ulimwengu wa tatu itakuwa ni miaka 50 hadi 100. Marekani yenyewe sasa hivi hali imekuwa ni ngumu kwani kuna jumla ya wagonjwa wa HIV kama 1.6Milion lakini imeshindikana kuwapatia dawa watu wote budget ya serikali ni US$ 25M na zinahitajika zaidi ya US$125M. Tusijipe moyo tuendelee kuwa waaminifu katika ndoa, na kuacha kufanya mapenzi nje ya ndoa kwa wale walio single. Tuendelee kumwomba Mungu ili aendelee kutuepusha na tamaa na anasa za duniani kwani zinatufupishia muda wa kuishi hapa duniani.
    Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
    Ndimi mdau wa Damu USA

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 17, 2010

    hizi sio habari ngeni kila baada ya muda hapa amerika wataalamu hupiga hatua moja mbele katika suala la utafutaji huu wa dawa au kinga ya maradhi haya lakini cha kuvunja moyo pia huweka wazi kuwa yote hayo mawili upatikanaji wake ikiwa hizo research zitaenda mswano basi itachukua kiasi miaka kumi kwa uhakika na upasishwaji na hili shirika la "food and drugs administration"{fda} linalosimamia utoaji vibali vya ubora wa misosi na madawa kwa ajili ya matumizi ya binadamu.
    sasa chonde chonde wazeee wa kazi kwa taarifa hizi msiache kuvaa jazi mkaanza kupiga kandanda matumbo wazi,tumieni hayo hayo majabulani japokuwa hayana dhamana mara ngoma wavuni{muhimbili}dawa au chanjo ikipatikana taarifa itakuwa wazi sisi tunaoishi hapa tunaelewa pia kuwa hii dawa hata ikiwepo itakawia kuuzwa au kunadiwa kuwa ipo kwa sababu hivi sasa mashirika yanayotengeneza dawa zinazotumika kurefusha maisha RVS wanatengeneza hela kichizi sasa kulitafutia ufumbuzi suala hili na kuanza kuuza dawa za kuponya haya maradhi ni hasara kwao na hapa hapendwi mtu pochi tu sasa kazi iko hapo.
    mdau.
    mama sebene.
    alaska,usa.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 17, 2010

    DAWA HAIJAPATIKANA BADO - HII KITU HAIJAFANYIWA CLINICAL TRIALS. IT WORKS IN THE LAB TU. ACHENI KUTOA MESSAGE ZA UONGO.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 17, 2010

    This is absolutely shame.... embu jaribu kufungua website ya WHO kama unaweza kupata habari yoyote inayousiana na unayoyaeleza!!! Jamani mambo mengine waachie wenye utaalamu huo wayafanye... msiingilie kazi za watu.. Nafikiri hapa ni shetani anapata nguvu kwa habari kama hii.. watu wafanya ngono zembe wakijua dawa inapatika... source ya habari yako is not a reliable scientific web source...
    Watanzania dawa ya ukwimwi bado... na hayo ni majaribio ya mwanzo hambayo bado kabisa

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 17, 2010

    Bwana michuzi nashangaa sana kuona watu na hata baadhi ya viongozi wanasema dawa imepatikana. Hizi habari hizi zina madhara makubwa kwa taifa letu. hata ukiwa mtaani unasikia baadhi ya vijana wanasema sasa ni kavu kavu, unategemea nini? Kama wewe ni mtaalamu wa biology na unayejua kiundani biology ya virus huwezi kusema dawa kamili imepatikana maana virus ni zaidi ya kinyonga, anabadilika badilika kiasi kwamba hata ukimpatia dawa hii leo na ukifanikiwa kudhuru kesho huenda isifanye kazi kabisa maana anajibadilisha. Naombeni tusikurupuke. Mimi ninayesema haya ni mwana biologia kwenye level ya PhD, NA NAELEWA WAZI UGUMU ULIOPO, NA HATUA ZINAZO HITAJIKA HADI DAWA KAMILI IPATIKANE. Sasa kuwa ridhisha zaidi na ninayoyasema na kuhusiana na dawa watu wamesema imepatikana basi fungua link hii hapa http://www.ilsole24ore.com/art/tecnologie/2010-07-10/svolta-vaccino-antiaids-100625.shtml?uuid=AYEdDj6B&fromSearch#continue . watanzania tupendane na tuwe makini kwa kila jambo. hasa viongozi wetu msikurupuke. tembelea website ya who hutaona ukweli kwamba dawa imepatikana. let us all be smart in analysing important issues.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 17, 2010

    Ankal tafadhali epusha balaa hili. Hata kama hiyo dawa itapatikana tafadhali usitangaze manake hivi kinasemekana kuna dawa ya kuzuia hiv virus wasimsumbue muathirika watu wanaendelea na tabia za ngono kama kuna usalama je wakijua kweli kuna dawa ya kutibu si itakuwa msalie mtume. Michuzi Pleaaaaase take my comment into consideration. Usaidie taifa na families

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 17, 2010

    ukimwi kama Malaria! Kutokomezwa kwake hakuna tija kwa mabeberu, hivyo upatikanaji wa dawa ni ndoto! Kungekuwa na nia thabiti ya kuutokomeza, au magonjwa haya yangekuwa yanawaathiri watu wa ulaya na marekani, usingepita hata mwaka mmoja yangemalizwa!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 17, 2010

    Huyu mtu aliyeleta hii habari ni muongo, kwa kifupi hajui anachoongea.VRCO1 na VRCO2 zipo kwenye experimental stage siyo dawa na wala hazijajaribiwa kwa binadamu. Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani yaijathibitisha hii dawa kwa sababu FDA wanashughulika na dawa amabazo zimeshafikia stage ya clinical trial, VRCO1 na VRCO2 hazijafika hatua hiyo. Tafadhali ndugu katibu usitoe habari juu ya mambo usiyoyafahamu unaposha watu; waachie watalaam watueleze habari sahihi.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 18, 2010

    mimi nakubaliana na mdau hapo juu.kama ukimwi ungekua unauwa watu wenye ngozi nyeupe sana kama dawa ishapatikana cku nyingi .maana hii virus sio natural imetengenezwa mahaabara so ukicreeeti virus lazima ue na antidote yake antidote yake ipo wapijamani?
    hizi ni mbinu wamepanga za kutumaliza sisi watu weusi.maana tukizaa ni kumi naa wao kuzaa hawazii tena kwa sababu ya kupenda sterhe saana afu istoshe kwao kila kitu hekla lazima alipie babysitter hata mzazi wake hawezi kukaa na mjukuu eti kisa wazazi wametoka.vijana wao wadawa yamewaathiri na kuendekeza starehe hapa na pale so wazeee wao wakaaa wakamua kuturushia hili kombola langoma washindwe na walaani na vizazi vyao vyote makaburu.jihadharini jamani

    mdau kigali makazi bokxini kusaka chake

    ReplyDelete
  13. Mtu makiniJuly 18, 2010

    Huyu Katibu TA naona kama anashabikia sana dawa imepatikana k'sababu yeye ni mmojawapo wa kupenda kutembeza. katibu dawa ipatikane au la, tunza zip yako.mana unavyopigia debe it luks personal to me than announcing good news.wanawake wazuri hawaishi hivyo tuliza acha ushabiki. Hiyo dawa hata km imepatikana, unafikiri watapeleka Africa leo. Fikiria kuhusu wamama wanaojifungua, huku Ulaya kuna dawa za kupunguza au kuondoa uchungu wa kuzaa (epidural/gas n air), kwani hizo dawa ziko nchi ngapi Africa? mpaka leo Tanzania wanawake kibao wanakufa na kuteseka kwenye kuzaa. jiulize hilo. Hivyo pliz B4 you announce something omba ushauri kwanza au fanya research, usikurupuke tu kwa furaha zako kwamba utaendeleza kutembeza.

    ReplyDelete
  14. HUNA MAKOSA MTU WANGU KUTANGAZA KWANI WAHUSIKA WAMEWEZA KUTOA TANGAZO WENYEWE NAWE UKATEGA SIKIO LAKO KUWATIA MOYO WAATHIRIKA ILA WAAMBIE YA KWAMBA KWELI WAFUNGE ZIPU ZAO NA WANADADA WABANE KOFULI ZAO WASITOE TU UFUNGUO. NA KUWASHAWISHI MABROTHER WAKASHINDWA KUVUMILIA. SINA BUDI KUWASHUKURU WOTE KWANI MAONI YETU WOTE NI MAZURI. ILA WAPENDWA UKIMWI UNATISHA NA UNAUWA SISI TULIFURAHIA KUSIKIA HIVYO KWANI HAKUNA NYUMBA AMBAYO HAIJAPIGWA NA JANGA HILI LA UKIMWI. NAWASHAURI WENZETU WATU WEUPE WAACHE KUTUANGAMIZA KWANI KWA MUNGU WATAJIBU NINI? INGEKUWA WAO TAYARI DAWA INGESHAPATIKANA KAMA MAFUA YA NGURUWE MBONA ILIPATIKANA MARA MOJA,TENA NA MAFUA YA NDEGE.HAWA WATU TUNAWAINGIZA TU NCHINI MWETU LAKINI WANATUFANYA WANYAMA KABISA. WATADAIWA DAMU YETU NA MUNGU. ILA LA ZAIDI SANA TUNAWAACHIA MUNGU KWA ALIYETENGENEZA GONJWA LA KUWAANGAMIZA WENZAO. LABDA WANATAKA KURIDHI AFRICA KWA KUWA TUNA RASILIMALI NYINGI HUSUSANI TANZANIA. ZAIDI SANA TUMSII MUNGU KWENYE MAOMBI ATENDE.MAANA SISI WENYEWE HATUWEZI.
    MANKA

    ReplyDelete
  15. jamani hamna kitu kama hicho, watu tuacheni uzinifu mana hamna dawa ya ukimwi

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 13, 2011

    NI KWELI LAKINI ?AMA POROJO TU LAKINI MBONA OBAMA HAKUTANGAZA KAMA ALIVYOTANGAZA KIFO CHA OSAMA

    ReplyDelete
  17. Am Anyah kutoka Singapore. Ninataka kupitisha hili kwa kila mtu ambaye ni mgonjwa wa aina yoyote ya ugonjwa, suluhisho la magonjwa yote ni Dr Sagbo, niliponwa na mtu huyu Mheshimiwa Sagbo mponya mkuu baada ya kupita kwa maumivu. Sijui kamwe nitaponywa ugonjwa huu wa Hiv katika maisha yangu kwa sababu walisema hakuna tiba. Ninajaa msisimko na nina kutumia hii kati ili kukujulisha kuwasiliana na mtu huyu kwa aina yoyote ya ugonjwa na yuko tayari kusaidia kutatua tatizo lako. Ikiwa unapitia magonjwa yoyote kwa njia ya kumsiliana naye kwa njia ya barua pepe yake: drsagbo6088@gmail.com. Ninaweka ahadi yangu kwa kugawana ushuhuda huu ninawahakikishia wale wote ambao walisema kuwa hakuna tiba mbaya ya sababu nimekuwa tubiwa na dawa za dawa za Dr Sagbo mponyaji mkuu, lengo langu ni kushika ushuhuda juu ya kile ambacho Mungu ametumia wewe kufanya katika maisha yangu. Piga simu na nambari hii na whatsapp yake kwenye +2347019642881.

    ReplyDelete
  18. Je, wewe ni mwathirika wa VVU? Wala wasiwasi tena Dr Sagbo atawatendea na kukuponya dawa zake za mitishamba na utakuwa huru na kushuhudia mwishoni mimi ni ushuhuda wa kazi yake nzuri. Nilipata VVU mwaka wa 2012, niliambiwa na daktari wangu kwamba hakuna tiba inayowezekana kwa VVU. Nilianza kutumia ARV. Nilikwenda kwenye mtandao kutafuta kama kuna uwezekano wowote wa tiba unaopatikana, huko nimeona ushuhuda mwingi kuhusu Dk Sagbo Diba juu ya jinsi alivyotumia dawa za dawa za kulevya kutibu VVU. Nilimsiliana naye na kumwambia shida zangu, alinituma dawa ya mitishamba na nikichukua kwa siku 20, baada ya hapo nilikwenda kuangalia na nilikuwa na matokeo ya kuponya na mabaya. Ninafurahi sana sasa. Alisema anaponya, HEPATITIS B, CANCER, HERPES, DIABETES na mengi zaidi. Unaweza kumfikia juu yake
    Barua pepe.drsagbo6088@gmail.com na umwita +2347019642881.

    ReplyDelete
  19. Hujambo
    Mimi ni vivian Regobert
    ni kuweka maoni hii kwa wale ambao VVU na wanahitaji tiba
    Tiba ya Dk Muli Jonathan Herbal ni 100% kuhakikisha uhakika wa tiba ya VVU.
    Yeye kutibu aina yoyote ya ugonjwa.
    MUME wangu na alikuwa VVU kwa zaidi ya mwaka 9.
    Nilikuwa mgonjwa sana na mzigo wangu virusi alikuwa > 225,000 wa nakala/ml
    Niliona post kuhusu Dr Muli Jonathan mtandaoni jinsi ina kutibiwa watu wengi na jinsi sana yeye imesaidia watu wengi mtandaoni
    hivyo kuwasiliana naye na alielezea hali yangu kwake
    Aliahidi Nitumie dawa zake za mitishamba na baada ya 4days nilipokea dawa ya mitishamba MUME wangu na kutumika kwa dawa za mitishamba kwa ajili ya 10days na kisha akaenda kwa ajili ya mtihani upya
    Na sasa sisi ni HASI VVU
    Asante Dr Muli Jonathan kwa ajili ya kurejesha amani kwa familia yangu
    Mimi nina kushiriki ushuhuda huu kwa sababu niliahidi Dr Muli Jonathan kwamba mimi watakishuhudia baada ya mimi kuwa wamekuwa na kutibiwa.
    Inaweza kufikia Dr Muli Jonathan kupitia:
    mulijonathanherbal@Gmail.com
    Simu/Whatsapp: +2349038544302

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...