Bosi mpya wa NHC Bw. Nehemiah Kyando Mchechu

Shirika la Nyumba ya Taifa (NHC) limeanza kuwaondoa kwa nguvu baadhi ya wapangaji ambao wamebainika kuishi kwenye nyumba hizo kwa kurithishana badala ya kufuata utaratibu maalumu uliopangwa na shirika.

Hatua hiyo imewakumba baadhi ya wapangaji katika maghorofa ya Keko Mtaa wa Magurumbasi A ambapo kazi hiyo ilisimamiwa na viongozi wa NHC na Kampuni ya udalali ya Msolopa. Mwandishi wa gazeti la DarLeo alishuhudia mpangaji Pantalelo Mushi akiondolewa vitu vyake ndani ya nyumba chini ya usimamizi wa wajumbe wa nyumba kumi.

Ofisa wa NHC, Anneth Natai, amesema kumekuwa na mazoea ya wapangaji kuwarithisha watu wengine bila ya idhini ya uongozi. Kutokana na kitendo hicho, NHC imekuwa ikipatwa na usumbufu pindi kunapotokea tatizo na hata wengine kushindwa kufuata masharti yao. “Kuna wapangaji wengine wamekuwa wakilipa kodi kubwa kwa kuwapa wamiliki halali ambayo hata sisi hatuijui na pia tumekuwa hatuwafahamu wapangaji halisi,” amesema.

Amesema kazi ya uondoaji wapangaji wasiotambulika na NHC inaendelea ili kuwabaini na kuwaondosha. “Tunaendelea na kazi hii na wale wote ambao wanalipa kodi kupitia migongo ya watu tutawaondoa kwenye nyumba hata hivyo kila mtu ana haki ya kupanga ispokuwa afuate masharti na tabia ya kurithishana haipo isipokuwa kila mmoja anatakiwa kufuata taratibu,”amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 17, 2010

    Mmeanzia wapi KEKO. wahindi wote hao mjini mmewaruka. safisheni wahindi kwanza hapo mjini

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 17, 2010

    hivi hii nchi inamatatizo gani,jamaa alivyochaguliwa nilidhani NHC itabadilika,lakini utumbo ule ule,rais kasema hizo nyumba ziuzwe,nyie eti wapangaji feki,hii ni njama ya wafanyakazi wa nhc kuwatoa watanzania masikini kwenye hizo nyumba na kuwapa wahindi.rais kasema nyuma ziuzwe,wauzieni nyumba hizo raia,watu wapangaji feki ni wale wahindi wako mjini,na hamsubutu kuwafata.kama huyu jamaa anasoma huku anatakiwa ajue akianza siasa sirika hata liweza.uza nyumba mjenge nyengine.sio kuwasumbua waatanzania na kuwapa wahindi nyumba.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 17, 2010

    bosi mwenyewe kumbe mdebwedo,JK aliahidi nyumba kuuza tangu mwaka jana nyie mmekaa kuonea watanzania.NHC inaongoza kwa rushwa,wapo huyo mtanzania masikini itakuwa alitishwa pembeni akashindwa kutoa kidogo dogo,sasa ndo wanamkomoa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 17, 2010

    Manakimbilia Keko kwa wachovu mbona msiende hapo Upanga mnkawaondoa hao watu hapo...Acheni uonevu wa hali na mali...

    Mngeanza upanga na down down tungeelewa huko Keko ni uonevu tu weeeeeeeeweweeee...Mungu atakulaani

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 17, 2010

    hawa jamaa wameshasikia nyumba zinauzwa,wanataka waweke ndugu zao ili zikiuzwa wafaidi wafanyakazi.mshindwe na mlege

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 17, 2010

    ANZENI NA WAHINDI KWANZA SIO MNAWATOWA JAMAA ZETU TU, WAHINDI TENA MNAWAUZIA KIHOLELA.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 17, 2010

    Safi sana,inaonekana Bosi mpya ni kijana na kazi anaiweza.
    Ila naomba isiwe nguvu ya soda pia na wahindi wa Upanga waguswe na zoezi hili.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 17, 2010

    Yaani mie mwenyewe nimeshangaa, badala ya kuanzia town huko na mtaa wa uhuru majumba yote wakazi si halali wamerithishana, wamekodishana na wengine wameuziwa kabisa kwa mamilioni na wenyewe walouza nchini hawapo tena, watu kibao na wengi tunawafahamu, baada ya kuanza huko mnaanzia KEKO Magulumbasi??!!!!!!! Kwa mlalahoi??!!
    Au mnawapa nafasi matajiri wahame pole pole na kina kajamba nani wakale wapi POLISI??!!
    Mchhhhhewwwwsss!

    Hii kazi haistahili pongezi kabisa.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 17, 2010

    MBONA WANAWAONEA WALALA HOI. KWANINI HAWAJAANZA SEHEMU ZA MJINI, UPANGA, NA MAENEO MENGINE WANAYOISHI WATU WENYE UWEZO

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 17, 2010

    naungana na mdau wa kwanza juu kabisa,wanawaonea walala hoi keko wakati wahindi matajiri wamekalia nyumba hizi miaka na miaka.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 17, 2010

    Mnakimbilia huko kwa walala hoi Upanga,Town Area,Kariakoo etc imejaa wahindi mbona hamuendi huko Boko NHC mmewauzia wakubwa wakati mwanadai ni nyumba za watu wakima cha chini huku wakiwa wamepangisha watu Please NHC muwe serious na mambo yenu.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 17, 2010

    Dogo Mchechu umechemusha. Habari ndio hiyo.

    Kumbe iko naogopa Patel veve! Kwenda katimue timue mutu inakaa kwa kurithishana pale Kisutu na Upanga.

    Vacha onea hii dagaa dogo dogo ya Keko.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 17, 2010

    ni wazo zuri lakini mwende na Upanga yote adi kariakoo na uhuru apo ndo tutajua mko serious zaidi ya hapo tutajua ni cheap politics koz uchaguzi unakuja na who pays the price? mtanzania mlalahoi kama mimi na wewe!!! Nehemiah you can do better than this we know you since stanchart acha mawazo ya kisiasa na wasikuendeshe wanasiasaukafanya vitendo kama vya keko again in your life otherwise go to townand turn it inside out na apo Mungu atakusamehe...

    ReplyDelete
  14. Mpangaji NHCJuly 17, 2010

    NYIE HUYU JAMAA ATAYAFANYA YOTE HAYO,HUWA HAMUOGOPI MTU,ALIANZA KWA KULISAFISHA SHIRIKA NDANI KWA NDANI KWA MAANA YA KUPANGA KIKOSI KAZI KITACHOENDANA NA KASI YAKE,AKAFUTA HIII HABARI YA ETI NHC KUINGIA UBIA WA UJENZI WA MAJENGO YAKE NA WATU BINAFSI WAKATI SHIRIKA KAMA SHIRIKA LINAO UWEZO WA KUKOPA KWENYE MABENKI NA KUJENGA LENYEWE MAJENGO YAKE,KUNA WAHESHIMIWA KIBAO WALIKUA WANAMILIKI NYUMBA ZA NHC NA KUZIPANGISHA HUMU MIJINI KAMA MAOFISI WAULIZENI NINI KIMEWAKUTA?NYIE FUATILIENI HISTORIA YA HUYU KIJANA MTAJUA,HASHINDWI KITU AMA MTAMUONA ANA RESIGN AKIONA KUNA MAMLAKA INAMUINGILIA KWENYE UTENDAJI WAKE,WAULIZENI WAFANYAKAZI WA NHC JASHO LINAWATOKA SASA HIVI

    ReplyDelete
  15. Hadj Drogba "mwana chelsea"July 17, 2010

    wapangaji feki wanaozungumziwa hapa wala si walalahoi kama mnavyodhani,hapa wanasakwa watu waliopanga nyumba za NHC then na wao wakawapangisha watu wengine hivyo kujipatia fedha zisizo halali,mtu anailipa NHC let say 70,000 per month,yeye anampangisha Mr.PATEL Kwa usd 500 per month!!,jina kule kwenye records za NHC ni lake,so anachukua dola zake 500 kwa Patel anatoa tshs,70,000 analipa NHC,Hebu niambie kwa mwaka anatengeneza kiasi gani?a lot of money.Hao ndio wapangaji feki jamani,msikurupuke tu muacheni kijana asafishe shirika kwa kuwa hao wapangaji feki wengi wao ni maofisa wakubwa wa NHC Wanapanga hizo nyumba kwa majina bandia then wanawapangisha wahindi kwa mamilioni wakati shirika likiambulia vijisenti.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 17, 2010

    Kweli mjini wamejaa wahindi, lakini kuna swali moja. Asilimia 90% ya njumba za mjini za NHC kajenga nani ??? Jibu ni Wahindi. Usisahau kuwa siyo nyumba zote mjini ni za NHC. Wakati Nyerere alipotaifisha nyumba aliweka sheria kuwa mwenye nyumba akiwemo mhindi au mdosi) amabyo anaiaikalia mwenyewe hanyang'anyanwi, atanyang'awnywa nyumba za ziada (kama anazo).

    Kiufupi bado ziko nyumba nyengine ingawa ni chache ambazo zinamilikiwa na wahindi wenyewe..

    Another fact.. Kuna majumba mengine (kama vile old Empress Cinema) yalirudishiwa wamailiki wao wa zamani kabla ya kutaifishiwha, kwa hiyo ukumuona Mhindi anaikalia uione ajabu, siyo ya NHC tena

    NHC tujenge nyumba zetu wenyewe halafu tupangishane wamatumbi wenyewewe halafu tukiona wamejezana wahindi ndiyo tupige kelele.

    Kumbukumbu ya haraka nyumba alizojenga NHC ni zile za Keko , Magomen Mapipa nk.. Hizo anazo haki ya kuzianzia...
    Kama hujatosheka uliza upat zaidi.

    Mmatumbi mwenzako!

    ReplyDelete
  17. NHC acheni uongo, kweli mmeamua kuanzia keko si kwamba mnazitaka nyie hizo nyumba. mi kuna mtu (mfanyakazi NHC) kanihakikishia nikimpa Mil 5, napata nyumba. hakusema ni za wapi. Naungana na wadau, Hebu kawaondoeni kwanza wahindi kule Town...! acheni dhuluma mtakufa kabla ya muda

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 17, 2010

    hivi ukitaka kupanga kwenye nyumba hizo unafnayaje fanyaje au kama kawaida tumuone dalali wa vyumba?

    ReplyDelete
  19. Nyumba za NHC zilijengwa kwa ajili ya walalahoi, sasa cha kushangaza kina dewji, bora, manji, etc etc wote walikua wanakaa humo!
    Na baada ya kuhama wakawarithisha hizo nyumba ndugu zao!
    Bado watu kibao wenye uwezo wa kujenga nyumba zao wanakaa humo, itabidi tu watolewe.
    Ila NHC watafanya hivyo?? Nyoo!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 17, 2010

    Why waanzie Keko? Upanga je? Mjini kule? Au waifanye sambamba bila kujali sehemu. HAKUNA KITU HAPA WALALAHOI WATANGOLEWA THEN WATAPEWA WENYE PESA, NA WATAUZIWA.FULL STOP.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 17, 2010

    Nyumba za Oysterbay je Wale Wakuu wa magereza Kazi wamemaliza mpaka leo wanakaa pia mtawatowa? kule pia kuna Nyumba zenu kule pia inakuwaje au UPANGA inakuwaje Kariakoo inakuwaje Nyie mnakula na wale wa KEKO tu na ILALA nomaaaaaaaaaa wakatutowa tu tunaripuwa.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 17, 2010

    Broda you are not there yet..Go go go in those areas like upanga, Kariakoo and mnazi mmoja plse otherwise you have done nothing. Make sure huonei wanyonge. Watumishi wa umma wanahaha mjini wakati watu wanatanua magorofani..hakuna serikali inafanya hivyo duniani ni Tanzania tu kila kitu chake kipo ndivyo sivyo..Tutahama wasomi wote nchini tuwaache na udanganyika

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 18, 2010

    Halafu tunasema Tanzania hamna ubaguzi wa rangi.

    Karibuni maoni yote yanalalamika Wahindi watolewe kwanza. Kuna mdau mmoja tu aliyewatetea wahindi kwa kusema kuwa nyumba hizo walijenga wenyewe na Nyerere alizitaifisha.

    Kuna nyumba nyingi tu za Wahindi ambazo serikali wanazitumia sasa hivi kama ofisi zao. Kama tunataka haki basi warudishiwe hizo nyumba pia. Juzi juzi tu serikali ndio imeanza kujenga nyumba zao. Asilimia kubwa za ofisi zao ni nyumba za watu zimechukuliwa kwa nguvu. Sasa iyo haki iko wapi?

    Tunapenda sana kula bila kutoa jasho. Wenwetu wana umoja, wana mashule yao, hospitali zao na biashara zao. Hii ndio sababu ya kuwa na uwezo kuliko Mmatumbi. Sisi tunapenda kulalamika tu kila siku halafu tukiumwa tunakwenda India kutibiwa bure. Tukitaka kusoma zaidi, tunaomba scholarship za kusoma Mysore na vyuo vingine vya India. Waosha vinywa kuna neno la kiingereza, jaribu kuuliza uliza ujue maana yake. Neno hilo ni HYPOCRITE. Sisi wamatumbi ni Hypocrites.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 18, 2010

    nyerere alituzowesha wamatumbi vya bure, baada ya kuendeleza nchi akaamua kutaifisha mali za watu binafsi, nchi mpaka leo maskini, jamaa wote wamekaa wanacheza bao/vibambazani, viongozi wote mafisadi, ukitazama miji mingi bongo imejengwa na wahindi, nyumba zote zimepewa msajili ambao hata kupiga rangi wameshindwa, hawa jamaa wote wanalalamika kuhusu wahindi, jamaa hawa ni kama jamaa zetu wa sauzi ambao hawataki kuona waafrika wenzao kwenda sauzi!!!! tumekalia kulalamika na kutafuta scapegoats kila siku.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 18, 2010

    Nehemia, salaamu. Usishangae kauliza wabongo. Watanzania kila kitu ni kulalamika. Hata kama ungeanza kumtoa baba yako kwenye nyumba wangekushangaa! Wangesema 'mwone mjinga kaanzia kwa wazazi wake'. Kila mtu hapa ni mjuaji na mlalamikaji. Kwani nani kasema Keko hakuna wezi? Mwizi aibe mweupe, akiiba mweusi rukrsa! Huu ni ujinga.
    Mimi nakufahamu sana kwa utendaji kazi wako. Bado nakumbuka pale kwa Mzee Mwinyi tulivyokuwa tunapumzika kutokana na juhudi zako. Chapa kazi. Achana na Watanzania. kazi yetu na sifa yetu mpya ni ya kulalamika. Unafiki umenda kweli kweli, ndio maana kuna majibu yanatukana watu. mabingwa wa kutukana hawaweki majina yao wala namba za simu. Unafiki mtupu.

    Mimi naweka namba yangu 0713 335469. Naitwa Manyerere Jackton

    Mwenye hoja ajitokeze hapa tupambane, badala ya kumlalamikia Nehemia kwa kazi kubwa na halali anayoifanya.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 18, 2010

    Mchechu mbona unaangaika na madalali kusaka watu kwenye nyumba? Hapa issue ni rahisi tu. Ina maana kama watu wanapangisha nyumba za NHC halafu wanaenda kupangisha tena kwa third party ina maana NHC wanacharge rent dongo sana kulinganisha na bei ya soko ndiyo maana kuna watu wako tayari kulipa zaidi. Kuondoa hii tatizo dawa yake ni kupandisha kodi ili ilingane na ya sokoni.

    Issue nyingi kama watu wanaokaa kwenye hizo nyumba sio wampangaji wenye mikataba na NHC ina maana NHC imeingia mikata na agents wa ambao wenyewe hawaitajikaa kwenye hizo nyumba ila wamezichukua tu ili wachume faida kwa mgongo wa NHC. Kwa kufanya hivyo na kwa jinsi NHC inavyosema hii ni kinyume na utaratibu wa mikataba. Basi kama hii ndio hali yenyewe solution hapa ni kuvunja mikataba yote na kufanya ukaguzi nyumba hadi nyumba na mtu ambaye atakutwa anatumia hii nyumba ndio NHC iingie naye mkataba mpya. Hapa mtachukuwa details zote za huyu mtu ili baadaye muwe mnafanya ukaguzi wa ghafla kuona kweli bado wapangaji ni halali.

    Mchechu usitumia utaratibu wa madalali kufanya kazi, hizi ni mbinu za kizamani sana. Fanya kazi kitalaam, pandisha rent au weka mikataba mipya na hao wanazitumia hizo nyumba kwa sasa kwani hao ndio wakazi halali na wanazitaji hizo nyumba kwa ukweli wa kuzitumia, wengi na agents tu.

    ReplyDelete
  27. Badala ya kuwalaumu Wahindi ambao wako wachache sana nchini na ambao walijenga nyumba za NHC kabla hazijataifishwa na kupewa NHC, mlaumu hao viongozi mafisadi waswahili wenzetu wanaotafuna nchi!

    ReplyDelete
  28. mnawazungumzia wahindi lakini hamjui kuwa nyumba za nhc nyingi zilikuwa zinamilikiwa na wahindi kabla hazijataifishwa? wewe ujenge jengo ulaya halafu itaifishwe na serikali kisha wewe unakua mmoja wa wapangaji, ni haki kweli? wahindi wanalipa kodi kila mwezi, walalahoi wanasumbua miaka nenda rudi anataka kukaa bure!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...