Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi wa Teknolojia mpya ya kisasa Bwana Suchek Sanjay (kushoto )akipeana mkono na Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Capt. John chilligati (kulia) akikabidhi Nyumba iliyojengwa na Kampuni hiyo kwenye Maonyesho ya Nanenane mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Teknohama (ICT) wa Ardhi Bwana Elias Nyabusani wa kwanza kushoto akimwonyesha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi nyumba iliyojengwa na Kampuni ya Ujenzi kwa Teknolojia mpya (Space Creation LTD)Bwana Suchek Sanjay kwenye maonyesho ya nanenane mjini Dodoma.
Bwana Pato Ninje (wa kwanza kulia) wa Wakala wa Taifa wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi(NHBRA)akimwonyesha matofali ya udongo saruji yanayofungamana Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Capt. John Chiligati wa pili kulia alipotembelea maonyesho ya Nanenane mjini Dodoma.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. John Chilligati ( wa tatu kushoto )akiwa na mgeni wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ujenzi wa Teknolojia mpya ya kisasa (space Creation Ltd) Bwana Suchek Sanjay (wa pili kushoto) akikabidhi Nyumba ya mfano iliyojengwa kwenye Maonyesho ya nanenane Mkoani Dodoma.
Wafanyakazi wa Ardhi . Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Capt.John Chilligati na viongozi wa Kampuni ya Ujenzi wa Technolojia ya kisasa kwenye maonyesho ya nanenane mjini Dodoma.
(PICHA NA ANNA ITENDA WA GLOBU YA JAMII)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Michuzi naomba details za hawa watu please ntakutumia email yangu.

    ReplyDelete
  2. Ankal kwani bado tuna MAWAZIRI?

    ReplyDelete
  3. wewe anony wa 08;08am nawe mgumu kuelewa!hukusoma muongozo siku ile!aah!kuhusu hizo nyumba kwakweli hata mimi nahitaji hizo information.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...