Afisa Mnadhimu wa Polisi kikosi cha usalama barabarani, ACP Johansen Kahatano akiongea na wanahabari waliofika katika hafla fupi ya kukabidhiwa fulana na stika za usalama barabarani,kulia ni Meneja Mawasiliano wa TBL,Editha Mushi.
Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Editha Mushi akibandika stika ya usalama barabarani kwa moja ya gari zilizokuwa zikipita eneo hilo.
Askari wa usalama Barabarani,PC Faustina Ndunguru akibandika stika katika moja ya gari.


Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) leo imekabidhi vifaa mbalimbali kwa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya makabidhiano hayo jijini Dar es salaam Meneja mawasiliano wa TBL Bi Edith Mushi alisema Tbl imeona kuna umuhimu wa kutambua juhudi za Jeshi la polisi hasa kitengo cha usalama barabarani katika juhudi zake za kupambana na hali ya usalama barabarani hivyo tumeamua kutoa msaada wa baadhi ya vifaa ambavyo tunaamini vitasaidia kwenye juhudi hizo.

Bi Mushi alisema msaada huo kwa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani unatokana na TBL kutambua umuhimu wa usalama hivyo tunaamini vifaa hivi vitasaidia katika juhudi za kikosi hicho kwenye kusimamia sheria na taratibu za usalama barabarani.

Aidha aliwataka wenye vyombo vya usafiri na watembea kwa miguu kwa pamoja kuzingatia sheria na taratibu za usalama barabarani ili kuhakikisha ajali zisizo za lazima zinaepukika kwa kipindi chote”Ajali za barabarani zimekuwa chanzo kikubwa cha vifo na vilema kwa jamii ya kitanzania ajalinyingi zinachangia kuzorotesha maendeleo ya nchi yetu hivyo sote kwa pamoja tuungane kupinga ajali zisizo za lazima “alisema bi Mushi.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na fulana za mduara mia tano,Fulana na kola mia tatu stika maalumu zenye maelekezo mbalimbali ya mambo ya usalama barabrani mia tano, Vifaa vyote hivyo vina ujumbe juu ya matumizi salama ya barabara nchini Tanzania.

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya mkuu wa kikosi cha usalama barabarani ACP Johansen Kahatano aliishukuru kampuni ya bia nchini kwa juhudi kubwa inayofanya kwenye jamii ya Watanzania na kuahidi kuvitumia vifaa hivyo kwenye kampeni mbalimbali za kuhamasisha jamii juu ya usalama barabarani.

Kamanda Kahatano alisema kutolewa kwa vifaa hivyo na TBL ni ishara tosha kwamba inawajali watanzania na vifaa hivyo vitakuwa chachu ya mapambano ya ajali zisizo za lazima nchini hasa kwa kipindi hiki cha wiki ya nenda kwa usalama barabarani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

 1. Kwa nini askari wa barabarani abandike stika ya siku ya usalama barabarani kwenye gari amabayo siyo yake?
  Ni kifungu gani kinacho mmpa madaraka hayo? Je, mwenye gari ana haki ya kukataa gari lake lisibandikwe stika hiyo bila kusumbuliwa na askari huyo?

  ReplyDelete
 2. kwa stika na fulana tu, walevi wa mataptap watakoma.

  ReplyDelete
 3. BINAFSI NAWAPONGEZA SANA CRDM YA MZEE KIMEI KWA MISAADA YAO YA AKILI NA GHARAMA KWA JAMII,NADHANI NYINYI TBL INABIDI MUIGE MFANO WA CRDB,NJIE MNATOA KIDOGO SANA MARA MIL5 MARA 10,WHAT MAMBO HAYO,TUTAKUWA HATUPIGI MITUNGI

  ReplyDelete
 4. kilichoniacha hoi ni picha ya pili.Hizi gari bado zipo barabarani? Angalia hizo rearview mirrors sehemu zilipo utadhani bado tupo 1960s.

  ReplyDelete
 5. Fausta Bigup!!!!!!!!! Hi to Fanuel

  ReplyDelete

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...