MWAKILISHI MPYA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA UMOJA WA MATAIFA, BALOZI OMBENI SEFUE AKIMKABIDHI KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA BAN KI MOON HATI ZAKE ZA UTAMBULISHO.
MWAKILISHI WA TANZANIA KATIKA UMOJA WA MATAIFA, BALOZI OMBENI SEFUE AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA, WA KWANZA KUSHOTO KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI KIONGOZI SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR. MHE. MSHAM ABDULLA KHAMIS, BI ABEIDA RASHID ABDALLA, MKURUGENZI WA IDARA YA WATU WENYE ULEMAVU, OFISI YA WAZIRI KIONGOZI(ZANZIBAR) NA NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI, DKT. SERVACIUS LIKWELILE. MUDA MFUPI MARA BAADA YA KUKABIDHI HATI ZAKE ZA UTAMBULISHO BALOZI OMBENI SEFUE AKIWA NA BAADHI YA MAAFISA UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA UMOJA WA MATAIFA

NA MWANDISHI MAALUM
NEW YORK-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amemtakia kampeni njema , Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, na mafanikio mema katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba.


Ban Ki Moon ametoa salamu hizo wakati wa Mazungumzo yake na Mwakilishi mpya wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ombeni Sefue, mara baada ya Balozi huyo kumkabidhi hati zake za utambulisho katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Katibu Mkuu wa UN, pamoja na kumtakia kila la kheri na mafanikio Rais Kikwete, pia amempongeza Rais Kikwete na Tanzania kwa ujumla kwa kuwa nchi kiongozi na ya mfano wa kuigwa Barani Afrika katika kutekeleza na kuendeleza malengo ya Umoja wa Mataifa. Hususani amani na usalama Duniani.


Aidha Ban Ki Moon, ameonyesha imani kubwa kwa mwakilishi huyo wa Tanzania huku akimpongeza kwa nafasi za ubalozi alizoshika nchini Kanada na Marekani kabla ya wadhifa wake huo mpya.


Akamtaka kuendeleza msimamo wa Tanzania wa kuwa nchi kiongozi katika Afrika na ndani ya Umoja wa Mataifa kwa kudumisha na kuendeleza malengo yenye maslahi kwa Serikali ya Tanzania, Bara la Afrika na Umoja wa Mataifa kwa ujumla.


Ban Ki Moon akatumia pia nafasi hiyo kutoa shukrani zake, kwa mtangulizi wa Balozi Sefue, Balozi Augustine Mahinga ambaye katibu Mkuu alimteua kuwa mwakilishi wake maalum huko Somalia.


Katibu Mkuu akabainisha kuwa kutokana na heshima kubwa ambayo Tanzania imejijengea ndani ya Umoja wa Mataifa, anaitegemea Tanzania katika kuwasiliana na mataifa mengine hasa yale yanayoendelea.


“Tanzania mmejijengea heshima kubwa ndani ya Umoja wa Mataifa, kwa hiyo usitegemee kuwa utakuwa unaisemea Tanzania peke yake, bali na mataifa mengine pia, na hilo ndio tegemeo langu kubwa kutoka kwako Mhe. Balozi” akasisitiza Ban Ki Moon.


Katika mazungumzo hayo, Katibu Mkuu amemhakikishia Mwakilishi huyo wa Tanzania ushirikiano kutoka kwake yeye binafsi na sekretariati ya Umoja wa Mataifa.


Kwa upande wake, Balozi Ombeni Sefue amemwahidi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kwamba atafanya juhudi zote kuendeleza maslahi ya Tanzania katika UN, kudumisha ushirikiano mzuri kati ya UN na Tanzania, na kuchangia katika kuendelelezaji wa majukumu na malengo ya Umoja wa Mataifa.


Akatumia nafasi hiyo Kumpongeza Katibu Mkuu kwa kusimamia vema utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia, huku akimwomba aendelee kuzihimiza na kuziomba nchini zenye uwezo mkubwa kiuchumi ziendelee kuzisaidia nchi zisizokuuwa na uwezo ili ziweze kutekeleza Malengo ya Maendeleo ya Millenia.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. mh. majority wamenona

    ReplyDelete
  2. Kama CCM wanaweza kumnunua hata Ban Ki Moon, basi mliopo Bongo poleni tuu, na msishangae kwamba inakuwaje CCM wanamnunua ankal wenu Mithupu.

    Mithupu na wewe endeleza libeneke la CCM tuu, lakini kumbuka "Nuremberg trials"..., na wewe pia utakuwemo zamu yenu ikifika.

    ReplyDelete
  3. Msham sikuweza kumjuwa bila ya kusoma jina lake namkumbuka tukiwa paunia pale jimkana ZANZIBAR wakati Ule Rais akiwa Mzee Aboud bin Jumbe lakini sasa naona amekonda na ameanza kuonesha umri

    ReplyDelete
  4. Kaka Mithupu nimevutiwa sana kuona mwanamke wa kitanzania "mlemavu" anamadaraka kama haya Hongera sana bibie. na bro mithupu kama utapata nafasi ya kumuinterview ili iwe changamoto kwa walemavu hasa watanzania. Godbless Tanzania.

    ReplyDelete
  5. BALOZI SEFUE HONGERA SANA, TANZANIA HOYEEEEE.
    SASA ANGALAU TUNA WEZA KURINGA MAANA TUNA MTU WAKUTUWAKILISHA UMOJA WA MATAIFA. MTU SAWA SAWA

    ReplyDelete
  6. SEFUE HOYEEE, WAPARE HOYEEE....MBONA WAPARE WANAWEZA SANA DIPLOMASIA?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...