Mkuu wa idara ya Afrika, Asia na Mashariki ya Kati wa Radio ya Ujerumani Dr Utter Schafer akipeana mkono na mtangazaji mkongwe wa Idhaa ya Kiswahili Bw.Ramadhani Ali huku mkuu wa idhaa ya kiswahili Andrea Schmidt akiangalia jioni hii katika ofisi za radio hiyo maarufu duniani mjini Bonn katika mnuso mdogo wa kumuaga rasmi mkongwe huyu baada ya kupiga mzigo hapo DW kwa miaka zaidi ya 40.
Mkuu wa Idhaa Andrea Schmidt akiwa na Ramadhani Ali akiwa kakumbatia rundo la zawadi alizopewa baada ya kuitumikia idhaa ya kiswahili kwa miaka zaidi ya 40 ambapo leo amestaafu na kuagwa rasmi
Watangazaji nguli toka shoto Sekione Kitojo 'Bundes', Ramadhani Ali,
Abdul Mtullya 'Konkoo' na Aboubakary Liongo ' Shekhe' Toka shoto ni watangazaji Bi. Halima Nyanza, Bw. Mohamed Abdul-rahman, Bw. Aliyu (wa Idhaa ya kihausa)na Aboubakary Liongo





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. heh jamani watangazi wengine nilikua nasikia tu majina yao nikiwa mdogo...Aboubakary Liong na Sekion Kitojo ...Hee nimekumbuka zama za kale... Sauti zao zilikua nzuri sana...Hiyo redio Ujerumani ya kiswahili tunaiipataje kwenye internet?

    ReplyDelete
  2. Heh jamani huyu babu atarudi bongo au ndo ashakuwa raia German?

    ReplyDelete
  3. Happy October 1st Beer Festival in Germany..
    Kuleni pombe wakongwe.

    ReplyDelete
  4. Jamani caption ya hiyo ya picha ya pili toka juu inasema huyu mstaafu kakumbatia "rundo" la zawadi.. jamani mi naona kashika ki box cha redio.. sasa hilo rundo la zawadi li wapi? hebu tuwe makini kuandika caption

    ReplyDelete
  5. Good! time to spend your pensions.
    Dont swap jobs like Tido.
    you really had great career,ur already missed!

    ReplyDelete
  6. Kumbe Abubakar Liongo yupo Deutsche Welle? Nilikuwa najiuliza kapotelea wapi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...