JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII



TANGAZO LA KAZI

Serikali inaendelea kufanya maboresho ya Sekta ya Afya kupitia Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) ikiwa ni pamoja na kuongeza vituo vya kutolea huduma, kuongeza idadi ya watumishi pamoja na kuboresha maslahi ya watumishi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ametoa Kibali cha Ajira kwa Wataalam wa Kada za Afya 7,471 kwa mwaka wa fedha 2010/2011 ili kutekeleza azima hii; Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, anapenda kuwatangazia wale wote wenye taaluma zifuatazo:-

Madaktari, Wafamasia, Maafisa Wauguzi, Wauguzi, Maafisa Afya, Wateknolojia wa Maabara/Mionzi/Dawa, Maafisa Tabibu na Matabibu Wasaidizi kwamba, Wizara ipo tayari kuwapangia kazi.

Wahitimu waliofuzu Mafunzo ya Afya, katika mwezi Julai, 2010 pamoja na Matabibu Wasaidizi waliohitimu Oktoba, 2009 watapangiwa kazi moja kwa moja na hawatalazimika kutuma maombi. Majina ya waliopangiwa vituo vya kazi yatatangazwa kwenye Magazeti na Tovuti ya Wizara www.moh.go.tz.

Pia Wahusika watatumiwa barua za kupangiwa kazi katika anuani zao za posta, na kwa waajiri wao watakakopangiwa.


Aidha, Waombaji wengine wanatakiwa kutuma maombi yao kwa Katibu Mkuu kwa kutumia Anuani iliyotajwa hapa chini. Muombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-

1. Awe ni raia wa Tanzania.
2. Awe na umri usiozidi miaka 45.
3. Wale wenye umri wa miaka zaidi ya 45 wataajiriwa kwa Mkataba baada ya kuombewa Kibali kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Waombaji wanashauriwa kupendekeza Halmashauri tatu ambazo wangependa kupangiwa kazi. Hata hivyo Wizara itatoa kipaumbele zaidi kwa Halmashauri zilizopo nje ya Dar es Salaam, na upangiwaji wa vituo utategemea uwepo wa nafasi wazi katika Halmashauri hizo.

Maombi yote yaambatanishwe na:-

1. Nakala ya Cheti cha Taaluma
2. Nakala ya Cheti cha Kidato cha nne/sita

3. Maelezo binafsi (CV) ikijumuisha anuani kamili, umri na namba ya simu ya kiganjani.
4. Picha (Passport size mbili) za hivi karibuni
5. Nakala ya Cheti cha usajili kutoka baraza la taaluma husika.

Vyeti vyote vya Taaluma na Kidato cha nne/sita vithibitishwe na Hakimu au Wakili.

Barua zote zitumwe kwa:-


Katibu Mkuu,
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
S.L.P. 9083,
DAR ES SALAAM.

kwa taarifa zaidi tembelea tovuti hiyo hapo chini

www.moh.go.tz

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Ubaguzi wa Umri Tanzania:

    Umri wa kustaafu kazi kwa lazima Tanzania ni miaka 60. Kwa hiari ni miaka 55. Kwa kigezi hicho, ni vipi serikali ya Tanzania inaainisha kuwa wenye umri wa miaka 45 hawastahili ajira ya moja kwa moja, isipokuwa kwa kibali maalum?

    Huu ni ubaguzi wa wazi wazi wa umri na unakatisha tamaa wale wanaotafuta kazi wenye umri uliozidi miaka 45.

    Nimepata kuona pia matangazo ya kazi yanayozuia ajira kwa wenye umri uliozidi miaka 35!

    Hivi hii imekaaje?

    ReplyDelete
  2. hivi hii wizara si ina sehemu ya social work.. mbona hawatangazi au ililazimishwa kuwekwa tu? wakati watu wa social work ni muhimu sana pia katika kila hospitali

    ReplyDelete
  3. Ni kweli umri wa kustaafu ni miaka 60 ila kawaida mtu ili aweze kupata mafao ya uzeeni anapostaafu ni lazma uwe umefanya kazi angalau miaka 15 ili utakachopata kikusaidie. Endapo umri wako ni miaka 45 sidhani kama utakuwa umeonewa kwa sababu unaajiriwa kwa mkataba utachangia mifuko mingine ila si ya watu wa masharti ya kudumu kwani hata calculation zitakuwa tofauti.

    ReplyDelete
  4. 2010,vijana zaidi.

    ReplyDelete
  5. nafasi za maafisa ustawi wa jamii hutolewa pamoja na kibali cha kada zingine,kama watu wa it,procuament,nakumbuka kuna kipindi kama sio mwishoni au mwanzoni mwa mwaka huu walitangaza nafasi kibao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...