Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa huko Somalia Dr augustine Mahiga akiwa na mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya redio ya Umoja wa Mataifa Bi. Flora Nducha baada ya mahojiano yao leo huko New York, Marekani

Muungano wa Afrika (AU) wataka
msaada wa UN kuinusuru Somalia

Hali ya usalama nchini Somalia bado ni tete, huku mamilioni ya watu wakiendelea kuwa wakimbizi wanaotegemea msaada wa kitaifa na kimataifa ili kuishi. Nchi jirani pia zimeingiwa hofu kutokana na ukweli kwamba wanamganbo wa Kiislam wa Al-Shabab wanatafuta nguvu za ziada kutoka nje kwa lengo la kuitoa madarakani serikali ya mpito.

Sasa muungano wa afrika umelivalia njuga suala la Somalia na umelitaka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kutoa msaada wa ghali na mali ili vikosi vya kulinda amani vya muungano wa afrika Somalia vifanikishe azma ya kuleta amani Somalia.
Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa Somalia Dr augustine Mahiga amemweleza mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa Flora Nducha kuwa ombi hilo lisipotekelezwa basi Somalia itaishia mikononi mwa magaidi.

Wasikilize kupitia
au moja kwa moja kwenye mahojiano yenyewe
http://www.unmultimedia.org/radio/kiswahili/detail/114852.html

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...