JK akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Igunga,Rostam Aziz katika uwanja wa SabaSaba mjini Igunga mchana huu

Mshairi Mwana Igunga akighani leo
Mwanaigunga akipongezwa na JK baada ya kughani shairi zuri sana
Mh. Rostam Azizi akihutubia umati uwanja wa SabaSaba Igunga leo
JK akisalimiana na wana Igunga leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Masikini Tanzania nchi yangu!

    ReplyDelete
  2. Ni aibu kwa Taifa, ni aibu kwa watanzania, ni aibu kwa Rais kumnadi Rostam Aziz. Ni ni ambacho tunawaambia watanzania maskini wanaotaabika kwa matendo ya kifisadi yanayofanywa na mtu huyu na genge lake? Unawaambia nini wale wanaokosa maji, dawa, elimu bora, chakula na makazi bora kwa kucheka na kutabasamu na RA mbele ya umati? Utu upo wapi? Kwa nini tunawafanya watanzania maskini na hohehae ngazi ya kupandia kwenye madaraka na kisha kuwakumbatia maskini? Inasikitisha sana!

    ReplyDelete
  3. huyu prezidaa sasa anafika mbali,kweli nchi imeuzwa.

    ReplyDelete
  4. naam Igunga,

    Hapo ndio nilipopata Elimu ya msingi. Nimesoma shule ya Msingi Iginga, al maarufu kama "Msingi", Namkumbuka Rostam alivyokuja kuomba kura mara baada ya kufariki kwa Mh Charles Kabeho. Rostam, tulimuuita "mburushi", ndo kwanza alikuwa ametoka USA kupata MBA yake, tukaona, vipi huyu msomi wa kiburushi anakuja kuchezea vumbi huku? Duh kumbe he was Clever, i think by now i understand, i wish to do an MBA like his. Salaam kwa wa Igunga wote, kuanzia Itumba hadi Mbutu, Makomero hadi Mwanzugi, Vipi wale wa Chipukizi mpo? nasikia stendi imejengwa kule karibu na uwanja wa mpra, nakumbuka timu zetu za Irrigation (Mhindo Msola), Town Stars, Kurugenzi, wachezaji kama kina Noah Kilimanjro etc, nita rudi tena, wasalamie pia kule "Uarabuni", vipi ilie ngome ipo bado? maana ilikuwa uarabunikweli.

    Mdau Kiwoso UK

    ReplyDelete
  5. Duh! kazi kweli kweli, watu corrupt kishenzi lakini wanapigiwa kampeni na ccm. nchi hii imeharibika sana yaani watu hawana hata aibu, jamani hivi mpaka mtu ashikwe red handed ndo tuamini kuwa ni ma-corrupt? lowassa, rostam na mramba hawa tunawajua kuwa ni wezi.

    ReplyDelete
  6. Wewe Mdau Kiwoso wa Uk ..Ni mjinga kupita maelezo.Sasa kiparagraph chote hicho,I thought utamake sense kumbe unatuma salaam.Michuzi didn't post them pictures and Info for you to write mindless things but to comment regarding the news.Mwenzio ana MBA wewe utaishia kuosha vyombo..Halafu kwanini unamsifia wakati he do corruption anyway.n.I wonder why you have to ask them damn questions.You just pissed me off big time.I wish I could meet and give you a good punch on your stupid face.

    ReplyDelete
  7. Semaa, usiogope semaa!
    Safi sana JK. Pigia kampeni watu safi waendelee kukusaidia kujenga taifa letu. Watu wenye wivu wa kike ni wa kuwaEPA kabisa.
    Ari zaidi
    NGUvu zaidi
    KAsi zaidi!

    ReplyDelete
  8. ACHENI UBAGUZI NA UMBEA!
    HE IS STILL INNOCENT UNTIL HE IS PROVEN GUILTY!
    Kama unayo data za uhakika zimwage basi, sio kumhukumu moja kwa moja!

    ReplyDelete
  9. ACHENI UBAGUZI NA UMBEA!
    HE IS STILL INNOCENT UNTIL HE IS PROVEN GUILTY!
    Kama unayo data ya uhakika zimwage basi, sio kumhukumu moja kwa moja!

    ReplyDelete
  10. Watanzania bwana mnachekesha sana....mnashangaa nini kwani...kuna cha ajabu hapo??? hata ningekuwa mimi watu wangu wa karibu lazima niwape shavu hata kama wakitafuna nchi yote....washkaji wa karibu ndio watakao kuokoa....hata kama wakiwa mabedui kiasi gani ningewapa maisha...nyie endeleeni kuosha vinywa weee mpaka mwisho...then mkasiamame masaa matano kwenye mistari ya kupiga kura...MWISHO WA SIKU NCHI INA WENYEWE..NA KWA TAARIFA YENU WAWILI KATI YA HAO MAFISADI WATARUDI SERIKALINI KAMA MAWAZIRI!! MTAKOMA!

    chaos JT

    ReplyDelete
  11. mie simlaumu RA,nalaumu wanaompa kura.Hajawahi kuongea bungeni

    ReplyDelete
  12. Mpewa hapokonyeki.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  13. Chadema,hamtaingia Ikulu na wala hamtakuwa na wabunge wengi!

    Kuna kilio na kusaga meno!

    ReplyDelete
  14. Wewe "Tarehe Sat Oct 02, 12:32:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

    mie simlaumu RA,nalaumu wanaompa kura.Hajawahi kuongea bungeni"
    Rostam is more business man than a politician. Angalia picha ya kwanza hapo anavyotambulishwa na JK yaani jamaa hadi anaona noma mwenyewe. Ila ndio Mbunge anayepita bila kupingwa tokea achukue jimbo toka kwa Kabeho. Hajawahi kuuliza swali au hata ku comment chochote bungeni. Haitaji kufanya hivyo kwani anajua atashinda tuu kwa kishindo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...