Balozi wetu nchini Japan Mh. Salome Sijaona akitoa salamu
kwa wanachama wa Tagawa Lions Club wakati wa
maadhimisho ya miaka 50 ya club hiyo jijini Tagawa leo
Mhe. Balozi Sijaona akiwa na viongozi wa Tagawa Lions Club
pamoja na Meya wa mji wa Tagawa.Mhe. Balozi Sijaona akipokewa kwa vifijo wakati alipokuwa akiingia kwenye ukumbi kwa ajili ya sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Tagawa Lions Club.
Tagawa Lions Club iliyopo katika mji wa Tagawa, mkoa wa Fukuoka, nchini Japan ilifanya sherehe ya kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.
Sherehe hizo zilihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe. Salome T. Sijaona ambaye alikuwa mgeni rasmi.Klabu hiyo itaendelea kutekeleza shughuli mbalimbali kama sehemu za maadhimisho hayo.
Moja ya shughuli hizo ni kuwaalika wasanii wa michoro ya Tingatinga kutoka Tanzania kuja kufanya maonyesho ya kuchora katika mji huo na kuuza michoro watakayoiandaa.

Huo ni mkakati mpya wa kuanzisha uhusiano wa kiutamaduni kati ya mji huo na Tanzania. Aidha, ni njia nzuri ya kuitangaza sanaa ya Tingatinga nchini Japan.Picha na Mdau Willna wa Globu ya Jamii, Nagoya-Japan.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...