Jumuiya ya watanzania ugiriki inapenda kuitumia fursa ya uchaguzi uliofanyika 31/11/2010 kuelezea machache yafuatayo:

1. Inatubidi watanzania popote tulipo tupongezane kwa kujikuta tunaendelea kupata maraisi kwa njia ya kura tangu tulipoungana 1964.Si siri kwamba mabalaa yanayotokea katika nchi za wenzetu wakati wa uchaguzi HAKUNA HATA MMOJA ANGEPENDA YATUTOKEE NCHINI KWETU.

2. Busara na ushujaa uliotumiwa na viongozi wetu walioshindwa kuchaguliwa na wakaamua haraka kuwapongeza walioshinda ni dalili ya wazi kwamba TUNAPIGA HATUA KUELEKEA MBELE.

3. Tunaelewa vizuri kwamba bado kutakuwa na wengine wataolaumu na kutuhumu kwamba uchaguzi ulikuwa na makosa na hata ulaghai, lakini hoja hizi haziwezi kuvunja ukweli usiopingika kwamba uchaguzi ulimalizika bila mabalaa makubwa yanayotokea katika nchi za wenzetu.HAKUNA kitu kilicho kamili duniani.Hata uchaguzi wa awamu ya pili ya GEORGE BUSH ulikuwa na matatizo na kasoro.Ni vizuri tuanze kujijengea ile hali ya kuangalia mengi mazuri na kuyapuuza mabaya machache.

4. Mwisho, watanzania kuwa na vyama tofauti ni hatua nzuri kuelekea katika demokrasi. Isipokuwa itasikitisha na kukatisha tamaa kama watanzania tutakuwa tunafuata chama fulani na kuwaona wale wengine wasiokuwa katika chama chetu kama ni maadui.Hali hii itaturudisha nyuma na inatubidi sote kwa pamoja tuipige vita.

Mwenyezi Mungu endelea kutulinda na kutubariki watanzania (Amen).

KAYU LIGOPORA

KATIBU MKUU

http://www.tanzaniansingreece.com/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

 1. NA HAO WANAJIDAI KUISHI HUKO WASHINGTON NA KUFANAY MAANDAMANO YA KUPINGA MATOKEO HAO NI WAKUKEMEWA KABSAA...WAO WANACHOCHEA KWA VILE WAO WAMEJIONA WAKO NJE YA TANZANIA HATA MATATIZO YAKITOKEA HAYATAWAHUSU NI WAONGO NA NI WANAFIKI TUNATAKIWA KUWAOGOPA KAMA UKOMA....

  WAO NI WATUMWA BABU ZAO WALIKATAA KUCHUKULIWA KUPELEKWA NCHI ZA WATU LAKIN WAO WAMEUKIMBILIA..PAMOJA NA HAYO WANAJIDAI WANA UCHUNGU NA NCHII MBONA HAWARUDI MAKWAO WAKAJENGA NCHI??? MBONA HAWACHANGISHANI WAKAJENGA MAHOSPITAL AU SHULE/...AU HATA KULETA WAHISANI AU VIFAA VYA SHULE....WANAJIDAI KUWATETEA WENZAO WA TZ KWA KUCHOCHEA CHUKI ZA KUANDAMANA BADALA KUWATETEA WENZAO WA TZ KWA KUWALETEA MAENDELEO.....HAO NI WANAFIKI...HONGERENI JUMUIYA YA UTURUKI KWA KULIONA NA KUKUBALIANA NA MATOKEO...

  ReplyDelete
 2. We fanya unachofanya uko Ugiriki, mambo ya huku tuachie sisi. Hata uchaguzi wenyewe hujui ulifanyika lini.

  mambo ya kulinganisha uchaguzi wetu na matatizo ya George Bush ni kupoteza mwelekeo. Kasoro za hapa zisifananishwe na za sehemu nyingne, tuzitatue sisi WaTZ wenyewe!!

  ReplyDelete
 3. Upuuzi mtupu.
  Na mkae hukohuko utumwani msirudi tena!

  ReplyDelete
 4. Anonymous wa kwanza, kwanza acha kupiga kelele kwa kuandika kwa herufi kubwa, it is most annoying! Pili, acha upumbavu wa kutaka kuwachagulia watu sehemu ya kuishi. Wewe kama umeshindwa kutoka Tanzania ni shauri yako, usilete uzalendo feki wa kwa sababu umebaki Tanzania, wote waliondoka wana kasoro fulani. Na kama utumwa kumbuka ata Tanzania kulikuwa na utumwa. If you ask me, naweza kukuambia waliokuwa watumwa nchi hizi mambo yao poa kuliko waliokua watumwa Tanzania. At least huku hamna umeme wa mgao na maji ya dhiki.

  Endeleza nchi, my foot? Nani amekupa madaraka ya kuwachagulia watu sehemu ya kuishi? Wewe hutoshi kuendeleza nchi? Rudi shule upate elimu kidogo itakusaidia kuchambua mambo kwa fikra na utulivu. Hiyo jumuiya ni ya Ugiriki, siyo Uturuki; go figure!

  ReplyDelete
 5. TATIZO KUBWA TULILO NALO BINDAMU NI KATIKA KUDHARAULIANA MTANZANIA AKIWA NJE AA NDA YA NCHI NI MTANZANIA NA HUKUNA MWENYE HAKI YA KUSEMA HUYU HANA HAKI. MIMI USHAURI KWA RAISI NI KUBADIRISHA KATIBA NA KUIFANYA IKIUBALIKE KWA WATANZANIA WOTE ILI KUONDOA MATATIZO KATIKA CHAGUZI ZA MBELE ILI KUILINDA NCHI YETU KATIKA UTULIVU WA KUDUMU MILELE BADALA KUWEKA MATATIZO YANOYOWEZA KUHARIBU NCHI YETU AMBAYO INASIFA YA UTULIVU NJE NA NDANI. MFANO MZURI NI ZANZIBAR SHERIA IMETUNGWA NA CCM PAMOJA NA CUF. SIKU ZOTE HAKI HULETA MAPENZI NA MAENDELEO YA KUDUMU. HIVYO USHAURI WANGU MKUBWA RAISI WETU KIKWETE AWEKE HISTORIA KATIKA MAISHA YAKE YA AKHERA NA DUNIA KWA KUBADIRISHA KATIBA AMBAYO ITAWAJUMUISHA VYAMA VYOTE ILI HUKO TUENDEKO TUSIPATE MATATIZO AMEN

  ReplyDelete

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...