Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dr. Jakaya Kikwete akiwa katika gari maalum pamoja na mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange wakati wakiingia katika uwanja wa Uhuru kwa ajili ya shughuli ya kuapishwa kwa Rais Jakaya Kikwete.
Wanausalama wakiingia kwa staili ya aina yake wakati Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akiingia kwenye uwanja wa Uhuru leo.
Marais wa nchi mbalimbali wamehudhuria katika sherehe za kuapishwa kwa rais Jakaya Kikwete kutoka kushoto ni rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, Rais Joseph Kabila wa DR Congo, Rais Rupia Babda wa Zambia Mke wa Rais wa Zanziba na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mama Mwanamwema Shein, Kiongozi wa Kutoka Swazz na wageni wengine.Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma naye amehudhuria katika Sherehe hizo kama unavyomuona akielekea jukwaa kuu.
Ankal akiwa na mdau wa habari,Adam Gille wakati sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete zikiendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Wageni mbalimbali wakishuhudia sherehe hizo mchana huu.
Huu ni umati wa wageni waalikwa katika jukwaa la upand wa kulia kwenye uwanja wa Uhuru ambapo sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Kikwete zikiendelea.Picha Zote Na John Bukuku na Tinganya Vincent.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. hongela JK kwa kuapishwa watanzania bado wana iman na wewe so keep cool presdaaaaaa!!!tuijenge tanzania yetu. mungu ibariki TANZANIA mungu mbariki raisi wetu, tuendeleze amani iliyopo nchini kwetu. yaliyopita yamepita tugange yajayo.
    AMEN.

    ReplyDelete
  2. Tunashukuru Mungu uchaguzi umeisha salama. Sasa tuungane pamoja kujenga taifa letu kwa bidii.

    Zemarcopolo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...