Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Mh. Jordan Rugimbana (kushoto) akimkabidhi bendera ya Taifa,Nahodha wa timu ya Taifa ya Pool,Aliakber A. Aliakber ambao wanataraji kuondoka leo usiku kuelekea nchini Ufaransa kushiriki mashindano ya Dunia ya mchezo huo.katikati ni Meneja wa Bia ya Safari Lager ambao ndio wadhamini wakuu wa mchezo huo hapa nchini,Fimbo Buttallah.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Mh. Jordan Rugimbana (katikati) akizungumza machache katika hafla fupi ya kuiaga timu ya Taifa ya Pool inayotaraji kuondoka nchini leo usiku kuelekea nchini Ufaransa kushiriki mashindano ya Dunia ya mchezo huo,katika ukumbi wa mikutano wa kampuni ya Inter Grated,iliopo Kinondoni Moroco.kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Pool Taifa,Fredy Mushi ambaye ataambatana na timu katika safari hiyo,na kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager,Fimbo Buttallah.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Pool,Dennis Lungu akihojiwa na wanahabari juu ya jinsi walivyojiandaa na mashindano hayo huku akiwa amezungukwa na wachezaji wake.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa wanaotaraji kuondoka leo usiku kuelekea nchini Ufaransa kwa kushiriki mashindano ya Dunia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...