Watu toka taasisi ambayo haukuweza julikana mara moja wakipima eneo la Coco Beach tayari kuligawa kwa jamaa ili afanye mradi wa kuchaji shilingi 1,000/- kwa kila gari.

Katika hali isiyo ya kawaida sasa wananchi watakaotaka kuja Coco Beach kupunga upepo watalazimika kujikunjua mfukoni kulipia Tshs 1,000 kwa gari kwa siku iwapo wataegesha katika maegesho yaliyopo ufukweni hapo kwenye hoteli ya Coco Beach
Ripota wa Globu ya Jamii ameshuhudia maafisa kutoka taasisi gani siuji wakipimapima eneo hilo kwa tepu, huku wakiandika andika kwenye vitabu.
Hata hivyo Wananchi waliokuwepo kwenye ufukwe huo walipinga kitendo hicho na kuwaamuru walipishaji hao kuondoka mara moja, nao wakatii maana inaonekana siku hizi Watanzania hawataki kupelekeshwa bila mpango.

Juhudi za kuwatafuta maafisa wa manispaa na watendaji wengine zinaendelea kujua uhalali wa zoezi hilo.
Uwanja unaotumiwa na watoto kucheza mpira nao ukipimwa bila shaka kwa ajili ya mradi huo wa kuchaji magari yanayokapi Coco Beach.

Wananchi wameshangazwa sana na kitendo hicho, wakikumbushia jinsi Rais Kikwete alivyowashushua madiwani wa manispaa za jiji ambao walipiga marufuku mwananchi wa kawaida kukanyaga ufukwe wa karibu na hospitali ya Aga Khan, na kuwataka wapaendeleze lakini hadi leo hakuna kinachofanyika, ingawa wananchi wa kawaida wanajinoma

"Ufukwe kwa Coco Beach ni eneo pekee lililosalia ambalo mtu wa kawaida yuko huru kwenda bila kukutana na bughudha, ikimaanisha kwamba mradi huu wa kulipisha magari hapo mahali sio tu utakera wengi ila uhalali wake lazima uthibitishwe kwa wananchi haraka sana", mwananchi mmoja alisikika akisema.


Mwinge alidakia "Hawa ndio wanaompakazia JK (Rais Kikwete) aonekane nchi ngumu kwake wakati kuna watu ambao badala ya kubuni vitu vya kufurahisha wananchi wao wanabuni vya kuwakandamiza.

Mbona Slipway kule wamemwachia mfanyabiashara ambaye kwa vile si mswahili basi anapeta atakavyo. Waache hizo na hapa hii kitu inaweza kuhatarisha usalama wa watu bial sababu. Ningekuwa na namba ya Profesa Tibaijuka ningempigia aone ardhi yake inavyotaka kuchezewa..."aliongeza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. wanapima nini sasa?
    nchi ndo inateketea hiyo,watu wanafikiri jinsi gani wataweza kuzidi kujilimbikizia mali tu.
    Kigogo kimoja kimeshampa mwanae mtaji hapo, kama ile ya Ubungo Termin, imeishia wapi???
    sirudi ng´o Tanzania.

    ReplyDelete
  2. Hiyo ndo Bongo bwana, tutapiga keleleeeeeee!

    Lakini parking itajengwa! Mafisadi wana nguvu bwana, sio mchezo!

    ReplyDelete
  3. Biashara ina miradi mingi sana na nchi inayoendelea lazima iende kwa mipango sasa hiyo nimoja ya miradi na mipango ya maendeleo. ikiwa unazo pesa za mafuta basi huna tatizo sasa tutafute mradi wa kupunguza mbu.

    ReplyDelete
  4. Kama wao wapimaji wakija na 'plan' nzuri ya kugeuza pwani ya Oysterbay Beach a.k.a Coco Beach kuwa kama fukwe ya CopaCabana (Brazil) au Cancun Mexico n.k basi ni mradi mzuri na ninaunga mkono Halmashauri ya Jiji La Darisalama kuhusu huu mradi.

    Maana beach hiyo inahitaji 'kuboreshwa' kila wiki kukanyangwa na nyanyo maelfu za wakazi wa Mzizima, kusipofanywa mradi-endelevu kama CopaCabana au Cancun basi si ajabu mmomonyoko wa ardhi ukaila pwani ya Coco Beach kugeuka kama maanguko(cliffs) na kuwa kama beach mbaya ya 'maanguko' a.k.a cliffs za Dover England.

    Ila kama mradi wenyewe ni kwa ajili ya 'maegesho' ya magari, basi siungi mkono 'mradi' huo usio na ubunifu-endelevu.
    Mdau
    Hawaii
    Visiwani Bahari ya Pasifiki.

    ReplyDelete
  5. Mbona hapo coco wameshaanza kulipisha magari siku nyingi tena ni mradi wa halmashauri ya kinondoni

    ReplyDelete
  6. Hawa wakubwa wanaenda cancun kufanya nini? tene wanatumiya pesa za jasho la watanzania walipa kodi... Mbona wahafuati mazuri wanaoyaona huko kwa wenzetu? Viongozi wengi wamesoma muda mrefu na muda mfupi nchi ziliendelea wajua kabisa lazima ardhi inayotumika kwa wananchi kama vile fukwe lazima zilindwe kwa kila hali pia ni kudumisha mazingira. Sasa kelele zote za kulinda mazingira ni siasa tu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...