Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika Oktoba, 2010 yanayoonyesha kuwa wasichana wanaongoza kwa kiwango cha ufaulu.

Hata hivyo matokeo hayo yameonyesha kuwa kiwango cha ufaulu katika mtihani huo kimeshuka kwa asilimia 22 ilinganishwa na matokeo ya mwaka 2009. Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Joyce Ndalichako, aliwaambia waandishi wa habari wakati akitangaza matokeo hayo jana, kuwa wasichana wamefanya vizuri zaidi kuliko wavulana.

"Kati ya watahiniwa kumi bora, sita ni wasichana na wanne ni wavulana," alisema Dk Ndalichako na kumtaja kinara wa matokeo hayo kuwa ni Lucylight Mallya kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana ya St Marian iliyopo mkoani Pwani. Hii ni mara ya pili kwa shule hiyo kutoa mwanafunzi bora katika mtihani wa kidato cha nne baada ya Immaculate Mosha aliyeibuka kinara katika matokeo ya mwaka 2009. Kwa mujibu wa matokeo ya mtihani wa mwaka jana, kati ya shule kumi bora katika kundi la shule zenye watahiniwa chini ya 40, saba ni shule za seminari na huku Shule ya Seminari ya Uru inaongoza shule kumi bora katika kundi la shule zenye watahiniwa zaidi ya 40.


Matokeo hayo yanaonyesha kuwa shule kumi za mwisho ni mchanganyiko wa shule za serikali na watu binafsi. Dk Ndalichako alitaja shule kumi bora zenye watahiniwa zaidi ya 40 na mikoa zinakopatikana kwenye mabano kuwa ni Uru Seminari (Kilimanjaro), Marian Girls (Pwani), St Francis Girls (Mbeya), Canossa (Dar es Salaam), Msolwa (Morogoro), Feza Boys (Dar es Salaam), St Mary Goreti (Kilimanjaro), Abbey (Mtwara), St Joseph Semiterambogo (Kigoma) na Barbro-Johansson (Dar es Salaam).
Habari kamili nenda Mwananchi
Matokeo Kamili ya mitihani hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Mh. mkuu wa libeneke,
    Hawa watoto wanaoshindwa mitihani siyo wapumbavu. Isikpokuwa wanashindwa kuchukua maarifa waliyonayo na kuyaandija kwa lugha ya kiingereza. Tatizo letu watanzania hatupendi kukubali ukweli kuwa tuna msingi mbovu wa kiingereza. Kama tumeamua kuwa kiswahili ni ligha ya taifa, basi tufundishi masomo yote kwa lugha ya kiswahili. Hawa watoto wanachanganyikiwa na lugha kama vile "technology"= teknolojia;"physics"=fizikia; management"= menejimenti; "budget"= bajeti. kwa staili hiyo hata tumalize masters UDS, mtoto wa highschool toka Kenya atkuwa na ulimi mwepesi kuliko sisi ambao tuanasubiri intervew ya kuandika ndipo tueleweke. Toka nimeanza kufutilia haya matokeo ni kuwa kila mwaka yanashuka. Na hawa walioshuka zamu hii wataenda kuwashusha wadogozao kwe shule za sekondari za kata miaka ijayo. Kuwa na elimu masikini maana yake ni kuukubali umasikini. Tujifunze kutika shule za seminary ili tulinusuru Taifa. Kama kiingereza kimetushinda siyo tatizo, basi tutumie kiswahili kufundishia watoto wetu. Mbona china, japan au ujerumani wanatumia lugha zao. Na tunaposema tutumie kiswahi maana yake tutafsiri majina yote ya madawa ya hospitarini na vitabu vya chuo kikuu kutoka kiingereza kwenda kiswahili fasaha, siyo Chloroquene = klorokwini,asprine = asprini,kwinini,injini,spark = sipaki,kilo,bored = kuboreka.Kwa mtindo huo watoto wetu wanachanganyikiwa mheshimiwa Mkuchika. I love my Tanzania and I am painfull for educational backwardness which means poverty.

    ReplyDelete
  2. ni kweli mi naunga mkono hii mada tatizo kubwa sana linalowafanya wanafunzi kufeli ni lugha tu.wengi wao wanaanza form one hawajui hata kuunga sentensi kwa kingereza sasa hatafaulu vipi na kingereza hakipandi? na shule wanazosoma hata kingereza kuongea kwa manati? na hata ukiangalia shule wanazofaulu vizuri hao wanafunzi wanamisingi mizuri ya kingereza tangia wadogo. mi nazani serikali inabidi ichunguze ili swala hamna mtu mpumbavu bali education system must change with tyme. ni hayo tu mdau nawakilisha...UK

    ReplyDelete
  3. Kutohoa maneno kutoka lugha moja kwenda nyingine si jambo la ajabu wala si chanzo cha vijana wetu kutojua Kiingereza. Lugha zote duniani hutohoa maneno kutoka lugha nyingi. Kiingereza ktk maneno 10,000 yatumikayo sana katika lugha hivyo, 60% yametoka katika Kilatini, Kifaransa na Kigiriki. Na wala si tatizo.
    Ukweli pia hata Kiswahili hakifundishwi vizuri kabisa. Fuatilia watu wanavyoandika na kusema Kiswahili kisicho fasaha.
    Taabu kubwa ni hakuna uwekezaji katika elimu kabisa. Kwa miaka mingi hatukujali kama walimu wana sifa na taaluma zinazotakiwa. Walimu hawaheshimiwi na wanakandamizwa hovyo. Hakuna vifaa vya kutosha mashuleni.Hatuwezi kulinganisha na sehemu nyingine duniani. Tumepuuza elimu sasa ugonjwa umekuwa sugu kabisa.

    ReplyDelete
  4. Jamani nisaidieni. How do I search for a school? Wangezipanga alphabetically nisingehangaika. Lakini wamepanga kadiri ya namba. Couldn't someone just put the sort command?

    ReplyDelete
  5. Mimi naomba tulishauri Baraza kuondokana na utaratibu wa kuwa na shule bora, tubakie tu na wanafunzi bora. Zile zinazotajwa kuwa ni shule bora mchango wao sio mkubwa kama tunavyodhani. Hivi manafahamu mchakato wa kujiunga na shule za FEZA au St Marian? Huwa wanachuja na kuchukua wale watoto ambao tayari walishajaaliwa na mwenyezi Mungu kwa vipaji maalumu na uwezo mkubwa wa kushika masomo. Halafu sisi tunadhani kuwa ni kwa juhudi za waalimu wao ndio zinawafanya watoto kufanya vizuri. Mbona mchakato wa kutafuta watoto wanaojiunga na shule hizo mnazoziita bora haufanyiki kwa njia ya bahati nasibu badala ya mitihani migumu kupita kiasi halafu ndio watuonyeshe huo ubora wao?

    ReplyDelete
  6. Ukweli in kwamba mfumo wa Elimu wa Tanzania Ni Mmbovu, acheni kuchezea maisha ya watoto, waliogundua hili wengi washakimbilia nchi zingine kusoma, Uganda sijui kenya...serikali angalieni hili, manfundisha mambo ambayao haya-apply sasa ivi due to technology, mambo mengine dah....haiwezekani watoto wa shule nzima wapate div 4 eti kingereza...hapana....hii ni Syllabus na watunzi wa mitihani wenyewe..Mna-mark kwa sifa sijui hasira....sielewi.... Tanzania tunairudisha nyuma sisi wenyewe bila kujijuja..hiki ndio kizazi cha baadae sasa... tunaifundishaje?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...