THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Safari Tripper wana 'Sokomoko'

Ni vigumu kupima raha ambayo Safari Trippers waliitoa na wanaendelea kuitoa katika ulimwengu wa muziki. Nyimbo zao bado zinapigwa na bendi chungu nzima mpaka leo hii. Unawajua walikuwa akina nani? Hiyo ni picha ya wanamuziki vijana hawa. Wadau tuanze kwa kuwataja wanamuziki hawa, anasema mkongwe John Kitime katika libeneke lake
BOFYA HAPA


Kuna Maoni 17 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Nawaona wa pili toka kulia waliosimama Hayati Dosser Mwana Manyema Marijani Rajab Jabari la Muziki, Hayati Chris Kazinduki na David Mussa. Chini aliyekaa na Guitar hayati Madi "Babu" Tumbo.

  Hapo lilikuwa likitimka tifu linamtika kweli: Viziwi watasikia, Bubu wataimba, Viwete watasimama, Vijana na Vikongwe wote wataingia uwanjani na kulicheza Sokomokooo.

  "..Ukweli Dada husemwa, nimeona leo nikuambia kweli
  Nimeona watu wengi wavivu sana ooh, lakini uvivu wakoo wee dada umezidi
  Siku Zote dada uko ndani, unatafutwa wala huonekani
  Wenzako wote wanatoka ooh wee Dada wewe hutoki

  Mi nakuomba tafadhali sanaa, Mi nakuomba tafadhali mi nakuomba! Mi Nakuomba uvivu hebu punguza wenzako wote wanakwenda kucheza Sokomokoo

  Wakina Baba na kina Mama njooni leoo, tuchezee, Sokomokoo
  Na Wazee njooni tucheze leo, Sokomokoo.."

  Sokomokoo ilikuwa shughuli nene!

 2. Anonymous Anasema:

  Huyo aliyechuchumaa upande wa kushoto ambaye ameshika Saxophone ni Kaka yangu MOHAMED IBUN SALEH yupo bado yuhai vile vile ni Architect, muziki ilikuwa part-time. Yeye sio kwamba akipiga muziki tu bali amesomea muziki na anatunga muziki mwenyewe na kujiburudisha mwenyewe nyumbani kwake akitumia organ. Nafikiri kama sikosei ni member of the Tanganyika Music Conservatory maana hata piano na flute yeye ni fundi sana.

 3. Anonymous Anasema:

  EBWANA MIMI NIMZITO KUTOA MAONI LAKINI PICHA HII INANIKUMBUSHA MBALI SANA,TULIKUWA NA UPINZANI MKALI SANA NA AFRO 70(AFROSA)WATU WA SOKOMOKO TUKIENDA KWENYE DANSI LAO WANATUWEKEA BITI,NAO WAKIJA KWETU BITI KALI TATIZO NI KUCHUKULINA MADEMU EBWANA NAKUMBUKA PRINCESS BAR KUNA SIKU MPIGA BESI WETU CHRISTIAN KAZINDUKI ALIPATA AJALI MBAYA YA PIKIKI PALE RELWE STAITION IKABIDI HATUNA SABSTUTE IKABIDI TUWAVAMIE JAMAA WA T.P SANTAFEE PALE GETA WAYS BAR GOROFA YA TANO NA KUMTEKA MPIGA BASS WAO JAMAA ALIKUWA NI MZAMBIA BAADAE AKAJA KUWA MPIGA SOLO MARUFU WA SIKINDE(JOSEPH MULENGA).PICA INANIPELEKA MBALI HIYO TIMU NI KINA MUSIBA ABDALAH,ALLY RAJABU,DAVID MUSA,CHRISTIAN KAZINDUKI MARIJANI DOZZA,BENNY PETTY,MBWANA MAKATA,MAHADI TUMBO,SISI WAPENZI ENZI HIZO UKIVAA BUGA LAZIMA UFUNIKE LAIZONI JUU UMEPIGA KITOP NYWELE LAZIMA UKATE KITOKOSI,NAWAKUMBUKA KINA MATINDA WHITE NA BLACK,RAY,KURUTHUMU CHEMBAMBA,SEGERE MATATA,MAKILO BOY,AWADHI PENGO HEMEDI YANGA,ADOLF,SULULU,ENDREW SIMKOKO,RICK BONDO.JAGAN BULL,JOE SHAWA,HAMISI GEGA,MZEE MRISHO WANTED ENZI HIZO MICHUZI NDIO KILIKUWA KIBRAZAMENI KINACHPUKIA HONGEARA SANA KITIME KWA KUMBUKUMBU SAFI DOHH NILITAKA KUSAHAU MAREHEMU SEMBULI ALIKU MCHEZAJI PEKEE ANAGARI FORD ESCORI TDW 1,KABLA YA SUNDA NA KIBADENI

 4. Anonymous Anasema:

  Safari Tripers umenikumbusha mbali, nimemkumbuka Marijani, nilihudhuria msiba wake pale Kariakoo, ukweli jamaa alikuwa Jabali.

  Wimbo wake maarufu sana kuliko zote mpaka sasa ni Georgina, na ni kisa cha kweli, Marijani akisoma Tambaza na Georgina akisoma Zanaki miaka hiyo.

  Pia nimeukumbuka wimbo wa Salama, na kumkumbuka Salama Mfamao (RIP)
  naukumbuka mistari michache tuu

  'nikilala naota sura yako
  nikitembea nasikia wanita
  nageuka sikuoni Salama mama
  umenitoroka bila kuniaga
  nawe ulijua kwamba nakupenda

  Kuoa siwezi kuoa
  mpaka niwe na Salama


  Nyimbo nyingine ni Rufaa ya kifo.
  huu ndio naukumbuka kidogo

  Kama ingalikuwa aaa
  binaadamu anakata rufaa ya kifo,
  inapotokea aa..
  mbele ya Mungu, na mimi ningekataa rufaa.

  Nirudishiwe wangu ehee
  niliyempenda aa
  hapa duniani lakini nimeshindwa sijua nifanyaje.

  KIITIKIO
  lakini mola yeye yeyee
  kazi yake haina makosa
  na wala hairekebishwi
  na binadamu yoyote..

  Mola ndiye muweza...mola ndie muweza jama
  Analotaka huamua, ....

  Pasco

 5. Anonymous Anasema:

  Enzi za princess Bar hizo!

 6. Anonymous Anasema:

  Pasco,

  Rufaa ya Kifo hiyo ilikuwa Dar International, Super Bomboka siyo Safari Trippers, Sokomoko.

  Mdogo wake Mohamed Ibin Saleh,

  Ni kweli aliyerecruit wanamuziki Trippers alilirecruit timu ya wanamuziki katika maana kamili ya wanamuziki. Hao jamaa walikuwa VIPUSA na HAZINA nadra na adimu ya muziki. Wengi wao walikuwa wanaweza kupiga ala zaidi ya moja na kuimba. Kwa mfano Mohamedi, David, Musiba, Tino, na Dosser. Hii haikuwa tu kwa Safari Trippers bali pia kwa wanamuziki wa bendi nyingi nyingine walikuwepo multi-instrumentalists, singers, and composers such as Patrick Balisidya, King Michael Enock, Mbaraka Mwishehe Mwaruka, Kulwa Salum, Juma Ubao, Joseph Mulenga, Vuli, George Mhuto na wengineo wengi ambao katika ulimwengu wa muziki wa leo wa Tanzania huwezi kabisa kupata sare yao.

  Anonymous:
  Thu Jan 13, 02:07:00 PM 2011

  Umenichekesha kwa kunikumbusha Mzee Mrisho Wanted. That Dude has a face!? Alikuwa character fulani kama Ray Abdul but subtle and reserved. Mzee Mrisho Wanted kila saa alikuwa anaonekana yupo njwiiii roaming between earth and outer space! Shiit, kulikuwa na mabrothermen na masister do yaani characters with style and confidence! Damned it, siku hizi characters hakuna just annoying clowns misusing space and abusing time.

  Gone are the characters. Gone are the bubbling spots Kibarua Bar later Amana, Gateways, Princess, New Palace later Mbowe, Rex Hotel, Cozy Cafe, Kwa Batenga, Kwa Tom, Zena Garden, Sea View Hotel,Lusaka By Night, Kwetu Bar, Sabasaba Ground. Empire, Empress, Avalon, New Chox not Odeon na Cameo were not our taste!

 7. Anonymous Anasema:

  Mohamed Ibuni Saleh (aliyechuchumaa kushoto) is one of those few cats that is indeed deep in-tuned with music as a form of Art. When I met him in the US a few years ago, I was fascinated by the wealth of the knowledge he has in classical music. Not only that he plays Bach, Bethoven and Mozart , but the guy mixes the stuff up with some African Flares like you wouldn't believe. He is an Architect by profession ( Among others, I understand his work is credited for vast portfolio including the design of Kariakoo Market). I'm a big fan!
  Mdau,
  Anchorage, Alaska

 8. Anonymous Anasema:

  Hapa nawatambua David Gordon Mussa [wa tatu kutoka kushoto waliosimama], Ibuni Saleh [wa kwanza kushoto aliyechuchumaa] na hayati Marijani. Juzi juzi nilikutana na kaka yake David ambaye nilimuuliza David yuko wapi? Alinijibu kuwa David hatoki sana kwa kuwa alipata kiharusi [stroke] mara mbili. Ibuni Saleh naonana naye mara moja moja anafanya kazi katika kampuni moja ya wasanifu majengo {architects; iitwayo Habconsult) iliyoko Seaview. Asante Ankal na JKitime kwa kutukumbusha mbali. Steady Eddy.

 9. Anonymous Anasema:

  Jamani wadau nisaidieni adress ya Mohammed ibun Salehe, mwanae hapo juu, chonde!!

 10. Anonymous Anasema:

  Mdau wa 06:50:00 PM na mdau wa 02:07:oo PM, mmenikumbusha enzi ambapo Dar ilikuwa ni jiji lenye wakazi 400,000 tu, lakini ilikuwa na sinema 10 (including Drive-in ambako watu walikuwa wakiingia sinema na magari yao na wasio na magari walikuwa wakikaa nje katika uwanja uliokuwa unaitwa kwa utani 'Drive-out' kutazama sinema bure). Enzi hiyo Jangwani kulikuwa na viwanja 36! ya vilabu vya mpira wa miguu (including Simba, Yanga, Cosmopolitans, Young Kenya, African Boys n.k.) kwa hivyo hakukuwa na uhaba wa sehemu ya vijana kukuza vipaji. Kulikuwa na viwanja vitano vya cricket, Aga Khan, Gymkhana, Khalsa, Burhani, St Xavier; viwanja karibu kumi vya hockey (ikiwemo cha TPDF) na timu ya hockey bingwa TZ ya wamatumbi (mostly Wa-Zenji) iliyokuwa ikiitwa Bantus, viwanja vya volleyball vingi tu (hasa cha YMCA kilichokuwa wazi kwa mtu yeyote); Tea Rooms zilikuwa hazihisabiki; kulikuwa na mashindano ya mitaa (hasa Uswahilini) ya drafti, bao, Keram, n.k. Majira ya joto, Kariakoo, Ilala, Magomeni na Kinondoni watu walikuwa wakilala nje. Watu walikuwa wanaweza kutembea usiku kucha mjini bila woga. Kulikuwa na 'Jazz Bands' zaidi ya 30, k.m. Dar Jazz, Western Jazz, Kilwa Jazz, Nuta/Juwata, Mlimani, n.k. na vukundi vya taarabu zaidi ya kumi, hasa Alwatani (pro-Simba) na Egyptian Musical Club (pro-Yanga); Aidha kulikuwa na vikundi vya ngoma za asili kutoka karibu kila mkoa, maarufu zaidi vilikuwa Hiari Ya Moyo (Wanyamwezi), Wingi Si Hoja (Wanyamwezi pia), Mganda (Wanyasa), Sindimba, Kitoto, Gobogobo (Wasukuma), msanja (kina mama Waswahili karibu kila mtaa), ngoma ya vijiti ya wahindi Makhoja (Aga Khan), etc etc. Kwa kifupi, kulikuwa na UTAMADUNI WA DARESSALAAM ULIOWAJUMUISHA WATU WA RANGI NA DINI ZOTE Dar, making Dar the most cosmopolitan, culturally vibrant and safest city in Eastern, Central and Southern Africa!!! Tulioijua Dar, mji wetu, ya wakati huo tunamshukuru Muumba kwa kutupa hiyo privilege ya kuishi Dar ya 50's (nilipoanza shule) 60's and 70's ambayo ilikuwa na "character", uungwana na ustaarabu, tofauti na Dar ya leo. (Pengine hii inaeleza kwa nini watu wengi wenye umri wa maika 60+ wana afya nzuri kuliko "vijana wa leo"). Mdau wa 02:07:00 PM, katika viota vya maraha naona umesahau Etenne's (mshindani wa Seaview) na White House (Ubungo). Nimefarijika kuona bado kuna watu ambao wana kumbukumbu ya 'golden age ya DSM'.

 11. Anonymous Anasema:

  Mdau wa Fri Jan 14 11:28:00 AM 2011, Address ya Ibuni ya posta siijui, lakini simu ya kampuni ya Habconsult architects (kazini kwake)iliyoko kwenye orodha ya TTCL ni 022 2114411. AA.

 12. Anonymous Anasema:

  Asante sana mdau wa 11:49!!naamini nitampata na nitawajulisha. thanks alot!!God bless u.

 13. Anonymous Anasema:

  Enzi hizo za Ibuni Saleh kulikuwa na wanamuziki kadha waliokuwa wanajua kusoma muziki (muziki ulioandikwa kwa lugha ya muziki) lakini wengi wao walikuwa wako katika bendi za polisi (marching bands na Polisi Jazz Band). Katika bendi za mjini Dar nawakumbuka Ibuni Saleh na Vuli (alikuwa mkimbizi kutoka Afrika Kusini) ambao walikuwa wanasoma muziki na kupiga ala mbalimbali katika nyimbo za classic na jazz. Of course, University ya DSM kulikuwa na piano pale Nkrumah Hall ambako mtu yoyote alikuwa na "ruksa" kuipiga. Ubunifu ulikuwa wa hali ya juu na wa mitindo aina mbalimbali kama vile nyimbo za jadi, Congo, cha cha cha, pachanga, bolero, rock, taarabu, na aina nyingi nyingine. Si sasa mitindo miwili tu kwa miaka 20 : rap na ndombolo tu na wanenguaji waliojichubua mpaka wanatisha (ha ha ha).

 14. Anonymous Anasema:

  ahhh namkumbuka Ibuni Saleh enzi hizo. Hawa ndio watoto wa mjini.Sio tu anaweza kutumia ala ya mziki, pia alikuwa mwalimu mzuri tu wa fundamentals za mziki. Lahaula, hawa Bongo flava inabidi wasome kutoka kwa wazee kama hawa. Mara nyingine nikiona vijana wa siku hizi wanavochafua hali ya hewa na visintisaiza vyao huwa natamani kutapika.

 15. Anonymous Anasema:

  Ankal na Kitime asanteni sana kwa picha kwa kweli nimekumbuka mbali sana na hasa ninapoiona picha ya Marijani Rajabu. Hayati Marijani nilisomanaye pale Olympio Street Primary School tukimaliza wote darasa la saba 1970. Alipoanza mziki alikuwa akifanyia mazoezi yake Dar Jazz na mimi na rafiki yetu mwingine akiitwa Abdul Karim tulikuwa tukimsindikiza kwenye mazoezi hayo na wakati huo mimi nikiishi Misheni Kota, wakati Abdul akiishi Kariakoo na Marijani akiishi Gerezani. Kipaji alikuwa nacho na kwa kweli alikionyesha hadi umauti ulipomkuta. Ninaomba wale ambao tulikuwa wote pale Olympio wakati ule watakaouona ujumbe huu tuwasiliane 0713 311408. Binafsi sikuwa mpenzi sana wa mziki ila nilikuwa napenda kuusikiliza tu. hobby yangu ilikuwa riadha na basketball.

 16. Anonymous Anasema:

  Anonymous
  Fri Jan 14, 03:11:00 PM 2011

  Duuh!, hockey umenikumbusha enzi za Tornadoes, Khalisa, Dar Institute na timu zingine. Mashindano yalikuwa yanafanyika viwanja vya Gymkhana. Ilikuwa kama unakwenda kwenye tamasha. Viwanja vya hockey ninavyovikumbuka ni Gymkhana, Diamond Jubilee na Lugalo Jeshini. Cricket nakumbuka Coast Gymkhana (Upanga), Gymkhana na Kinondoni Leaders Club. Kulikuwa na mashindano ya magari East African Safari yaliyokuwa yakipitia, kiuishia au kuanzia Kilimanjaro Hotel. Washiriki wake maarufu walikuwa kina Joginder Singh, Bank Shackland, Hannu Mikolla, Zul Rhemtullah na Lyaruu.

  Jangwani! Jangwani kulikuwa mahala pa kwenda kila jioni kuangalia mazoezi ya timu mbali mbali na weekend kuangalia mechi. Mara ya mwisho nilikwenda Jangwani kwenye miaka ya 80 kuangalia mazoezi ya timu ya UFI. Mbali na Simba, Yanga, Pan, Nyota Nyekundu, na timu zingine za taasisi za serikali kulikuwa timu ndogo ndogo vyingi zikifanya mazoezi Jangwani. Nakumbuka kulikuwa na Sosoliso, Jangwani Fresh, Black People baadaye ikaitwa Nungu. Timu hizi ziliunganisha vijana toka sehemu mbali mbali za jiji aidha kwa kuchezea au kukutana kwenye mechi au ligi uchwara. Kulikuwa na siasa za Jangwani za kunyatia wachezaji toka timu ndogo kwenda timu kubwa.

  Mwaka 2009 nilinunua kitabu kinachoelezea historia za jiji la Dar es Salaam (Dar es Salaam - Histories from Emerging African Metropolis). Kitabu hiki kimeelezea mengi kuhusu jiji la Dar es Salaam. Wachangiaji wengi walioandika katika kitabu hiki ni wanataaluma na si wazawa. Wameandika zaidi katika mtazamo wa kitaaluma na jicho la mtu wa nje. Wangepatikana wazawa na kuzi wa Dar es Salaam amabao ni wanamichezo na wanamuziki kuchangia katika kitabu hiki hususani kwenye michezo na muziki kingelikuwa maridhawa zaidi.

 17. Anonymous Anasema:

  Bwana Michuzi naomba fikisha ujumbe huu kwa Kitime maana naona ile blog ya wanamuziki wa Tanzania anayoiendesha ni kama imekufa. Hapa ninapoandika maoni haya hakuna kilichobadilika katika blog hiyo kwa wiki mbili sasa, sasa hii ni blog au jarida la kila mwezi? Yaani blog kwa mwezi inakuwa na post moja au mbili. Ikumbukwe kuwa kuendesha blog inataka nidhamu ya hali ya juu na kujituma ili uwe na post za mara kwa mara. Kama Kitime amebanwa na shughuli nyingine ni vyema akaikabidhi blog hiyo kwa mtu mwenye uwezo wa kui-‘update’ kila siku aiendeshe.