Timu ya Altetico Paranaense ikiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Kampuni ya RBP Oil & Industial Technology (T)Ltd ,Mama Rahma Al Kharous kabla ya kuelekea uwanjani kwa mchezo dhidi ya Yanga.
Mshambuliaji wa timu ya Atletico Paranaense,Gabriel Lima De Oliveira akijaribu kumtoka kipa wa Yanga,Nelson Kimath wakati wa mcheo wao wa kirafiki uliochezwa leo jioni katika uwanja wa Taifa.timu ya Atletico Paranaense imeshinda 3-2 dhidi ya Yanga.
Beki wa Atletico Paranaense,Diego Alexandre Petri akichuana vikali na kiungo wa timu ya Yanga,Abuu Zubeir katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo jioni katika uwanja wa Taifa.timu ya Atletico Paranaense imeshinda 3-2 dhidi ya Yanga.
Mshambuliaji wa Yanga,Nsa Job akiwa na mpira kuelekea langoni mwa timu ya Atletico Paranaense huku beki wa timu hiyo,Diego Alexandre Petri akimkimbiza ili kuondoa hatari hiyo.
Davis Mware wa Yanga akijaribu kumtoka beki wa timu ya Atletico Paranaense,Bruno Costa De Souza katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo katika uwanja wa Taifa.timu ya Atletico Paranaense imeshinda 3-2 dhidi ya Yanga.
Rais wa Kampuni ya RBP Oil & Industial Technology (T)Ltd ,Mama Rahma Al Kharous akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kumalizika kwa mechi kati ya timu ya Yanga ya jijini na Atletico Paranaense ya nchini Brazil uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar leo.Mama Rahma Al - Kharous amewataka watanzanzia kujitokeza kwa wingi katika mchezo unaofuata dhidi Simba ya jijini na timu hiyo ya kigeni utakaochezwa kesho kutwa uwanjani hapo,pia amesema kuwa hakutakuwa na kiingilio siku hicho watanzania tujitokeze kwa wingi kuisapoti timu hiyo.
Rais wa Kampuni ya RBP Oil & Industial Technology (T)Ltd ,Mama Rahma Al Kharous akiwa na viongozi wa timu ya Atletico Paranaense wakiwa wameshikilia bendera za mataifa mawili ikiwa ni ishara ya umoja katika michezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Bendera yetu imegeuzwa kichwa chini miguu juu. Cha ajabu Watanzania wengi hawajui bendera yetu inatakiwa ikaaje.

    ReplyDelete
  2. Pole sana mama Rahma, Naona watu wakampuni yako hawakujipanga kama ipasavyo! Tanzania ni moja ya nchi Masikini duniani. Kwa hiyo kiingilio kikiwa cha juu, wataingia wapenzi wachache. Naona kamati ya maandalizi,haikujifunza siku Timu ya Taifa ya Brazil ilipokuwa nchini. Ushauli wa bure ni kwamba, siku nyingine mpange bei kama ifuatavyo:-
    Tsh 30,000 Watu wa Khali ya juu kama Mawazili, Wadosi, Waarabu n.k
    Tsh 25,000/- wafanyakazi wa kawaida, kama wale wa vodacom na Tigo, 20000/-Waalimu na Wafanya biashara kama wamiliki wa daladala, 15,000/-madereva wa daladala na walimu wa shule za msingi, 10,000/- wanafunzi wa vyuo vikuu, kama UDSM,IFM,na CBE 5000/- Wauza mitumba wote $1000/- watu wasio na ajili woteeee, Dar es Salaam wamejazana sana! Kwa kufanya hinyo mngepata motisha ya kuleta timu nyingine Tanzania na Uwanja ungefulika.

    ReplyDelete
  3. bendera yetu ilivyo shwika , na wananchi ndivyo walivyo shikwa sasa hivi. ndo nchi ilivyo , so awajakosea !

    mdau Paris

    ReplyDelete
  4. Hii issue ya bendera kugeuzwa kidiplomasia huwa ina maana mbaya.. kuwa nchi iko katika matatizo au aliyeishika hivyo anaonesha kuasi au kupinga jambo fulani kwa nchi hiyo.. mbaya zaidi imeshikwa na wageni..naomba aidha uitoe hii picha hapa na ikibidi umueleze mama Kharous na watu wa TFF kosa hili ili wasirudie tena.

    Tafsiri hii Check katika wikipedia: "When a national flag, with some exceptions, is flown upside down it indicates distress...Further, a nation's flag is commonly flown inverted as a sign of protest or contempt against the country concerned..."

    ReplyDelete
  5. hii inaonyesha jinsi gani hatuma utamaduni wa kujua alama zetu za taifa. Tanzania zaidi ya uijuavyo. kazi kweli kweli!!!!!!!!!!1

    ReplyDelete
  6. well done Rahma

    ReplyDelete
  7. Alexander! Acha ubaguzi! Watu wenye mioyo ya korosho utawajua tu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...