Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Hao ccm wamezidi mabavu hivi angekuwa ni mbunge wa ccm wangefanya huo utumbo wa kudhalilisha kiasi hik? naichukia sana ccm chama cha mabavu hadi naona kinyaa pyuu! NAJUA MICHUZI LEO UTABANA SANA , KULIKO IWE HIVYO UONDOE NA HIYO CLIP KABISA

    ReplyDelete
  2. Kumbe shughuli hazikuanzia Tunisia, bali Tanzania...

    ReplyDelete
  3. Hii ndio CCM ambayo inatuambia kuwa Chadema ndio walifanya fujo. Je uchaguzi wa MEYA Arusha ulikuwa halali?!! Tunahitaji nguvu ya umma na JK usikie hili.

    ReplyDelete
  4. Mbunge anapodhani kuwa yuko juu ya sheria na kufanya mambo kienyeji. Lema don't waste your time using muscles rather than brain. Kuitwa mpinzani si kwamba uwe unapinga kila kitu. Kitendo cha kuwepo Polisi pale kilitosha kuwafanya ninyi mjue kuwa mpango wenu mlioundaa wa kuvuruga kile kikao ulikwishawafikia wenzenu wa upande wa pili tena watoa habari wakiwemo miongoni mwa madiwani wenzenu wa CHADEMA.
    Tatizo lililopo ndani ya Arusha si u-CCM na u-CHADEMA, bali ni ukabila ambapo ninyi mnaotoka mkoa wa jirani mnataka kubinafsi kila kitu cha watu wa Arusha as if Arusha haina wenyewe.

    ReplyDelete
  5. inasikitisha sana ndugu yangu nichuz mie nadhan hata usingeiweka hii hapa lakin ni jukumu lako kutuelimisha maana tena aibu kwa nchi bingwa tegemez kwa wakubwa huku nje! yaan mbunge!? nini maana yake mbunge? tena hao askari shule hamna kabisa mie nadhani bado hatuna elimu ya dhamana na nini maana mamlaka kwa serikali ya demokrasia, maana hata hizi taratibu ndogo ndogo kuzifuata ngumu jaman? kaka michuz bado tunahitaji elimu sna kwa majeshi yetu, au tuambiwe nchi yetu ipo chini ya utawala wa kijeshi, sio wanakuja huku kuomba misaada kwa kisingizio wanafuata utawala wa kisheria na demokrasia ya kweli. pia hao wajumbe wa ccm wanaofurahia wakati mh. mbunge anatolewa mie nadhan hawajui wanachokifanya ni bora wote wakajiuzulu, ukweli ni kwamba hamna kitu hapo home ni biashara za watu tu ziendelee kwenye kivuli cha nchi kuiongoza, sasa wanamuongoza nani? maana mwakilishi wa watu ni huyo mbunge nae anafanyiwa unyama kiasi hicho ni tusi kwa watanzania wote.
    mdau japan.
    al hamdulillahi, nashukuru kaka nimesalimika na hii disaster iliyotokea hapa.

    ReplyDelete
  6. HUU UHUNI UTAKWISHA LINI KATIKA MATAIFA YASIYO ENDELEA NA YASIYOTAKA HATA KUENDELEA? mataifa makubwa nayafikiria plann za maana zenye scientific base,vijitaifa vilivyoduni kiteknolojia vinafanya ujinga mbuzi usio na mbele wala nyuma kwa sababu tu kuendelea kuukumbatia umaskini, ujinga na maradhi kwa umma wake huku hao wachache wakijifurahisha wakati wamezungukwa na umma fukara.
    HOVYO KABISA, shame on you!!!

    ReplyDelete
  7. Ili Viongozi na Mafisadi wetu wanyooke, ile adhabu ya kupigwa risasi hadharani itumike na kwetu!

    ReplyDelete
  8. Hii itafikia sehemu tukatae kwa njia yeyote ila na kumbuka kilicho na mwanzo kina mwisho.

    ReplyDelete
  9. kwa kweli hapa hakuna demokrasia hata kama ni swala la mloa jirani kuchukua kila nafasi ya Arusha sidhani kama madiwani wote wa Chadema wanatoka moa jirani. pia polisi wajifunze haki za binadamu wanamfanyia mbunge hivyo mtu wa kawaida inakuwaje? ndo maana watu wanafia kwenye vituo vya polise coz polisi na watuhumiwa hawajui haki za biadamu. polisi mmejidhalilisha kwakuwa mmeonyesha kabisa kuwa shule yenu ni chekechea wala hat utandawazi hauwasaidii chochote. Tendeni haki kama wafanyakazi na si kuegemea upande mmoja wa siasa.

    ReplyDelete
  10. Kuna kitu hapa lazima tuwekane sawa kwanza. Inapofika wakati wa uchaguzi huyo meya wa Arusha kwanza anakuwa kishatoka kwenye kiti chake anakuwa siyo meya na wala hana hadhi ya kuitwa meya mpaka achaguliwe tena, hata kama alikuwa meya kabla ya uchaguzi. Kwahiyo huyo mpambe mtangazaji ajue sheria kuwa Lema alikuwa hana hadhi ya umeya wakati wa uchaguzi, nafasi ya umeya huwa inakuwa tupu au (vacant). Hii ndio sheria.

    Pili, hata kama kuna kosa limefanyika kwenye uchaguzi Lema alikuwa aonyeshe mfano mzuri wa uongozi kuchukua sheria mahakamani na polisi walivyofanya sawasawa. Kwahiyo Lema kajidhalilisha mwenyewe.

    Tatu, wenzetu wanamsemo "two wrongs don't make it right". Kwahiyo chadema ni watu wa shari tu na wanataka kutuingiza kwenye balaa hawa watu kwa kutaka uongozi kimabavu.

    ReplyDelete
  11. Tunaomba kuona na Part 1.
    Kama hijaipata ni:

    http://www.youtube.com/watch?v=BFoTXb7Kiwc
    Vinginevyo tunadhani kuna kitu unaficha hapa.Hii siyo Far hata kidogo.

    ReplyDelete
  12. INAWEZEKANA MTU AKAWA AMESOMA AKAKOSA MAARIFA.UJINGA WA KIDINI WANAOUNDESHA CHADEMA UTATUFIKISHA PABAYA.UKIFUATLIA KWA KARIBU KWABLA YA UCHAGUZI WALIVOKUWA KWENY KAMBI YA UPINZANI NA WANAVOYUMBAYUMBA BASI UTAJUWA HAMNA SIASI ZAIDI YA UJINGA.

    ReplyDelete
  13. Umbumbu wa askari wa kushindwa ku-reason intelligently na uongozi wa kifisadi umekuwa chanzo cha fujo za Arusha. Unless CCM wana mkanda wao nao watoe ila kwa hali ilivyo serikali na CCM ndio wa kulaumiwa kwa yote yaliotokea AR. Uchaguzi batili wanataka kuuhalalisha, NOOOO!!Watafute mlango wa kutokea 2015. Ikarakara

    ReplyDelete
  14. hivi mbona michuzi hakuweka chanzo ambapo wana chadema walipanga kwenda kituo cha polisi je mbona hukuweka ile mvua ya mawe wana chadema waliokuwa wanaivurumishaia kituo cha polisi jamani angalieni upande mwingine wa shilingi msilaumu bila kujua chanzo.

    ReplyDelete
  15. Am SORRY TO SAY THIS: KATIKA VYAMA AMBAYO NI MAPUNGUANI NI CCM, TENA KIKWETE HANA ALIFANYALO, HUWEZI UKAAMURU MBUNGE WAKUCHAGULIWA NA WANANCHI ATOLEWE KWA NGUVU NAMNA ILE NA KUPINDWA MKONO. KIKWETE ISHI UKIJUA UTATOKA HAPO MADARAKANI, NA IPO SIKU KA SI WANAO BASI WAJUKUU ZAKO WATARUDISHIWA. MUNGU ANAJUA HUWA HAVIISHII HAPA, VIZAZI NA VIZAZI VYENU!

    ReplyDelete
  16. WEWE ANONYMUS SAIDI: LEMA HAKUFANYA FUJO, ILA HATA KAMA INGEKUWA WEWE, UNAAMBIWA UCHAGUZI WA ENEO LAKO UNAFANYIKA SEHEM FLAN UNAFIKA PALE HUWAKUTI KUMBE WAPO SEHEM NYINGNE WANACHAGUANA BILA IDAD HALISI KUKAMILIKA! SASA UNAPOSEMA LEMA KATUMIA NGUVU, NI IPI? HAKI YAKE YAKUDAI UCHAGUZI HURU, AMA HAYO MAKOFI WANAYOPGA WENZAKO HAPO MEZANI? HAYA MAMBO YANAMWISHO, UKITUMIA DOLA NA KUWAPA WACHACHE WENGI UKIWANYIMA MALI[PO WAMECHOKA! INSHORT HATA DOLA YENYEWE IMECHOKA!!!!

    ReplyDelete
  17. inasikitisha kuona Polisi wakitumia live rounds kuwapiga watu wanaodai haki yao.Kweli polisi hapo wamedhamilia kumuua mwananchi. Polisi wanasahau kitu kimoja, wameweka kwa ajiri ya protection kwa wananchi na si vinginevyo. Halafu baada ya tukio hakuna Independent investigation, kuona kwa nini tukio hilo limetokea na jinsi gani ya kujiandaa isitokea tena.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...