Marehemu Lilah siku za mwisho za uhai wake akiwa hospitali.

Lilah, yule mwananchi aliyechomwa moto kwa kosa la kuzamia Disco kwenye hoteli ya South Beach Kigamboni jijini Dar es salaam, amefariki dunia.

Wakizungumza kwa masikitiko ndugu wa marehemu Lillah alifariki dunia jana jioni na mipango ya mazishi inafanywa huko Kigamboni ambapo anatazamiwa kuzikwa leo jioni katika makaburi ya Mji Mwema.

Marehemu Lilah ambaye alikuwa mfanyabiashara maarufu wa nguo za kuogelea na vitu vya kitamaduni kwa waendao Beach za Kigamboni, alikumbwa na mauti baada ya kukutwa ndani ya Disco akiwa hana tiketi maalumu inayovaliwa mkononi kwa wale wote wanaoingia ndani ya ukumbi huo wa South Beach.

Spoti na Starehe ni mmoja wa marafiki wa marehemu kwani alikuwa akitembelea na kuuza bidhaa zake katika fukwe Mbalimbali za Kigamboni ikiwemo Chadibwa Beach.

Marehemu Lillah alikamatwa na walinzi wa fukwe ya South Beach Jumapili iliyopita kwa kudaiwa kuingia bila kulipa kiingilio kwenye Disco linalopigwa mwishoni kwa kila wiki fukweni hapo, Lillah hatimaye alipelekwa kwa meneja wa hoteli hiyo ambaye aliamrisha achomwe moto.

Akionge kwa taabu na Mwandishi wetu katika Hospitali ya Kigamboni kabla ya kuhamishiwa Muhimbili alikoagia dunia, Marehemu Lillah alisema hata Kupona mpaka pale anamshukuru Mungu kwani hakutegemea kupona kutokana na kipigo na maumivu ya moto ule.

Tunaomba haki itendeke ili kukomesha unyama huu, hata kama Marehemu Lilah alikuwa mkosaji au kibaka kama walivyodai hapaswi mtu yeyote kutoa hukumu ambayo Lillah amepata.

Huu ni mfululizo wa kujichukulia sheria mikononi ambapo wezi na vibaka wamekuwa wakichomwa moto na wakati mwingine bila hatia yeyote, kwani matukio mengine yakitokea akishakamatwa anatafutwa aliyeibiwa haonekani.

Mwanzoni mwa mwaka kijana mmoja alipoteza maisha maeneno ya Mwenge kwa kuitwa mwizi ilihali yeye ndio alikuwa ameibiwa Laptop yake na alipojaribu kuwakimbiza wezi walimgeuzia kibao na hatimaye wananchi walimvamia na akapoteza maisha.


Marehemu Lillah ameacha mke na watoto.

Chanzo: SPOTI STAREHE BLOG

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 42 mpaka sasa

  1. yaani disco tu linaua mtu sijui alafu tanzania ni tulivu yaani tuwaachie polisi na sheria ifanye kazi yake,lakini utakuta polisi nao wanaenda kupanga foleni ya kuchukua kitu kidogo mwisho kesi haina ushaidi wa kutosha taNZANIA HAAAAAAAAAA

    ReplyDelete
  2. SASA USTAARABU WASHEREHE HAUPO KABISA,KWANI SHEREHE NIKUZAMIA NA KUSHEREHEKEA.KAMA JAMAA ALIIBA KITU NAUNGA MKONO ILA KAMA ALIZAMIA TUU,WAHUSIKA WASHTAKIWE KWANI HAWAKUMTENDEA HAKI MAREHEMU,KWANI HATA WAO NIWAZAMIAJI KATIKA SHEREHE NA MADISCO KIBAO.WANGE WACHOMA WALIOKUWA MLANGONI NA KUMRUHUSU MAREHEMU KUINGI.DR.DAKO

    ReplyDelete
  3. INNA LILAH WAINNA ILAYHI RAJIUN>>> KWELI LOFA HANA HAKI DUNIANI

    ReplyDelete
  4. Tunaomba serikali ifuatilie swala hili na mmiliki wa hoteli au uwanja huo wa disco na wafanyakazi wake walioshiriki kumchoma huyu kijana wakamatwe na kufikishwa mahakamani,kutokana na tabia ya nchi yetu kuwakumbatia wenye pesa utakuta hapo hakamatwi mtu,itashia kimya kimya,mimi nawaomba wananchi wote tuungane kuhakikisha wahusika wanafikishwa mbele ya sheria,tukiacha mambo kama haya yaendelee basi masikini tutakuwa tunauwawa kila siku,Pia yule tajiri aliyetuma mabaunsa kwenda kuvunja nyumba Tegeta na mwisho ikawa mauaji ya kikatili nae akamatwe na kufikishwa mbele ya sheria.Watu wasiwe wanajichukulia sheria mikononi,hata kama wamekosewa kuna vyombo vya sheria vinaweza kutumika na siyo kujiamulia mambo bila kujali sheria,eti kwa kuwa fulani ni tajiri.Tuamke watanzania kabla nchi yetu haijakuwa Rwanda au Sudani,Somalia nk.
    mdau Kigamboni,Dar

    ReplyDelete
  5. Jamani inasikitisha sana. Mungu amrehemu. Hao waliomchoma nao wauwawe. Na wananchi walikuwa wapi mpaka mtu anachomwa na watu 3?

    ReplyDelete
  6. Poleni sana wana familia na marafiki kwa ujumla

    kwa kweli huo ni unyama mkubwa unaofanywa na watu wasiokuwa na imani na wenye roho ngumu hivi jamani kwanini maisha ya watu wanachukuliwa kirahisi namna hiyo?

    hivi serikali yetu wahusika wa mambo ya usalama wa raia wanafanya nini wakati mambo kama hayo yakitokea?

    hivi polisi hawana mawasiliano ya haraka ambayo mtu yeyote akiona tukio kama hilo aweze kupiga simu polisi na waweze kufika kwa muda muafaka kwenye tukio kama hilo?

    hivi jamani mtu anapotezewa maisha yake kirahisi kama hivyo?

    masikini mtu wa watu ameacha mke na watoto wanamtegemea na maisha yake yanaishia kwa kosa la kuingia disco bila kulipa? hata kama ni kweli hakulipa kiingilio cha disco kinaweza kufananishwa na uhai wa mtu??

    mambo hayo na mengine mengi ndio yanayochangia sisi wengine tukubali kufia huku ughaibuni kana kwamba hatuna makwetu maana huko kwetu hakuna sheria hakuna haki za kibinadamu

    may god bless u R.I.P Lilah

    ReplyDelete
  7. sina shaka , wahusika wakuu watakuwa wamehifadhiwa na vyombo vya dora kwa usalama wao. tunavyofahamu ktk kadhia kamaa hii huwa hakuna dhamana hasa kulingana na hali ya mgonjwa inavyoendelea , nina imani kabisa baada ya tukio hili sheria itashika njia kwa huyo MTANZANIA MWENYE ASILI YA KIASIA.

    ReplyDelete
  8. UNYAMA UNYAMA UNYAMA UNYAMA UNYAMA UNYAMA UNYAMA UNYAMA UNYAMA UNYAMA

    SERIKALI YA WADANGANYIKA IMELALA KUPITA KIASI HALI INATISHA SANA

    NCHI IMEKUWA KAMA HAINA KITENGO CHA USALAMA WA RAIA AIBU AIBU AIBU

    MTU ANAPOTEZEWA MAISHA KWA KOSA LA KIINGILIO CHA DISCO WANA SHERIA MPO WAPI?

    HALI NI MBAYA NA NI HALI YA KUTISHA SANA ILI HALI NCHI INATANGAZWA KUWA YA AMANI

    WATU WANAJICHUKULIA SHERIA MIKONONI KUTOKANA NA KUMIRIKI VYOMBO VYA SHERIA

    MTU ANAJICHUKULIA SHERIA ANAJUWA HATA AKIFIKISHWA MBELE YA HAKI ATASHINDA KESI KWA KUTOA RUSHWA

    NCHI INAZIDI KUWA INATISHA SANA SHERIA ZINAONGOZWA NA WENYE HELA

    POLENI SANA WAFIWA MUNGU YU PAMOJA NANYI NA PAMOJA NA MAREHEMU LILAH

    KILA GOTI LITAPIGWA SIKU HIYO IKIFIKA

    mdau wa mahakama kuu ya dunia naomba nipewe mimi hiyo kesi nisimamie nitaleta mwana sheria wa huku ughaibuni ndio adabu itapatikana kwa wengine.

    ReplyDelete
  9. Common mwananchiApril 17, 2011

    Hii haikubaliki hata kidogo. Kama jamaa alizamia au alikuwa ni kibaka, SI WALISHAMKAMATA?????. Aliyempa meneja mamlaka ya kutoa hukumu ya kumchoma moto ni nani??? Kosa alitatuliwi kwa kutenda kosa. Na ningependa ieleweke, tofauti na mob justice za mabarabarani ni kwamba, wengi wanaoshiriki wanafuata mkumbo, hakuna majadiliano wala kiongozi/mtu anayeratibu zoezi lile kwa wakati ule, wote wanashiriki. Lakini kwa tukio hilo, ni mauaji yaliyoratibiwa. Alikamatwa, akapelekwa kwa meneja, akasema choma moto na amri ikatekelezwa.

    Hii ni kesi ya mauaji na iko wazi kabisa. Tunaomba sheria zichukue mkondo wake kwa uzito unaostahili. Pia tunaomba Ankal na wadau wengine kama mnaweza muendelee kutupa-update ili tujue haki inaenda mkondo upi. Kuna bwana amejadili hapo juu na kusema kama aliiba, basi anaunga mkono hatua hiyo, sio kweli na unakosea, HAKUNA SHERIA YA KUUA MTU ALIYEKUIBIA NA UKAMKAMATA.

    Watu wanapata wapi hii jeuri? Kuuana eti mtu kazamia disco? Disco? Dadisi

    Naomba kuwakilisha.

    ReplyDelete
  10. jamani inasikitisha, utu uko wapi siku hizi, hivi kweli binadamu unamchoma binadamu mwenzio moto tena kwa kuzamia tuu??
    Mungu aiweke roho yake pema peponi, poleni familia, ndugu na marafiki.
    Natumaini haki itatendeka this time

    ReplyDelete
  11. Hii habari ya kifo imenisikitisha saana, kwani nadhani nilichangia kwa kulaani vikali adhabu aliyopewa huyo jamaa ambaye kwa sasa kisha kuwa marehemu (maskini) katika post ya awali ilipotoka hapa, yaani still bado siamini kweli eti Tanzania nchi inayojisifia amani na utulivu leo hii kusikia ati mtu anapoteza maisha kwa kosa la kipuuzi kama hilo. Mimi nina imani damu ya mtu inapomwagika huwa haiendi bure, sasa na nyie mliojihusisha na kitendo hicho subirini laana mtakayo ipata. Nawaombea amani ya Bwana iwe nanyi nyote mlipoteza ndugu yenu mpendwa, Mwenezi Mungu awatie nguvu hasa katika wakati mgumu kama huu.

    ReplyDelete
  12. Yaani una mchoma mwanadamu mwenzio kwasababu hajalipa kiingilio cha disko..Nashindwa kuendelea kuandika maana kuandika maoni ambayo hayabadilishi chochote ni kupoteza wakati. Wewe Michuzi una contact na watu wa serikali hebu waamshe maana tunakoenda ni kubaya mno. Jeshi la polisi limekosa hadhi na inabidi tufikirie suala la mafunzo kwa askari kukabiliana na matukio ya karne ya sasa. maana naona mbinu zao zimepitwa na wakati. huu ni wakati wa sayansi na teknolojia watoe nafasi kwa wanasayansi kusaidia kupunguza uhalifu.

    ReplyDelete
  13. wewe wa ugaibuni unayesema hurudi hufai hata kuandika comnt

    ReplyDelete
  14. Sasa huyo meneja wa hapo na hao walinzi walioshiriki kumuangamiza mwenzao kwa ajili ya starehe za dunia hii, wala sio mwizi, wakumbuke haya yote ni ya dunia, yaani kuingia disco kwa kujipenyeza ndio ukamtoe roho mwenzioo, kazi kweli kweli, daa kama ni ivyo basi wengi wangetolewa roho kwa hayo, hayo ni ya kawaida kwa watu kuzamia, na ukimkuta hajalipa unamtoa nje aende zake, jamaani binadam kuweni na miyoyo ya kibinadam. na sheria ichukue mkondo wake kwa kweli, kuanzia kwa huyo meneja uchwala, na hao walinzi uchwala, huyo meneja nae si anafamilia, yaweza jurudia hata kwa familia yake, ikaja mkuta balaa kama hili, kama sio yeye.

    ReplyDelete
  15. RIP. Katika nchi ya wadanganyika iliyojaa kila aina ya ufarauni wa kuzuia haki isitendeke, hii issue itazimwa kama ilivyozimwa ya mtoto wa mbunge wa URAMBO MAGHARIBI aliyepiga mtu risasi na kumuua kwa kugombea mwanamke.

    Siku moja wafu wote wa aina hii watatendewa justice, iwe siku ya hukumu kwa mwenyezi au hapahapa duniani wa waliowadhulumu tunu ya uhai wao kwa nguvu kupambana na mkono makini wa sheria

    ReplyDelete
  16. mimi nafikiria kuitoa familia yangu Bongo kwani kutokana na matukio haya hakuna haja tena ya kuishi Tanzania mara wanajeshi wamemuua fundikira, mara mabounsa wamepiga watu mara Mbeya mtu kachomwa moto kwa kusadikiwa kaiba viti vitano kanisani hii haikubaliki jamani watanzania ebu kuweni na moyo wahuruma kwa binadamu wenzenu kwani tukiendelea hivyo itafika wakati tutachinjana kama kuku kwani hata huko Ruanda chuki zilianza hivyohivyo. Kwa upande wa serikali hivi kweli serikali inasimamia barabara usalama wa raia zake? wakiambiwa kuwapiga wamachinga pale kariakoo na kupora vitu vyao ndani ya dakika 5 wameshafika hila wakiambiwa kuna tukio la watu wanauana watakwambia hatuna silaha hila wanasilaha yakuwapiga watu wanapoandamana. Wananchi msikubali kuuana kama wanyama haya ni maisha kesho na wewe au ndugu yako anaweza akapigiwa kelele za wizi na kuuliwa bila hatia yoyote. TUSIJICHUKULIE SHERIA MIKONONI NAWAOMBA WATANZANIA WENZANGU. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amen

    ReplyDelete
  17. Lofa hana lake duniani, akamatwe nani fyoko, atakamatwa lofa fulani hivi (mlinzi wa hotel ile aliyekuwa zamu siku na saa hizo) na sio meneja au muhusika haswa. Mambo yote Pochi jamani, na kwa jinsi dola zetu povert tupu, nyie msio nazo mjinyonge.

    ReplyDelete
  18. hivi disko ni la muhimu sana mpaka mtu ukazamie bila kujali hatari inayoweza kukukuta au kuharibu heshima yako katika jamii. nafikiri mtu unaweza kufanya kitu kingine kama kuspend time na family endapo mfuko hauruhusu kwa siku hiyo.Ni sawa wakati mwingine utakuta mtu anakwenda bar akiwa hana hela ya bia, kisha husubiri na kuanza kuomba anunuliwe bia na kila anayemjua kwa kisingizio kuwa yeye hayuko safi siku hiyo.
    RIP na sheria itende haki.

    ReplyDelete
  19. Ingekuwa nchi za wenzetu basi hiyo hotel na mali yote ya hotel wangekabidhiwa watoto wake na mke wake na wakubwa wote wa hotel jela maisha na waliohusika but kwa bongo tambarare hakuna kesi hapo msibishane bure, mnyonge nyongeni tu bongo bwanaaaaaaa

    ReplyDelete
  20. Tabia za kuchukua sheria mikononi zinaleta maafa kila kukicha,na serikali isipofanya kweli basi amani tanzania imekwisha

    ReplyDelete
  21. Kwa sheria ipi? kwa haki ipi? kwa utu upi Watanzania? Wapi tunaelekea? Natoa wito kwa yeyote atakaeguswa kwa Wanasheria wa nyumbani ajitokeze na kuhakikisha familia ya marehemu inapata haki,

    Watot wake wataenda wapi, kwa kipi alichokifanya? kuingia bure? KWELI NDUGU MENEJA ULIETOA AMRI KWELI? Tumefikia hatua hii? wapi tunakwenda ma kuelekea,

    Huyo meneja, hao walinzi na kila aliehusika wanapaswa kuchukuliwa HATUA KALI ZA KISHERIA, kwani hata kama ni bosi wako akikuamrisha kama kitu ni kinyume cha sheria HUPASWI KUKUBALI, HAKUNA ALIYE JUU YA SHERIA NDUGU ZANGU,

    Kalale pema Lilah, Mwenyezi Mungu akuafu,

    Matukio

    ReplyDelete
  22. Tatizo la watu kujichukulia sheria mkononi lipo sana na si ajabu kusikia kuwa kibaka aliyekwapua simu kavishwa tairi shingoni na kutiwa kiberiti. Polisi hufika katika matukio haya wakiwa wamechelewa, kuchukua maiti yao na kwenda wakujuako. Kamwe husikii watu waliohusika wakuchukuliwa hatua yo yote.

    Kama serikali ingekuwa kali na kukemea tabia hii kwa nguvu zote, naamini mambo yangebadilika ingawa pengine kiini chake hasa ni hasira walizonazo watu kuhusu ugumu wa maisha na matatizo yetu katika mfumo wa utoaji haki.

    Mbona tumeweza kupunguza mauaji ya albino na vikongwe kule kanda ya Ziwa? Bila shaka hata hili tukilivalia njuga tunaweza kulikomesha.

    Nilishawahi kulizungumzia suala hili katika blogu yangu hapa:

    http://matondo.blogspot.com/2010/08/kweli-yote-haya-ni-kwa-ajili-ya-simu.html

    Tukisubiri mpaka hawa masikini wachoke kuchomana moto wao kwa wao na kugeuzia hasira zao kwa wamiliki wa mfumo, tutakuwa tumechelewa.

    Mungu Ibariki Tanzania!

    ReplyDelete
  23. Halafu Meneja mwenyewe ni Mhindi.

    ReplyDelete
  24. Afrika kuna mambo ya ajabu kama nini? Hivi ni lack of education? upumbavu? au nini? Inaiskitisha sana. Hii ndio Afrika yetu na waafrika wanaona kama ni normal.

    I hope sheria itachukua mkondo wake.

    ReplyDelete
  25. touched with this ! this person did this he/she will get it back 100 times. God is watching you! u can run but u will never hide!

    ReplyDelete
  26. Wandugu, tumesema sana nadhani sasa inabidi kuchukua hatua. Nashauri yafuatayo:

    1. Kila anayesoma maoni haya kama uko Dar, basi wewe, familia yako na rafiki zako MSIENDE SOUTH BEACH TENA! Mimi nimeshaweka azimio - SITAKANYAGA TENA!

    2. Mwambie kila atakayekusikiliza kama ana mpango wa kwenda huko - ASIENDE TENA. Dar Beach ni bwerere, tumejaaliwa

    3. Tumbane mbunge wa Kigamboni Dr. Faustine Ndugulile AFUATILIE haki ya wahusika kushtakiwa na pia Hoteli ichukue jukumu la kutunza familia a marehemu

    4. Chama cha haki za binadamu Tanzania (Francis Kiwanga), tafadhali FUATILIENI haki itendeke!

    5. Kila mmoja wetu anayependa Amani ya kweli sio amani feki ambayo watanzania tunajivunia, basi shawishi mwenzako asiue mwizi! Kumbuka wewe unakuwa muuaji!

    Kama kuna mwingine ana maoni zaidi, naomba aongezee.

    Kwa kweli imeniuma sana!

    Mdau Leanji Kyangwe

    ReplyDelete
  27. Ankal unatupa maendeleo ya huyu jamaa tu, huyo meneja na mwenye hoteli vipi? Piga simu polisi wakueleze wamechukua hatua gani utuhabarishe! TUMECHOKA MAMBO HAYA KUTUIBIA MTUIBIE NA HATA MAISHA MTUONDOLEE! AAAARGH!

    ReplyDelete
  28. Yaaani nimeishiwa na nguvu hata ya kutoa maoni. nimeumia kiasi kwamba nashindwa kujielezea.Natoa tuu pole mke,watoto, ndugu, jamaa na marafiki kwa kuondokewa na mtu wenu.Serikali imeozaaaa.

    ReplyDelete
  29. Jamani Meneja wa Hiyo Hoteli ya South Beach ahusike na kifo cha mwananchi huyo. Ni tabia mbaya kumchoma mtu na kama alizamia na hakuimba kitu si walitakiwa wamtoe nje ili asirudie tena lakini jambo la kumchoma moto mtu ambaye wanamwona siku zote anauza biashara zake si vizuri hata kidogo. Sheria ichukuwe mkondo wake la sivyo hoteli hiyo ifungiwe. Na Meneja huyo Mhindi awekwe ndani aisaidie polisi vile vile.

    ReplyDelete
  30. jaman hapana hapana hapana kweli mtu kazamia unamchoma moto jaman na wewe bosi ulieamrisha hutadumu huku duniani kabisaaaa unamchoma mwezio moto kwani mngemtoa nje ingeathiri nini????? imeniuma sana sana yani wewe huna huruma kabisaaaaa na mungu hatakuacha wewe mjinga sana mnyama wewe gaidi wewe jaman serikali ichukue hatua msikae kimya plzzzzzzz huyo ni binadamu kama nyie haki itendeke tz hakuna haki jamaniiiii

    ReplyDelete
  31. kampuni inayoimririki hiyo hoteli inatakiwa ichukuwe jukumu la kuihudumia familia ya marehemu ikiwa ni pamoja na kuwasomesha watoto wa marehemu hadi ukomo wa elimu zao na ahadi za kutimiza jukumu hilo alikiri mahakamani na hadharani kupitia vyombo vya habari , ili ikiwa na utofauti jamii ipate pa kuanzia ; michuzi kama waweza fuatilia hili tafadhari .
    mdau
    Kakola , Bulyanhulu

    ReplyDelete
  32. KOSA NI KOSA BILA KUJALI NANI AMEFANYA, AWE NI MUHINDI, MWAFRIKA, MWARABU, MZUNGU, HAKUNA TOFAUTI. NA SOTE TUMETOKA KWA ADAM NA ADAM AMETOKA KWA UDONGO.

    LILILO MUHIMU VIONGOZI WATILIE UMUHIMU KUKEMEA DHULMA, NA WANAOKOSEA WAHUKUMIWE BILA YA KUTOFAUTISHA TAJIRI NA MASKINI, HADHI YA MTU AU RANGI YAKE. NA ADHABU IWE WAZI ILI WENGINE WAPATE SOMO NA WACHUKUE TAHADHARI WASIJARIBU KUFANYA DHULMA ZA NAMNA HIYO.

    ReplyDelete
  33. fundisho kwa wengine hapa mamlaka za leseni ikishirikiana na jeshi la police zishirikiane ili leseni ya huu ukumbi ibatilishwe hilo litakuwa fundisho kwa mwenye kumbi wote na watakuiwa na discipline. pia watu wachukuliwe hatua kwa sheria za nchi. kama sheria za kubatilisha lesseni hazipo basi ziongezwe ili ziwalinde wananchi mbona hata bungeni juzi sheria ya upigaji kura bungeni ilibadilishwa kukidhi matakwa ya bunge???

    ReplyDelete
  34. jamani we should not take the Law in to our own hands. we should be human even if marehemu alikuwa mwizi or kazamia klub but kumchoma moto sio solution mtachoma wangapi?? violence never solved anything sasa management ya south beach inaharibu reputation because of making the wrong decisions.

    ReplyDelete
  35. Kwanza natoa pole kwa familia, Mungu awajalie Neema na uwezo wa kukabili haya mazito yaliyowakuta.

    Mimi maoni yangu kwanza ni kwa upande wa familia. Tafuteni NGO inayotoa misaada ya kisheria ili hiyo hoteli ya South Beach iwajibishwe. Kwa sababu maamuzi yalitoka kwa meneja, hivyo hilo ni swala la hoteli nzima kwa iyo najua mna maumivu na uchungu mwingi kwa kumpoteza ndugu yetu ila pigeni moyo konde na haki itendeke nasi wote tupo pamoja nanyi.

    Kwa Watanzania, tusitegemee serikali kurekebisha kila jambo linalotokea, muda umefika sasa kusimama imara na kuchukua hatua sahihi. Haimaanishi kulipiza kisasi, haimaanishi kutumia nguvu ila endapo mtu unaona jambo baya linatendeka, usikae kimya. Ukimya wetu ndio unazidi kutupeleka pabaya na kwa maoni yangu tutafika pabaya SAANA TU kama hatutajua jinsi ya kuwasilisha hoja zetu na kuona kuwa zinasikilizwa na kushughulikiwa.

    Alafu, sehemu kama izo, Watanzania mnaenda kufanya nini baada ya tukoi kama hilo? Acheni kwenda mpaka msikie kuna usalama au wahusika wamewajibishwa kisheria. Haya mambo yanaweza kumkuta mtu yoyote kwani usikute jamaa alilipa kiingilio!! tusimame pamoja jamani, sawa wale walioshuhudia hawakuweza kufanya lolote ila sasa yamekwisha tokea na maisha ya ndugu yetu yamepotea kwa hiyo tuungane pamoja na familia yake na kuhakikisha haki inatendeka kwa niaba ya Lillah na kwa nia ya kuona wenye maamuzi katika hiyo hoteli wana utu ndani yao na sio wanyama.

    ReplyDelete
  36. Watu wamekuwa wakichukua sheria mkononi za kupiga au kuchoma moto mtu mpaka kuua kwasababu sheria kali haijaweka ambayo zitafanya mtu kuogopa kuchukua sheria mkononi.

    Sheria yetu imetokana na sheria ya uingereza nchi ambayo iko mbele kimaendeleo kupita sisi, kuuwa mwizi bila ushadidi wa kutosha kuonyesha kwamba maisha yako yalikuwa hatarini ni kinyume na sheria uingereza.

    Basi kwanini hatufuati sheria hii pia Tanzania.

    ReplyDelete
  37. Hakuna kifo ambacho ni kizuri nami ninaungana na waliosikitishwa na kuumizwa na kifo cha huyu ndugu.

    LAKINI NINAOMBA JAMII IKUMBUKE KUWA UJAMAA UMEKWISHA. SASA HIVI NI SOKO HURIA NA UJASIRI AMALI. KILA MTU ANATAFUTA PESA NA ANAWEKEZA ILI AVUNE. KAMA MTU HUNA PESA USILAZIMISHE KUTUMIA VITU VISIVYOKUWA VYAKO ETI TU KWA SABABU HAPA NI NYUMBANI.

    WATU KUVAMIA VIWANJA VYA WATU, WATU KUNG'ANG'ANIA NYUMBA ZA WATU BILA KULIPA KODI, WATU KUNG'ANG'ANIA WAINGIE DISCO AU DANSI BILA PESA!!!! SIYO UTAMADUNI MZURI.

    MBONA WEZI WANACHOMWA KWA KUIBA SIMU YA TSH. 100,000 TU.

    KILA MTU ALE JASHO LAKE KAMA HUNA OMBA USAIDIWE!

    ReplyDelete
  38. OOOh jamani huruma, sasa ndo hao wahindi wamekuja kutupa msaada, au aliyewekwa leo hii jumatatu kuwa ameleta msaada,amekuja kutusahaulisha? Naomba tupate taarifa Meneja aliyetoa kibali cha kuchoma naye apewe adhabu na wenzake. Mungu akuone ili utubu dhambi hii kubwa ya kuua.Jamani nimeumia sana poleni familia

    ReplyDelete
  39. Jamani, mbona inasikitisha!
    Hivi aliyeamuru achomwe moto anakula chakula kinamuingia nakulala usingizi unamjia! kama kweli maisha ya mwenzio yanaweza yakawa hayana thamani kwa sababu ya kiingilio cha disco! Hivi hatuna hata fikira ya kupambanua adhabu kulingana na kosa jamani! binadamu sasa ni mnyama hekima imekwenda wapi!
    Hakuna anayependa watu wavamie mali zao bila idhini lakini si kuna utaratibu wa sheria? hivi nchi ndiyo sasa hali ya sheria imefikia hapa jamani! Na huyo meneja bado ameajiriwa kwa maamuzi ya namna hii! ndio anafikiri ni njia ya kupandishwa cheo au kuendelea kubaki na madaraka aliyo nayo? Kama mwajiri wake bado amemhifadhi na kudhani ana-integrity basi biashara hiyo inapaswa ichunguzwe vizuri na serikali kupitia mkono wa sheria ifanye kinachotakiwa na wananchi tufahamishwe ni hatua gani iliyochukuliwa dhidi ya hao wauaji wa huyu ndugu. Tunastahili kujua ili tuwe na imani na serikali iliyopo madarakani.
    Mungu aihenzi roho ya ndugu huyu.
    Milka

    ReplyDelete
  40. HUYU MENEJA INAWEZEKANA NI BANIYANI, MAANA WAMEZOEA KUCHOMANA KATIKA MAHEKALI YAO, HAPA TANZANIA NA HUKO INDIA NDIO KABISA.
    HALAFU TUNAWAKUMBATIA ETI NI WAWEKEZAJI, MARA TUNAWAUZIA RELI, MARA NI MAMENEJA, MARA.... MPAKA WAPI?
    MUNGU WAFUNGUE MACHO VIONGOZI WETU WAJUE WANALOFANYA.

    ReplyDelete
  41. Tatizo la nchi hii, hakuna polisi atakaechukua hatua za msingi katika suala hili, ona kesi ya ajali ya chenge, ona rostam azizi, wanakula nchi. Cha msingi tutumie nguvu ya umma kushinikiza mkurugenzi akamatwe na wasaidizi wake, then hoteli ifungwe na muwekezaji wa kihindi asipewe nafasi ya kuendesha biashara ktk eneo hilo. Or else kisasi ni lazima either hoteli tuifanyie hujuma au wahindi wote wanaokwenda kigamboni tuhakikishe mmojawapo anachomwa moto kila mwezi.

    ReplyDelete
  42. KIMYA CHA VIONGOZI MBALIMBALI KUHUSU JAMBO LA RAIA KUULIWA OVYO OVYO, HATUELEWI NI WOGA RUSHWA AU NINI, HASA INAPOKUWA MUUAJI ANAPEWA DHAMANA, HATA SIJUI TUNAFUATA SHERIA ZA WAPI. HAYA NA SASA IMEFIKIA MTANZANIA MTAANI KWAKE ACHOMWA MOTO AKIWA HAI HADI KUFA.
    JAMANI TULIO MADARAKANI TUOGOPE MUNGU, TUNA DHAMANA, TUSIPOWAJIBIKA MUNGU ATATUHUKUMU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...