Ankal akiwa na mtangazaji mwandamizi wa Voice of America Bi. Khadija Riyami aliyeongozana naye White House jijini Washington DC leo tayari kuanza kazi ya kuripoti kutokea Ikulu hiyo ya Marekani, akijaza nafasi iliyoachwa wazi na Mh. Juma Nkamia, ambaye sasa ni Mbunge wa Kondoa.

Ankal ameiambia Globu ya Jamii usiku huu kwamba wadau wake wala wasiwe na hofu kwani libeneke litaendelea kama kawa kwani kaacha timu kubwa ya kuendeleza libeneke na wakati huo huo atakuwa akileta mambo moja kwa moja toka sebuleni kwa Obama. VOA wamekuwa wakimzengea sana Ankal ili akafanye kazi kwenye idhaa hiyo ya Kiswahili upande wa habari za mtandaoni.

Ankal akielezea mambo ya libeneke kwenye ukumbi wa mkutano wa White House baada ya waandishi wa White House na wa nchi mbalimbali kumuomba aelezee jinsi tasnia ya habari ilivyo Bongo kwa hivi sasa, hususan swala la kuibuka kwa 'vikombe' karibu kila kona ya nchi. Ankal aliwaambia kwamba ni kweli kumezuka watoa dozi sehemu kadhaa lakini hadi sasa Babu wa Loliondo ndiye anayetamba kuliko wengineo wote. Ankal alipata wakati mgumu sana kuelezea ni namna gani kikombe kimeshika hatamu Bongo.
Ankal akivinjari kwenye viunga vya White House
jijini Washington DC baada ya kutoa mada ya vikombe

Ankal akiwa ofisi za masuala ya nje ya Marekani (State Department) ambako ndiko ziliko ofisi za Bi. Hilarly Clinton. Kazi yake ya kuripoti habari za Ikulu ya Marekani huhusika na ofisi hii pia. Ameiambia Globu ya Jamii kwamba anamshukuru Mungu kwa 'kudakwa' na VOA na hivi sasa anajiandaa kupigana vikumbo na wanahabari wa dunia. Kasema ana uhakika kwamba endapo kama mambo hayatokua mswano ataingia mtaani kubeba boxi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 310 mpaka sasa

 1. hangera kaka michuzi zikuzote mtu ukifanya kazi kwa uangalifu na umakini uwaminifu matunda yake utaiyona.Congratulation brother michuzi keep it up tuwakilishe vizuri tunakuaminia waaeleze hao wazungu kwamba hata sisi tunaweza waambiee tumegundua dawa ya magonjwa sugu kama vipi nao waende tz kwa babu ambi wapate kikombe waachekujifanya wao wanajua kila kitu

  ReplyDelete
 2. Congratulations Mr.Soups.We are glad to have you close, but we will miss Bongo event's. Mark this event in your calender for Michuzi's promotion. He is trying to pull our legs! I don't wonna spoil the events keep rolling!!

  ReplyDelete
 3. Sikukuu ya Wajinga...April fools

  ReplyDelete
 4. Haya sasa....mapemaaaa.... a prank for April fools day!Ankal sijakupa bado pongezi zangu,teh!teh!Nitafanya hivyo ikitokea umetujuza siku tofauti na hii!

  ReplyDelete
 5. happy foolish day

  ReplyDelete
 6. hongera ankal ingawa duh hii aprili mosi inakua na balaa kweli unaweza ukapongeza ujinga kwakweli otherwise siku hii imepoteza mwelekeo kabisa

  ReplyDelete
 7. HAPPY FOOLS DAYS! NICE ONE ANKAL!
  Phatlorenzo-MN

  ReplyDelete
 8. Fools Day

  ReplyDelete
 9. Hongera sana ankal, na karibu sana Ughaibuni


  Mdau.

  ReplyDelete
 10. congratulation on your knew career. God bless u

  ReplyDelete
 11. hahaha ankal nimefurahin sana kuwa umepata chance hiyo yaani ni great news kwa sisi wadau wa libeneke. sasa ankal nakushauri japo siku moja hebu pata nafasi ukabebe box ulione tamu yake maana unalisanifu sana box letu.
  madau maisha utani

  ReplyDelete
 12. sikukuu ya wajinga, mimi hujanipata ankal

  ReplyDelete
 13. Hongera Ankali na mungu akuzidishie
  Mdau Iceland

  ReplyDelete
 14. APRIL 01, FOOOOOOOOLS DAY

  ReplyDelete
 15. Is this an April fool joke or the real thing? utakua a photograph reporter au mwaandishi wa kalamu...If it not an april fool welcome to the USA the land of freedom of speech natumaini utakua muwazi sasa tukishakupiga kikombe cha freedom...

  ReplyDelete
 16. Nyie hamumjui Ankali, Mwaka jana alikuwa mbunge wa kata mpya...hii ni April 1

  ReplyDelete
 17. HAHAHAHA APRIL FOOLLLLLLLLLLLLLLLLLLLLLLLLLLLLL

  ReplyDelete
 18. unam-fool nani sasa? au kabisa una m-fuuuuuuuul nani Ankal?

  ReplyDelete
 19. April fools

  ReplyDelete
 20. Tevez wa TandaleApril 01, 2011

  Ankal kuna tetesi huku mitaani kuwa ulipata kikombe cha babu wa Loliondo ambacho kimekupa dhali la kukwea pipa na kuelekea kwa mzee Obama..Powa mkuu..muombe Mzee Obama aje atutembelee kama vile Mzee kichaka (Bush)..

  ReplyDelete
 21. Anka umejuwa kuwadanga miaka YOTE UMETENGENEZA HII PHOTOSHOP TEHTEH SAFI SANA UMEWAPATIA KWELI LOL TEHTEH PAZI. APRIL FOOL.

  ReplyDelete
 22. Happy April 1 Fools day everybody!!!!!

  ReplyDelete
 23. APRIL 1 BADO NI SIKU KUU YA WAJINGA ?

  ReplyDelete
 24. Michuzi u dont fool me,i m far away smart.LEO NI SIKU YA WAJINGA!!!!!!

  ReplyDelete
 25. April fools day !! haha!

  ReplyDelete
 26. Hii ni Friday,April 1.= Fools day


  Mdau
  Boston

  ReplyDelete
 27. Uncle leo ni April 1...na unajua habari za siku kama ya leo inabidi kuziangalia kwa umakini kidogo. Je, kuna uhusiano wowote kati ya hii post yako na siku ya leo au hakuna? Kama hakuna basi mimi nakutakia kila la kheri katika kitengo chako kipya.

  ReplyDelete
 28. Michuzi comment yangu itabidii tu uipublish siku ikiisha lol!!! Mwanzo I almost believed then nikakumbuka ya mwaka jana kuhusu zefulanazzzzzz yaani nimecheka sana. Ur good at this! Well done

  ReplyDelete
 29. Kaka,ni April 1st-fools day!Hope hutanii!Kila la Heri kaka.

  ReplyDelete
 30. "FOOLS DAY NI TAREHE NGAPI" / SIKU YA WAJINGA NI TAREHE NGAPI "NAOMBA KUELIMWISHWA"

  ALIYETENGENEZA PICHA AMEJITAHIDI KIDOGO NAKUPA MARKS 51%

  ReplyDelete
 31. APRIL FOOLS DAY SIO?????

  ReplyDelete
 32. Acha wee Ankal, leo ni April fool!!!
  mdau singapore.

  ReplyDelete
 33. Mmmmh..Leo siyo sikukuu ya Wajinga kweli!!!

  Anyway HONGERA SANA KAKA MISUPU

  ReplyDelete
 34. AzaniaBitozApril 01, 2011

  Michu

  Karibu sana ndugu yangu. Mie mdau wa tokea enzi hizo. Ninataka kukukaribisha rasmi nyumbani

  ReplyDelete
 35. Ankal hongera sana kwa kupata chaka la nguvu, nina matumaini kuwa sasa blogu yako itatoa habari zaidi katika wigo mpana sana kwa sababu umehamia sehemu itayokufanya uweze kupata habari za kuelimisha na kusisimua zaidi kwa wadau wako.
  Kila la kheri Ankal, tupo nawe kukuombea kwa Rabana akuzidishie kheri..

  ReplyDelete
 36. Siku ya wajinga imeanza before 12midnight hapa washington d.c
  wajinga ndo waliwaoooo, ule mwaka mwingine uliwakamata wajinga na ile stori ya kuwa jk kakuteua ukuu wa wilaya ya tegeta.

  ReplyDelete
 37. Michu!!!

  hongera sana jamani...

  ReplyDelete
 38. AzaniaBitozApril 01, 2011

  Duh,naona umetupata kweli kweli. Nilisahau TZ tayari April 1st !!!!! . Haya ngoja tuone maajuza tuko wangaapi LOL

  ReplyDelete
 39. Siku kama hii mwaka fulani ankal alichaguliwa na JK kuwa mkuu wa wilaya ya Tegeta... hii siku ina bahati sana kwa ankal lol...

  ReplyDelete
 40. Ankal nina wasiwasi hii ni april fool, hizi picha umezitunza kwa muda mrefu zaidi ya mwaka mmoja sasa! Najua unatuzuga tu ni yale yale ya mkuu wa wilaya ya nanihii! hahahaaaaa! hizi picha ulipiga wakati zile ulipoenda CA silicon valley mkapitia ikulu kwa Obama! acha kutuzuga ankal.
  Ni mimi mdau wa damu USA.

  ReplyDelete
 41. hongera kaka michuzi.lakini hii haendani na april fool ili kuturusha roho ya kukosa habari! haya hongera sana.

  ReplyDelete
 42. Ankal ni mimi mdau wa damu USA usijejisahau ukapost ile message niliyokutumia kwani watu wanachechetuka wamesahau kwamba ni april fool jichukulie umaarufu kwanza mpaka baadae au kesho ndo ulipue bomu hapa umewapata wengi na kila mtu atakuamini.

  ReplyDelete
 43. mmh sio April fool hii kweli?

  ReplyDelete
 44. MISUPU ONCE AGAIN ITS ME,i m far a way smart u cant fool me,LEO NI SIKU YA WAJINGA!!!!!!

  ReplyDelete
 45. Kama ni hivyo na mimi nina daraja la kuvuka kigamboni naliuza.

  ReplyDelete
 46. Mtani Muhidi,
  Sijui umekunywa kikombe kipi Loliondo TBR au Mbeya ? ila nakupa heko kwa kupenya hadi nyumba nyeupe. Tuwasiliane nikutupie ngalau viatu vya baridi maana ndio unaanza kibarua. Mtani Ottawa, Canada.

  ReplyDelete
 47. Hongera sana Kaka Michuzi, Mungu akupe nguvu ya kufanya kazi vyema, kila la kheri. Inshallah. Razia

  ReplyDelete
 48. jamani ni april full mweeee..........ankal bwana

  ReplyDelete
 49. April Fools na wajinga ndio waliwao!! hamuoni hata tarehe!! !lol!!

  ReplyDelete
 50. Naona umewapata wajinga. Keep it up leo ni Fools' day

  ReplyDelete
 51. HONGERA Michuzi kwa kuwapata wadau karibia sita hapo juu. Jamani Leo ni SIKU YA WAJINGA.

  Michuzi kawapata watu kibao nafikiri hii inaipiku ile kwenye gazeti miaka ya nyuma kuwa kuna Kampuni inatoa kazi hakuna cheti, uzoefu na hata kama wewe mwizi njoo tu.

  Kufikia saa tano watu kibao walijipanga kidongo chekundu

  Mimi simo

  Observer

  ReplyDelete
 52. he he he! Hii sio sikukuu ya wajinga kweli? manake dah! Wajanja hatuamini kirahisi

  ReplyDelete
 53. msemaKweliApril 01, 2011

  Ankal amesogezwa jikoni. Alipoulizwa kutoa ufafanuzi zaidi Ankal alisema "wajinga ndio waliowao" 4/1

  ReplyDelete
 54. happy April fools to you too.

  ReplyDelete
 55. april hiyo anachengua huyu ni sikukuu ya wajinga.umewapata wengi misupu

  ReplyDelete
 56. kumbe hata wa majuu hawajui siku ya wajinga....kweli box ni noma, linaweza kukukatia mawasiliano na dunia hata kama upo duniani.

  ReplyDelete
 57. April Fools.
  u tried.

  ReplyDelete
 58. ankaaal!ankaaaal!ucje ukawa uatutenda na april fools!!!!!!!!!!!!!!!!

  ReplyDelete
 59. Uncle
  i think its APRIL'S FOOLS DAY

  ReplyDelete
 60. Ankal in your dreams!!!!!!!!!!!!Utawapata wajinga tuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!!hilo ni chaka bovu......utambeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!Unafiri voice of america mchezo!!!!!!!!!eti white house!!!!!!!!!!utakaa sana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!labda ukanywe vikombe vya morogoro na sio Loliondo!

  Mdau...........

  ReplyDelete
 61. Mie nina wasiwasi na ankal, leo si ni tarehe 1 April siku ya wajinga!!!, ankal isije ikawa unataka kutuuzia mbuzi kwenye gunia. hiyo nafasi ilitangazwa lini jamani???

  ReplyDelete
 62. fools day.....

  ReplyDelete
 63. Hakuna lolote, siku ya wajinga leo. Mtoa habari umejitahidi kurubuni watu na pia habari yako imeukaribia uhalisia wa jambo. Hongera sana mwandishi.
  Kikongoti

  ReplyDelete
 64. isije ikawa april fool!

  ReplyDelete
 65. foolish day Ankal....try next time!!!!!!!!!!Keep dreaming men!one day yes!!!!!!!!!!!!

  Mdau.

  ReplyDelete
 66. April Foolzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz!

  ReplyDelete
 67. Leo umechakachua vizuri picha hizo na umewaweza wabeba box kweli kumbe wajinga bado wako wengi tena ughaibuni wanaokotwa kirahisi, safi sana ankal

  ReplyDelete
 68. As I always say. Preparation meeting an opportunity. Nimefurahi sana na ninakupongeza, sikujui lakini nashukuru kuwa unawaonyesha vijana kuwa kazi ngumu hulipa. Karibu Marekani.

  ReplyDelete
 69. its 01/04 pipo wake up!!! inadhihirisha ni jinsi gani wa TZ siyo wachunguzi wa mambo na ni wa2 wa kukurupuka tu, no wonder babu anakula vinchwa vya haja tu huko Loliondo

  ReplyDelete
 70. Ankal, hapo utawapata wengi wenye sikukuu yao, mimi hunipati ng'o.


  Abiola Jr, New Albany- Ohio

  ReplyDelete
 71. Mmmmmm! Leo siku ya wajinga!!!!

  ReplyDelete
 72. Hongera ankal kumbukeni leo ni siku ileeeeeeeeeeeeeeeeeeeee ya wa.......nga

  ReplyDelete
 73. Hamna lolote...
  humpati mtu..
  Sikukuu ya Wajinga hii

  ReplyDelete
 74. Ankal Jana tu nimekuona Bongo acha utani hatudanganyiki wewe upo na sisi hapa hapa Bongo maana wewe ni Mkuu wa Wilaya fulani JK alikuteua hahahahahahahahahaha wadau mpo?????? Karibu tupate kikombe cha Babu na cha dada........................TZ oyeeeeeeeeeeeeeeeeee.

  ReplyDelete
 75. Ankal, hongera kwa kulamba vichwa kisawasawa.
  Nimewakuta jamaa hapa Columbu, Ohio wanabishana sana juu ya ulaji uliupata.
  Sikutaka kukuharibia deal yako ya sikukuu, nikaondoka kimya kimya.
  Teh Teh Teh!!!!!!!!!!!!


  Kipara Siugonjwa, safarini Mikanjuni TA

  ReplyDelete
 76. Heri ya siku ya wajinga..........lol!

  ReplyDelete
 77. Tehe tehe tehe tehe tehe! Fools day leo umpati mtu Kaka! Wakati tulikuwa wote kwenye foleni za magari leo.

  ReplyDelete
 78. You reap what you sow! Juhudi zako hatimaye zimeonekana.
  Hongera sana Ankal.

  Mdau wa Mwenge

  ReplyDelete
 79. Jamani leo sikukuu ya wajinga, chunguza kwanza taarifa unayopata.

  ReplyDelete
 80. Umewakamata wengi! APRIL FOOLS!

  ReplyDelete
 81. Lakini leo ni siku ya WAJINGA

  ReplyDelete
 82. Uncle Michuzi, hii habari ni ya kweli au ni janja ya kuwapata wajinga leo?

  ReplyDelete
 83. Hongera saaaaaaaana Ankal Mithupu, tunakutakia kila la kheri katika kazi zako na maisha yako huko kwa Ankal Obama. Naomba ile ze fulanaz usiiweke pembeni kwani huenda ilichangia katika uteuzi huo.

  All the best brother!

  ReplyDelete
 84. Duh...Ankali kweli wewe kiboko, wakati nimeona habari hii na kuona tarehe yake nimekukubali kwa kuweza kuwapata wajinga wengi namna hii...na hii inaonyesha ni jinsi gani wabeba mabox wenzentu walivyo na IQ ndogo na no wonder tunabeba box wakati tunaweza rudi home na kufanya mambo makubwa zaidi...poleni mliopatikana na dhahama hii ya ankali kwenye siku ya wajinga..lakini ankali dini yako si hairuhusu huu upuuzi? that means umetenda dhambi ya kusema uongo...haaaa,kweli pepo kazi!

  ReplyDelete
 85. thanks Uncle Michu kwa kutufurahisha, lakini watu wakumbuke leo ni FOOOOOOOOOOOOOOOOOL's DAY (kwa kimatumbi - Siku ya WAJINGA)!!

  ReplyDelete
 86. SASA ANKAL.. NAONA ILE TOPIC YA WABEBA BOKSI IMENIFANYA MIMI NICHEKE SANA.. Nakutakia kila la heri huko. Duh sasa tutakumiss sana hapa bongo maanake.. duh.

  Sasa wewe ni mkurugezi wa wabeba maboksi washington..
  Jamani usitusahau. Mungu akubariki

  ReplyDelete
 87. happy april fools day to you all

  ReplyDelete
 88. Hivi leo ndio Aprili mosi, siku ya wajinga??

  ReplyDelete
 89. No big News ankal. Mi nilijua,BREAKING NEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEWS ankal naye Aoteshwa, aanza kugawa kikombe Nyumbani Lounge. Yaani sikukuu ya wajinga, umewapata wengi. Ni april mosi.

  ReplyDelete
 90. Leo ni April fools day

  ReplyDelete
 91. kaka michu leo ni siku ya wajinga mweh

  ReplyDelete
 92. sikukuu ya wajinga (fools day)??

  ReplyDelete
 93. Yaani wote mmeingizwa mkenge na ankal Happy Fools Day , ankal tupo naye hapa samora tunakula bata.

  ReplyDelete
 94. LEO NI SIKU YA WAJINGA ACHA POROJO ZAKO.HA HA HAH!

  ReplyDelete
 95. April fool

  ReplyDelete
 96. Well come to the World. New career and life. Well come. No job no money.

  Mdau Duke University- Durham ,North Carolina

  ReplyDelete
 97. Wajinga ndo wali wao...Happy april fools day ankal........kwikwikwi

  ReplyDelete
 98. Aucle,hongera...ila yantia shaka kama sio kwamba umetukamata masikio kwani leo ni fool's day!

  ReplyDelete
 99. Jamani hii sio april fool?

  ReplyDelete
 100. hahahaha hongera and happy fools day ankal

  ReplyDelete
 101. Utakuwa umewapata wengi!! Fools day!!!!!!!!!!!

  ReplyDelete
 102. 01/04/2011 uncleeeeeee!!!!

  ReplyDelete
 103. Hii ni tarehe 1 April, Au...?

  ReplyDelete
 104. April Fools Day.

  ReplyDelete
 105. HONGERA SANA BRO MICHUZI AS LONG AS HAIHUSIANI NA SIKU YA LEO. KILA LA KHERI!

  ReplyDelete
 106. Ehhh nyie wa juu wote leo ni tarehe ngapi vileeee..........!!!!!!

  ReplyDelete
 107. Siamini nadhani kama siku ya wajinga vile!!!! Mmmmh!

  ReplyDelete
 108. MMMh nawasiwasi na Misupu!! Leo ni siku ya wajinga isije ikawa unatuingiza town.

  ReplyDelete
 109. Michuzi siyo mambo ya fools day hayo???
  Mi sikubali leo tarehe 1 April. te te teheeeee......

  ReplyDelete
 110. Nahisi kama sikukuu ya wajinga hivi

  ReplyDelete
 111. Happy Fools day Ankal!

  ReplyDelete
 112. hahah sikukuu ya wajinga...umewapata wengi sana

  ReplyDelete
 113. fools day leo

  ReplyDelete
 114. April 1 sikukuu ya Wajinga. haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

  ReplyDelete
 115. Mangi wa KiboshoApril 01, 2011

  Muongo tu huyu jamani. Leo ni siku ya FOOL DAY shauri yenu!

  ReplyDelete
 116. Ankal hapo c kama unatuingiza mjini kweli hapo kwenye fools day . Jana tu nimekuona pale mzalendo aloo

  ReplyDelete
 117. Ankal hivi sio ndo umewavuna watu nadhani leo ni April 01, siku ya wajinga vile

  ReplyDelete
 118. Its a fools day leo

  ReplyDelete
 119. tumeshuka kaka leo ni april fool jaribu mwakani kaka

  ReplyDelete
 120. mh hii sio april fools day????

  ReplyDelete
 121. Happy fools day! Ha ha ha ha, mwaka jana mkuu wa wilaya mpya, mwaka huu VOA, ha ha ha haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, umeshawakamataaaaaaaaaaa. Mbavu sina mie ha ha ha

  Mdau Singida

  ReplyDelete
 122. Hope this has nothing to do with the April fools day!
  If not so, hongera!

  ReplyDelete
 123. Hivi Mnajua kwamba leo ni "Fools Day"

  ReplyDelete
 124. Hii ni April fools day.. Michuzi wewe upo Bongo. Hizo picha ni when Kikwete alipokuja USA.. Si unaona bendera ya TZ ipo kwa press conference..
  Ikulu ya Marekani hamna Bendera ya Tanzania wala nchi nyingine..
  Kamata bajaji.. wewe mwezetu bado.

  ReplyDelete
 125. SIKU YA WAJINGA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!TEH TEH TEH

  ReplyDelete
 126. Kila la kheri Michuzi katika siku hii ya wajinga duniani.

  ReplyDelete
 127. Duh! Hongera sana ankal. Sasa na wewe umekuwa mbeba mabox sio? usije ukawa umebeba binoculars. teh!

  Malisa(BG)

  ReplyDelete
 128. siku ya leo ikipita ndio nitaamini. labda ndio fools daya hiyo ankal, ila umewapata wadau wengi sana. yote hii ni kukuonesha kwamba tuko pamoja na wewe, na tunakuombea salama na kazi njema.

  ReplyDelete
 129. Amewapata! Bro Michu, umefanikiwa kuwapiga changa la macho wengi leo, hawakujua kwamba kumbe LEO NI SIKUKUU YA WAJINGA

  ReplyDelete
 130. Alhamdulillah! Tunasema Mungu ni Mkubwa!

  Ankal, juhudi huzaa matunda kaka, na Mungu kamwe hamtupi mja. Hongera ndugu yangu. Utuwakilishe vyema huko mjengoni.Ni juzi tu nilikuomba utoe suala la mashimo hapo Mbagala R/3, kumbe umeisha kwaa pipa kaka. Nakutakia mafanikio mema, na Allah akulinde, wabaya wasikusogelee, Inshallah!
  Wala usibebe box, we yakishindikana rudi tu kitaani tuendeleze libeneke hapa hapa kwetu, mbona kuzuri tu.
  Angalizo: Mashimo tayari yamefukiwa siku Mama Salma anakwenda Nyamisati na Balozi wa Japan - kituo.

  ReplyDelete
 131. Hongera Ankal Kwa kuula.
  Though kwako ni habari njema sana kwangu nakuwa na hofu kwani nishazoea kupata habari zilizovunjikavunjika muda wowote,na hapa nilikuwa nipo mbioni kukuuliza kuwa kwa nini siku hizi hupost habari kama zamani,kumbe ankal ulikuwa busy huko mastate,haya bana. Msalimie Obama! Mwambie asisahau kuja kunywa chikombe,nadhani hii itasaidia kutengenezwa kwa ile barabara!

  ReplyDelete
 132. wadau mmesahau leo ni siku ya wajinga duniani.

  ReplyDelete
 133. Ha ha haaa... ANKAL...Ama kweli umewatoa wengi kwenye hii APRIL FOOLS DAY! Hongera sana!

  ReplyDelete
 134. hongera kaka yangu ila usiache mbachao si unajua glob yako ilivyo muhimu sana kwetu wa tz

  ReplyDelete
 135. jamani its fools day.....mbona hii comment hamuweki

  ReplyDelete
 136. Ni kweli siku ya wajinga leo ?sina hakika sana ila naona kama kuchukua nafasi ya Juma Mkamia Haina ukweli kabisa najua wewe ni mpiga picha

  ReplyDelete
 137. Jamani jamani jamani naomba kuwatakia wadau wote wa blog hii ya jamii happy to be fooled day especially kwa Ankal Misupu kuweza kuwazoa wachangiaji waliopita ambao kwa kweli wameweza kuwa fooled happily..

  Kweli kaka Michu kazi unaiweza mpaka umeleta ma-library na kupata abiria wa kuwa-fool, hii inaonesha ni kwa kiasi gani unakubalika na jamii ya kitaifa na kimataifa!

  Mdau kutoka Moshi!!!

  ReplyDelete
 138. Mhhnnnnnnnn......Kama kweli, Hongera sana Mithupu lakiniiiiiiii????

  Isije ikawa April Fools Day

  ReplyDelete
 139. Mmmmmmmmh!hizo picha mbona kama zimepachikwa ankal?
  nona umewapata wengi,happy foolish day ankal!

  ReplyDelete
 140. Hahahaha.... Ngoja nicheke kwanza... Maelezo badae. Kazi njema wana globu ya jamii

  ReplyDelete
 141. SIKU YA WAJINGA HADI SASA UMEPATAWAJINGA TISA AMBAO WAMEKU SUPPORT , MASKINI WEWE UMEWAPATA KWELI

  ReplyDelete
 142. jamani leo sikukuu ya wajinga....khaaa....mmepatwa wengi kweli

  ReplyDelete
 143. duh ankal kawapa kweli... eti ohhh hongera sana... siku ya wajinga. wajanja hatudanganyiki!!!

  ReplyDelete
 144. April the 1st joke.
  Wabeja.

  ReplyDelete
 145. Asalaam alaykhum ankal, Hongera sana kwa mafanikio inshaalah mola atakulinda na uendelee kupaa zaidi katika ulimwengu wa habari.

  Wajina

  Chef Issa

  ReplyDelete
 146. hongera ankal, be blessed

  ReplyDelete
 147. April fools days tehe tehe tehe.... Wajinga ndo wanaopatikana siku huu ukiwasubiri kona tu wanatokea...

  ReplyDelete
 148. Ahhhhh! michuuuuu!! naamini u-ccm utakutoka au kupungua u will be thinking internationally not locally.

  ReplyDelete
 149. hongera mkubwa!!!!

  ReplyDelete
 150. hii kama April fool flani hiviiii

  ReplyDelete
 151. TEH TEH TEH...
  DANGANYA TOTO...CKUKUU YA WAJINGA HUMPATI MTU ANKAL...

  ReplyDelete
 152. Mh leo siku ni ya wajinga!

  ReplyDelete
 153. Happy fools day!

  ReplyDelete
 154. Hongera sana ankali wetu wa ukweli mungu akuzidishie nafasi za juu zaidi ili tupate habari na matukio zaidi tunakubali kuwa wewe ni muongoza jahazi la libeneke oyeee bongonl inakutakia kazi njema na maisha mema na familia ameen.
  bongonl.

  ReplyDelete
 155. siku ya wajingaaaaaaaaaaa

  ReplyDelete
 156. April Fool's Day!!!!

  ReplyDelete
 157. april fooooooooooooools day

  ReplyDelete
 158. Congrats!

  ReplyDelete
 159. KAKA HII TAARIFA UMEITOA SIKU MBAYA SANA KWANI NI TRH 1/APRIL NI SIKU YA WAJINGA DUNIANI NA KAMA ULIVYOWAPATA HAO WATOA COMMENT.KAMA NI KWELI BASI HONGERA SANA.
  MDAU

  ReplyDelete
 160. Michuzi!!! Leo ni siku ya wajinga

  ReplyDelete
 161. leo si ni siku ya wajinga jamani?

  ReplyDelete
 162. HAHAHAAA SIKUKUUU NJEMA ANKAL!(1Aprili)

  ReplyDelete
 163. 1 April...

  ReplyDelete
 164. heheheehe foools day yako serius kweli kweli

  ReplyDelete
 165. it is April Fools Day ~ Good luck

  ReplyDelete
 166. Congratulations and God bless
  Wakatabahu

  ReplyDelete
 167. Félicitations!! Pamoja na habari toka sebuleni kwa Obama, tunaomba kasi ya nyuz za bongo liendelee kama kwa!
  Tout le meilleur,

  Mdau, Geneva!

  ReplyDelete
 168. SIKU YA WAJINGAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA

  ReplyDelete
 169. mnh!!! hizi habari sio kwamba ni za 1st April fools day!!!!

  ReplyDelete
 170. LEO NI SIKU YA WAJINGA DUNIANI.KAWAPATA KWELI.

  ReplyDelete
 171. binafsi nimefurahi kuona umepata nafasi hii bro karibu sana huku wengine tumezamia.wengine tumekuwa tukisoma michuzi kila siku kupata kujua kinachoendelea back home.kwa kazi nzuri ulikuwa unaifanya i hope team uliyo iacha itaendeleza kazi hiyo.sijawahi kukuona but i feel like i know you very well.natumai one day tutakuona kwa macho star wetu,haa celebrity wetu.pooowa.again karibu sana ugenini kwetu kwa mr mkenya.haa obama.

  ReplyDelete
 172. Siku kuu ya wajinga hiyoooooo....umewapata

  ReplyDelete
 173. Success Is A Result Of Deeds And Not Dreams.

  HONGERA SANA - I FEEL LIKE ........AAHAMMM........ THATS ALL.

  PRINCE SAB - WERRASONIQUE

  ReplyDelete
 174. APRIL FOOL'S DAY

  ReplyDelete
 175. Leo ni tarehe 1 April. Umejua kuwapata watu.

  ReplyDelete
 176. Mh! Ankal, mie napatwa wasiwasi, maana leo ni SIKU YA WAJ....

  ReplyDelete
 177. Section ya waandishiwa habari wanaofuatil;ia speech yako mbona hujaweka? Kweli leo sikukuu ya wajinga.

  ReplyDelete
 178. Kumbukeni leo ni 1st April.............

  ReplyDelete
 179. April fools day....Ankal naona umewapata wajinga wachache

  ReplyDelete
 180. Acha hizo michuzi, au kwakuwa leo ni siku ya wajinga.....

  ReplyDelete
 181. WADAU MLIOTOA MAONI HAPO JUUU KUMPONGEZA MICHUZI IMEKULA KWENU.HAMNA TOFAUTI NA WALE WAJINGA WAPANGA FOLENI KWA AJILI YA KIKOMBE CHA BABU.

  MDAU KAMANDA TOKA UGHAIBUNI.

  ReplyDelete
 182. HIVI HAMJUI LEO NI APRIL FOOL...WABONGO BWANA,NA HONGERA JUU..LOL

  ReplyDelete
 183. Bendera ya Tanzania inafanya nini ofisini kwa Hilary Clinton? April FOOL. Mie hata hujanipata..

  ReplyDelete
 184. Uncleeeeeee!

  Naona umeamua kuhusisha mambo ya 1st April na jumbe jeupe sasa!!

  ReplyDelete
 185. Ankal umewapata hao siku ya leo ila siyo mimi. Is not a fool day today??
  ha haha !!

  ReplyDelete
 186. Ankali Michu.... kweli!!!!? au ndio unatufanya wajinga sisi with your 1st of April pranks!!

  Utanisamehe.... HONGERA yangu itasubiri 24hours.

  ReplyDelete
 187. Auncle michuzi,leo ni siku ya wajinga kaka.Nimekukamata

  WWW.LOCUSIMPEX.COM

  ReplyDelete
 188. happy fools day ankal

  ReplyDelete
 189. april fullllllllllll.

  ReplyDelete
 190. HONGERA SANA MKUU. HAYO NDO MAMBO. BINAFSI NAKUTAKIA KAZI NJEMA NA UWE MWAKILISHI MZURI WA WABONGO. Mdau wa Australia

  ReplyDelete
 191. Hi watanzania tuna matatizo gani jamani? tuko kama wanyama poli tunafuata sana mkumbo bila kutafakari. Hii habari ya Michuziikija kesho nitampa hongera lakini si leo siku ya wajinga. Imagine lugha au radio na TV zote za duniani ziliport kutoka white House, kutajaa sana. siyo? Michuzi anasifa kiasi za kuriport kukokea white house lakini sikubaliani na habari hii mpaka hapo kesho. Ninajua kuna uwezekano watu wengi wameliona hili lakini Bwana Michuzi amezuia posts zao ili kuwa-encourage wajinga wa leo kujinafasi. Michuzi please niwekee hii. Tafadhali.

  ReplyDelete
 192. ZISIJE ZIKAWA KAMBA. TAREHE YA LEO SI UNAIJUA -SIKU YA ......WEREVU. ILA KAMA NI KAMBA IMESUKWA VIZURI.

  ReplyDelete
 193. MICHUZI LEO NI SIKU YA WAJINGA 1st April , HUWEZI KUTUPATA WENGINE

  ReplyDelete
 194. SIKU YA WAJINGA NYIE MSIKURUPUKE KUTOA HONGERA..WAJINGA NDIO WALIWAO....!!!

  ReplyDelete
 195. happy fools day.......hahaaaa mithupu

  ReplyDelete
 196. mmh!siku ya wajinga leo,kalagha bao!we ankal hizi picha mbona ni za mwaka juzi ulivyokuja na msafara wa rais huku!?hao unaowaeleza habari za kikombe cha babu mbona hatuwaoni!!???
  But hongera kwa kuingia ikulu ya Obama ankal.

  ReplyDelete
 197. Ankali siku uliyotumia (tarehe moja mwezi Aprili!) kutanga hii kitu ni ya utata kidogo, isije ikawa unatupeleka pori!

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...