Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Halima Dendego akiangalia Tella ya matrekta madogo yaliyonunuliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kwa matumizi ya Halmashauri hiyo lakini yalibaikika kuwa hayana viwango vya ubora na kukidhi mahitaji ya matumizi.Halmashauri hiyo imesababisha hasara ya Mamilioni ya Fedha kwa kununua Trekta hizo ambazo hazina viwango vya ubora.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kilosa , akiangalia matrekta madogo na zana zake kwenye jengo la Ujenzi Wilayani humo ambayo hayana ubora na viwango.
Matrakta madogo 'power tiller' yakiwa hayana vifuniko kwenye matenki yake na hivyo kusababisha maji kujaa ndani, hivyo kukosa ubora wake.
Zana za matrekta madogo power tiller ambazo hazina ubora.

Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. inakuwaje haya ma trecta yame lala ?wakati wana nchi wanayaitaji sana .
    tutafika kweli ?

    mdau paris

    ReplyDelete
  2. Jamani muyarejeshe haraka huko yalikotoka. Hizo ni fedha zetu sote walipa kodi.

    Au mumeshakatiwa 30%.

    ReplyDelete
  3. Walionunua wamechukuliwa hatua gani? Hizo nyumba zao walizojenga zichukuliwe ziuzwe hela irudishwe.

    na huko walikonunua kulikua hamna contract? Ni heri waingie gharama ya kuyarudisha huko yalikotoka.

    Bongo tambarare...nani wa kumlaumu? Baba, mama, watoto nao wote wachakachuaji nai wakumwambia mwenzake stop...

    ReplyDelete
  4. Du, kweli kazi bado tunayo! Lilikuwa ni wazo la nani kununua hayo ma-toy? na akina nani wakapitisha na kuhakiki hayo malipo jamani???????????? Nasikia hasira sana kwa vitendo kama hivi!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...