Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI wakiwafafanulia wakazi wa Sumbawanga huduma mbalimbali wanazotoa kwa wananchi pamoja na Taasisi zake kwenye maonyesho yanayoendelea kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga. maonyesho haya yalifunguliwa rasmi tarehe 24 Juni, 2011 na Mkuu wa Mkoa wa Sumbawanga Mhe. Daniel Ole Njoolay.
Mwakilishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda akiwa katika Banda la Halmashauri ya Mpanda na baadhi ya zawadi ambazo halmashauri hiyo imewahi kushinda katika kipengele cha usafi ngazi ya miji nchini ambapo kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo Halmashauri hiyo imefanikiwa kushika nafasi ya kwanza na ya pili kitaifa.
Baadhi ya Mabanda ya Halmashauri na Taasisi mbalimbali zinazotoa huduma katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kama yanavyoonekana katika Uwanja wa Nelson Mandela, Mjini Sumbawanga. Maadhimisho haya yalifunguliwa tarehe 24 juni 2011 na yatafikia kilele chake tarehe 01 julai 2011 na Waziri Mkuu Mhe.Mizengo Kayanza Peter Pinda.
Kikundi cha ngoma ya asili ya Wafipa kikitumbuiza katika uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga mahali ambapo maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika. kauli mbiu ya mwaka huu ni Sherehekea miaka 50 ya uhuru kwa kuimarisha ugatuaji wa Madaraka kwa wananchi kwa maendeleo yao.
Sehemu ya umati wa watu wanaofurika kila siku kwenye maonyesho ya siku ya Serikali za Mitaa ambayo yanaendelea kufanyika katika viwanja vya Nelson Mandela mjini Sumbawanga.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...