Home
Unlabelled
shaggy atinga kijiji cha makumbusho ya wasukuma Bujora,asimikwa ubalozi wa kabila hilo, atumbuiza kirumba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Balozi wa Wasukuma, duh:-)! Toleho lolo mkaya mkingwa Shaggy, washika!
ReplyDeleteUmasikini ni kitu kibaya
ReplyDeleteShaggy u rock woooooooooooooooooow. i love this guy.
ReplyDeleteMdau wa monday 27 06:42:00 ASANTE sana umesomeka mkuu.halafu swali kwa hawa waandaaji wa hizi BURUDANI mbona wanamuziki ni wengi nje mnakalia kuleta hao hao wa aina moja mnaboa sana.ebu amkeni!
ReplyDeleteHUYO ANAESEMA UMASIKINI KITU KIBAYA UNA MAANA GANI KWANI KUNA UBAYA GANI SHAGY AKIENDA USUKUMANI HUJUI NDIO MOJA YA MAENDELEO
ReplyDeleteSAFI SANA HONGERENI MLIOFANIKISHA ,NIMAENDELEO MAKUBWA SANA,
ReplyDeletemoney and power rule the world
ReplyDeletewe mdau uliosema hayo ni maendeleo kweli??? Hivi mandhani akitoka hapo anaenda kutangaza utamaduni wetu..nooo way. Yeye ilimradi kapewa mshiko wake..na kwanza hata Marekani hawajui kuwa Shaggy yupo TZ na kwanza kafulia. wanamziki wanaokuja bongo wote wachovu.Jaribuni kuchukua mtu kama Beyonce aje kuburudisha tuone itakuwa cipi na kiingilio kitakuwaje...
ReplyDeleteyou are right Money and Power rule! Hata mzungu ukiwa na pesa au kitu anachokihitaji atakunyenyekea.
ReplyDeleteShaggy chifu wa Wasukuma!!!, ama kweli Wasukuma tumeishiwa. Jamii yetu imejengwa katika matabaka mbalimbali ambayo nguzo zake kuu ni mila na desturi. Tatizo kubwa ambalo linaikabili jamii yetu kwa sasa ni uhaba wa watu wenye fikra na hekima nzuri katika kupambanua mambo mbalimbali yanayo iathiri na yatakayo iadhiri jamii yetu katika kizazi kijacho.
ReplyDeleteInanishangaza na kunisikitika sana ninapoona wazee wetu tunaowategemea kuzilinda na kuziendeleza hizi nguzo zetu kuu katika jamii wanapoanza kuzibomoa hasa pale pesa inapokuwa ndio mzizi wa utoaji wa maamuzi. Pomoja na kwamba Mwalimu Nyerere aliamua kufutilia mbali uongozi wa machifu katika jamii ya kitanzania. Nikiwa mmoja wa wajukuu wa aliyekuwa chifu wa Itilima, Marehemu Limbe Mwinula, inaniumiza sana ninapoona kuna watu kwa sasa wanajifanya ndio vinara katika maamuzi ya mila na desturi kwenye jamii yetu. waswahili wanasema, ashakumu si matusi na nisamehewe kama nimekosea, ni lini na wapi Mark Bomani amepewa haya madaraka ya kutuamualia maswala mazito kama haya. Kwanza, yuko pale kwa ajiri ya masilahi yake kama mmoja wa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya serengeti breweries. Huyu Shaggy, Ninaamini kwanza hajui chochote juu ya historia, mila na desturi ya wasukuma, kama serengeti breweries wanataka wajulikane katika bidhaa zao(market exposure), inanisikitisha sana kuona wanafanya hivi kwa kupitia kwa wazee wetu ambao hawajui nini maana ya ''market economy'' katika dunia ya sasa iliyojaa ulaghai katika masoko ya bidhaa. Ama kweli, elimu bila fikira na hekima ni kazi bure.