Ilikuwa saa, siku, wiki miezi, mwaka na sasa ni miaka 10 tangu ulipotutoka na kutuachia pengo kubwa katika maisha yetu hapo Julai 06 mwaka 2001, pengo ambalo asilani halitozibika. 
Hayati Christine Elias Nducha
Unakumbukwa sana na mumeo Jairos Nducha, watoto wako Pius, Flora, Elias, Ben na George Nducha, wajukuu zako Emmanuel, Jairos, Angel na Billgates, wadogo zako, baba na mama zako wadogo, wifi na shemeji zako, ukoo mzima wa Kaombwe, Kassanga na Nducha. 

Pia jamaa, marafiki na jirani zako ulioishi nao kwa amani, wema na upendo usioelezeka. Wema na upendo wako usio na mpaka,ushauri na mchango wako katika maisha yetu ni kumbukumbu inayotusaidia kusonga mbele na kuendelea kukuenzi. Ingawa ni miaka 10  tunaona kama umetutoka jana kwani uchungu na majonzi mioyoni mwetu havielezeki, tulikupenda sana lakini Mungu amekupenda zaidi.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake na lihimidiwe!
AMINA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...