Mwenyekiti wa CCM taifa, Jakaya Kikwete, Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar, Aman Abeid Karume (wa tatu kushoto), Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi (kushoto), Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa (kulia) na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Willson Mukama, wakiwa katika ufunguzi wa Kikao cha Kamati kuu kilichofunguliwa leo Julai 31, katika Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika ufunguzi wa Kikao cha Kamati Kuu  kilichoanza leo Julai 31, 2011 katika Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma. Katikati ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mkataba mwingine kama wa Dowans huu hapa!
    Na Gerald Kitabu

    Ni ule mwekezaji aliyepewa ardhi kwa miaka 99
    Kodi ya ardhi sh. 200, Halmashauri kupata sh.500


    Wananchi, watendaji wa vijiji na Madiwani wa kata za Litapunga na Mishamo Wilayani Mpanda, Mkoa mpya wa Katavi, wamepinga yaliyokuwa makazi ya wakimbizi ya Mishamo na Katumba, kukodishwa kwa mwekezaji ambaye ni kampuni ya Agriosol ya Marekani, kwa maelezo kwamba uwekezaji huo, hautakuwa na tija kwa taifa.

    Makubaliano ya awali (ambayo NIPASHE inayo nakala yake), kati ya mwekezaji huyo na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda, yanaonyesha kwamba kampuni ya Agrisol itakodisha kwa miaka 99, eneo la Katumba hekta 80,317 na Mishamo hekta 219,800.

    Mwekezaji pia atalipa Sh. 200 kama kodi ya ardhi kwa ekari na Halmashauri itapata Sh. 500 kwa ekari, hata hivyo haijulikani malipo hayo yatalipwa kwa muda gani yaani kwa mwezi au kwa mwaka.

    Makubaliano hayo yanaonyesha pia kwamba iwapo kutatokea mgogoro, serikali itatumia busara kuutatua lakini ikishindikana, shauri hilo litasikilizwa jijini London, Uingereza na msuluhishi ambaye atakuwa Chemba ya Biashara ya Kimataifa (International Chamber of Commerce).

    Kadhalika, inaelezwa kwamba mwekezaji huyo ataajiri mameneja wa mashamba kutoka nje hususan Afrika Kusini na ataendesha kilimo cha mbegu za kimaabara.

    Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa serikali wakiwemo Mawaziri na wale wa Halmashauri ya Mpanda, wamekuwa 'wakipigia debe' uwekezaji huo, kwa madai kwamba utaongeza uzalishaji wa chakula na kuongeza ajira kwa Watanzania.

    WANANCHI

    Watendaji wa vijiji na Kata zinazozunguka maeneo hayo, wamepinga uwekezaji huo kwa maelezo kwamba hawajashirikishwa kikamilifu na hati hiyo haina maslahi kwa taifa.

    Wakizungumza na waandishi wa habari walioongozana na timu ya watafiti kutoka shirika la HakiArdhi kuhusiana na uwekezaji huo, viongozi hao na wananchi wameitaka serikali ijifunze kwa yaliyotokea kwa kampuni tata ya Dowans kwa kujifunga na mikataba mibovu, ya muda mrefu kwa bei chee.

    Mwekezaji pia anaitaka serikali ibadili sheria ili kuruhusu kilimo cha vinasaba (Genetically Modified Crops), ambacho kimsingi kinaua mbegu za asili na kudhoofisha ardhi.

    Diwani wa kata ya Litapunga, Godfrey Lusambo, alisema madiwani wa kata zinazozunguka eneo hilo, hawakuwahi hakualikwa kwenye mikutano iliyopitisha makubaliano hayo tata wala kwenda kwenye ziara nchini Marekani.

    “Viongozi wa wilaya wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Wenyeviti wa kamati na Madiwani wa kutoka mbali na hapa kama vile Mpimbwe na Ulwila ndio waliokwenda Iowa- Marekani na waliporudi tu sisi tukawa tunaletewa maagizo bila kujua undani wake,” alisema.

    Msafara wa wajumbe kumi waliokwenda Iowa-Marekani uliongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa, Salum Chima, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Rajabu Rutenge, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpanda, Philip Kalyalya, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpanda Silvester Nswima, Mkurugenzi wa Wilaya Eng. Emmanuel Kalobelo, Mjumbe wa kamati ya fedha Rose Mayaya, na Mjumbe wa Kamati ya maadili Teddy Nyambo.

    Wengine ni Mwanasheria wa Halmashauri Patrick Mwakyusa, Afisa Kilimo na Mifugo Fabian Kashindye, na Haruna Mwakitanile (cheo hakikuweza kupatikana mara moja).

    Ofisa Mtendaji wa kata ya Mishamo, Agustino wanga, alisema hawajawahi kuiona kampuni ya AgriSol wala wawakilishi wao ambao ni Agrisol Tanzania Limited, na kwamba wamekuwa wakiwasikia viongozi wakieleza kuwa makazi hayo ya wakimbizi yatakodishwa kwa Wamarekani kwa miaka 99.

    “Mimi binafsi nina mpango wa kuhama kabisa maana wakiondoka wakimbizi tu, huduma muhimu nazo zitakoma, hatuwezi kuwezana na mwekezaji ambaye hatumjui,” alisema.

    Kwa upande wake, Katibu wa jumuiya ya wafugaji mkoani Rukwa, Masanja Katambi, alisema inashangaza kuona serikali inaingia mkataba usio na maslahi kwa taifa badala ya kuwapatia wafugaji maeneo hayo ambao wamekuwa wakigombea malisho na wakulima.

    CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...