Familia ya Mchungaji Aron Ngowi wa Old Moshi Tella Mande,kwa moyo mkunjufu, tunapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru ndugu, jamaa, majirani na marafiki wote waliofanikisha shughuli zote za msiba wa Marehemu mama yetu, Eunice Ngowi (pichani) ambaye alifariki katika hospitali ya KCMC na hatimaye kuzikwa tarehe 1/Agosti/2011 kijijini Tella Mande.


Shukrani za pekee tunaomba ziwafikie wauguzi wa hospitali ya KCMC na watumishi wote wa KKKT - Dayosisi ya Kaskazini. 


Asanteni sana kwa kumhudumia mama, kwa sala, maombi na kujitokeza kwenu katika kutufariji na kututia nguvu wakati wa majonzi. 
Shukrani za pekee ziwaendee kamati nzima iliyoratibu na kufanikisha shughuli nzima yakuusitiri mwili wa mama.
Tunapenda pia kutoa shukrani nyingi kwa majirani, ndugu, jamaa na marafiki kwa misaada yenu ya hali na mali na pia kushiriki katika shughuli zote za mazishi. 


Asanteni sana na MUNGU awabariki.
Shukrani kwa wote mliofika nyumbani  katika kutufariji, mliotupigia simu au kutuma ujumbe kwa njia zingine kwa nia ya kutufariji na kututia nguvu.
Kwa kuwa ni vigumu kumshukuru kila mtu kipekee, tunaomba shukrani hizi mzipokee wote mliohusika kwa njia moja ama nyingine katika kufanikisha shughuli nzima ya msiba huu wa mpendwa mama yetu Eunice. Hatuna cha kuwalipa bali tunamwomba Mwenyezi Mungu awajalie na kuwazidishia katika shughuli zenu za kila siku.

"Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo na kufa ni faida"
Wafilipi 1:21
Jina la Bwana lihimidiwe.
Amen

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Fadhili na Neema
    Poleni sana ndugu zangu.
    Tuzidi kumwamini Mungu. Kuweni imara na msikate tamaa
    Mungu wa mbinguni ataendelea kuwapigania na kuwafariji.
    Haiyenyi lanye!
    nyi inyi monomae onyu - mana o saichi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...