VIINGILIO STARS v ALGERIA
Viingilio kwa ajili ya mechi ya mchujo kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon kati ya Taifa Stars na Algeria vitakuwa kama ifuatavyo;

Viti vya kijani ni sh. 3,000, viti vya bluu sh. 5,000, viti vya rangi ya chungwa sh. 7,000, VIP C sh.10,000, VIP B sh. 20,000 na VIP A sh. 30,000. Tiketi zitaanza kuuzwa Septemba Mosi mwaka huu.

Taifa Stars tayari iko kambini tangu jana (Agosti 28 mwaka huu) na inaendelea na mazoezi Uwanja wa Karume ambapo wachezaji wote wa ndani waliripoti jana mchana na kuanza mazoezi jioni.

Wachezaji wan je waliofika jana usiku ni Abdi Kassim na Dan Mrwanda kutoka Vietnam na Mbwana Samata kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Athuman Machupa (Sweden), Henry Joseph (Norway) na Idrisa Rajab (Kenya) wanaingia leo jioni.

Nizar Khalfan wa Vancouver Whitecaps ya Canada ndiye atakayekuwa mchezaji wa mwisho kuripoti kambini. Khalfan atatua nchini kesho saa 5.15 usiku kwa ndege ya PrescisionAir akitokea Nairobi.

TWIGA STARS KUAGWA KESHO
Timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu (Twigs Stars) inayoondoka Agosti 31 mwaka huu kwenda Maputo, Msumbiji kwenye michezo ya All Africa Games itakayofanyika nchini humo kuanzia Septemba 3-18 mwaka huu itaagwa kesho (Agosti 30 mwaka huu).

Twiga Stars wataagwa saa 6 mchana kambini kwao hoteli ya Itumbi iliyopo Magomeni Mwembechai, Dar es Salaam. Wakati huo huo Kocha Mkuu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa leo ametangaza majina ya wachezaji 16 watakaokwenda Maputo.

Wachezaji hao ni Sophia Mwasikili, Fatuma Omary, Mwanaidi Tamba, Fatuma Bashiri, Mwajuma Abdallah, Asha Rashid, Mwanahamisi Omari, Pulkeria Charaji, Ester Chabruma, Zena Khamis, Fridian John, Fatuma Mustafa, Ettoe Mlenzi, Ftuma Khatib, Maimuna Said na Mwapewa Mtumwa.

Viongozi watakaofuatana na timu hiyo ni Mkwasa, kocha msaidizi Nasra Mohamed, daktari wa timu Dk. Gania Seif wakati Meneja wa timu hiyo ni Furaha Francis.

Mechi ya kwanza ya Twiga Stars itakuwa Septembe 5 mwaka huu dhidi ya Ghana wakati ya pili dhidi ya Afrika Kusini itachezwa Septemba 8 mwaka huu. Twiga Stars itacheza mechi yake ya mwisho katika hatua ya makundi Septemba 11 mwaka huu dhidi ya Zimbabwe.

KIM AITA 30 TIMU YA VIJANA
Kocha wa timu za vijana Kim Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 30 wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kwa ajili ya mazoezi mwezi ujao.

Wachezaji walioitwa ni Saleh Ally (TSA), Jackson Wandwi (Azam), Hassan Kessy (Mtibwa Sugar), Khamis Mroki (Mtibwa Sugar), Yassin Mustapha (Polisi Dodoma), Andrew Kasembe (Moro United), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Ally Teru (Simba), Said Ruhava (Kagera Sugar), Samuel Mkomola (Azam), Frank Damayo (JKT Ruvu), Omega Seme (Yanga), Atupele Green (Yanga), Thomas Ulimwengu (ABC Sweden) na Jerome Lambele (Moro United).

Wengine ni Simon Msuvan (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Alex Joseph (Majimaji), Ibrahim Rajab (Azam), Renatus Patrick (Polisi Dodoma), Abdallah Kilala (AFC), Rajab Zahir (Moro United), Amani Kyata (TSA), Edward Shija (Simba), Alfred Amede (Russia), Khelf Hassan (Kenya), Emily Mgeta (TSC Mwanza), Ramadhan Salum (Simba), Frank Sekule (Simba) na Hassan Dilunga (Ruvu Shooting).

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...