THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA YAADHIMISHA MIAKA 50 YA UHURU

Na Anna Titusi – MAELEZO.

Vyombo vya ulinzi na Usalama nchini Tanzania vimefanikiwa kusimamia ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi na kuwawezesha wananchi kutekeleza majukumu yao katika hali ya amani na utulivu.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi wakati wa ufunguzi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.

Amesema Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kukomesha vitendo vinavyosababisha kuwepo kwa uvunjifu wa amani huku akiwapongeza wananchi kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kudumisha amani, utulivu na mshikamano.

“ Nachukua nafasi hii kuwapongeza watanzania wenzangu kwa kudumisha amani , Utulivu na Mshikamano katika kipindi chote cha miaka hamsini tangu tupate uhuru, ni matumaini yangu Amani , Utulivu na Mshikamano huu utaendelezwa kwa maslahi ya taifa” Amesema Dkt. Mwinyi.

Kwa Upande wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange amesema kuwa jeshi limekuwa na mchango mkubwa wa usalama tangu uhuru mpaka sasa na kuongeza kuwa uimara wake katika miaka hamsini ni jambo la kujivunia.

Amefafanua kuwa Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania limeundwa na watanzania kwa ajili ya kulinda na kudumisha uhuru wa Tanzania na kubainisha kuwa JWTZ limetoa mchango katika ujenzi wa miundombinu,utoaji wa huduma za afya, uokoaji wakati wa majanga na ulinzi wa amnai ndani na nje ya Tanzania.

Pia amesema maandalizi ya kuunda jeshi dogo yanaendelea ili kuweza kuchukua vijana kwa ajili ya kulitumikia jeshi na kuongeza kuwa sheria ya kutumikia jeshi kwa vijana haijafutwa.

“Bado tunaendelea na utaratibu wa kuchukua vijana wanaomaliza vyuo kwa ajili ya mafunzo na tutaendelea kuboresha jeshi letu katika hali ya ulinzi na usalama katika Afrika mashariki” amesema Jenerali Mwamunyange.

Maadhimisho hayo ya miaka hamsini tangu Tanzania bara ipate uhuru yanaongozwa na na kauli mbiu ya Tumethubutu,tumeweza na tunazidi kusonga mbele”


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    WATANZANIA WANAIMANI SANA NA JESHI LAO,LAKINI TUNASIKITISHA NA TAARIFA ZA UFISADI NA DHURUMA WANAZOFANYIWA WANAJESHI WETU WA VYEO VYAO CHINI.
    WENYE MAMLAKA ACHENI KUDHURUMU HAKI ZA WAFUASI WENU. AIDHA ALIYEFANYA KITENDO HICHO AWAJIBISHWE.