Basi la Abiria la Raha leo lenye nambari za usajili T431 ARM lifanyalo safari zake kati ya Dar - Tanga likiwa limesheheni abiria mpaka mlangoni leo wakati likielekea Dar.picha hii imepigwa na mdau wa Globu ya Jamii ambaye yuko safari kulekea mkoani Tanga.Watu wa Usalama Barabarani tafadhalini liangalieni swala hili.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. ndo ivyo.. mamgari mengi sana ya mikoani yanajaza abiria kama kuku.. halafu ajili ikotokea eti bahati baya tunajifunza kutokana na makosa.. makosa gani kila siku tunarudia uzembe.. rushwa inachangia kwa sababu sio kwamba askari wa barabarani hawalijui hilo..

    ReplyDelete
  2. yap.
    hilo ni angalizo. wahusika mpo??
    tusije tukajikuta tunaomboleza kila siku.

    ReplyDelete
  3. HIZI tabia za kudharau sheria ndio zinazotuletea vilio na machozi
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  4. Kwanini aliye chukua picha au abiria wengine, hawa kulalamika? Yaani abiria mnaona, na kujua hatari, lakini mmekaa kimya! Mimi nadhani usalama wangu una aanza na mimi mwenyewe. Ni jukumu langu kuhakikisha kuwa niko salama. Laiti kila abiria kwenye basi hilo angetambua hilo, ujinga kama huu usinge tokea. Watu wangepiga simu polisi au trafiki au kutoa report sumatra, au wangegoma mpaka abiria nyongeza washushwe.

    ReplyDelete
  5. TATIZO HAPA NI U-FI-SA-DI NDANI YA JESHI LA POLISI(TRAFIC-POLICE) KUCHUKUA RUSHWA

    ReplyDelete
  6. AJALI hazitokwisha abadan na tutaendelea kuwa mayatima na wajane kwa uzembe na rushwa mpaka kila mmoja wetu atakapo wajibika ama kuwajibishwa kikweli.Tusiwe wepesi wa kusahau yanayotokea kila siku kwa kupotea roho za wenzetu kwa tamaa ya wachache.kumbuka leo mimi kesho wewe.

    Mdau endelewa kuwapasha habari wahusika na wakati huohuo tukijipatia elimu ya usalama wa maisha yako. Wito, 'timiza wajibu wako'.

    ReplyDelete
  7. Kwa kuangalia picha tu, unajua kuwa mpiga picha hii ambae ndie alieileta hapa yumo ndani ya basi hili. Tena picha inaonyesha kabisa kuwa basi hili liko njiani likendelea na safari yake. Suali ni kwa nini huyu mdau hakudai kushushwa? au tu kwa vile amepata kiti basi amesahau ajali? Kwa nini waliojazwa na kusimama humo ndani ni watoto tu? Hata majaraha ya maafa ya zanzibar yaliosababishwa na kujazwa abiria melini hayajapatiwa dawa, watu bado wanaendelea kuhatarisha maisha yao namna hii?

    ReplyDelete
  8. Duh Mimi nilisafiri na MV Victoria kutoka BKB wiki mbili zilizopita Mizigo ya ndizi ni hatari. Nilipiga picha lakini naweza kushare nanyi lakini ni hatari tupu.

    Observer

    ReplyDelete
  9. Usafiri hakuna au bei ya kupanda basi au meli yenye nafasi ni kubwa huimudu. Msikae mkalaumu watu wenye vyombo au serikali au abiria bure kwa sababu uko ughaibuni. Hata hiyo London metro watu wanajazana kama kuku isipokuwa haijatokea ajali. Nigeria na Comoro abiria wanapanda ndege huku wengine wanasimama. Huu unaitwa umasikini. WaTZ hatuna utamaduni wa kukaa foleni, kila mtu anataka apande basi au meli siku hiyo hiyo anayotaka kusafiri hata akiona meli imejaa hataki kusubiri siku nyengine. Tuanze kujifunza utamaduni wa kusubiri na kutumia foleni. Wenye vyombo wakubali kuanza kutumia kitu kinautwa "Reservation" na abiria nao waanze ustaarabu huo wa kupanga kusafiri kwa kuweka foleni, chombo kichukuwe abiria kwa uwezo wake tu waliobaki wasubiri siku nyingine. Wenye vyombo vya usafiri waache tabia ya kuuza tiketi siku ya safiri. FOLENI ndio ustaarabu. Ughaibuni kila pahala pana FOLENI. Tuache kupigania kila pahala au kuruka FOLENI. FOLENI maana yake ANAYEKUJA MWANZO NDIE ANAYEHUDUMIWA. Tusiwe WANAFIKI ndio maana tunauwana hovyo kama kuku kwa UNAFIKI. Maendeleo hayaji kwa UNAFIKI bali kwa mipango thabiti!!!

    ReplyDelete
  10. HILI GARI LIKIFIKA TANGA LIKAMATWE KWA KUJAZA ABIRIA USHAHIDI SI HUO. KAKA MICHUZI TUSAIDIE WATATUMALIZA HAWA WAZEMBE. HII PICHA IPELEKWE TRAFFIC.

    ReplyDelete
  11. Nimependa sana maoni ya anonymous wa Septenber 13 01.38.00. Ni kweli kabisa usalama wa mtu anao yeye mwenyewe, kama umeona basi limejaa teremka tafuta usafiri mwingine. Kama ulibuku usafiri mapema ukawa na kiti; na ukaona madereva au wamiliki gari bado wanajaza ripoti polisi (ingawaje nao wataona ni ulaji) Wizara ya Mawasiliano (naamini wana kitengo ya usalama barabarani) walikazanie hili. Dawa yake ni kuweka faini kubwa mno ambazo zitawauma wakiukao kanuni za usalama barabarani. Kwa kweli tunajimaliza wenyewe. Ukiweka faini kama shilingi milioni moja na kwenda juu wataacha tu hii tabia.

    ReplyDelete
  12. Hao askari wa usalama rushwa tu wanachoangalia ni pesa tu.nchi inanuka rushwa, viongozi wanajari maslahi yao,Roho inaniuma sana ninaposikia watanzania wanakufa kila siku tena idadi kubwa,ingawa sipo Tanzania, mungu yupo ipo siku atawaadhibu nyie wachinjeni ndigu zagu.mungu ibariki Africa.

    ReplyDelete
  13. haya ndio yaleeee mambo ya islander au mshasahau.

    ReplyDelete
  14. Siyo ya huko Tanga tu.Panda ya Dar-Ifakara,Dar-Mahenge utalia mpaka utajuta kuzaliwa.Yanapakia mpaka kushuka inakuwa kero. Na wanausalama unakutanao ukiwaambia wanazunguka pembeni na konda mara hao mna ondoka.

    ReplyDelete
  15. wewe ulieleta taswira hii tupe sababu ya msingi kwa nini ulikubali safari wakati ukijua si salama?

    ReplyDelete
  16. Hawana lolote hao Sumatra,kuna jamaa yenu mmoja anaitwa shirio anajifanya mkali sana pale ubungo lakini amechemsha

    ReplyDelete
  17. Uchu wa pesa:

    Jaza tu upate nyingi!
    Honga askari!

    ReplyDelete
  18. MKANDA MUHIMU SANA UNAPOKUA SAFARINI KUNA BREKI ZA GHAFLA ZAWEZA SABABISHA MTU KUCHOMOKA KAMA INAVYOONYESHA HAPO MBELE KWA KWELI NI HATARI SANA DEREVA HAJAFUNGA MKANDA,HAO WALIOJAZWA HAPO MBELE KAMA LINATOKEA LA KUTOKEA eeeh MUNGU TUEPUSHE NA HAYA MABALAA.

    ReplyDelete
  19. we mtoa maoni wa sa 01:38 ni kweli usalama unaanza kwa ko mwenyewe lakini ikiwa wewe umeuziwa tiket ya sa moja unataka kuwahi kazini na wenzako 100 wameuziwa tiket hivo hivo unafikiri nani wa kulaumu?
    Hakuna database ya kujua abiria wangapi wamekata tiket? mi nitajuaje kama kutakua na abiria 100 wengine kama mimi nimefika mwanzo? ujue bongo hakuna health and safety wala passengers right

    ReplyDelete
  20. Ajali hizi zote zinaweza kuzuiliwa. Jamani mimi kwa maoni yangu nadhani inabidi wananchi wapewe elimu juu ya USALAMA WAO. kama wananchi, abiria wakikataa kujazwa kwenye vyombo hivi vya usafiri, basi wao wana nguvu na uwezo wa kuzuia hizi ajali. Kwa maoni yangu naona ABIRIA na WENYE vyombo vya usafiri wote wana makosa.Hawa abiria ni watu wenye akili timamu, kwa nini wasikatae kuingia kwenye hivi vyombo. Wananchi wakiungana na kuweka mgomo wa kukataa kuingia kwenye hivi vyombo vya usafiri vilivyojaa kupita kiasi, inawezekana kabisa tukazuia hizi ajali mbaya.Pia abiria wanaokubali kuhatarisha maisha yao na ya watoto wadogo wasio na kauli za kutoa maamuzi inabidi nao wachukuliwe hatua za kisheria. hawa abiria inaonekana kuwa wanaingia kwenye hivi vyombo kwa hiari hawalazimiswhi. unaona basi limejaa mpaka mlangoni, bado unaingia kweli hii ni busara. I dont mean to be isensitive, nikiwa kama mzazi wa watoto wawili, inahuzunisha, inakasirisha na kukera kuona kua wazazi wanaingia kwenye vyombo kama hivi na watoto wadogo. sikatai kwenye nchi kuna matatizo ya usafiri, lakini inabidi tuelimishane kuhusu usalama wetu. KAWIA UFIKE.KAMA ABIRIA WATAKATAA KUPAKIWA KAMA KUKU BASI WENYE VYOMBO HIVYO HAWATAKUA NA UWEZO WA KUJAZA VYOMBO VYAO KUPITA KIASI

    ReplyDelete
  21. Ngugu yangu hata ukilalamika hutafanikiwa.

    Mimi niliona hali hii kwenye Abood Dar-Moro. Nikaamua kumwambia mashaka yangu dreva. Nakwambia alinitukana matusi ya nguoni mkapa nikajiona mtupu, na hamna hata abiria aliyesaidi.

    Bahati nzuri tulikuwa kwenye foleni pale ubungo mataa. Nikamwona traffic, nikamwita na kumonyesha ile hali. Akaongea na dreva toka dirishani. Akaanza kuondoka, nilipomuuliza kulikoni akajibu "usinifundishe kazi". Na upande wa abiria wenzangu wakaanza kunishutumu kuwa nawacheleweshea safari yao.

    Dreva akaapa kuwa atanishusha Kibaha, lakini hakufanya hivo maana Kibaha alishusha watu wa nyuma kwa ajili ya mzani.

    Kwahiyo shida iko kote kote- sis abiria tukiona hali hii hatugomi (mf. kwenye meli), askari nao wanategemea hao madreva kwa kula yao, na madreva wanajaza ili wapate cha juu nk nk

    Ni shida kumaliza hii shida kama kila mmoja hatachukua nafasi yake.

    Mdau

    Amsterdam

    ReplyDelete
  22. Makonda na madereva wanaojaza mabasi kupita kiasi wawe wanaswekwa jela sha sha, hakuna cha kesi wala nini, ni Kova tu kusaini.

    ReplyDelete
  23. Sasa ni wakati watanzania tuache tabia za lawama na kuwajibika! Katika hali kama hii abiria wametulia tuli! Ikitokea ajali ooooooh Waziri ajiuzulu! Hivi kila jambo lifanywe na serikali? Tumegeuka mang'ombe? Hatuwezi kufikiri wenyewe? Tunadai haki yetu kwa serikali maafa yakitokea lakini hatutaki kuwajibikia haki hizo. Hata kuhakikisha usalama wetu! Ni aibu! Ni aibu kubwa!Gari limejaa, huna pa kukaa unachoma ndani! Waziri afanye nini? Maana sheria zipo kwanini usimamiwe kufuata sheria! Pweeeh!

    ReplyDelete
  24. mdau wa 01:38pm nakuunga mkono kabisaaaaaaa. tunalaumu wenye mabasi wakati sheria zinavunjwa na abiria wenyewe. ulionena ni 100000000000% sawa kabisa. siku hizi kila mtu ana cha kichina mkononi kwa nini wasiwalipue kwa polisi. hata kama wakija na kuvuta, apigiwe mkuu wao na mchuma usiondoke. waweke hata magogo. jamaa wakiua hawaendi jela. mtaona nahodha aliyechumpa na kuacha mv spice ikizama na abiria ataishia wapi. atapewa tuzo ya ujasiri kwa kuokoa maisha yake na kuua waso na hatia.

    ReplyDelete
  25. HIVI KAMA WAKOLONI WANGEKUWA BADO WAPO TANGANYIKA HII HALI INGETOKEA? AFRIKA NZIMA IKO HIVI. AIBU TUPU.

    ReplyDelete
  26. yani kwa kweli inasikitisha. sijui hali hii mpaka lini. Sijui ni uelewa mdogo au vipi. Abiria wenyewe kwa kweli tunasababisha hali hii, hatujionei huruma wenyewe, umeona kabisa gari ilivyojaa hata kama umekata tiketi wakati huo, unavyopanda na kuona hali hiyo kwa nini usikate shauri ya kuomba urudishiwe nauli yako au kutoa taarifa kituo cha polisi au kwa trafik njiani, Madereva na konda wao wanaangalia maslahi yao tu hawafikirii hata kidogo utu wa mtu. Kwa hali hii tutaendelea tu kupiga kelele na hazitosaidia. jamani ndugu zangu tujali, tuthamini afya njema aliyotujalia Mwenyezi Mungu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...