Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye utiaji saini mkataba wa miradi ya Makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya nchini China, uliofanyika kwenye ukumbu wa Mlimani City Dar es Salaam, leo Septemba 21.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akishuhudia zoezi la utiaji saini na kubadilishana mkataba wa miradi ya Makaa ya mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya China, wakati Mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Christant Mzindakaya na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Liu Canglong, wakisainiana mkataba huo katika ukumbi wa mlimani City jijini Dar es Salaam, leo Septemba 21, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) Christant Mzindakaya, nje ya ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam leo Septemba 21, baada ya kumalizika kwa zoezi la kutiliana saini mkataba wa ya Makaa ya mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya China, wakati Mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Christant Mzindakaya na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Liu Canglong, wakisainiana mkataba huo katika ukumbi wa mlimani City jijini Dar es Salaam, leo Septemba 21, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya Sichuan Hngda Corporation Ltd, Liu Canglong, baada ya kuhudhulia zoezi la utiaji saini mkataba wa miradi ya Makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, uliofanyika leo septemba 21 kwenye Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam, baina ya Shirika la maendeleo ya Taifa (NDC) na kamuni hiyo kutoka nchini China.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika Bendera maalum ya kumbukumbu ya watu wa China, wakati Mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Christant Mzindakaya (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya China, Liu Canglong, (kushoto) wakisainiana mkataba wa miradi ya Makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga katika ukumbi wa mlimani City jijini Dar es Salaam, leo Septemba 21, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akishuhudia zoezi la utiaji saini mkataba wa miradi ya Makaa ya mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga, baina ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Kampuni ya Sichuan Hongda Corporation Ltd ya China, wakati Mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Christant Mzindakaya na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Liu Canglong, wakisainiana mkataba huo katika ukumbi.Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Natumaini huu mkataba sio wa "mawengewenge". Hatukawii siku hizi kuingia ubia na wageni kuchota rasilimali zetu kwa kubadilishana na vipande vya nguo.

    ReplyDelete
  2. Tunawatakia NDC na Sichuan Hongda mafanikio katika utekelezaji wa mkataba huu. Inawezekana wapo wengine katika serikali ya Tanzania hawajafurahia mafanikio haya ila inahitajika kuthubutu ili kuweza kupiga hatua. EEM

    ReplyDelete
  3. wengi tumeshuhudia utiwaji saini kati ya viongo wa NDC chini ya mwenyekiti wake Christant Mzindakaya na Mwenyekiti wa Sichuan Hongda Co., Ltd Liu Canglong. Na hafla yenyewe ilifanyika pale Milimani City mgeni rasmi akiwa Makamu wa Raisi Dkt Gharibu Bilal,

    Nilipotaka kupata taarifa zaidi juu ya kampuni hii huko chini inaonekana haina hata website ila kwa kupekua nimepata baadhi ya taarifa ambazo naona kuwa zina utata kidogo... na nilichofanya nichukue hatua hiyo ni kwamba kwenye utiaji saini kwa mradi mkubwa kama huo hakukuwepo na hata mwambata wa ubalozi wa china hapa nchi au kutokea china..

    Ukipitia hiyo site hapo chini utaona huyu mchina aliyekuja kutia saini mkataba huu hayuko hata kwenye bodi ya wakurugenzi wa kampuni hii huku yeye akija kama mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Sichuan Hongda Co., Ltd. (Liu Canglong)


    Sasa naomba embu kila mtu apitie na upate ukweli wa kampuni hii

    http://www.reuters.com/finance/stocks/companyOfficers?symbol=600331.SS&WTmodLOC=C4-Officers-5

    ReplyDelete
  4. Anonymous wa 22:00 acha kuwa soooooooooooooooooo pessimistic. huu ni mkataba baina ya wahusika na Ubalozi si lazima uwepo hapo ili kuepuka kuonekana umetoa aina fulani ya upendeleo fulani. Kuhusu huyo Bwana, acha kukurupuka na vi-link vyako vilivyopitwa na wakati kwani huyo bwana ni kweli ni Board Chairman wa hiyo kampuni kwani hata Google inaweza kuksaidia kwa hilo.

    http://www.forbes.com/lists/2011/74/china-billionaires-11_Liu-Canglong_TCOY.html

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...